Pac the Don

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
1,576
2,000
Upinzani hawana watu wenye USHAWISHI wa kukubalika na nchi nzima.....

Ndio maana wanakiangalia CHUO KIKUU CHA SIASA TANZANIA....CCM.....

CCM ndiko wanakopikwa makada nguli ,wabobezi wanaoendana na SIASA ZA TAIFA HILI......

Siasa za CCM ni umbile safi linaloendana na TANGANYIKA NA ZANZIBAR iliyoleta TANZANIA.....nje ya hapo ni HISIA TU.....HISIA TU....nje ya hapo hakuna UHALISIA......


#SiempreCCM
#CCMNiImaniHaswa
Sasa inakuaje wanawachukua wapinzan kwa gharama na kuwapa nafasi za uongoz mpaka uwazir, ukuu wa mkoa na wilaya?
 

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
11,307
2,000
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Pamoja na yote lakini Edward Lowassa alijitahidi kuipambania CHADEMA kwenye uchguzi mkuu wa 2015 ingawaje alishindwa kuipigania baada ya uchaguzi kupita. Lakini hali kwa Lowassa ikiwa hivyo, Membe ndio sikumuelewa kabisa. Kwanza ile anaingia tu ACT na kupewa fursa ya kuipeperusha bendera, muda mfupi anaingia kwenye malumbano na Maalim Seif. Hivi nyie wenzangu mnafahamu Membe alifanya kampeni kwenye mikoa ipi hapa Tanzania?
View attachment 1964845
Unawashauri wajifunze lipi? Na wakajifunze wapi maana hawaruhusiwi kufanya siasa.
 

Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
15,365
2,000
Tuache ushabiki!! Hivi tunaweza kulinganisha utokaji wa Dr. Slaa na Lowassa kwenda CCM? Isitoshe, nimesema mwaka 2015 CHADEMA kulikuwa na mtu imara! Kukataa ukweli ni kutaka kuleta ushabiki usio na maana. Tusijisahaulishe uchaguzi mkuu wa 2010 Dr. Slaa ndie alipeperusha bendera ya CHADEMA, na alipata zaidi ya kura 2M. Baada ya uchaguzi wa mwaka 2010, Dr. Slaa hakukata tamaa. Aakaendelea kukipigania chama, na kuzunguka huku na huko hadi dakika ya mwisho tulipomuona HAFAI na akaletewa Lowassa! Kwa kinyongo, Dr. Slaa akamwaga manyanga na kujiendea zake ughaibuni. Lakini hata huyo Lowassa, nae alijitahidi kuipambania CHADEMA pamoja na kuwa na matatizo ya kiafya, lakini kwavile shida yake ilikuwa urais tu, ndo maana alipoukosa, akarejea CCM.

Uhuni zaidi umefanywa na Membe.
Nakubaliana nawe kidogo kwenye uhuni wa Membe. Lakini kwenye swala la wasiasa kuhama toka chama A na kwenda cha B sikubaliani nawe. Hapa masilahi binafsi huchukuwa nafasi kuliko itikadi.

Ni wakosoaji wengi wa upinzani. Naona wanataka kuiona Cdm ikiwa na roho ya malaika na kuibariki ushetani wa Ccm . Wakihama toka upinzani na kuzawadiwa vyeo hatuoni ajabu. Lakini wakihama toka Ccm na kwenda upinzani tunahoji credibility !!
 

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,546
2,000
Siasa kokote iliko....ina watu wake.

Usisahau SIASA ni ushawishi bwana "Ahmednejad"

Ndio maana hata huko kwenu "Iran" inaongozwa na KIKUNDI CHA WATU.

Sijapatapo kuona jambo linasimamiwa na kuendeshwa na MTU/WATU wasio na ushawishi kwa wengine....hili huanzia ngazi ya mtu binafsi,familia ,kikundi mpaka TAIFA.

