Mastory ya bey
Hello my people
Kuna msemo unasema aliwazalo mjinga basi humtokea,hakika hao walio Sema hakika hawajakosea kabisa
Na kuna msemo unasema ukitaka kujua tabia ya mtu basi angalia marafiki zake
Iko hivi hakika mawazo huambukiza au huathiri maisha yetu kwa namna moja au nyingine, ukiwa na marafiki ambao wanawaza kwa mlengo fulani basi maadamu upo nao kwa muda mwingi basi hakika watakuathiri kwa tabia zao
Mawazo yao yatadhihirika katika maongezi yao ya kila siku na mwisho wa siku utaathirika nayo, wakiwa marafiki wema watakuambukiza tabia nzuri, na kinyume chake wakiwa marafiki wenye tabia mbaya watakuathiri kwa tabia mbaya
The same kwa aliwazalo mjinga basi litamtokea,kwasababu mawazo ndio nishati inayo fanikisha kutokea kwa matokeo kadhaa,mfano hatufanyi jambo lolote lile ila huanzia mawazoni kwetu,kwahiyo mawazo ni nishati ambayo inabadilishwa kuwa matendo
Sasa mtu akijiwazia kuwa yeye dhaifu na hawezi kupambania jambo fulani analolitaka basi atapata matokeo hayo hayo ya kuwa dhaifu na kweli hatopata jambo analolitaka
Let me put this way kama mfano,eti home boys kama mnashindwa kuwatongoza wanawake mnao wataka mkikaa kimya na bila kuchukua hatua yoyote,mnadhani mwanamke atakuja mbele yako na kusema hi home boy do you want me?
Jibu hapana, kwahiyo ukiwaza na kuamini wewe ni mtu imara na unajiamini basi hakika utapata kile ambacho unakiamini
Kwahiyo kuwa makini sana na kile unacho kiwaza mara kwa mara,mawazo yako ndio yataendesha mfumo wako wa maisha,ukiwa chanya au positive basi yatakujenga,utajiamini na nothing can stop you, na kinyume chake ukiwa na mawazo hasi au negative yatakufanya uwe weak na usiye jiamini
Kumbuka jinsi uwazavyo na ndivyo huwavyo,think big
Ni hayo tu.