Mama Salma Kikwete atumia Usafiri wa Bodoboda kuwafikia Wapiga kura wake walioathiriwa na Mafuriko

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
86,683
147,789
Mbunge wa Mchinga mkoani Lindi mama Salma Kikwete amelazimika kutumia usafiri wa bodaboda kuweza kuwafikia Wapiga kura wake walioathiriwa na Mafuriko jimboni kwake

Mama Kikwete amekuwa Mbunge wa mfano katika kuwajali Wapiga kura wake

Credit: Kitenge Tv

---
Salma.png

MBUNGE wa jimbo la Mchinga na Mke wa Rais mstaafu Awamu ya Nne, Mhe. Salma Rashid Kikwete amelazimika kutumia usafiri wa Pikipiki maarufu kama Bodaboda katika ziara yake alipofika kutoa pole kwa wananchi na kuangalia athari mbalimbali zilizojitokeza kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali katika jimbo la Mchinga.

Aidha, akizungumza na baadhi ya wananchi waliojitokeza katika maeneo aliyotembelea Mhe. Salma Kikwete ameonyesha masikitiko yake makubwa na kuwataka wananchi wa maeneo hayo kuwa watulivu kufuatia baadhi ya miundombinu ya barabara kuharibika na huku baadhi ya wakazi wakikosa nyumba zao za kuishi pamoja na mazao yao kutokana na mvua kubwa zilizonyesha huku akiwataka wananchi hao kuendelea kuchukua tahadhari hasa kwa wanaoishi maeneo ya mabondeni na kuepuka kutembelea maeneo ya mito na mabonde pindi mvua kubwa zinaponyesha.

"Leo (jana) ni tarehe Nane, mwezi Machi, tunasherehe kubwa ya kuadhimisha siku ya Wanawake, nimeshindwa kujizuia kuendelea na sherehe hizi wakati huo wananchi wakiwa katika hali ya changamoto hizi, nikaona lazima nifike kuwapa pole na kuangalia athari hizi zilizojitokeza. Tunamshukuru Rais wetu Dkt. Samia kwa kutuletea miradi na kwa hakika tulianza kuifungua Mchinga lakini hatuwezi kulaumu kwasababu ni mipango ya Mwenyezi Mungu, na majanga haya yamejitokeza maeneo mbalimbali katika mkoa wetu na hata Taifa letu, tunaimani serikali yetu sikivu itaendelea kutusaidia na Mwenyezi Mungu atuongoze katika hilo, poleni sana ndugu wananchi wenzangu" alisema Mhe. Salma Kikwete.

Katika hatua nyengine wananchi wamepongeza hatua hiyo ya Mbunge kufika kuwapa pole huku wakiomba serikali kuwapelekea chakula cha bei nafuu kutokana na mazao mengi kusombwa na maji mashambani. Katika ziara hiyo Mhe. Salma Kikwete ameambata na wataalamu wa TARURA na viongozi wengine wa Chama na serikali.
 
Mbunge wa Mchinga amefika jimboni kuwapa pole wananchi walioathiriwa na mvua, mbunge alitinga maeneo yote ya jimboni kwa usafiri wa bodaboda, akiwapa pole wananchi waliopata madhara kwa mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jimboni humo.

Amezungukia maeneo yote ambayo miundo mbinu imeharibiwa na mvua, na kuwataka wananchi hao kuwa watulivu.
1709975660563.jpg
 
Mbunge wa Mchinga mkoani Lindi mama Salma Kikwete amelazimika kutumia usafiri wa bodaboda kuweza kuwafikia Wapiga kura wake walioathiriwa na Mafuriko jimboni kwake

Mama Kikwete amekuwa Mbunge wa mfano katika kuwajali Wapiga kura wake

Credit: Kitenge Tv
Anapanda bodaboda huku anafurushi la mamilion ya mwenza wa rais mstafu

USSR

Sent from my Infinix X6511G using JamiiForums mobile app
 
Mbunge wa Mchinga amefika jimboni kuwapa pole wananchi walioathiriwa na mvua, mbunge alitinga maeneo yote ya jimboni kwa usafiri wa bodaboda, akiwapa pole wananchi waliopata madhara kwa mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jimboni humo.

Amezungukia maeneo yote ambayo miundo mbinu imeharibiwa na mvua, na kuwataka wananchi hao kuwa watulivu. View attachment 2929243
Hapo anafurushi la mamilion yale ya mwenza wa rais

USSR

Sent from my Infinix X6511G using JamiiForums mobile app
 
Mbunge wa Mchinga mkoani Lindi mama Salma Kikwete amelazimika kutumia usafiri wa bodaboda kuweza kuwafikia Wapiga kura wake walioathiriwa na Mafuriko jimboni kwake

Mama Kikwete amekuwa Mbunge wa mfano katika kuwajali Wapiga kura wake

Credit: Kitenge Tv
Cha ajabu ni nini! Hao wanaodhaniwa ni wapigakura wake wao hawatumii hizo bodaboda?
 
Mbunge wa Mchinga mkoani Lindi mama Salma Kikwete amelazimika kutumia usafiri wa bodaboda kuweza kuwafikia Wapiga kura wake walioathiriwa na Mafuriko jimboni kwake

Mama Kikwete amekuwa Mbunge wa mfano katika kuwajali Wapiga kura wake

Credit: Kitenge Tv
Sio kwamba mfano angefanya lobbying ili kuhakikisha mafuriko hayana athari ya mawasiliano in the first place ?

Siasa mamboleo hata shortcomings wanazigeuza zionekane kwamba jambo jema limefanyika....
 
Mbunge wa Mchinga mkoani Lindi mama Salma Kikwete amelazimika kutumia usafiri wa bodaboda kuweza kuwafikia Wapiga kura wake walioathiriwa na Mafuriko jimboni kwake

Mama Kikwete amekuwa Mbunge wa mfano katika kuwajali Wapiga kura wake

Credit: Kitenge Tv
Nani alimpigia kura huyu maza?
 
Back
Top Bottom