puza46b

Member
Nov 3, 2010
91
261
ZITTO ANAJUA NINI ANAFANYA.

Mbowe alipompeleka Lowasa CHADEMA (inasadikika kidikteta) alisema wamebadilisha gia angani. Mbowe alikuwa anaamini Lowasa atashinda uchaguzi, alitegemea kuwa ile mitandao ya Lowasa italinda kura na CHADEMA kitashika madaraka. Baada ya matokeo ya uchaguzi (inasadikika yalichakachuliwa)CCM wakaweka nia ya kuua upinzani (Chadema) kabla ya 2020. Lowasa akatishiwa kupotezewa hela na mwanafamilia wa karibu akafunguliwa kesi. Lowasa akakubali yaishe akarudi CCM, the rest is history.

Sasa swali la kujiuliza ni kwanini Zitto na ACT warudie yaleyale CHADEMA waliyafanya? Jibu rahisi ni kuwa Zitto anajua nini anafanya kama ilivyochambuliwa hapo chini:

  • Anajua kuwa Magufuli anashinda urahisi 2020 kwa sababu:
  • Hakuna tume huru
  • Wametayarishwa wakuu wa wilaya na watendaji wengine kuhakikisha hilo linatimia
  • Vitisho vya polisi vimeshaanza
  • na kadhalika, na kadhalika
Sasa kama anajua hawatashinda urahisi kwanini wanamtanguliza Membe na kwa nini alimkaribisha Maalimu ACT?

