Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 3,811
- 2,765
Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete, rais uliyetokea kupendwa na Watanzania wengi hadi ukaweza kupata kura nyingi kukupa ushindi wa kishindo, sisi Watanzania tunakuomba ukirudi kutoka Marekani usafishe hali hii. Mkoloni mweusi kaingia nchini. Anatutukana sisi Watanzania. Anakejeli hali yetu ya Umasikini.
Kwa kawaida sisi wananchi wako tunaishi maisha magumu sana kwa siku tunatumia chini ya dola moja. Hali hii si kwamba bei ya bidhaa ipo chini la hasha bali ni hali ngumu ya maisha. Tunajitahidi kuwa watulivu wakati wewe mwenzetu unasafiri huku na huko kutafuta uwezekano wa kujikwamua na maisha haya tuliyo nayo, hilo tunakusifu kwa juhudi hizo.
Wakati unaingia madarakani ulituahidi mengi sana hata hatuwezi kuyakumbuka yote sidhani kama hata wewe unakumbuka labda hadi upekue makabrasha yako ukaweza kukumbuka ulichotuahidi.
Katika hali isiyo ya kawaida juzi juzi ulisafiri kwenda China wewe na ujumbe wako akiwemo Andrew John Chenge, ambaye aliwahi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali katika awamu ya tatu. Kipindi hicho ndicho tulichoshuhudia usaliti wa serikali dhidi ya wananchi wake kwa mambo mengi mathalani ubinafsishaji wa mashirika ya umma na kuwapa wawekezaji au niwaite wapangaji wa uchumi wetu. Inaelekea kwamba wote waliofanikisha ubinafsishaji huu walikuwa na maslahi binafsi kwani ndicho kipindi tulichoanza kushuhudia mgawanyiko wa matabaka katika jamii. Hii ilitokana na viongozi kuanza kujilimbikizia mali za umma. Zoezi hili limevuka mpaka ambapo sasa tunashuhudia mtu kama waziri anakuwa jasiri wa kukejeli wananchi.
Hali hii ni picha dhahiri kwamba ndani ya suti yako kuna chawa, sisi wananchi tunakupigia kelele kwamba katika kola za koti lako kuna chawa mkubwa sana anajaribu kutoboa ili akunyonye shingoni. Kelele hizi sijui kama hujasikia kwani hata watoto unaowapenda na kuwasikiliza wameshakwambia usizibe masikio vua hilo koti chawa aondolewe atakunyonya.
Ni aibu sana kwako kusafiri pamoja na mtu mwenye kejeli kiasi hicho kwa wapiga kura wako. Sisi wananchi wako TUMEKATA TAMAA hatuna imani na baadhi ya mawaziri wako. Tunajua kwamba huwezi kuwa na mawaziri wazuri kwa asilimia mia moja lakini inapojitokeza waziri wako akaonyesha tabia mbaya kiasi hicho macho yetu tunakuelekezea wewe kuangalia UNASEMAJE.
Kumekuwa na mabadiliko makubwa ya kiuchumi, tukadanganywa kwamba uchumi utajirekebisha wenyewe, tukakaa kimya. Kumekuwa na mfumuko wa bei ya bidhaa mbali mbali tena muhimu ikiongozwa na bei ya mafuta ya kuendesha mitambo n.k. nalo pia tukakaa kimya. Bila shaka ingekuwa nchi kama Zambia jirani zetu kuhusu hilo wangeandamana.
KWA HILI
PAMOJA NA MENGINE YANAYOFANANA NA HAYO, SISI WANANCHI HATUTAKUELEWA KAMA HUTAYASHUGHULIKIA IPASAVYO.
Mwisho tunakupongeza kwa juhudi zako za kutafuta wawekezaji kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI AFRIKA
NOTE: Ukimaliza kusoma hii, pitia na hizi ili upige kura bila upendeleo:

- Huyu ndiye 'The Real JK'
- Kikwete: Majina ya wauza Madawa ya Kulevya ninayo
- Kikwete awajibu TUCTA, kura zao si mali kitu!
- Sababu 10 za kutomchagua Kikwete 2010
- Why I love Kikwete
- Kilaini: Kikwete bado ni 'Chaguo la Mungu'
- Kikwete: A failure in Leadership
- Matukio tisa yaliyomdhalilisha rais Kikwete
- Kikwete awe mgombea pekee 2010
- I'm done with Kikwete! - Say NO to Second Term!
- Nyerere alisema 'Kikwete bado hajakomaa...'
- 2010 Kikwete T-shirts?
- Mabilioni ya Kikwete na dhana ya kuondoa umasikini
- Pesa za nani zinajenga mahekalu haya kijijini kwa Kikwete?
- The Economist takes gloves off on Kikwete!
- Prof Shivji aiponda kauli mbiu ya rais Kikwete
- Kikwete: Every student to have a computer in five years
- Kikwete sio safi, YES I said it!
- Rais Kikwete na safari za nje
- Kwa nini Tanzania ni Nchi Maskini? Kikwete hajui!