Jaji Ndunguru anachekesha sana

Jaji Ndunguru anachekesha sana

CCM inabidi washikilie madaraka kwa muda mrefu sana la sivyo hiki kituko lazima tukifufue.

Mahakama hiki ni kituko, Majaji mna hudumiwa kila kitu kwa pesa za umma ili mfanye vituko. 🚮
Sijui majaji wanamuogopa nani? Kwani kutenda haki ni shida? Wanatuangusha sana.
 
Kwakweli Jaji Ndunguru anachekesha sana.

1. Kichekesho cha kwanza, awali kwenye rulling ya case to answer, Jaji Ndunguru alidai Mh Tundu Lissu ana kesi ya kujibu kuhusu tuhuma zake za uhaini. Cha kushangaza Leo kadai hakuna ushahidi wa kumtia hatiani na kwamba ushahidi wa Jamhuri ulikuwa kwenye assumptions. Kwa maana hiyo, Jaji Ndunguru anatuambia ya kwamba Jamhuri walimshtaki Mh Lissu kwa kutumia ushahidi wa kufikirika usio kuwepo.

Hiki kama sio kichekesho ni Nini? Yani unasema Lissu ana kesi ya kujibu kwenye ushahidi wa assumptions?. Kwanini usinge itupilia mbali hiyo kesi kama hapakuwa na ushahidi wowote wa msingi?. Leo ndio umegundua ya kwamba ushahidi wa msingi haukuwepo, Sasa Lissu alikuwa anajitetea dhidi ya Nini? Kwa kweli Jaji Ndunguru wewe ni comedian wa hatari sana. Inafaa kuacha ujaji na kuwa mchekeshaji, ndio kazi inayokufaa.

2. Kichekesho cha pili, Jaji Ndunguru anadai kwenye hukumu yake ya kwamba mahakama imeangalia tafsiri ya shahidi wa 1,2 na 16 na kuona ni assumption haziwezi kuthibitisha kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali.

Dah! Kwa hivyo Jaji Nduguru anadai ya kwamba Lissu hakuitisha serikali na Wala hakuna ushahidi Wala Nia ya kuonesha Mh Lissu alilenga kuitisha serikali. Sasa ndugu zangu huyo huyo Jaji anadai Mh Lissu hakuitisha serikali lakini aliichochea umma dhidi ya serikali. Hivi unaweza kuichochea umma dhidi ya serikali bila serikali kutishika?. Kwa hivyo serikali haikutishwa Wala kutishika ila uchochezi uliofanyika. Aibu sana.

Dah! Nduguru anachekesha sana kama sio Jaji kwenye kesi yako. Serikali haikutishika sawa, Sasa kama uchochezi haukulenga kuitisha serikali, hatia inatokea wapi?. Aiseeh!

3. Kichekesho cha tatu ndio kikubwa Zaidi, huyo Nduguru hata simuiti Jaji tena, anadai Mh Lissu amepatikana na kosa ndogo la uchochezi. Anadai kwenye ushahidi wake ya kwamba kwenye kesi ya msingi ya uhaini kulikuwa na vimelea vya uchochezi ambavyo vinaonesha kulikuwa na uchochezi na kwamba mshatakiwa hakuvipinga.

Ila Ndunguru amesahau ya kwamba Kuna kesi nyingine, dhidi ya Mh Lissu dhidi ya uchochezi, ipo kwenye mahakama ya Kisutu, tena ilikuwa imefika kwenye ushahidi. Na shahidi wa kwanza alikuwa ametoa ushahidi wake. Inakuwaje Tena Jaji anaileta kesi hiyo kwenye kesi ya uhaini?.

Anachekesha sana. Kimbelembele cha nini kuamua kesi ambayo ipo kwenye hatua ya ushahidi kwenye mahakama nyingine?. Ina maana DPP alitenganisha Uhaini na uchochezi ila mahakama inalazimisha kulileta kwenye kesi ya uhaini. Kwanini wasinge subiria kesi hiyo ya uchochezi Kisutu ifikie mwisho?.

Huyu comedian kapewa kesi ya uhaini ashughulikie kweli kaishughulikia kagundua ya kwamba hakuna uhaini, hapo hapo akarukia kesi ya Kisutu ya uchochezi ambayo haimhusu akidai Sheria inamruhusu kumhukumu mshitakiwa kwa kosa ambalo hajashtakiwa nalo, eti kosa dogo. Kosa dogo kivipi wakati DPP alitenganisha makosa yote mawili Kila Moja lijitegemee? Moja liendee mahakama kuu na linguine lisikilizwe mahakama ya Kisutu? Aiseeh ni kichekesho hiki.

