Hahaha kumbe watu wengi hawapendi kuingiliwa na wanadamu katika mazingira yao.
Nadhani moja ya watu wasiopenda watu nami nipo. Naweza kutunukiwa hata papuchi ila ghafla nikaacha kufuatilia na siendelei tena. Sipendi kupigiwa simu ambayo haina japo la maana, yaani mtu akipiga simu kwa lengo la kupiga story nitatafuta dharura nimwambie anipigie baada ya dakika 5 na hapo hata apige sipokei.
Sipendi kupewa kazi ya kufuatilia kitu na mtu, ukiniambia nenda sokoni ulizia bia bei gani ujue mawasiliano yangu na wewe hayapo. Kuna jamaa aliniagiza nimuulizie kifaa cha gari sehemu nikamwambia anitafute baada ya siku 2 nimpe jibu, tangu mwaka jana mwezi wa 11 hadi leo sipokei simu maana naona ana usumbufu mwingi sana.
Huwa nakaa sehemu zaidi ya mwaka ila ni watu chini ya 10 wanaoweza kujua walau jina langu tu, sipendi kuchangamana na watu nachukia mikusanyiko ambayo naweza kuwa mmojawapo.
Nyakati fulani nilikuwa nakaa na mzee wangu nilikuwa naongea naye maneno kama 5 hivi kwa siku. Salamu ya asubuhi, karibu lunch, karibu dinner na usiku mwema. Kesho pia hivyohivyo.
Na watu wenye tabia hizi huwa wana akili sana anaweza kuchunguza jambo gumu akapata jibu na kuendelea kujifanya hajui lolote, wengi wao ni wadadisi, wana hisia za kweli na hupenda zaidi kutumia hisia na akili zao.
Nimepata mpenzi Extrovert naona ni kama upinzani ndani ya nchi, mwenzangu anaweza kuongea masaa 40 mfululizo ila mimi huongea pale linapokuja suala la kuongea ama kujibu. Kazini naenda kwa ratiba sipendi kwenda kukaa kazini bila ratiba yaani nashindwa kabisa.
Mengine njoo PM nikwambie
Saint Anne