Kuchangia maendeleo sio ufisadi.
Mafisadi papa waliofilisi mabenki, vyama vya ushirika,miradi ya kuchapisha na kubadili fedha,ufisadi wa mabilioni ya fedha kule bandarini,wizi wa madawa na vifaa vya maabara,wizi wa fedha za pembejeo,uchashaji wa vitabu feki vya shule,kukwamisha miradi ya maendeleo kama reli n.k. Ununuzi wa rada na vifaa vya kijeshi vya chini ya kiwango,misamaha ya kodi,tanesco kufanya hujuma za wazi kwa utetezi wa richmond,tanesco kununua umeme kwa mawakala na kuwauzia wananchi kwa bei ya juu. Haya matatizo yote yana mafisadi wanaolinda hizi hujuma endelevu na hawagusu kwa sababu wengi wao sio wanasiasa ! Hatuwaoni wakichangia maendeleo popote zaidi ya kuongeza nyumba ndogo na kujenga majumba ya kifahari ! Waige mfano kwa nimrodi mkono ,ndesamburo . Wameshafisidi nchi sasa wajenge mashule watoto wetu wasome kwn hawawezi kurudisha walikoiba. Vinginevyo ccm ni kama mzoga wale wanaojifanya ni watakatifu ni kama mifupa isiyoweza kunyanyuka kwa sababu tu haijaoza kama nyama.