Hapa hatubishani ndugu yangu PAPAA JIWE. Unatakiwa kutushawishi ni sifa zipi za zaidi alizonazo EL zaidi ya watanzania wanasiasa wengine kuonekana anastahili kuwa the next president au kuwa mtu au kiongozi wa kupigiwa mfano ktk nchi hii. Naomba unitajie sifa 10 muhimu za raisi wa tanzania ajae huku ukioanisha sifa alizonazo EL na ni kwa namna gani matatizo yanayolikumba taifa hili kwa sasa yanaweza kutatuliwa na mtu mwenye sifa kama EL. Kwa kifupi nchi hii kwa mtazamo wangu inakabiliwa na mambo yafuatayo;
1. Mpenda nchi yetu Tanzania zaidi ya chama na sehemu anakotoka.
2. Utawala wa sheria - Tuna sheria na taratibu nzuri lkn siku hizi sheria zinapindishwa kwa kuangalia uwezo wa mtu, itikadi za kisiasa na kujuana. Mifano iko mingi. Tanzania inahitaji raisi anayeweza kuondosha mapungufu haya.
3. Rushwa na ufisadi miongoni mwa viongozi na serikali na kisiasa. Tunataka kiongozi atakae kuja kupambana na rushwa na ufisadi kwa dhati bila woga wowote. Sio wale viongozi wanaosema ukiwagusa "mafisadi nchi itayumba".
4. Mtetezi wa haki za binadamu zinazovunjwa kila siku bila kujali upendeleo wowote
5. Mcha mungu na mtetezi wa wanawake na watoto hasa watoto wa kike.
6. Mkweli daima bila kujali itikadi ya chama chake.
7. Raisi hasiyependa matumizi ya pesa ya umma yasiyo na tija na ya anasa!
8. Mtetezi wa katiba bora na demokrasia ya kweli ya vyama vingi kwa ajili ya maslahi ya watanzania wa leo na miaka 50 au 100 ijayo.
9. Mfia nchi. Kiongozi aliyetayari kufia nchi yake kwa kupigania maslahi ya walio wengi kuliko ilivyo sasa.
10. Mlinzi wa raslimali za nchi kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.
Ndugu yangu PAPAA JIWE sasa tunaweza tafakari na kuchukua hatua. .....
Lowassa hapo amekosa sifa No.6 & 8 zingine zote anaziweza kwa vitendo yule Chief Legwainani. Kumtoa mtu yeyote nduki kwake sio tatizo na ndio maana genge la waganga njaa ndani ya nchi hii wanamuogopa hata akikaa kimya wanasema tulimuona akitaka kusema.
Wengine wote ni kama hawa mitume na manabii feki wa siku hizi wanaojitakasa kwa kuacha pombe tu huku wakifanya maaswi makubwa makubwa.
Rais mzalendo ni yule anayeweza kuwafanya watu wote kuwa wazalendo kwa kuijenga nchi yao wenyewe.
Huwezi kujenga uzalendo kwa kuuza ardhi kwa wageni toka ulaya na Asia ili walime mpunga badala ya kuwawezesha wazawa wenyewe ili walime kwenye vikundi vyao.
Uzalendo unajengwa kwa kuwapa wazawa nafasi ya upendeleo katika kutumia rasikimali zao.Hapo watu wataipenda nchi yao.
Lakini tukikimbilia ulaya kuwaleta wageni ili washindane kuja kujifunza kupiga risasi na kulenga shabaha kwenye wanyama wetu hatutaweza kujenga uzalendo.
Usidanganyike/usitudanganye ,kuhusu rushwa kwa sasa hakuna mtu mmoja atakayeweza kupambana na rushwa.Kwenye mfumo wa kibepari kila mtu ni mbinafsi ,kama sio mtu binafsi basi ni kikundi au hata taifa.Angalia mataifa ya magharibi ambayo yanahubiri kuhusu utawala bora lakini ndio wavunjaji wa kubwa wa haki za watu linapokuja suala la maslahi yao.
Mfano mdogo tu ni pale bungeni linapokuja suala la kuongeza posho hakuna mbunge anayetoka nje kwa maana ya kushinikiza posho zao zipunguzwe,badala yake wote wanaungana.
Leo hii hakuna msomi anayekaa kwenye kikao bila malipo kujadili namna bora ya kutekeleza majukumu yake mwenyewe.
Watu wanapigana vikumbo kusoma masters na phd sio kwa ajili ya kuwahudumia wananchi bali wapate fursa ya kuongeza mishahara na posho zao.Ndio maana wizi uko kila sehemu na wanaoupanga ni wasomi.
Je,hapa mtu moja atapambambana na nani?
Leo hii mpaka kwenye chaguzi za viongozi wa serikali za wanafunzi vyuoni rushwa imekithiri. Na hao ndio mara nyingi wanaotengeneza mitandandao ya kiuongozi baadae.
Leo hii tumeona Mwigulu Nchemba anavyohangaika kuhakikisha misamaha ya kodi inapunguzwa kama sio kufutwa kabisa lakini angalia jinsi watu wa vyama vyote wanavyojitokeza kupinga. Mwingine anatumwa na watu wa dhehebu lake au dini yake kutetea misamaha ya kodi.
Huo uzalendo utajengwa na nani?
Kwa sasa hakuna kiongozi mzakendo kama Mwigulu Nchemba. Anakerwa na watu wanaovuruga amani ,watu wanaokataza watu kuchangia maendeleo ,misaada inayotufanya tuwe ombaomba.Huyu ndiye mfuasi halisi wa Nyerere. Cha ajabu wanaojiita wapinzani pia hawamuungi mkono.
Uzalendo utajengwa na nini?