JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,356
5,601
Kuna taarifa nimezipata kutoka kwa mtu wangu wa karibu anadai Watu 11 wamefariki Dunia ndani ya Kiwanda cha Mtibwa Sugar kilichopo Morogoro kutokana na hitilafu za kiufundi.

Wenye taarifa kamili tujuzeni

==== ===


Watu 11 wakiwemo raia watatu wa kigeni wamefariki dunia na wawili wamejeruhiwa kwa ajali iliyotokea katika kiwanda cha uzalishaji wa sukari cha Mtibwa baada ya kutokea kwa hitilafu ya mtambo wa mvuke wa kuzalisha umeme.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama amesema tukio hilo limetokea majira ya saa saba na nusu usiku wa kuamkia leo Mei 23,2024.

Kamanda Mkama amesema raia wa kigeni waliofariki ni kutoka nchini Kenya, India na Brazili

Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Mtibwa Sugar na majeruhi wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Misheni ya Bwagala.

Waliokufa ni wataalamu wa umeme na mitambo ambao walikuwa kwenye chumba cha kudhibiti mitambo hiyo.

Chanzo: AZAM TV
 
Kuna taarifa nimezipata kutoka kwa mtu wangu wa karibu anadai Watu 11 wamefariki Dunia ndani ya Kiwanda cha Mtibwa Sugar kilichopo Morogoro kutokana na hitilafu za kiufundi.

Wenye taarifa kamili tujuzeni
Mtu ww karibu? 😁
Ni official taarifa imetoka usiku.
 
Back
Top Bottom