J. Samwel Malecela ni mgonjwa

J. Samwel Malecela ni mgonjwa

Ugua pole Mzee. Mungu akusaidie upone haraka na kurejea katika afya yako

Huyu mzee ni mzee wetu wote...na zaidi ya hapo ni baba wa mmoja wa member mwenzetu na rafiki yetu ...sasa you can not hate him on both.....

Ugua pole mzee jsm....mungu akupe uponyaji ...na aijalie familia yake na madaktari kumuuguza vyema!![/b]

Ugua pole mzee Male tingatinga linakukokotoa magugu,

Mungu akupe tawfif,mchango wako bado unahitajika sana katika taifa hili.

Kama tunataka augue pole, atapona kweli???!!

Tumwombee apone haraka na si augue pole!!!
 
Naona jamii forums wakati mwingine kuna kuna na tabia zisizojali maadili na utu. Masuala ya itikadi yasiingizwe kwenye nafsi ya mtu au familia ya mtu. Tunapingana na hoja hatupingani na mtu. Tunajadili hoja na kama mtu anaelewa abadilike na si kumpinga mtu huko ni kuishiwa hoja na kuwa mfinyu wa mawazo.

Mzee Malecela amekuwa mtumishi wa umma katika maisha yake, na wengi tunamkumbuka sana, na tunasikitika kwa yaliyompata, na Tunamwomba Mungu amrejeshee afya yake apate nguvu maridhawa. Na poleni kwa familia yake na wote wenye mapenzi mema.

ametusaidia nini kwa utumishi wake wa umma zaidi ya kutuharibia nchi yetu,
mimi sio mnafikie,,mwacheni afe aondoke zake tupunguze mizigo
 
Ugua pole Mzee. Mungu akusaidie upone haraka na kurejea katika afya yako

Ugua pole mzee jsm....mungu akupe uponyaji ...na aijalie familia yake na madaktari kumuuguza vyema!![/b][/QUOTE]

Ugua pole mzee Male tingatinga linakukokotoa magugu,

uGUA POLE MZEE WATU!

Ugua pole Mzee JSM

ugua pole mzee wetu

Duh!! Kazi ipo!!!

ugua pole

Ugua Pole Mzee John Samwel Malecela
 
Naona jamii forums wakati mwingine kuna kuna na tabia zisizojali maadili na utu. Masuala ya itikadi yasiingizwe kwenye nafsi ya mtu au familia ya mtu. Tunapingana na hoja hatupingani na mtu. Tunajadili hoja na kama mtu anaelewa abadilike na si kumpinga mtu huko ni kuishiwa hoja na kuwa mfinyu wa mawazo.Mzee Malecela amekuwa mtumishi wa umma katika maisha yake, na wengi tunamkumbuka sana, na tunasikitika kwa yaliyompata, na Tunamwomba Mungu amrejeshee afya yake apate nguvu maridhawa. Na poleni kwa familia yake na wote wenye mapenzi mema.
Labda huo ndio u CDM, maana inaonekana jambo la maana hapa ni kutukana viongozi hata wakati ambao tulipaswa tuwe na ubinadamu.
 
Labda huo ndio u CDM, maana inaonekana jambo la maana hapa ni kutukana viongozi hata wakati ambao tulipaswa tuwe na ubinadamu.

ecoli hakuna mtu aliyetukana zaidi ya kila mtu kutoa alicho nacho moyoni
 
Pole sana Mzee Mungu akuponye .Ukisha pona uje kuwasumbua watanzania kuwaongezea umasikini kwa jina la CCM . Sitasahau maneno ya huyu mzee kwa kweli . Mungu ampe afya njema in Jesus name.
 
malecela.jpg

Wednesday, June 22, 2011
MWANASIASA mkongwe na kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Samwel Malecela ni mgonjwa na taarifa za uhakika zinaeleza kwamba amefanyiwa upasuaji wa moyo nchini Uingereza. Habari za kuumwa kwa mwanasiasa huyo ambaye ameshika nyadhifa mbalimbali serikalini na katika chama tawala zilitangazwa jana na Spika wa Bunge, Anne Makinda wakati akiahirisha kikao cha bunge. “Naibu Spika (Job Ndugai) haonekani hapa kwa kuwa amesafiri, yuko Uingereza. Naye mheshimiwa Anne Kilango hayupo pia hapa kwa kuwa mzee Malecela (mume wake) anaumwa na amefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo kule Uingereza," alisema Spika Makinda bila ya kufafanua.

