robinson crusoe
JF-Expert Member
- Oct 22, 2020
- 740
- 1,214
Tulianza na shopping mall Dodoma, sasa tena ni kiwanda cha Tumbaku. Yasemekama wahusika ni wale wale!
Ukiingia mjini Morogoro, umbali kidogo kutoka mzunguko wa Msamvu kuelekea Iringa, unakutana na daraja la reli na pembeni yake unakuta shughuli za ujenzi wa kiwanda kipya cha Tumbaku.
Eneo hili kwa miaka mingi lilieleweka ni eneo la wazi, na kwa sheria zetu za ardhi, hakuna aliye na madaraka ya kubadili matumizi ya eneo la wazi.
Naomba kufahamishwa nani mmiliki wa kiwanda hiki kipya ndani ya eneo hili? Huu ni mwenendo mpya wa uporaji wa maeneo ya wazi. Ilifanyika sana wakati wa serikali ya Mwinyi, sasa tena imerudi kwa serikali ya Samia.
Kama kawadia yetu taarifa rasmi huwa ni ngumu na za upotoshaji, lakini taarifa za mtaani zinaonesha ni waziri mmoja mchanga sana ktk uwaziri, tayari ana ubavu wa kujenga kiwanda ambacho sasa kimebatizwa kuitwa MKWAWA!
Mbele zaidi insemekana yupo na mkuu zaidi ndani ya mpango huo. Nchi haina tena uungwana. Kila mtu anaitafuna anavyoweza.