JamiiForums Usiku wa manane
Unaweza fanya meditation ya kutafuta usingizi pia
Meditation kwangu ilidunda. Bro, kuna demu ametoka Botswana alikuja tukawa tunasoma nae hapo UD, Feb hii 2019, sasa kumbe alikotoka alikua anafanya Meditation yupo sijui stage ya ngapi, akaniambia kuhusu mimi, akaomba nimsindikize kule Mikocheni kuna Wachina wana Meditation (TZ Meditation) duh mi uchu wangu kwakua namtamani nikasema twende. Kufika wakanishawishi na mimi nika register. Aisee ile kitu siwezi. Yaani haielezeki. Eti naangalia kitu kimoja naanza kukumbuka matukio yote im chronological order kutokea nikiwa katoto primary secondary chuo hadi sahivi. Hahahaha. Nililipa ila nilienda twice nikasema hapana. Kama demu wa Kibotswana nikose tu.
 
Hahahaaa pole sana.. mimi nilikua nafanya mida ya jioni. Nimeacha kama mwezi wa 4 mwaka huu. Yahitaji moyo kukaa na ku concentrate kitu kimoja..
Kilichonifanya niache nina shida jwa uti wa mgongo so nikapotezea

Labda vile vinyimbo nyimbo nikiwekaga kwenye cm uwa vinajitahidi kubembeleza. Ila siku hizi nimejulia kutafuta usingizi kwa kusikiliza Podcasts. Ni faster kiasi chake kukiwa hakuna mbu, mashuka masafi na nina angalau hela ya kula kesho asubuhi.
 
Back
Top Bottom