Itakuwaje Lowassa akifukuzwa CCM, CHADEMA watampokea?

Kwa wale mlikuwa hajui, huyu ndie mgombea wa Chadema 2015 na ndie rais 2015 Chadema itakapochukua nchi na pia litimie lile neno rais wa 2015 lazima atoke Kaskazini haswa kwa kuzingatia, ukimuondoa ZZK, Chadema haina any other candidates wanaoweza kuwapatia ushindi kwenye urais!.
Tena hata mimi nitaingia rasmi kwenye siasa kwa kujiunga rasmi Chadema na kuna jimbo nitalichukua kama nimeliokota!, mgombea wa CCM nitampiga chini kama kumsukuma mlevi!.
Pasco

Pasco Umetisha una_focus ya miaka miwili mbele,ur a great thinker.

Weka kumbukumbu ya kauli yangu tutakumbushana 2015!.
Pasco
 
CHADEMA kwa sasa hawapokei "viongozi" toka CCM, hivyo Lowassa hawezi kujaribu kuomba kujiunga CHADEMa.

Ila wanachama wa kawaida wa CCM wanaoguswa na elimu ya uraia pamoja na kuzinduliwa toka usingizi wa ujinga, maradhi, ufisadi na kulindana (hivyo kukosa uzalendo na haki zao za msingi) hao wataendelea kupokelewa kila iitwapo leo.
Leo mpo nae na fomu mlimpatia bila kupingwa
 
Akifukuzwa hapokelewi,ila akitoka mwenyewe anapokelewa
 
Acha kupotosha umma, Lowasa sio waziri mkuu mstaafu, ni waziri aliyejihudhuru kwa matumizi mabaya ofisi ya umma, huyo ndiye mzee wa richmundi, kuhusu kwenda Chadema, unaota ndoto za alinacha, hiki ni chama cha watu makini.
Leo mpo nae humo
 
Nilishawahi kusikia kuwa jeuri ya EL ni kwamba anawatishia eti wakimtema, ataenda upinzani. Tusije tukawa mbulula tukampokea CCM wakapata credit. Huyu jamaa nadhani ndio katuletea matatizo ya umeme kwa maslahi yake binafsi. Umeme unapanda mara dufu tunahoji tukiwa bar afu tunatulia (tuingie barabara kidogo-tuonyeshe anger). Wenzetu Kenya walipandishiwa bei ya chakula, wakaingia barabarani na mabango, tumekuwa wabinafsi sana.
Lowassa leo anazunguka nchi nzima na gia yake kubwa ni ruswa kwa watanzania maskini na bodaboda. Na matatizo mengi tunayoyapata, kielimu(shule za kata), kiuchumu (ki-umeme) yalikuja akiwa PM, leo aje upinzani tumpokee. Tutakuwa waroho wa madaraka.
kaja hukohuko,
 
Kwa wale mlikuwa hajui, huyu ndie mgombea wa Chadema 2015 na ndie rais 2015 Chadema itakapochukua nchi na pia litimie lile neno rais wa 2015 lazima atoke Kaskazini haswa kwa kuzingatia, ukimuondoa ZZK, Chadema haina any other candidates wanaoweza kuwapatia ushindi kwenye urais!.
Tena hata mimi nitaingia rasmi kwenye siasa kwa kujiunga rasmi Chadema na kuna jimbo nitalichukua kama nimeliokota!, mgombea wa CCM nitampiga chini kama kumsukuma mlevi!.
Pasco
Duh!!! Kadi yako ya Chama ndani ya CHADEMA ni namba ngapi vile?.
 
Kwa wale mlikuwa hajui, huyu ndie mgombea wa Chadema 2015 na ndie rais 2015 Chadema itakapochukua nchi na pia litimie lile neno rais wa 2015 lazima atoke Kaskazini haswa kwa kuzingatia, ukimuondoa ZZK, Chadema haina any other candidates wanaoweza kuwapatia ushindi kwenye urais!.
Tena hata mimi nitaingia rasmi kwenye siasa kwa kujiunga rasmi Chadema na kuna jimbo nitalichukua kama nimeliokota!, mgombea wa CCM nitampiga chini kama kumsukuma mlevi!.
Pasco
ulijitahidi ila hayakutimia
 
Back
Top Bottom