Imegundulika kwamba Kampuni ya JATU PLC iliyosajiliwa DSE ni ya kitapeli

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,906
Tanzania haiishi vituko.

Soko la Hisa la Dar es Salaam wanafuatilia kampuni ambayo imesajiliwa kwenye soko hilo inayoitwa JATU PLC.

Hii ni kutokana na hisa za kampuni hiyo kushuka kutoka TZS 2,900 hadi TZS 290 sawa na angulo la asilimia 90.

Angalia hapa.
036E6C7E-24AD-45E0-9D76-5546EC42A407.jpeg

Swali la kujiuliza, kabla ya kusajiliwa DSE, je ilifanyiwa Due Diligence hii kampuni?
 
Kwa miaka hiyo miwili ya usajili feki wamepiga how much? Wanaomiliki hisa za hiyo "kampuni" nini hatma yao? Au ndio imekula kwao?
 
Wamepiga kama billion 5.1 na jamaa ni chalii tu miaka 32 ndo CEO aliyewaliza watu.
 
Duh! Hatari sana. Board ya DSE waje na majibu kwanini wali-approve kampuni feki; pili hatma ya wenye fedha zao. Hii nchi inaelekea uelekeo wa Nigeria sasa.
 
Jatu is obvious scam.. Tuliwaambia vijana hapa ukiona wanatoa business plan yao na compensation plan yao ikiwa na risk free wao wamebase kweny kuwaaminisha faida tu tambua kabisa huo ni utapeli..

Jamaa kakopa mwaka Jana mil30 eti anaenda kulima na Jatu ,nilimwambia utapigwa mara ananionyesha ipo kweny list ya DSE 😂😂.
 
Bongo hatari sana😂😂huyu jamaa juzi niliona wanasumbuana nae mahakamani iyo pesa yote Katia mfukoni..

Kwa bongo kesi ikifika hapa wawekezaji wataambulia maumivu maana pesa inaenda Kwa serikali ,watafreeze account yote na kuzichukua wawekezaji watalia mpaka wakome.
Screenshot_20230101-095049.png
 
Jatu is obvious scam.. Tuliwaambia vijana hapa ukiona wanatoa business plan yao na compensation plan yao ikiwa na risk free wao wamebase kweny kuwaaminisha faida tu tambua kabisa huo ni utapeli..

Jamaa kakopa mwaka Jana mil30 eti anaenda kulima na Jatu ,nilimwambia utapigwa mara ananionyesha ipo kweny list ya DSE 😂😂.
Sahivi anasemaje. Huyo CEO tayari akapata pesa ya kuishi USA uk akanunua apartments akapangisha na akaishi na yeye akanunua hisa kampuni za Mana akawa anaishi kazi take Ni kuwaza namna ya kutumia pesa Mana ameshapanda.
 
Jatu is obvious scam.. Tuliwaambia vijana hapa ukiona wanatoa business plan yao na compensation plan yao ikiwa na risk free wao wamebase kweny kuwaaminisha faida tu tambua kabisa huo ni utapeli..

Jamaa kakopa mwaka Jana mil30 eti anaenda kulima na Jatu ,nilimwambia utapigwa mara ananionyesha ipo kweny list ya DSE 😂😂.
Kwanza watanzania tuna upungufu wa wachambuzi na washauri wa mahesabu, yaani financial analysts and financial advisors.

Kwa tatizo hilo watu wengi hawawekezi kutokana na kupata ushauri wa kutosha wa kitaalamu, wanafuata ushauri wa marafiki na ndugu na jamaa ambao pia hawana ufahamu wowote juu ya uwekezaji, wao pia wameshauriwa na watu wao wa karibu wasio jua chochote, it goes on and on, ni viscous circle of poor investment.

Ununuaju wa hisa sio jambo la kuchezea maana unaweka pesa yako hapo, ikitokea kampuni imepata shida unafilisika ama kuingia kwenye madeni ma matatizo makubwa.

Kwa Tanzania ni simple sana kuwaibia watu, anzisha kampuni, isajili brela, fanya figisu isajili DSE kisha anza kuwaaminisha watu kwamba imesajiliwa , ina usajili, iko DSE nk. Watu hawahoji imesajiliwa kufanya nini, wao wanatoa tu hela.

Ni changamoto sana.
 
Elimu wengi hawana kila kitu wanafikiria ni fursa.
 
Tanzania kuna wajinga wengi sana

Nahisi ktk afrika tanzania ndiyo inaweza,kuwa nchi inayoongoza
Kuwa na wajinga

Ova
 
DSE ni taasisi ya Serikali inapoorodhesha Kampuni kwenye soko la mitaji na Fedha maana yake wamefanya uchambuzi n a kujiridhisha.

Sioni kosa la Wateja hapa walionunia his a ya Kampuni hiyo bali nayaona makosa ya Serikali kupitia DSE.Kama kuna wahanga walinunua hisa za Kampuni hiyo waende waishitaki DSE mahakamani.

Serikali inajukumu la kulinga wealthy ya watu wake,DSE washitakiwe.
 
kuna siku nilishawai kuandika kuhusu serikali inavotumia kuwaibia watu ulifutwa haraka .ila huyu mod kama kuna sehemu ya kueleza upigaji wa serikali unavotumika hapa tz. utacheka
 
Japo watanzania wapo wajinga ila DSE nao wanashiriki kwenye kuwatapeli wajinga. Kampuni feki inakusanyaje 5B kisha tuseme wanahisa wameshatapeliwa na kila mwaka kampuni inatuma hesabu zao BRELA, TRA na taasisi nyingine? si wangeona hizo 5B zinaenda wapi? Balance Sheet na Cashflow ingeonyesha kila kitu kinavyokwenda kila mwaka na namna hisa za wawekezaji zinavyotumika.

Kama 5b zimenunulia Asset ziuzwe wanahisa walipwe au wagawiwe hizo asset kama haziuziki.

Kama zilikuwa zinaliwa na hesabu zinadanganya wakaguzi wa hesabu wakamatwe hata kabla ya mkurugenzi waseme walikuwa wanakagua nini.
 
Back
Top Bottom