Imani yetu kwa serikali ya Kikwete

Bado una imani na serikali ya Kikwete?

  • NDIYO (YES)

    Votes: 215 19.4%
  • HAPANA (NO)

    Votes: 834 75.1%
  • Sijui (Undecided!)

    Votes: 64 5.8%

  • Total voters
    1,111
Maboksi ya kura yako wapi au yameibiwa, mimi naimani hata yeye kama ni member humu atajipigia hana imani na maamuzi yake mwenyewe, maana anajichanganya sana juzi alisema takrima ni rushwa leo anasema si rushwa.
 
Michango mingi inayotolewa humu ukiangalia kwa makini kinachosababisha madhaifu yote hayo ni UDHAIFU WA KATIBA YETU. vote of no confidence ilipaswa iwepo kwenye katiba, sio kwa Rias tu hata Wabunge na Madiwani. Kipengele hiki kingemfanya Kiongozi aliyechaguliwa kujituma na kuwafanya waliomchagua kumu-asses mara kwa mara.

CHANGAMOTO: Tunapoimizana kuchagua wabunge wa upinzani wengi lengo la msingi ni kwenda kubadilisha katiba. Sasa hivi inakuwa ngumu kwani Mbunge wa upinzani akipeleka changamoto ya kubadili Katiba kitaitishwa kikao cha wabunge wa CCM na kuelezwa madhara ya kuingizwa kipengele hicho kwa CCM bila kuangalia madhara yake kwa wakulima na wafanyakazi.

SHIME SHIME WANAJAMII TUONGEZE WABUNGE WA VYAMA VYA UPINZANI.

Tatizo kubwa ni kwamba vyama vya upinzani havionyeshi dalili zozote za kutaka kuleta mabadiriko. Kwa mfano Chadema walikuja na agenda ya michango ya sms, lakini wakapotelea kusikojulikana. Nina imani kama wangekuwa serious wangeweza kupata fedha ambazo zingewawezesha kuwafikia watanzania wengi iwezekanavyo, na wangekuwa na nafasi kubwa ya kupata wabunge kwenye uchaguzi ujao.
 
Hivi kwa nini tutafute njia ndefu za kutibu magonjwa yetu wakati ipo njia fupi sana ya kutibu?

Tumeshaongea sana juu ya udhaifu wa viongozi wengi wa CCM. Dawa ni kuiondoa na kwa serikali za KI-AFRICA, dawa ni kuuwa kichwa na mwili utajifia wenyewe. Nakubaliana na maneno ya Kitila Mkumbo kuwa "JK is beatable!! ".

Bunge la Tanzania hata likiwa la UPINZANI, milele halitafanya mabadiliko. Tumeona Kenya, Zimbabwe nk. PRESIDENT TAKES ALL.https://www.jamiiforums.com/uchaguz...mbea-urais-mwaka-2010-jiandikishe-hapa-9.html
 
JK hafai kama wengi mlivyosema lakini pasipo nahodha mwingine kujitokeza sioni sababu...Atashinda uchaguzi unaofuata kiulaini na tutaendelea kusema hivi hadi Yesu arudi! Pili, Mnaposema JK hafai inaonyesha mlikuwa na viongozi bora huko nyuma hivyo tatizo sio CCM ila ni JK..maadam bado yeye ni nahodha mtaipanda meli hii japokuwa kwa shingo upande.. Hakuna namna..
 
Wale wote wenye mtazamo kama wangu kuwa JK ameshindwa kuongoza nchi, hivyo asipitishwe tena kugombea 2010 kwa maslahi na usalama wa nchi yetu wagonge thanks hapa.
 
MzeePunch hii itatupeleka wapi? Kwa sababu kwa ujumla kila Mtanzania aliyefumbua macho hahitaji kuulizwa jinsi gani asivyoitaka serikali ya CCM kuendelea kuongoza nchi yutu! Wameshindwa and stahili yao ni kuwang'oa kitendawili hapo ni how? Kuna kipindi Moi aliwahi kusema with everything in my power who cab dare to challenge KANU. Wakati ulipowadia aling'olewa na akasahaulika. Can Tanzanian answer this call unanimously?
 
Wale wote wenye mtazamo kama wangu kuwa JK ameshindwa kuongoza nchi, hivyo asipitishwe tena kugombea 2010 kwa maslahi na usalama wa nchi yetu wagonge thanks hapa.

si JK ndiyo abembe zigo la lawama bali ni CCM imeshindwa kuongoza nchi.
 
Tunaye tu JK wetu. Tatizo ni kwamba wengi mnaomkataa mlikuwa na "Marais" wenu ambao hawakuwa! Ajaribu tu kupunguza nguvu za kisiasa za wanafamilia wake wanazotaka kuwa nazo.
 
Wabongo najua mnavumilia uvumilivu wa uwoga zikipambwa na nidhamu ya uwoga na kinafiki. Kimsingi hali ni mbaya lazima tuseme na hili linachangiwa na system nzima akiwemo Rais mwenyewe. Sijaona chochote alichowafanyia wapiga kura wake...

