Ulimwengu wa introverts na suala zima la mahusiano

Cainan

JF-Expert Member
Jun 14, 2017
421
476
Habarini Wana Jamii forum.

Siku ya leo nimeona nijikite katika kutoa ya moyoni , kubwa zaidi ntaangazia kundi la watu ambao hujulikana kama introvert na mahusiano ambayo hujihusisha na namna zake.

Kwa kuanza kabisa mimi ni introvert wa kutupwa , linapofika swala la mahusiano kwa kweli sinaga vitu vingi vya kuongea na marafiki zangu wengi wamekuwa wakiniambia Mimi ni msiri sana hivyo kutoweza kuwaambia wenzangu mtu ambae nipo nae kwenye mahusiano

Hivyo katika muda mwingi nikikaa na kufikiria kuhusiana na suala zima la mahusiano Huwa nahisi kama sipo serious kabisa hii kutokana na kutoyapa kipaumbele sifahamu , lakini katika suala zima la kuchagua partner ambaye nahisi anaweza kunifaa katika mahusiano ni changamoto kubwa , sio kwamba Sina uwezo wa kuwatongoza hapana , ni kutokana na nilivo kuwa na uwezo wa kuswitch kwenye kuongea sana na utani mwingi ila mda mwingi nipo kimya hasa one to one engagement

Pia hata kama nikipata mtu ambae naweza Anza nae mahusiano basi hatutafika mbali kwa sababu Mimi Huwa natumia mda mwingi kufanya reasoning na logic napenda sana hivyo naweza detect kama Kuna kitu hakipo sawa hivo kushusha emotions kupelekea ku lower relationship stability

Hivyo kutokana na suala la introverts katika dunia yetu ni mtihan katika swala la socialization nikaona tupeana tips au changamoto ambazo tunakumbana nazo katika maisha ya Kila siku
CHANGAMOTO GANI KUBWA AMBAZO WATU WA AINA HII TUNA KUTANANAZO ? NI VIZURI KUZIJUA HILI KUEPUKANA NAZO

Karibuni wana introverts wenzangu na wengine pia mnaruhusiwa hatujawatenga ...nawasilisha

Kwa wale ambao wanapenda kujisomea vitabu ...Kuna mwandishi mmoja wa marekani anaitwa SUSAN CAIN yeye anafahamika zaidi kwa kuandika kitabu kuhusiana na INTROVERSION EXPERIENCE ambacho kimewafunua watu wengi sana katika dunia yetu ya leo ...
Hiki kitabu kinaitwa THE POWER OF INTROVERT IN A WORLD THAT CAN'T STOP TALKING
yeye anakuwa Moja kati ya waandishi wa mwanzo kabisa kuandika kuhusiana na field ya introverts au personality disorder
View attachment 1952959
View attachment 1952968View attachment 1952972
View attachment 1952998
 
Kuna mtu alinambia hivi "luckyline wewe ni burudani tosha hata kama mtu hana tv wewe ndani unatosha.😂😂😂

Nawaza familiya ambayo mwanaume ni introvert na mwanamke introvert wanaishi vipi? Utajuaje huyu leo hana mood?

Kuna shemeji yangu ni mkimya saaaaaana ila dada anatuambia eti anaongea. Kuna siku alicheka mpaka nikauliza shem na wewe unachekaga?😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom