11 Wafariki dunia baada ya mtambo wa kiwanda cha Mtibwa Sugar kulipuka

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
569
1,238
Watu 11 wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya mfumo wa joto wa kiwanda cha kuzalisha sukari cha Mtibwa Sugar kulipuka wakati wakijiandaa kuanza uzalishaji wa sukari kwenye kiwanda hicho kilichopo Turiani mkoani Morogoro.

Akizungumza na Mwananchi digital leo Alhamisi Mei 23, 2024 Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Shaban Marugujo amesema mlipuko huo ulitokea saa 7 usiku na umeua 11 na wengine wawili kujeruhiwa.

"Ni kweli watu 11 wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya mlipuko wa mpira wa joto wakati wanajiandaa na uzalishaji wa sukari pale kiwandani, ifahamike kwamba ili sukari ichakatwe kuna kiwango cha joto ambacho kinatakiwa kifikie sasa wakati maandalizi ya uzalishaji yakifanyika na kile kiwango cha joto kikingojewa ndipo ukatokea mlipuko huo na kuwakuta watu hao 11 ambao kwa kiwango kile cha joto wakafariki papo hapo,"

"Chanzo halisi cha mlipuko huo bado hatujakipata ila bado tunaendelea na uchunguzi, timu nzima iko hapa kiwandani tangu usiku huo na mpaka sasa tunaendelea na tukikamilisha tutatoa taarifa rasmi" amesema Marugujo.

CHANZO: MWANANCHI
 
Kwenye viwanda vya sukari, boilers zinawekwa ili kuzalisha umeme kwa kutumia mvuke unaotokana na kuunguza mabaki ya miwa na majani. Mvuke huo wenye pressure unazungusha turbine ambayo nayo huzungusha mitambo ya kuzalisha umeme.

Maintenance ya boilers na pipes zake ambazo zinabeba pressure kubwa sana ili kuweza kusukuma turbines, lazima uzingatie weledi, ujari muda na taratibu za kufanyia maintenance hizo.

Tunajua nini kuhusu maintenance schedules za mitambo hiyo? Mtibwa kulikuwa kuzuri sana enzi zake. Kiwanda kilisaidia jamii iliyokuwa imewazunguka kwa kuwapa fursa ya kulima na kuuza miwa kiwandani. Wale wakulima wa miwa walikuwa vibopa, wazee wa madizini. Hivi bado wanalima na kuwauzia kiwanda miwa yao?

Pengine Prof mwingine atatoa lecture ya kitaalamu kuhusu mengi yaliyopo kwenye jamii yetu kama Prof Mkandara, ili tujifunze na kuanza kurekebisha kasoro za hapa na pale.

Kuna elimu nyingine inapatikana kwa gharama kubwa sana. Tufikiri, tuamue na kusonga mbele, bila kuhukumiana na kubebeshana lawama
 
Mlipuko huo ungetokea Iran, tungekuwa tunasoma tu hapa taarifa za kichambuzi za uhusika wa taifa teule

Na hata mlipuko huu unaweza kuleta taarifa za ulofa wetu unaochukulia kila tatizo ni matakwa ya Mwenyezi Mungu, hata kama ni uzembe au ubabaishaji.

Niliwahi kuambiwa Kagera Sugar miaka ya sabini, boiler pia ililipuka na kusababisha mauti.
 
Back
Top Bottom