Introverts Vs Relationship

Feb 15, 2013
64
109
Habari zenu wadau? Poleni na mihangaiko na vita vya Corona.

Ninakuja mbele zenu kuomba kujua kuna changamoto gani ambazo watu wa ndani ( introverts) wanazipata wakitaka kuanza mahusiano na jinsi gani wanaweza kuzishinda ukizingatia personality yao inawafanye wawe waoga kiunteract na watu wengine.

Nawasilisha !

Sent using Samsung Galaxy A7 (2018)
 
Introverts kundi la phlegmatic ni wakimya mno na huwezi kujua kama wamekasirika au wamefurahi . Wanaweza kuwa wananyanyasika bila kusema . Kwa kifupi they are too dull .

Introverts kundi la melancholics siyo waongeaji lakini unaweza kuwatazama usoni ukajua kiwango chake cha furaha au hasira . Mara nyingi ni kundi la watu wanaolenga kwenye ukamilifu ( perfectionists ) , sasa changamoto ni kwamba hakuna mtu asiyekuosea ; nd'o maana wakikosea wao hawawezi kujisamehe na akikosea mwenzie hawezi kusamehe , kwa hiyo ni watu complicated ingawa ukiwaelewa huwa ni wakarimu mno na ni waaminifu na wenye vipaji vikubwa vya akili , utunzi na uvumbuzi .

Naomba kuwasilisha .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakitaka kuanza mahusiano inawawia vigumu sana kuchukua hatua ya kwanza hasa kwenye kutongoza ni midomo zege!,Ni watu wenye hofu kuichukua hatua yoyote ile bila kuona usahihi wa yeye kuichukua hatua husika! Ni logics people so kufikia maamuzi kitu kimepangwa kikapangika!.

Wanakuwa disappointed ama wao wenyewe au watu waliomzunguka kutokana na ugumu walionaokuichukua hatua hiyo wengine huwaona kama si binadamu aliekamilika so husemwa vibaya sometime na yakimfikia hujisikia hovyo na huenda akaacha jambo husika.

Tabia pia za mhusika huenda zikamkwaza asichukue hatua ya kuamua kuingia kwenye mahusiano!

Let's say yeye ni mpole ila anatokea kumpenda mtu mwenye gubu,kukurukakara aisee hawapendi hivi.. wao wanapenda utulivu na maelewano.

Kutokuwa karibu na watu huwaleteleza kuwa na aibu,kutokujiamini mbele ya watu hasa jinsia iliyotofauti nae so hayo yanaweza mpatia ugumu ktk kutongoza n.k

Mkuu moja ya usuruhishi wa tatizo ni kulitambua tatizo introvert husubiri mahusiano ila pindi yafikapo huruka mbali😅

Akiweza tambua kuwa ili kupata ushirikiano na watu na kujiongezea kujiamini ni lazima ashiriki na watu hili litamfanya awazoee watu,maana kwanza introvert wana akili nyepesi ya kutambua na pia inaweza mrahisishia kupata mwenza humohumo kutokana na mazoea n.k

Nadedaga Lolo😂😅
 
Back
Top Bottom