Siwalaumu wanasiasa....hasa CCM ya Tanzania ....kwani kwa kuwa inanipa AMANI NA UTULIVU wa kutafuta RIZIKI yangu halali basi haina makosa makubwa....mengine ni ya kibinadamu tu

Kujitahidi kufuatilia SIASA ZA DUNIA sijapata kusikia nchi isiyowalaumu WANASIASA NA SIASA ZAO ZINAZOWATAWALA ...hiyo nchi haiko.....unaweza kunitajia?
Ijapo SIASA NI UONGO WENYE MANUFAA... kuna waliopitiliza hata wanafanya raia wachukiane kutokana na ulafi wa madaraka... Tuliokota maiti, watu walifilisiwa... Haikutosha tukapata vibepari uchwara vilivyotumia ofisi na mamlaka kudhulumu huku vikipewa baraka zote za chama kizee!! Kisa mkubwa hasemwi... Wasio wenyewe walipojaribu kusema wapewa hongo wakapewa kitumbua cha watoto!!
Je nikisema ni sawa yanafanyika kote lakini haya ya kubambika watu kesi ngumu zisizo na ushahidi ili wateseke KISA KATIBA MPYA, KISA UPINZANI UTAINUKA...
Pamoja tunajenga taifa!!!
 

stakehigh

JF-Expert Member
Aug 9, 2019
5,441
2,000
Ni ujinga kusema eti chama changu kinapendwa wakati kinatumia vyombo vya dola kubaki madarakani

Kusema kweli CHADEMA inaogopwa ña CCM,, CHADEMA ni chama chenye nguvu na ushawishi sana

yawezekana kuna chama kinapendwa sana mpaka kinachukua mgombea upande wa kijani
 

Benny Haraba

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
7,244
2,000
Tuache ushabiki!! Hivi tunaweza kulinganisha utokaji wa Dr. Slaa na Lowassa kwenda CCM? Isitoshe, nimesema mwaka 2015 CHADEMA kulikuwa na mtu imara! Kukataa ukweli ni kutaka kuleta ushabiki usio na maana. Tusijisahaulishe uchaguzi mkuu wa 2010 Dr. Slaa ndie alipeperusha bendera ya CHADEMA, na alipata zaidi ya kura 2M.

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2010, Dr. Slaa hakukata tamaa. Aakaendelea kukipigania chama, na kuzunguka huku na huko hadi dakika ya mwisho tulipomuona HAFAI na akaletewa Lowassa! Kwa kinyongo, Dr. Slaa akamwaga manyanga na kujiendea zake ughaibuni. Lakini hata huyo Lowassa, nae alijitahidi kuipambania CHADEMA pamoja na kuwa na matatizo ya kiafya, lakini kwavile shida yake ilikuwa urais tu, ndo maana alipoukosa, akarejea CCM.

Uhuni zaidi umefanywa na Membe.
Comments reserved
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,997
2,000
Acha kuandika upumbavu wewe!!!


CCM ni zaidi ya chama cha siasa.

CCM ni IMANI na UMBILE la nchi hii.

Kalaghabaho
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,997
2,000
Kwanini mnapenda kuonyesha ujuha wenu hadharani?


CCM ni zaidi ya chama cha siasa.

CCM ni IMANI na UMBILE la nchi hii.

Kalaghabaho
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
10,818
2,000
Kwanini mnapenda kuonyesha ujuha wenu hadharani?

.....hoja yako ya Dr.Bashiru kusema kuwa kuna "majizi" bado hakukifanyi kuwa CHAMA CHOTE kiwe cha hovyo.....

Yaani kwa kuwa kuna PADRI kamnajisi mtoto seminarini basi KWAKO WEWE ukatoliki wote ni mbaya na haufai.....

Yaani kwa kuwa kuna USTADHI kamnajisi mtoto amfundishaye madrasa basi KWAKO WEWE Uislam wote ni mbaya na haufai........

Duuuh kweli kazi 😳😳🤣🤣
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
15,354
2,000
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Pamoja na yote lakini Edward Lowassa alijitahidi kuipambania CHADEMA kwenye uchguzi mkuu wa 2015 ingawaje alishindwa kuipigania baada ya uchaguzi kupita. Lakini hali kwa Lowassa ikiwa hivyo, Membe ndio sikumuelewa kabisa.

Kwanza ile anaingia tu ACT na kupewa fursa ya kuipeperusha bendera, muda mfupi anaingia kwenye malumbano na Maalim Seif. Hivi nyie wenzangu mnafahamu Membe alifanya kampeni kwenye mikoa ipi hapa Tanzania?

View attachment 1964845

Ukweli mchungu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom