Jaji Ndunguru anachekesha sana

Jaji Ndunguru anachekesha sana

Wakuu pigeni kimya Kimya tu... Mdomo uliponza kichwa.

Thanks God that he's been given a few number of years to save.. the rulling could have gone further...
He better stay calm and save his terms....
Or else it will be worse...
You will have to thank the devil when Samia meets her deserved fate.
Reserve those sentiments for her.
 
Na alivyo mpumbavu wa Sheria, akasahau. Minor offence can not be tried and judged by high court. Hiyo ni kazi ya lower courts ndio maana kesi ya uchochezi ikapelekwa kisutu. Jaji mbumbumbu kabisa. Ametomba Sheria.
Yani kwa kweli Jaji Ndunguru alifanya kosa kubwa sana. Tena la wazi kabisa. Ngoja tuone kwenye rufaa.
 
Inakuwa ngumu sana kwa Watanzania kupata international jobs na itakuwa mbaya zaidi huko mbele ya safari.
The elites kwa tamaa zao au ujinga wameamua ku compromise standards zao.
Ikitokea leo international firms zinahitaji majaji na mahakimu sidhani kama watampa thamani mtanzania.
Watapewa.
 
Wewe bwana,Unafahamu kitu kinaitwa Balance of Probaility kwenye Sheria?Unafahamu kwamba Jaji anapotoa Hukumu anazingatia nini?Unafikiri Kelele za kwamba ni Lissu zinamfanya afikiri tofauti?Wewe huu Ujinga auliandika hapa kwa unaonesha kwamba wewe ni Bushloya mwingine tu.Kwamba unatak Jaji atoe hukumu ya kukufurahisha wwewe ni ujinga wako?


Sasa elewe hivi,TUNDU LISU alitoa kauli husika na hilo hajalikataa,Tafsiri ya sheria iko wazi kwama kutoa kauli tata sio kosa ila sasa kisheria kuna technicalities ambazo jaji anabanwa nazo.Mfano Nikisema Hana Hatia JE tunaruhusu kauli hizo ziwe kawaida?Sasa kwa mbululas kama ninyi mnafikiri mngekuwa na uwezo wa kuamua tofauti kumbe mngekuwa majaji hata kesi mngeikimbia.
Ndio maana nikasema andiko langu hujalielewa. Nimesema mambo ya uchochezi yangebishaniwa Kisutu ambako kesi inaendelea Tena kwenye hatua ya ushahidi. Ndipo tungepata ukweli halisi, sio Jaji kudai serikali haikutishwa halafu kuja Tena kudai kosa la uchochezi.
 
Inakuwa ngumu sana kwa Watanzania kupata international jobs na itakuwa mbaya zaidi huko mbele ya safari.
The elites kwa tamaa zao au ujinga wameamua ku compromise standards zao.
Ikitokea leo international firms zinahitaji majaji na mahakimu sidhani kama watampa thamani mtanzania.
Kwa hukumu kama hizi na kesi kama hizi, ni ngumu kuajiriwa kwenye international firms.
 
You are misleading, when Lissu uttered those words who was incited ? You mean people kept calm in March when to those words were uttered and got incited when Lissu was already remanded in October? Let's be serious.
Exactly 💯💯💯💯
 
Ko anaweza kuhukumiwa mara mbili kwa kosa moja la uchochezi au ile kesi imesha kufa kibudu kwa sababu ibakwa kabla haijabalehe na msomi Ndunguru?
Sheria ipo wazi kwamba 'ni marufuku mtu kuhukumiwa adhabu mara mbili kwa kosa hilo hilo moja'.

Hivyo basi kama wamemhukumu kwa uchochezi na kesi iliyopo Kisutu ni ya uchochezi, ile kesi ya Kisutu imeshakufa.
 
Kwakweli Jaji Ndunguru anachekesha sana.

1. Kichekesho cha kwanza, awali kwenye rulling ya case to answer, Jaji Ndunguru alidai Mh Tundu Lissu ana kesi ya kujibu kuhusu tuhuma zake za uhaini. Cha kushangaza Leo kadai hakuna ushahidi wa kumtia hatiani na kwamba ushahidi wa Jamhuri ulikuwa kwenye assumptions. Kwa maana hiyo, Jaji Ndunguru anatuambia ya kwamba Jamhuri walimshtaki Mh Lissu kwa kutumia ushahidi wa kufikirika usio kuwepo.

Hiki kama sio kichekesho ni Nini? Yani unasema Lissu ana kesi ya kujibu kwenye ushahidi wa assumptions?. Kwanini usinge itupilia mbali hiyo kesi kama hapakuwa na ushahidi wowote wa msingi?. Leo ndio umegundua ya kwamba ushahidi wa msingi haukuwepo, Sasa Lissu alikuwa anajitetea dhidi ya Nini? Kwa kweli Jaji Ndunguru wewe ni comedian wa hatari sana. Inafaa kuacha ujaji na kuwa mchekeshaji, ndio kazi inayokufaa.

2. Kichekesho cha pili, Jaji Ndunguru anadai kwenye hukumu yake ya kwamba mahakama imeangalia tafsiri ya shahidi wa 1,2 na 16 na kuona ni assumption haziwezi kuthibitisha kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali.

Dah! Kwa hivyo Jaji Nduguru anadai ya kwamba Lissu hakuitisha serikali na Wala hakuna ushahidi Wala Nia ya kuonesha Mh Lissu alilenga kuitisha serikali. Sasa ndugu zangu huyo huyo Jaji anadai Mh Lissu hakuitisha serikali lakini aliichochea umma dhidi ya serikali. Hivi unaweza kuichochea umma dhidi ya serikali bila serikali kutishika?. Kwa hivyo serikali haikutishwa Wala kutishika ila uchochezi uliofanyika. Aibu sana.

Dah! Nduguru anachekesha sana kama sio Jaji kwenye kesi yako. Serikali haikutishika sawa, Sasa kama uchochezi haukulenga kuitisha serikali, hatia inatokea wapi?. Aiseeh!

3. Kichekesho cha tatu ndio kikubwa Zaidi, huyo Nduguru hata simuiti Jaji tena, anadai Mh Lissu amepatikana na kosa ndogo la uchochezi. Anadai kwenye ushahidi wake ya kwamba kwenye kesi ya msingi ya uhaini kulikuwa na vimelea vya uchochezi ambavyo vinaonesha kulikuwa na uchochezi na kwamba mshatakiwa hakuvipinga.

Ila Ndunguru amesahau ya kwamba Kuna kesi nyingine, dhidi ya Mh Lissu dhidi ya uchochezi, ipo kwenye mahakama ya Kisutu, tena ilikuwa imefika kwenye ushahidi. Na shahidi wa kwanza alikuwa ametoa ushahidi wake. Inakuwaje Tena Jaji anaileta kesi hiyo kwenye kesi ya uhaini?.

Anachekesha sana. Kimbelembele cha nini kuamua kesi ambayo ipo kwenye hatua ya ushahidi kwenye mahakama nyingine?. Ina maana DPP alitenganisha Uhaini na uchochezi ila mahakama inalazimisha kulileta kwenye kesi ya uhaini. Kwanini wasinge subiria kesi hiyo ya uchochezi Kisutu ifikie mwisho?.

Huyu comedian kapewa kesi ya uhaini ashughulikie kweli kaishughulikia kagundua ya kwamba hakuna uhaini, hapo hapo akarukia kesi ya Kisutu ya uchochezi ambayo haimhusu akidai Sheria inamruhusu kumhukumu mshitakiwa kwa kosa ambalo hajashtakiwa nalo, eti kosa dogo. Kosa dogo kivipi wakati DPP alitenganisha makosa yote mawili Kila Moja lijitegemee? Moja liendee mahakama kuu na linguine lisikilizwe mahakama ya Kisutu? Aiseeh ni kichekesho hiki.

Mwisho, niseme hivi, Ndunguru amefanya kazi ya kuisaidia Jamhuri kumtia hatiani Lissu wakati sio kazi ya mahakama kuanza kutafuta makosa kwa tochi ili tu mtuhumiwa apatikane na hatia. Mahakama zinatakiwa ziwe adversial zinaletewa kesi na kuamua sio kutafuta makosa ambayo hayapo kwenye mashtaka mbele yake. Niseme tu, Ile haikuwa hukumu Bali ilikuwa ni kichekesho tu. Namshukuru Mh Tundu Lissu kwa kumwambia ukweli huyo Ndunguru ya kwamba asome adhabu yake aliyoelekezwa na Samiah.
Mkuu,

Hapo issue yenye swali kubwa ni namba 3.

