Japokuwa ninaweza kuwa nimepitwa na wakati katika kuyasema haya hasa kwa kuwa aliyasema siku nyingi sana, napenda kukubaliana Msemaji aliyetangulia {Nd. Kitia) katika karibu kila jambo alilogusia. Lakini kwa kuongezea tu ni kwamba inasikitisha namna ambavyo WATANZANIA, walio wengi wanavyojitenga na SIASA. Ukiuliza mitaani watu wengi watakujibu, "mimi na siasa mbali mbali." Watu kama hawa, ukifuatilia, utakuta hawana muda hata kidogo wa kujifunza hata mambo ya msingi ya husuyo nchi hali ya kuwa ni wananchi na ndio nchi inawategemea katika kuijenga.
Mtu wa aina niliyoisema awali, pamoja na jibu lake la kutojihusisha na siasa, kwa kiasi kikubwa anategemea UONGOZI uliopo madarakani katika kujiletea maendeleo binafsi & kuliletea maendeo taifa kwa ujumla. Lakini mtu huyu hashiriki katika kuuweka madarakani uongozi huo, hali inayoweza kutoa mwanya kwa kiongozi asiye na sifa kuingia madarakani, kiongozi ambaye watu wote, pamoja na wale wasiomchagua watalazimika kumtii kwa mujibu wa sheria. Inapotokea mtu wa aina hiyo niliyoitaja awali (asiyejihusisha ma siasa) akaamua kuitumia fursa na haki yake ya kikatiba, anaweza kumchagua mtu kwa kuangalia picha inayovutia machoni maana ndio kigezo pekee anachoweza kutumia. Lakini pia ikiwepo mifumo iliyo HAI ambayo inaweza kuhakikisha viongozi wote, waliochaguliwa na kuteuliwa wanasimamiwa na kutathminiwa kiutendaji ili kuona kama wanaweza kuondolewa katika nyadhfa wanazoshika {Hata Rais mwenyewe} iwapo hawatoshi katika nafasi walizo nazo, hali isingekuwa ilivyo sasa. Kwa nchi kama Marekani ambapo kila Mwananchi, kwa nafasi yake anashiriki kikamilifu katika MCHAKATO wa kumchagua Rais ambaye anaamini ataleta maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla, kutokuwa na imani na RAIS ama uongozi ulio madarakani ni SWALA LENYE MAANA KUBWA kikatiba na huanzia katika kura kama hizi tunazopiga humu lakini katika kiwango tofauti cha UMUHIMU na hata MAPOKEO na mifumo ya UFUATILIAJI wa matokeo yenyewe. Ipo siku mambo yatabadilika japo siku hiyo haijulikani leo.