Hata hivyo, taarifa zilizopatikana baadaye jana mchana mjini hapa zilieleza kuwa Malecelea alifanyiwa upasuaji huo nchini Uingereza na afya yake imeanza kuimarika. Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel aliieleza Mwananchi kuwa ofisi yake haikuwa na taarifa kuhusu kuumwa kwa Malecela kwa kuwa si mbunge tena. “Hata sisi tumesikia mle ndani (bungeni), lakini hatukuwa na habari hizo. Kwa hiyo, sina zaidi cha kueleza,’’ alisema Joel. Mmoja wa wabunge ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema jana kuwa Malecela yuko Uingereza na amefanyiwa upasuaji huo tangu Juni 14 na kwamba hali yake sasa imeanza kuimarika. “Kimsingi, mimi sijui amelazwa hospitali gani, lakini ukweli ni kwamba yuko Uingereza na alifanyiwa upasuaji Jumanne iliyopita na jana (juzi) nimezungumza na mtu wa karibu yake ambaye anasema kuwa hali yake ni nzuri. Tunamshukuru Mungu,’’ alisema mbunge huyo.

Alisema kuwa Malecela alikwenda Uingereza kwa safari za kawaida ikiwa ni pamoja na kuangaliwa afya yake, lakini baada ya vipimo iligundulika kuwa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo na alitakiwa afanyiwe upasuaji mapema. Aliongeza kuwa baada ya majibu hayo, Malecela alitoa taarifa serikalini ambapo walimtumia fedha haraka na kumsafirisha mke wake (Anne Kilango) ili akamuuguze wakati amefanyiwa upasuaji. Nyumbani kwa mwanasiasa huyo, wasaidizi wake wa karibu walisema kuwa hali ya mzee huyo inaendelea vizuri. “Taarifa tulizoletewa kutoka kwa mmoja wa watu wanaomsaidia mzee, wanasema kuwa anaendelea vizuri na tuna imani kuwa Mungu atamsaidia, atapona na kurudi nyumbani haraka,’’ alisema mmoja wa watu wanaoishi nyumbani kwa Malecela,eneo la Kilimani mjini Dodoma. Malecela,77, ameshika nyadhifa kadhaa zikiwamo za uwaziri, uwaziri mkuu na mbunge kwa vipindi tofauti hadi alipostaafu siasa mwaka jana akiwa mbunge wa Mtera. Aliwahi pia kuwa makamu mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara, ambako alishiriki katika kazi nyingi zikiwamo za kuwapigia kampeni wagombea wa wa chama hicho kila ulipojitokeza uchaguzi mdogo.

Chanzo: Mwananchi
 
ametusaidia nini kwa utumishi wake wa umma zaidi ya kutuharibia nchi yetu,
mimi sio mnafikie,,mwacheni afe aondoke zake tupunguze mizigo

- Rosemarie, kwa hoja kama yako kwanza unatakiwa kuueleza umma wewe umelisaidia vipi hili taifa ndio uombee wasiolisaidia wafe, na kama wewe hujalisaidia hili taifa kufa kwanza wewe ndio wengine wafuaatie, je wewe umelifanyia nini hili taifa mpaka unafaa kuishi as per hoja yako! ha! ha! imenichekesha sana!

Es!
 
Alisema kuwa Malecela alikwenda Uingereza kwa safari za kawaida ikiwa ni pamoja na kuangaliwa afya yake...

Malecela alitoa taarifa serikalini ambapo walimtumia fedha haraka na kumsafirisha mke wake (Anne Kilango) ili akamuuguze wakati amefanyiwa upasuaji.
Kakimbilia Uingereza kama Nyerere.

Malecela na Anna Kilango hawana dola 800 za tiketi ya Anna kwenda Uingereza mpaka waiminye Serikali bankrupt? Pole tujipe Watanzania tutakaofia majumbani jioni ya leo kwa kukosa anti-malaria pills, sio hivi vi vizee self-serving masquerading as socialist leaders.
 
Kuna hoja zingene kwa kweli unabaki kucheka na kushangaa maana huwezi kuipinga wala huwezi kuiunga mkono! Hii hoja inaitwa hoja tata.
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Malecela azungumzia afya yake
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Wednesday, 22 June 2011 21:40 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] digg

Boniface Meena
MWANASIASA mkongwe na kada maarufu wa CCM, John Malecela, amezungumzia afya yake kutokea nchini Uingereza, akieleza kuwa inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo katika Hospitali ya Wellington North nchini humo.

Hata hivyo, taarifa za kitaalamu zilizolifikia gazeti hili zinaonyesha kuwa Malecela alipata tatizo la kuvimba kwa mishipa inayotoa damu moyoni kwenda mwilini na kusababisha mtiririko wa damu kuyumba kwa kiasi.

Taarifa zilisema kutokana na hali hiyo, njia pekee ya kuondoa tatizo hilo ilikuwa kumfanyia upasuaji mkubwa wa moyo ambapo madaktari walilazimika pia kuchukua mishipa kutoka katika mguu wake na kuweka kwenye moyo wake.

Lakini jana, Malecela mwenyewe aliyezungumza na Mwananchi kutoka Uingereza alikolazwa baada ya kufanyiwa upasuaji huo, alisema kuwa madaktari wamemshauri afanye mazoezi kwa muda wa wiki tatu hadi sita ili waangalie hali yake na baada ya hapo wataweza kumpa ruhusu ya kurudi nchini.

"Ninaendelea vizuri na madaktari wameniambia nifanye mazoezi kwa muda wa wiki tatu hadi sita kuiangalia hali ikoje ili waweze kunipa certificate (cheti) ya kuweza kurudi nyumbani,"alisema Malecela.

Mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, amezungumzia hali ya mwenendo wa afya yake baada ya juzi Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuwatangazia wabunge taarifa za kutokuwapo bungeni kwa Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela kutokana na mumewe kuwa mgonjwa na kufanyiwa upasuaji wa moyo.

Mama Kilango naye azungumzia
afya ya mumewe

Akizungumzia hali ya mumewe, Kilango alisema kuwa walikwenda nchini Uingereza Mei 11 mwaka huu wa ajili ya kumfanyia Malecela uchunguzi wa kawaida wa afya kama ilivyo kwa viongozi wa Serikali na alikuwa hana tatizo lolote.

Alisema kuwa yeye na mumewe wana kawaida ya kufanya mazoezi kila siku na kwamba walipokuwa katika mazoezi ya kawaida nchini Uingereza ambapo Malecela alianza kulalamika kuwa anapumua kwa shida, ndipo walikwenda hospitali ambapo alipimwa na daktari kumweleza kuwa ana matatizo ya moyo.

"Madaktari walimpima wakaona kuna mishipa inayotoa damu moyoni kwenda mwilini ambayo ilikuwa imevimba kutokana na Calcium kujikita kwenye mishipa na kuzuia mtiririko wa damu," alisema Kilango.

Kilango alisema upasuaji huo ulifanyika Mei 31 mwaka huu katika Hospitali ya Wellington North na daktari aitwaye Rakesh Uppal.

"Upasuaji umefanikiwa na yuko nyumbani sasa. Anatakiwa afanye mazoezi mara tatu kwa siku, dakika 20 asubuhi, dakika 20 mchana na dakika 20 jioni. Anafanya mazoezi akiwa na mlinzi wake pamoja na mimi hapa,"alisema Kilango.

Habari za kuumwa kwa mwanasiasa huyo ambaye ameshika nyadhifa mbalimbali serikalini na CCM zilitangazwa juzi na Makinda wakati akiahirisha Kikao cha Bunge.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Malecela azungumzia afya yake
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Wednesday, 22 June 2011 21:40
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]digg

Boniface Meena
MWANASIASA mkongwe na kada maarufu wa CCM, John Malecela, amezungumzia afya yake kutokea nchini Uingereza, akieleza kuwa inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo katika Hospitali ya Wellington North nchini humo.

Hata hivyo, taarifa za kitaalamu zilizolifikia gazeti hili zinaonyesha kuwa Malecela alipata tatizo la kuvimba kwa mishipa inayotoa damu moyoni kwenda mwilini na kusababisha mtiririko wa damu kuyumba kwa kiasi.

Taarifa zilisema kutokana na hali hiyo, njia pekee ya kuondoa tatizo hilo ilikuwa kumfanyia upasuaji mkubwa wa moyo ambapo madaktari walilazimika pia kuchukua mishipa kutoka katika mguu wake na kuweka kwenye moyo wake.

Lakini jana, Malecela mwenyewe aliyezungumza na Mwananchi kutoka Uingereza alikolazwa baada ya kufanyiwa upasuaji huo, alisema kuwa madaktari wamemshauri afanye mazoezi kwa muda wa wiki tatu hadi sita ili waangalie hali yake na baada ya hapo wataweza kumpa ruhusu ya kurudi nchini.

"Ninaendelea vizuri na madaktari wameniambia nifanye mazoezi kwa muda wa wiki tatu hadi sita kuiangalia hali ikoje ili waweze kunipa certificate (cheti) ya kuweza kurudi nyumbani,"alisema Malecela.

Mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, amezungumzia hali ya mwenendo wa afya yake baada ya juzi Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuwatangazia wabunge taarifa za kutokuwapo bungeni kwa Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela kutokana na mumewe kuwa mgonjwa na kufanyiwa upasuaji wa moyo.

Mama Kilango naye azungumzia
afya ya mumewe

Akizungumzia hali ya mumewe, Kilango alisema kuwa walikwenda nchini Uingereza Mei 11 mwaka huu wa ajili ya kumfanyia Malecela uchunguzi wa kawaida wa afya kama ilivyo kwa viongozi wa Serikali na alikuwa hana tatizo lolote.

Alisema kuwa yeye na mumewe wana kawaida ya kufanya mazoezi kila siku na kwamba walipokuwa katika mazoezi ya kawaida nchini Uingereza ambapo Malecela alianza kulalamika kuwa anapumua kwa shida, ndipo walikwenda hospitali ambapo alipimwa na daktari kumweleza kuwa ana matatizo ya moyo.

"Madaktari walimpima wakaona kuna mishipa inayotoa damu moyoni kwenda mwilini ambayo ilikuwa imevimba kutokana na Calcium kujikita kwenye mishipa na kuzuia mtiririko wa damu," alisema Kilango.

Kilango alisema upasuaji huo ulifanyika Mei 31 mwaka huu katika Hospitali ya Wellington North na daktari aitwaye Rakesh Uppal.

"Upasuaji umefanikiwa na yuko nyumbani sasa. Anatakiwa afanye mazoezi mara tatu kwa siku, dakika 20 asubuhi, dakika 20 mchana na dakika 20 jioni. Anafanya mazoezi akiwa na mlinzi wake pamoja na mimi hapa,"alisema Kilango.

Habari za kuumwa kwa mwanasiasa huyo ambaye ameshika nyadhifa mbalimbali serikalini na CCM zilitangazwa juzi na Makinda wakati akiahirisha Kikao cha Bunge.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Habari njema.
 
get well mzee wetu,hawa wanaokosa maadili humu kwa kuchulia watu wale ban wote,inakera sana hasa kwa heshima ya jamvi hili.poleni familia yake pia.
 
"Ninaendelea vizuri na madaktari wameniambia nifanye mazoezi kwa muda wa wiki tatu hadi sita kuiangalia hali ikoje ili waweze kunipa certificate (cheti) ya kuweza kurudi nyumbani,"alisema Malecela
Mungu wangu...... huyu mtu atatia umaskini watz
 
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Benard Membe amesema hali ya mwana siasa mkongwe nchini,John malecela inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo nchini uingereza.
 
umri aliofikisha unamtosha sana hata akifa hakuna hasara kwa taifa coz ni mzigo toka zamani

HIVI UNA DINI? NAAMINI MBWA ANAWEZA KUWA NA BUSARA ZAIDI KULIKO KICHWA CHAKO.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Benard Membe amesema hali ya mwana siasa mkongwe nchini,John malecela inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo nchini uingereza.

Dua zetu zipo pamoja naye mungu amuamuafu na kumpa nguvu njema. Amen

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Back
Top Bottom