Inadaiwa Maganga wa CWT aandaliwa kashfa ya ngono, chongolo ‘style’ kutumika

DodomaTZ

Member
May 20, 2022
71
107
CP3J0452.JPG
Vita vya madaraka ndani ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) imezidi kushika kasi huku kiasi cha watu wanaodaiwa kuwa nyuma ya mkakati wa kuuondoa uongozi wa sasa madarakani, wakitumia mitandao ya kijamii kuwadhalilisha baadhi ya viongozi wa chama hicho.

Katika kile kinachoelezwa kuwa sababu ya vita hiyo ni nafasi ya Ukatibu Mkuu, miongoni mwa waathirika wakubwa wa udhalilishaji huo unaoandaliwa aliyelengwa moja kwa moja ni Katibu Mkuu wa sasa wa CWT, Mwalimu Japhet Maganga ambaye mikakati ya kumchafua imeanza kwa kutengenezewa kashfa za ngono ikiwa ni siku chache kabla ya maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 30 ya Chama hicho yanayotarajiwa kufanyika Jijini Mwanza, baadaye mwezi huu (Desemba 2023).

Mwalimu Maganga anatajwa kuwa mlengwa mkuu kutokana na msimamo wake wa hivi karibuni wa kulinda katiba ya CWT kwa kukataa kujiuzulu ukatibu Mkuu licha ya kuwepo mashinikizo ya makundi mbalimbali ya mahasimu wake wanaotumia ofisi za umma kutaka kumuondoa madarakani.

Jambo Tv Online lina taarifa za kina kuwa kabla ya Mwalimu Maganga kuukwaa ukatibu mkuu wa CWT watangulizi wake waliondolewa kwenye ofisi hizo kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za matumizi mabaya ya fedha za CWT huku ikielezwa kuwa hawajaridhika na namna walivyotoka katika nafasi za uongozi kiasi cha kupanga na kuratibu kile kinachoitwa migogoro ndani ya Chama

“Walioondolewa hawajaridhika kiasi cha kuanza kupanga na kuratibu hiki watu wanachodhani ni vurugu ndani ya CWT na kwa sasa watu hawa wanatumia udanganyifu kuwa vita hivyo ni maagizo kutoka juu kwa kuwa serikali haimtaki Mwalimu Maganga” alisema mtoa taarifa ambaye ni mwalimu katika moja ya shule mkoa wa Pwani.

AANDALIWA TUHUMA KAMA ZA CHONGOLO
Katika kile kinachodhaniwa ni muendelezo wa vita hivyo vya kuhakikisha Mwalimu Japhet Maganga anaachia madaraka ndani ya CWT inadaiwa baadhi ya mahasimu wake wametengeneza jumbe fupi za kwenye WhatsApp zikionyesha kuwa ni mawasiliano baina ya Mwalimu Maganga na mmoja wa wasichana katika moja ya chuo kikuu nchini anayeahidiwa ajira ndani ya chama hicho.

Jumbe hizo zinafana na zile zilizokuwa zikisambaa na kumhusisha aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ambaye kwa hiari yake aliomba kujiuzulu katika siku za hivi karibuni.

Jambo TV imefanikiwa kuziona baadhi ya jumbe fupi za maneno ambazo ziadaiwa kutengenezwa na kusambazwa ikiwa na nembo ya Chombo kimoja maarufu cha Habari nchini cha Millard Ayo ikimueleza binti huyo kuwa amvumilie Maganga.

Baadhi ya jumbe hizo ambazo zimeambatanishwa kwenye logo ya chombo cha habari cha Millard Ayo zikionyesha ahadi ambazo zinadaiwa Mwalimu Maganga anazitoa kwa Binti huyo kwamba amvumilie kwani anapitia kwenye changamoto kubwa ndani ya CWT ila mambo yakipoa ndani ya CWT basi "watakula bata".

Hata hivyo Uongozi wa Ayo.com umeuthibitishia Jambo TV kuwa hauhusiki na ujumbe huo wala nembo iliyotumika si ya Chombo chao na kutoa onyo kwa watu wanaoigiza nembo hiyo kwa maslahi yao binafsi

"Hapana hatuhusiki na hizo picha na habari zilizotengenezwa na kuwekewa nembo yetu,hata ukiitazama hiyo nembo ni tofauti na hii ambayo tunatumia sisi ofisini,hao watu wametengeneza nembo feki na kutuhusisha na imekuwa mara nyingi tunapokea taarifa za wahalifu mitandaoni kutumia jina letu kuhalalisha mambo yao” umesisitiza uongozi wa millardayo.com

Chanzo: Jambo TV

Pia soma:
Mwalimu Japhet Maganga wa CWT ajibu madai ya uwepo wa mipango ya kutengenezewa tuhuma
 
Hivi Maganga tabu yote ya nini hii unatujazia seva asee. Wenyewe hawakutaki si utoke tu

Katika nchi za kiafrika hizi hakuna mtu amewahi shindana na serekali akashinda. Use your brain mwalimu. Unapigana vita usivyoweza kuvishinda.
Mkwanja wa Ukatibu Mkuu CWT sio mdogo anaendelea kukusanya maokoto kwanza kila mwisho wa mwezi Mshahara unaingia iambie Serekali iuzuie Mshahara wake labda atajifikiria
 
Vita vya madaraka ndani ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) imezidi kushika kasi huku kiasi cha watu wanaodaiwa kuwa nyuma ya mkakati wa kuuondoa uongozi wa sasa madarakani, wakitumia mitandao ya kijamii kuwadhalilisha baadhi ya viongozi wa chama hicho.

