Pole sana Mzee Mungu akuponye .Ukisha pona uje kuwasumbua watanzania kuwaongezea umasikini kwa jina la CCM . Sitasahau maneno ya huyu mzee kwa kweli . Mungu ampe afya njema in Jesus name.
Mnamuombea we na nani? Jiongelee mwenyewe.Mzee JSM.........tunakuombea ili upone haraka........Familia ya Mzee
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Malecela azungumzia afya yake
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Wednesday, 22 June 2011 21:40
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]digg
Boniface Meena
MWANASIASA mkongwe na kada maarufu wa CCM, John Malecela, amezungumzia afya yake kutokea nchini Uingereza, akieleza kuwa inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo katika Hospitali ya Wellington North nchini humo.
Hata hivyo, taarifa za kitaalamu zilizolifikia gazeti hili zinaonyesha kuwa Malecela alipata tatizo la kuvimba kwa mishipa inayotoa damu moyoni kwenda mwilini na kusababisha mtiririko wa damu kuyumba kwa kiasi.
Taarifa zilisema kutokana na hali hiyo, njia pekee ya kuondoa tatizo hilo ilikuwa kumfanyia upasuaji mkubwa wa moyo ambapo madaktari walilazimika pia kuchukua mishipa kutoka katika mguu wake na kuweka kwenye moyo wake.
Lakini jana, Malecela mwenyewe aliyezungumza na Mwananchi kutoka Uingereza alikolazwa baada ya kufanyiwa upasuaji huo, alisema kuwa madaktari wamemshauri afanye mazoezi kwa muda wa wiki tatu hadi sita ili waangalie hali yake na baada ya hapo wataweza kumpa ruhusu ya kurudi nchini.
"Ninaendelea vizuri na madaktari wameniambia nifanye mazoezi kwa muda wa wiki tatu hadi sita kuiangalia hali ikoje ili waweze kunipa certificate (cheti) ya kuweza kurudi nyumbani,"alisema Malecela.
.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
du kumbe hata humu JF kuna vichaa,kweli mtu mwenye akili timamu unaweza kumuombea binaadamu mwenzako kifo?huyu mzee kakufanya nini mpaka umuombee kifo au wewe umekuwa jiwe ,kumbuka ndugu wote tu wapita njia na marehemu watarajiwa,tunapishana tu kupata mauti,kila mtu ikifika zamu yake ataaicha dunia,kwa utamaduni wa kitanzania hatujafikia katika hayo unayofikiria,wasiwasi wangu wewe huenda umezaliwa miaka ya 2000 ndio maana huujui mchango wa Mzee Malecela katika nchi hii,na kama hujui Mzee Malecela ni moja ya watu wanaokufanya uandike na utoe maneno yasio na busara hapa JF,kwani ndio viongozi wa mwanzo wasaidizi wa Mwl J.K Nyerere ambao wameifanya Tanzania iwe nchi yenye misingi imara ya umoja,upendo n.k. namalizia kwa kusema kwa mila na desturi za kiafrika tunatakiwa tuwaheshimu walio tuzidi umri,na mwisho wewe ambaye ni kijana je una faida gani kwenye taifa hili,tujaribu kuwa waungwana na tuone aibu kwa maneno ya sio na busaraumri aliofikisha unamtosha sana hata akifa hakuna hasara kwa taifa coz ni mzigo toka zamani
Hii ni opinion yako wewe kuhusu Malecela. Legacy ya Malecela ni "go to hell" statement aliyowaambia wananchi akiwa kiongozi. Sio kila mtu anadhani Malecela ana mchango mkubwa kwa nchi hii.... ndio maana huujui mchango wa Mzee Malecela katika nchi hii,na kama hujui Mzee Malecela ni moja ya watu wanaokufanya uandike na utoe maneno yasio na busara hapa JF,kwani ndio viongozi wa mwanzo wasaidizi wa Mwl J.K Nyerere ambao wameifanya Tanzania iwe nchi yenye misingi imara ya umoja,upendo n.k.
Mnamuombea we na nani? Jiongelee mwenyewe.
Tuwe na huruma mbele!Ugua pole mzee Male tingatinga linakukokotoa magugu,
Mwananyamala wanafanya operation ya moyo? Clear your mind.
Dunia ya sasa ni vigumu sana kumchagulia mtu sehemu anayohitaji kupata huduma. Huu ni ulimwengu wa kibepari, mteja anafuata panapomfaa. Pamoja na hayo Mh. Malecela ni mmoja wa mawaziri wakuu wastaafu, nadhani ana stahili anazopokea ambazo zinamwezesha kutibiwa njeAmetaja Mwananyamala au Muhimbili...Mwananyamala hawafanyi operation ya moyo, Muhimbili wanafanya zaidi ya mwaka sasa na matokeo ni mazuri tu, kwa nini hakwenda hapo?
"Mteja" anatumia hela yake, huyu Malecele anatumia hela yetu, ingekuwa ya kwake yasingetuhusu.Dunia ya sasa ni vigumu sana kumchagulia mtu sehemu anayohitaji kupata huduma. Huu ni ulimwengu wa kibepari, mteja anafuata panapomfaa.