Namba 1 na 2 zina maelezo.

Namba 1

Inawezekana Jaji kuona Lissu ana kesi ha kujibu, kabla hajasikiliza ushahidi, halafu akasikikiza ushabidi, akaona Lissu hana hatia.

Hapo kuna mambo mawili tofauti, Lissu kupatikana kuwa ana kesi ya kujibu, na Lissu kupatikana hana hatia.

Jaji anaweza kuona Lissu ana kesi ya kujibu, akasikiliza ushahidi, akaona jshahidi wote una matatizo, Lissu hana hatia.

Ili kujua Lissu hana hatia, ilimbidi Jaji asikilize ushahidi kwanza.

Namba 2.

Haya maneno mengi kama "kuitisha serikali" na "uchochezi" pengine yana maana yake specific kisheria na tukiyatumia kama maneno ya kwenye Kiswahili cha kawaida tunaweza kukosa muktadha mzima wa kisheria, hapo ndipo unapokuja umuhimu wa kupata tafsiri ya kisheria, si ya Kiswahili.

Namba 3.

Hapa ndipo kuna utata na rufaa itakatwa na Lissu kuangalia uhalali wa Lissu kuhukumiwa kwa kosa tofauti na aliloshitakiwa, kutopewa nafasi ya kujitetea kwa kosa hilo, etc.
 
Hii kesi, kwa mnaosoma Sheria imewavua nguo. Utajiitaje wakili msomi wakati sisi tusionaelimu tunaona mnapuyanga. Hivi kwa akili za la Saba, unaweza mhukumu mtu kwa kutamani mke wa mtu wakati ulimshitaki kuwa amebaka? Hilo jina la wasomi futeni tu.
 
Observation yako ni kweli kabisa.
Kutakuwa na vi-reform vya hapa na pale vya danganya toto. Hii nimemsikia Namba moja huko koridon akilisemea. Limeshapangwa~!
Hii ndio sababu ya Namba2 kujilipua wakamficha, Sasa kazi kwenu Watanganyika~!!
 
Kama hujui jaribu kujifunza kwanza ndio uchallenge.

Mtuhumiwa akiwa na case to answer haina maana kwamba kapatikana na hatia. Maana yake ni kuwa anawajibu wakujibu tuhuma zilizowekwa mbele yake, anaweza akajibu tuhuma na kuiwezesha mahakama kutoa hukumu sahihi bila hivyo atafungwa bila kusikilizwa.

Ndio maana Majaji kwenye hukumu yao wamesema kuwa charge ilikuwa sahihi tofauti na Lissu ambaye aliweka pingamizi kuwa charge haikuwa sawa.
Charge gani ilikuwa sahihi Mkuu.?
 
huyo samia anadhani atakaa madarakani hadi lini.
Mwenyewe kachoka mbaya. Wizi kila kona na nguvu ya kukemea aitoe wapi.

Kazi yake kuu ni kupambana na wale anaowaona wana nguvu ya ushawishi kuliko yeye. Jambo ambalo kalishindwa. Hebu fikiria wale Wamama watatu tena wako nje ya nchi, hawana majeshi. Lkn wakikohoa tu, anakosa usingizi. Vyombo vyote vya ulinzi na usalama vinamwagwa barabarani. Je wangekuwa hapa nyumbani?

Watu wameuliwa kwa maelfu wametekwa na kupotezwa kwa mamia wamefungwa kwa mamia na bado wanaendelea wakitegemea nchi itatulia wapate amani lahasha. Ndiyo kwanza moto unazidi kukolea. Hakuna siku wameacha kulala na viatu.
 
Kwakweli Jaji Ndunguru anachekesha sana.

1. Kichekesho cha kwanza, awali kwenye rulling ya case to answer, Jaji Ndunguru alidai Mh Tundu Lissu ana kesi ya kujibu kuhusu tuhuma zake za uhaini. Cha kushangaza Leo kadai hakuna ushahidi wa kumtia hatiani na kwamba ushahidi wa Jamhuri ulikuwa kwenye assumptions. Kwa maana hiyo, Jaji Ndunguru anatuambia ya kwamba Jamhuri walimshtaki Mh Lissu kwa kutumia ushahidi wa kufikirika usio kuwepo.

