econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 25,741
- 41,198
Kwakweli Jaji Ndunguru anachekesha sana.
1. Kichekesho cha kwanza, awali kwenye rulling ya case to answer, Jaji Ndunguru alidai Mh Tundu Lissu ana kesi ya kujibu kuhusu tuhuma zake za uhaini. Cha kushangaza Leo kadai hakuna ushahidi wa kumtia hatiani na kwamba ushahidi wa Jamhuri ulikuwa kwenye assumptions. Kwa maana hiyo, Jaji Ndunguru anatuambia ya kwamba Jamhuri walimshtaki Mh Lissu kwa kutumia ushahidi wa kufikirika usio kuwepo.
Hiki kama sio kichekesho ni Nini? Yani unasema Lissu ana kesi ya kujibu kwenye ushahidi wa assumptions?. Kwanini usinge itupilia mbali hiyo kesi kama hapakuwa na ushahidi wowote wa msingi?. Leo ndio umegundua ya kwamba ushahidi wa msingi haukuwepo, Sasa Lissu alikuwa anajitetea dhidi ya Nini? Kwa kweli Jaji Ndunguru wewe ni comedian wa hatari sana. Inafaa kuacha ujaji na kuwa mchekeshaji, ndio kazi inayokufaa.
2. Kichekesho cha pili, Jaji Ndunguru anadai kwenye hukumu yake ya kwamba mahakama imeangalia tafsiri ya shahidi wa 1,2 na 16 na kuona ni assumption haziwezi kuthibitisha kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali.
Dah! Kwa hivyo Jaji Nduguru anadai ya kwamba Lissu hakuitisha serikali na Wala hakuna ushahidi Wala Nia ya kuonesha Mh Lissu alilenga kuitisha serikali. Sasa ndugu zangu huyo huyo Jaji anadai Mh Lissu hakuitisha serikali lakini aliichochea umma dhidi ya serikali. Hivi unaweza kuichochea umma dhidi ya serikali bila serikali kutishika?. Kwa hivyo serikali haikutishwa Wala kutishika ila uchochezi uliofanyika. Aibu sana.
Dah! Nduguru anachekesha sana kama sio Jaji kwenye kesi yako. Serikali haikutishika sawa, Sasa kama uchochezi haukulenga kuitisha serikali, hatia inatokea wapi?. Aiseeh!
3. Kichekesho cha tatu ndio kikubwa Zaidi, huyo Nduguru hata simuiti Jaji tena, anadai Mh Lissu amepatikana na kosa ndogo la uchochezi. Anadai kwenye ushahidi wake ya kwamba kwenye kesi ya msingi ya uhaini kulikuwa na vimelea vya uchochezi ambavyo vinaonesha kulikuwa na uchochezi na kwamba mshatakiwa hakuvipinga.
Ila Ndunguru amesahau ya kwamba Kuna kesi nyingine, dhidi ya Mh Lissu dhidi ya uchochezi, ipo kwenye mahakama ya Kisutu, tena ilikuwa imefika kwenye ushahidi. Na shahidi wa kwanza alikuwa ametoa ushahidi wake. Inakuwaje Tena Jaji anaileta kesi hiyo kwenye kesi ya uhaini?.
Anachekesha sana. Kimbelembele cha nini kuamua kesi ambayo ipo kwenye hatua ya ushahidi kwenye mahakama nyingine?. Ina maana DPP alitenganisha Uhaini na uchochezi ila mahakama inalazimisha kulileta kwenye kesi ya uhaini. Kwanini wasinge subiria kesi hiyo ya uchochezi Kisutu ifikie mwisho?.
Huyu comedian kapewa kesi ya uhaini ashughulikie kweli kaishughulikia kagundua ya kwamba hakuna uhaini, hapo hapo akarukia kesi ya Kisutu ya uchochezi ambayo haimhusu akidai Sheria inamruhusu kumhukumu mshitakiwa kwa kosa ambalo hajashtakiwa nalo, eti kosa dogo. Kosa dogo kivipi wakati DPP alitenganisha makosa yote mawili Kila Moja lijitegemee? Moja liendee mahakama kuu na linguine lisikilizwe mahakama ya Kisutu? Aiseeh ni kichekesho hiki.
Mwisho, niseme hivi, Ndunguru amefanya kazi ya kuisaidia Jamhuri kumtia hatiani Lissu wakati sio kazi ya mahakama kuanza kutafuta makosa kwa tochi ili tu mtuhumiwa apatikane na hatia. Mahakama zinatakiwa ziwe adversial zinaletewa kesi na kuamua sio kutafuta makosa ambayo hayapo kwenye mashtaka mbele yake. Niseme tu, Ile haikuwa hukumu Bali ilikuwa ni kichekesho tu. Namshukuru Mh Tundu Lissu kwa kumwambia ukweli huyo Ndunguru ya kwamba asome adhabu yake aliyoelekezwa na Samiah.