  • Zitto plan yake ni kuwa chama kikuu cha upinzani kabla ya 2025. Hili halihitaji ufafanuzi.
  • Anataka kuweka mazingira ya yeye kuwa mgombea wa uraisi kwa niaba ya upinzani 2025. Anajua kuweka jina lake kugombea urahisi sasa hivi alafu ashindwe ni kujichafulia jina. Hayuko tayari kushindwa alafu agombee tena miaka na miaka kwani hiyo haiendani na imani yake ya ukishindwa waachie wengine (rejea ugonvi wake ndani ya chadema). Akigombea tena baada ya kushindwa ataitwa mnafiki.
  • Membe anaweza kumsaidia kupata wabunge maeneo ya kusini. Ikumbukwe CUF ndiyo alikuwa mpinzani mkuu maaneo haya. Kumpata Membe kutapunguza zaidi wafuasi wa CCM maeneo hayo.
  • Ataongeza kipato cha ruzuku kwa kuwa na wabunge wengi bungeni. Pemba na maeneo yote ambapo CUF inanguvu yatageuka kuwa ACT. Hela itamruhusu kufanya shughuli nyingi za chama.
  • Kumweka Membe kunaua jinamizi la hoja ya udini iliyotumika kuikandamiza CUF. CCM walitumia ukanda kuipinga Chadema na udini kuipinga CUF. Kumkaribisha Membe kumeua ndege wawili kwa jiwe moja na hizo hoja zote mbili za CCM zimepotea.
  • Vindication.. pamoja na yote Zitto anayosema hadharani moyoni bado anamachungu na kuondolewa kwake CHADEMA. CHAEMA inakufa kifo cha kuchanwa chanwa na wembe mara 1000. Mwaka 2025 chadema hawatakuwa na mtu yeyote mwenye wasifu wa kugombea uraisi, labda Lisu agombee tena au wamweke Halima Mdee. CHADEMA kupona kisiasa wanahitaji miujiza kwa sasa. Baada ya chadema kusukumwa kwenye kona hawatakuwa na jinsi bali kumpa ushirikiano Zitto atakapotangaza nia 2025 kwani chama chake kitakuwa na nguvu zaidi. Na Zitto alishasema "Zaburi 118:22 jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la msingi", Wote tunashuhudia taratibu anavyotimiza huo usemi.
  • Magufuli hajali nani atakuwa raisi 2025 ila anaogopa kushitakiwa. Hii itaonekana zaidi kwenye matukio yatakayofuata baada ya uchaguzi. Magufuli keshabadili sheria ili imlinde, ila kama tulivyoona Malawi na Zambia, hilo pekee halitoshi. Unahitaji raisi anayekufuata akulinde Nkurunzinza alimweka mtu wake mungu akampenda, Kabila kaweka mtu wake na mpaka sasa wananchi wa congo wanapiga kelele. Magufuli katika kujaribu kujilinda anaweza weka mtu ambaye CCM na Taifa haitakuwa tayari kumpokea na hivyo kumpa Zitto nafasi 2025.
  • Hukumu ya Mahakama ya Africa iliyotolewa siku chache zilizopita inampa nafasi 2025. Hii haikuwa kwenye mahesabu ya Zitto lakini ni kama zawadi ya mungu na ataipokea kwa mikono miwili. Uchaguzi wa 2025 utakuwa ni uchaguzi wa kwanza Tanzania ambapo mshindi wa uraisi anaweza shitakiwa mahakamani. Hili ni pigo kubwa kwa CCM kwa sababu itafuta uhalali wakujipa kuongoza inchi. Kwa Zitto na ACT hii ni nafasi kuitoa jasho CCM. Kwa mgombea yeyote wa uraisi 2025 anajua kuwa ana nafasi ya kudai haki mahakamani.
  • Anapiga mahesabu ya magufuli na CCM kuendelea kuwasomesha namba watanzania. hasira ya wa watanzania 2025 haitapimika kama hali ya hela haitabadilika mifukoni mwa watanzania.
  • Haitaji kura za ukanda wa kaskazini mashariki kushinda uraisi. Ikumbukwe Zitto alikuwa wa kwanza kulalamika ukaskazini ndani ya Chadema. Mpaka sasa chadema mizizi yake mikuu bado ipo kaskazini mashariki. Zitto kashachukua Zanzibar na kusini mashariki. Hesabu zake kwa sasa ni jinsi ya kuipata mikoa ya kati na magharibi kaskazini. Hili atalifanyia kazi miaka mitatu ijayo. Ila kazi anayo kushindana na hoja za flyover, ringroad, SGR, vivuko nakadhalika nakadhalika.
  • Anajua kinyongo kinatoa mtu mwaminifu kwa adui. Ingawaje wengi wanakejeli Membe kuhamia ACT na kusema ni sawa na Lowasa, hasira ya Membe si kufukuzwa chama bali ni kunyimwa nafasi aliyoamini ni ya kwake kugombea uraisi 2015. Ikumbukwe, mkapa na kikwete wote walishikilia mambo ya nje, kichwani kwa Membe kupewa majukumu ya kidiplomasia ni kutayarishwa kuwa raisi. Hivyo basi hakukuwa na mwingine zaidi yake ndani ya CCM aliyekuwa na haki ya kuwa raisi. Uelewa wa Zitto kuwa hicho kinyongo kinampa amani kuwa Membe ni pons mzuri kwenye bigger chess game.
  • Anajua hamuitaji tena Membe baada ya Miezi 6. Membe akishindwa hana haki ya kugombea tena, Membe akishampa wabunge wa kusini hamuitaji tena. Ila thamani ya Membe si hapo tu bali pia ni mahusiano aliyojenga na mataifa ya nje wakati wa kazi zake. Mataifa makubwa ndo watatumika kuweka pressure pale inapohitajika kuilazimisha CCM ibadili muendeleo wa kisiasa Tanzania. Zitto anachohitaji kwa Membe ni kutambulishwa tu kwa walioishika dunia na mengine yatafuatilia.
  • Anajua watanzania kwa sasa wamekata tamaa ya kuiondoa CCM. Hii itathibitishwa na idadi ya watu watakaojitokeza kupiga kura. Dalili zote zilianza kuonekana wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, watu walikata tamaa. Hakuna sababu ya yeye kuweka jina lake kugombea uraisi wakati anajua watanzania wamekata tamaa.
  • Haitaji kuichafua CCM wapo wengi watakayoyaweka mabaya yake hadharani. Hapa naongelea jinsi gani Lisu atamsafishia njia Zitto. CCM wawe waangalifu sana na jinsi watakavyo deal na Lisu. Dunia nzima inaangalia na Lisu anaweza kuwa Ken Saro-Wiwa wa Tanzania, kitakachomtokea yeye ikawa ndo fimbo iliyovunja mgongo wa ngamia. Hii ni ya kuongelea siku nyingine.
  • Haitaji kusubiri miaka kumi kugombea uraisi. Membe hatashinda uraisi, period. Angeshinda inamaana zitto angehitaji kusubiri miaka 10. Miaka kumi ni mingi sana kwenye siasa anaweza tokea mtu mwingine machachari akaidumaza nyota ya Zitto. Zitto mwenyewe hayuko tayari kusubiri mda mrefu hivyo.
Membe alisema mengi yatatokea kabla ya uchaguzi. Hili la hukumu ya african court imerusha karata nyingine ambayo hatujui hatma yake itakuwaje. Labda wanasheria tufafanulieni hii hukumu inaweza kutumika kubatili matokeo 2020?

Ushari wangu kwa Zitto, wape Chadema an offer they cant resist before this election. Itakuwa vigumu wao kukuunga mkono baada ya 2020 ukisubiri wadhalilishwe kwanza kwenye uchaguzi. Ningekuwa niko kwenye nafasi yako ningewapa hii offer Chadema kabla ya uchaguzi: Tundu Lisu awe mgombea mweza wa Membe na baada ya uchaguzi 60% ya wabunge wa kuteuliwa watachaguliwa kutoka Chadema. Viongozi wengi wa Chadema na wanaharakati wa kweli wako katika hatari ya kupotea kisiasa. Hawa watakuwa wanajeshi wazuri kwa ACT pale upinzani wa kweli utakapoitikisa CCM 2025. This is a win-win situation, viongozi wazuri wa chadema wataendelea kuwepo bungeni na ACT itaheshimika kaskazini mashariki na ukanda wa kati.

Mwisho nasema msiwakejeli ACT na Zitto wanajua nini wanafanya. Wana chadema jitayarisheni kisaokolojia kumeza matapishi yenu (Zitto) na kuwa chama kikuu cha pili cha upinzani Tanzania. Ila mjue kuwa hakuna adui kwa wanaotaka mabadiliko ya kweli. Kupanda kwa Zitto inaweza kuwa baraka kubwa sana kwa Chadema kama vichwa vilivyotulia vikifanya kazi.
akhsanteni
Puza

Update!
Leo nimejifunza kipya. Katiba ya Tanzania hairuhusu Membe na Lisu kuwa tiketi moja ya uraisi. Ila hoja inabaki kuwa Zitto na ACT watoe offer ambayo chadema hawawezi ikataa. In the long run ACT watafaidika. Samahani kwa niliowakwaza.

Pia tunaweza ongeza kuwa Zitto anajua kumuachia mwingine agombee uraisi kunafuta hoja ya kuwa yeye ana uchu wa madaraka. Hii itamsaidia 2025.
 
Great analysis, ingawa nahisi hukupatia Sana kwa hatma ya CDM.

Natamani ungefafanua pale uliposema "...Lissu anaweza kuwa Ken Sarowiwa wa Tanzania.."

As long as membe atasimama kura zinaenda kugawiwa , chadema hawwezi kubali tena umoja na mtu kutoka ccm.

Pili nauwakika na sote tumeona siasa za Zitto ni za kubebwa na policcm. Na tutegemee hilo kwa wagombea wote wa act.
 
Membe hawezi kuchukuwa kura za Waislamu waliokuwa cuf kwa sababu Membe siyo Muislamu, kama hio ndiyo nia ya Zito kabwe ni bora hata angemlamba miguu Lipumba amsaidie ili kupata kura za Waislamu lkn siyo Membe, ni rahisi kihivyo tu, ...
 
puza46b nimefatilia walaka wako nukta kwa nukta, kipengele kwa kipengele na point kwa point. Umechoandika unakifahamu. Nimependa uchambuzi wako. Kasumba ya wa tz wengi wavivu wakusoma afu tunapenda kuchangia, sasa mtu hujasoma had mwisho ukaelewa afu unataka u koment !.

By the way naunga mkono hoja ila napata wasiwasi kwa jambo moja ,
"upinzani wa tz sio halisia (apa namaanisha chazo cha wapinzani wa bongo si msukumo wa ndani wa mioyo yao bali ni baada ya kukosa MASLAHI au kuharibiwa malengo yake katika nafasi yake, kitu kinacbompa hasira na kujikuta akihamia upinzani ili kulipa kisasi) hivyo mtu wa hivi punde MASLAHI yake yanapokaa sawa ni rahisi sana kutelekleza jukumu. Binafsi bado naiona sana Ccm katika dollah mana hakuna upinzani asilia bali ni upinzani wa kisasi na hamasa tu
 
Uchambuzi mzuri. CHADEMA ilikuwa katika nafasi ya Zitto 2015, walipata wabunge wengi, na pesa nyingi ya ruzuku. Badala ya kuzitumia kama mtaji wa kujenga chama na kujiimarisha, viongozi waliamua kufanya yao. Baada ya uchaguzi, Zitto atatakiwa kuchagua moja - ama kufanya yake kama CHADEMA walivyochagua au kujenga chama. Akiamua kutumbua pesa za ruzuku, basi 2025 ACT itakuwa kama CHADEMA leo hii.
 
Zitto hajui lolote

zaidi ya hapo analijua jina lake tu

laiti angejua lolote angeweka nia ya dhati kuunganisha upinzani dhidi ya fisiem

Zitto hana tofauti na hayati Mtikila...just a loose connan

No Vision No Mission.
 
Umeandika makala ndefu iliyojaa uongo kwanza Mbowe alijua Lowassa hawezi kushinda yeye alipiga hesabu za ruzuku pili Lowassa nguvu yake ilikuwa ccm alipotoka alipoteza robo tatu ya nguvu zake hakuna habari ya kuibiwa kura bali ni hadithi za kujifariji kama angeibiwa chadema wasingepata idadi ya wabunge waliopata
 
Lisu mgombea mwenza tena? Hii inatosha ku disregard uchambuzi wote

Bora umeiona hiyo, hapo ndio nimejua mleta hoja kaja na hoja ile ile ya kuidogosha cdm, kisha kuikuza ACT kwa faida ya ccm. Kuna nyuzi nyingi zinakuja hapa jukwaani kutaka kuipoteza maboya cdm, na kuikuza ACT lakini kwa lengo la kuibeba ccm. Ukweli ni kuwa chini ya tume hii hakuna uchaguzi bali uhuni kama uhuni mwingine. Wapinzani kutokupigania tume huru ya uchaguzi ni kutaka kuwatakatishia ccm ushindi haramu.
 
Back
Top Bottom