Naamini na natabiri, kuwa kisipofanyika kitu cha kurekebisha hali hii haraka iwezekanavyo, tutajikuta tunaingia kule kule walipoingia wenzetu kama Rwanda, Burunid, Siera leone, Congo DRC na wengineo. Najua baadhi yenu mtasema "ooh kwa Tanzania haiwezekani" lakini ninachoamini mnyonge utamwonea sana lakini siku akifanya maamuzi kubadilisha ni ngumu sana, mpaka kieleweke. Upuuzi mwingi unafanyika nchi hii na watu wamenyamaza tu.

There will be an end for this. Hata kama sio leo au kesho au kwa kipindi ambacho tutaishi, basi watoto na wajukuu zetu watatimiza hili ninalosema leo. Things are worse men, why don't we wake up and do something. It is better dying trying rather than sit down and watch some few stupid individuals who make the situation worse.

When should we eliminate those guys and their generations so that we remain peacefully?
 
Mimi sikuwa na imani na Kikwete toka mwanzoni, hayuko makini ni mtu wa kuunga unga tu
 
Tunaye tu JK wetu. Tatizo ni kwamba wengi mnaomkataa mlikuwa na "Marais" wenu ambao hawakuwa! Ajaribu tu kupunguza nguvu za kisiasa za wanafamilia wake wanazotaka kuwa nazo.

Yaani uongozi wa nchi una suggest ufanyiwe majaribio! Huu ni udhaifu ambao wewe unaanza kuuona sasa! Hujatoa suluhisho ya hayo mengine mengi!
 
Watanzania wenzangu tunajua nini kinatakiwa kufanyika. tunajua kama serekali yetu inaipeleka hii nchi pabaya kila siku tunalizungumza hilo je sisi watanzania tunafanya nini kulibadilisha hali hii. tukindeleya kuwategema hawa wabunge/waziri hata raisi wmatajiri watazidi kutajirika na wamaskini kutazidi kuumia. sisi watanzania inabidi tichukue hatua huijulisha serekali kama wananchi wamechoka tunataka mabadiliko.
 
Nimekuwa najiuliza kuhusu kura ya kutokuwa na imani (a vote of no confidence) Hii kura iko applicable kwenye sheria zetu za Tanzania au haipo. Lini bunge au baraza la mawaziri laweza kuitumia against waziri mwenzao au bunge juu ya waziri mkuu au raisi wa nchi. Katika matukio mbali mbali kama vile Israel waliishawahi kumpigia waziri mkuu Nentenyahu kura ya kutokuwa na imani http://findarticles.com/p/articles/mi_qn4158/is_19970625/ai_n14101252. Kenya leo wabunge wamempigia waziri wa fedha Amos Kimunya kura ya kutokuwa na imani baada ya kuuza hoteli ya kitalii kwa siri Reuters.com. Katika nchi yetu hasa wabunge wetu je inawezekana kwa wao kupiga kura ya kutokuwa na imani bungeni kwa Rais, Waziri Mkuu au Waziri yeyote kama wanafikiria hawako –effective kutekeleza majukumu yao?

JF kama kuna mtu anaweza kutupa sheria na mazingira ya kura ya kutokuwa na imani rusha msaada basi!
Unajua chini ya makubaliano ya serikali iliyo madarakani hivi sasa kule Kenya, Waziri anapoteuliwa ni lazima aidhinishwe (yaani going through CONFIRMATION process - ambayo Bongo hakuna kitu kama kama hicho) na Bunge la Kenya. Hivyo basi inapotokea Waziri yule akavurunda au Wabunge kukosa imani naye katika utendaji wake wana uwezo wa kumpigia vote of no confidence. Na Waziri Mkuu (Kama Kiongozi Mkuu wa Serikali ndani ya bunge) atalifikisha suala hilo kwa Rais (ambaye ndiye Mteuzi) na kufanya maamuzi juu ya Waziri husika. Na ndio kesi ya Waziri Amos Kimunya.

Ni mfumo mzuri wenye kufanya Mawaziri kuwajibika kwa Wabunge (Wananchi) na Bongo inauhitaji sana ili kuweza kuona maendeleo na Mawziri wenye nidhamu na uwajibikaji. Nimewahi kusikia Mawziri wengi wakjitapata kuwa hawababaishwi kwa kuwa bosi wao ni JK, which I think is stupid!
 
Bado nina imani Serikali hii ya awamu ya nne inaweza kufanya mazuri zaidi. Imeweza kudumisha amani na utulivu. Imekabiliana na changamoto kubwa ikiwemo kupoteza Waziri Mkuu na baadhi ya Mawaziri na kuwepo na msukosuko wa uchumi duniani.

Tumchague Rais Kikwete ili aendeleze mazuri yaliyopo na hata kuzidisha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom