Jatu Plc ni Pyramid Scheme

GLA

New Member
Jun 1, 2015
1
0
Wadau wa kilimo nchini wana kilio kikubwa sana baada ya kutapeliwa mabilioni ya shilingi na kampuni ya Jatu Plc ambayo imeendesha pyramid scheme tangu 2019.

Kampuni hii imekuwa ikitangaza kama mkombozi wa watanzania wenye nia ya kuwekeza kwenye kilimo biashara katika mazao mbalimbali. Mwaka 2020 walipokea pesa nyingi kwa ajili ya kulima maharage, mahindi, mpunga alizeti na mazao ya muda mrefu kama parachichi na machungwa. Lakini tangu wavune mazao hayo mwezi Juni 2021 hadi leo hawajawahi kuwalipa watu waliowekeza.

Pia June 2021 waliingia kwenye soko la hisa DSE na kufanikiwa kukusanya kiasi çha Tzs 7.7bn kutoka kwa wananchi takribani 12,000 ila hizo pesa pia zetoweka. Serikali imetaarifiwa kuhusu hili ila Wizara ya Kilimo inapiga danadana. Tahadhari kwa wanaotamani kuwekeza na Jatu Plc. Hii kampuni ni scam kuna watu wamelizwa zaidi ya Tzs 21bn.
 
Serikali wanatabia ya kuingilia hizi projects wakiona tu zimeanza kutengeneza pesa na kuanza kuomba vibali visivyoeleweka ili tu wapate sababu ya kuzifungia na kulazimisha kesi mahakamani kisha wanazifungia na kutaifisha pesa walizozuia.

Nyuma ya pazia ni watu wanatake advantage ili kudhurumu raia pesa zao walizowekeza kwa shida ili kujikimu.
 
Wadau wa kilimo nchini wana kilio kikubwa sana baada ya kutapeliwa mabilioni ya shilingi na kampuni ya Jatu Plc ambayo imeendesha pyramid scheme tangu 2019.

Kampuni hii imekuwa ikitangaza kama mkombozi wa watanzania wenye nia ya kuwekeza kwenye kilimo biashara katika mazao mbalimbali. Mwaka 2020 walipokea pesa nyingi kwa ajili ya kulima maharage, mahindi, mpunga alizeti na mazao ya muda mrefu kama parachichi na machungwa. Lakini tangu wavune mazao hayo mwezi Juni 2021 hadi leo hawajawahi kuwalipa watu waliowekeza.

Pia June 2021 waliingia kwenye soko la hisa DSE na kufanikiwa kukusanya kiasi çha Tzs 7.7bn kutoka kwa wananchi takribani 12,000 ila hizo pesa pia zetoweka. Serikali imetaarifiwa kuhusu hili ila Wizara ya Kilimo inapiga danadana. Tahadhari kwa wanaotamani kuwekeza na Jatu Plc. Hii kampuni ni scam kuna watu wamelizwa zaidi ya Tzs 21bn.
Naona hatimaye serikali imechukua hatua. Wizara ya kilimo imeichunguza na ripoti itakabidhiwa kwa vyombo vya dola.
 
Yametimia.

CEO ameshtakiwa.

9599b44b-6064-41e6-861b-9893cd156d81.jpg

34edb3ca-ae49-444d-b2c8-83aed0be49ed.jpg
 
Back
Top Bottom