Hiki kama sio kichekesho ni Nini? Yani unasema Lissu ana kesi ya kujibu kwenye ushahidi wa assumptions?. Kwanini usinge itupilia mbali hiyo kesi kama hapakuwa na ushahidi wowote wa msingi?. Leo ndio umegundua ya kwamba ushahidi wa msingi haukuwepo, Sasa Lissu alikuwa anajitetea dhidi ya Nini? Kwa kweli Jaji Ndunguru wewe ni comedian wa hatari sana. Inafaa kuacha ujaji na kuwa mchekeshaji, ndio kazi inayokufaa.

2. Kichekesho cha pili, Jaji Ndunguru anadai kwenye hukumu yake ya kwamba mahakama imeangalia tafsiri ya shahidi wa 1,2 na 16 na kuona ni assumption haziwezi kuthibitisha kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali.

Dah! Kwa hivyo Jaji Nduguru anadai ya kwamba Lissu hakuitisha serikali na Wala hakuna ushahidi Wala Nia ya kuonesha Mh Lissu alilenga kuitisha serikali. Sasa ndugu zangu huyo huyo Jaji anadai Mh Lissu hakuitisha serikali lakini aliichochea umma dhidi ya serikali. Hivi unaweza kuichochea umma dhidi ya serikali bila serikali kutishika?. Kwa hivyo serikali haikutishwa Wala kutishika ila uchochezi uliofanyika. Aibu sana.

Dah! Nduguru anachekesha sana kama sio Jaji kwenye kesi yako. Serikali haikutishika sawa, Sasa kama uchochezi haukulenga kuitisha serikali, hatia inatokea wapi?. Aiseeh!

3. Kichekesho cha tatu ndio kikubwa Zaidi, huyo Nduguru hata simuiti Jaji tena, anadai Mh Lissu amepatikana na kosa ndogo la uchochezi. Anadai kwenye ushahidi wake ya kwamba kwenye kesi ya msingi ya uhaini kulikuwa na vimelea vya uchochezi ambavyo vinaonesha kulikuwa na uchochezi na kwamba mshatakiwa hakuvipinga.

Ila Ndunguru amesahau ya kwamba Kuna kesi nyingine, dhidi ya Mh Lissu dhidi ya uchochezi, ipo kwenye mahakama ya Kisutu, tena ilikuwa imefika kwenye ushahidi. Na shahidi wa kwanza alikuwa ametoa ushahidi wake. Inakuwaje Tena Jaji anaileta kesi hiyo kwenye kesi ya uhaini?.

Anachekesha sana. Kimbelembele cha nini kuamua kesi ambayo ipo kwenye hatua ya ushahidi kwenye mahakama nyingine?. Ina maana DPP alitenganisha Uhaini na uchochezi ila mahakama inalazimisha kulileta kwenye kesi ya uhaini. Kwanini wasinge subiria kesi hiyo ya uchochezi Kisutu ifikie mwisho?.

Huyu comedian kapewa kesi ya uhaini ashughulikie kweli kaishughulikia kagundua ya kwamba hakuna uhaini, hapo hapo akarukia kesi ya Kisutu ya uchochezi ambayo haimhusu akidai Sheria inamruhusu kumhukumu mshitakiwa kwa kosa ambalo hajashtakiwa nalo, eti kosa dogo. Kosa dogo kivipi wakati DPP alitenganisha makosa yote mawili Kila Moja lijitegemee? Moja liendee mahakama kuu na linguine lisikilizwe mahakama ya Kisutu? Aiseeh ni kichekesho hiki.

Mwisho, niseme hivi, Ndunguru amefanya kazi ya kuisaidia Jamhuri kumtia hatiani Lissu wakati sio kazi ya mahakama kuanza kutafuta makosa kwa tochi ili tu mtuhumiwa apatikane na hatia. Mahakama zinatakiwa ziwe adversial zinaletewa kesi na kuamua sio kutafuta makosa ambayo hayapo kwenye mashtaka mbele yake. Niseme tu, Ile haikuwa hukumu Bali ilikuwa ni kichekesho tu. Namshukuru Mh Tundu Lissu kwa kumwambia ukweli huyo Ndunguru ya kwamba asome adhabu yake aliyoelekezwa na Samiah.
Huyu Jaji alivyokaa kaa tu, anachekesha sana.
 
Back
Top Bottom