Katika kile kinachoelezwa kuwa sababu ya vita hiyo ni nafasi ya Ukatibu Mkuu, miongoni mwa waathirika wakubwa wa udhalilishaji huo unaoandaliwa aliyelengwa moja kwa moja ni Katibu Mkuu wa sasa wa CWT, Mwalimu Japhet Maganga ambaye mikakati ya kumchafua imeanza kwa kutengenezewa kashfa za ngono ikiwa ni siku chache kabla ya maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 30 ya Chama hicho yanayotarajiwa kufanyika Jijini Mwanza, baadaye mwezi huu (Desemba 2023).

Mwalimu Maganga anatajwa kuwa mlengwa mkuu kutokana na msimamo wake wa hivi karibuni wa kulinda katiba ya CWT kwa kukataa kujiuzulu ukatibu Mkuu licha ya kuwepo mashinikizo ya makundi mbalimbali ya mahasimu wake wanaotumia ofisi za umma kutaka kumuondoa madarakani.

Jambo Tv Online lina taarifa za kina kuwa kabla ya Mwalimu Maganga kuukwaa ukatibu mkuu wa CWT watangulizi wake waliondolewa kwenye ofisi hizo kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za matumizi mabaya ya fedha za CWT huku ikielezwa kuwa hawajaridhika na namna walivyotoka katika nafasi za uongozi kiasi cha kupanga na kuratibu kile kinachoitwa migogoro ndani ya Chama

“Walioondolewa hawajaridhika kiasi cha kuanza kupanga na kuratibu hiki watu wanachodhani ni vurugu ndani ya CWT na kwa sasa watu hawa wanatumia udanganyifu kuwa vita hivyo ni maagizo kutoka juu kwa kuwa serikali haimtaki Mwalimu Maganga” alisema mtoa taarifa ambaye ni mwalimu katika moja ya shule mkoa wa Pwani.

AANDALIWA TUHUMA KAMA ZA CHONGOLO
Katika kile kinachodhaniwa ni muendelezo wa vita hivyo vya kuhakikisha Mwalimu Japhet Maganga anaachia madaraka ndani ya CWT inadaiwa baadhi ya mahasimu wake wametengeneza jumbe fupi za kwenye WhatsApp zikionyesha kuwa ni mawasiliano baina ya Mwalimu Maganga na mmoja wa wasichana katika moja ya chuo kikuu nchini anayeahidiwa ajira ndani ya chama hicho.

Jumbe hizo zinafana na zile zilizokuwa zikisambaa na kumhusisha aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ambaye kwa hiari yake aliomba kujiuzulu katika siku za hivi karibuni.

Jambo TV imefanikiwa kuziona baadhi ya jumbe fupi za maneno ambazo ziadaiwa kutengenezwa na kusambazwa ikiwa na nembo ya Chombo kimoja maarufu cha Habari nchini cha Millard Ayo ikimueleza binti huyo kuwa amvumilie Maganga.

Baadhi ya jumbe hizo ambazo zimeambatanishwa kwenye logo ya chombo cha habari cha Millard Ayo zikionyesha ahadi ambazo zinadaiwa Mwalimu Maganga anazitoa kwa Binti huyo kwamba amvumilie kwani anapitia kwenye changamoto kubwa ndani ya CWT ila mambo yakipoa ndani ya CWT basi "watakula bata".

Hata hivyo Uongozi wa Ayo.com umeuthibitishia Jambo TV kuwa hauhusiki na ujumbe huo wala nembo iliyotumika si ya Chombo chao na kutoa onyo kwa watu wanaoigiza nembo hiyo kwa maslahi yao binafsi

"Hapana hatuhusiki na hizo picha na habari zilizotengenezwa na kuwekewa nembo yetu,hata ukiitazama hiyo nembo ni tofauti na hii ambayo tunatumia sisi ofisini,hao watu wametengeneza nembo feki na kutuhusisha na imekuwa mara nyingi tunapokea taarifa za wahalifu mitandaoni kutumia jina letu kuhalalisha mambo yao” umesisitiza uongozi wa millardayo.com

Chanzo: Jambo TV
Ndani ya ccm hakuna kuachiana maji
 
Back
Top Bottom