Mambo yanayotokea sasa Tz yananikumbusha miaka ile ambapo masheik na maaskofu walikuwa wanapeana zamu za kutoa "matamko". Wakitoa maaskofu tamko dhidi ya serikali, masheikh nao wanainuka kutoa tamko kupinga lile la maaskofu.
Nakumbuka kipindi fulani hata Rais aliibuka na kuhutubia "wazee wa Jiji la Dar es salaam" kujibu waraka wa baraza la maaskofu, akiwakumbusha kutenganisha ya "Mungu na Kaizari", lakini hapohapo hadhira yake ikimwitikia kwa vibwagizo vya "takbiir!"