Mwisho, niseme hivi, Ndunguru amefanya kazi ya kuisaidia Jamhuri kumtia hatiani Lissu wakati sio kazi ya mahakama kuanza kutafuta makosa kwa tochi ili tu mtuhumiwa apatikane na hatia. Mahakama zinatakiwa ziwe adversial zinaletewa kesi na kuamua sio kutafuta makosa ambayo hayapo kwenye mashtaka mbele yake. Niseme tu, Ile haikuwa hukumu Bali ilikuwa ni kichekesho tu. Namshukuru Mh Tundu Lissu kwa kumwambia ukweli huyo Ndunguru ya kwamba asome adhabu yake aliyoelekezwa na Samiah.
Jaji Ndunguru na jopo lake wote ni machoko tu mama'e zao.
 
Wakuu pigeni kimya Kimya tu... Mdomo uliponza kichwa.

Thanks God that he's been given a few number of years to save.. the rulling could have gone further...
He better stay calm and save his terms....
Or else it will be worse...
 
TAML aliitishia serikali hadi ikaogopa kujitokeza mahakamani kuthibitisha kutishwa kwake.Halafu,TAML alichochea watu wasiende kupiga kura,kati ya watu milioni 32,wakajitokeza watu milioni 31 na malaki kadhaa wakapiga kura kwa kumpa ushindi mtu mmoja kwa asilimia 97 nukta kadhaa.Approximeatly, asilimia 98 karibia 100 kabisa!Sasa alimtisha nani huyo TAML?This cadava won't end up until it ends up!
Very true. Na hiki ndicho cha msingi. Uchaguzi haukususiwa kabisa halafu mahakama Inadai aliichochea watu kuzuia uchaguzi.
 
Wakuu pigeni kimya Kimya tu... Mdomo uliponza kichwa.

Thanks God that he's been given a few number of years to save.. the rulling could have gone further...
He better stay calm and save his terms....
Or else it will be worse...
No way. Staying calm means being fearful to the stupid regime. Also, staying silent means agreeing to the injustices that have been committed against Lissu and other Tanzanians.
 
No way. Staying calm means being fearful to the stupid regime. Also, staying silent means agreeing to the injustices that have been committed against Lissu and other Tanzanians.
From his utterances, it's without a doubt that the MO29 aftermath his burden.
Let it go..
 
sasa nimejua kwa nini mawakili wa serikali huwa hawashindi kesi ambazo serikali ya JMT inashtakiwa nje ya chi!
Nawavulia kofia wawekezaji kulazimisha korti za nje ndio zisikilize kesi za mikataba!
Hebu fikiria umewekeza matrilioni ya pesa, halafu kesi ya mgogoro wa kimaslai anapewa JAJI NDUNGURU!
Kwa kweli kwa Hali hii, inaonesha mawakili wa serikali huwa wanabebwa na mahakama. Yani mahakama zinawasaidia kushinda kesi .
 
Mlongo, huyo mzee ni mlafi, mpenda rushwa, fedhuri, ndio maana ndugu zake wanasema wangemuacha ataabike na hali ya ajabu aliyoipata akiwa Mbeya huko
Toka jana ndugu zake wanampopoa, huyo mzee wa hovyo kabisa
Wafanye jambo basi ndugu zake. Maana wanaweza kumfikia.
 
Ingekua Serikali na sikivu au ile yenye Weledi, huyo Dastan alipaswa asiwe hata hakimu wa mahakama ya mwanzo, cha ajabu eti Jaji wa mahakama kuu.

Ni msiba huu, tena mzito haswaa.
Hana hadhi hata ya kuwa karani wa mahakama
 
Kwa kweli kwa Hali hii, inaonesha mawakili wa serikali huwa wanabebwa na mahakama. Yani mahakama zinawasaidia kushinda kesi .
Zaidi ya 50% ya majaji walikuwa mawakili wa serikali na hili halikuja kwa bahati bali ni mkakati wa kuifanya Mahakama iwe wakala wa serikali.
 
Kwa hiyo Lisu ataendelea kuhudhuria kesi ya uchochezi Kisutu au DPP atajifanya kutokuendelea nayo?
DPP itabidi aifute. Maana ilisimama kwa ajili ya kusubiria kesi ya uhaini iishe, Sasa Ndunguru kakimbilia kutos adhabu.
 
Ndunguru ni bush lawyer kwenye moja ya Kangaroo court za Tanzania. Hakika ameonyesha uwezo wake wa kitaaluma mpaka mwisho wa upeo wake.....

Kumfurahisha Wasira na wengine lakini zaidi kusaidia lengo la Samia kuifuta Chadema kama chama cha siasa.
Kweli kabisa. Yeye anafikiria kuwafurahisha wanasiasa na sio kutenda haki.
 
Back
Top Bottom