Imani yetu kwa serikali ya Kikwete

Bado una imani na serikali ya Kikwete?

  • NDIYO (YES)

    Votes: 215 19.4%
  • HAPANA (NO)

    Votes: 834 75.1%
  • Sijui (Undecided!)

    Votes: 64 5.8%

  • Total voters
    1,111
Michango mingi inayotolewa humu ukiangalia kwa makini kinachosababisha madhaifu yote hayo ni UDHAIFU WA KATIBA YETU. vote of no confidence ilipaswa iwepo kwenye katiba, sio kwa Rias tu hata Wabunge na Madiwani. Kipengele hiki kingemfanya Kiongozi aliyechaguliwa kujituma na kuwafanya waliomchagua kumu-asses mara kwa mara.

CHANGAMOTO: Tunapoimizana kuchagua wabunge wa upinzani wengi lengo la msingi ni kwenda kubadilisha katiba. Sasa hivi inakuwa ngumu kwani Mbunge wa upinzani akipeleka changamoto ya kubadili Katiba kitaitishwa kikao cha wabunge wa CCM na kuelezwa madhara ya kuingizwa kipengele hicho kwa CCM bila kuangalia madhara yake kwa wakulima na wafanyakazi.

nakubaliana na Shoo Gap. msingi mkubwa wa matatizo tuliyo nayo ni katiba ndiyo maana kuna kuoneana haya katika kufanya maamuzi ya maslahi ya TAIFA na kundekeza USHIKAJI.
LEO Mtikila hana thamani ktk jamii lakini ali waambia wapinzani tushughulikie katiba kabla ya uchaguzi lakini kwa kwa sababu ccm wanajua mdhara walitumia mapandkizi yoa kwenye upinzani na uchaguzi ukafanyika. katiba ina ruhusu ubinafsi hata udikteta kutokana na madaraka makubwa aliyo nayo RAIS
 
Nyerere ndiye mkufunzi mkuu wa Mkapa na JK. Kwa hiyo kama wanafunzi wake wamechemsha basi na yeye si mwalimu mzuri.

Mkapa ndiye aliyemjenga Dr. Slaa mwaka 1995 pale alipomtupia virago vya uteuzi wa kuwa mgombea ubunge wa jimbo la Karatu na kumkweza kipenzi chake Bw. Patrick Qorro. Vile vile Mkapa ndiye aliyeongeza sifa za mgombea Uraisi wa CCM mwaka 2005 ili kumnufaisha swahiba wake JK. Na JK miaka mitano iliyopita ametetea ufisadi kwa nguvu zote na wananchi wamepoteza imani naye. Kwa nini Mkapa asionekane ameiua ccm kwa kukusudia?

JK ccm ndiyo inamfia mikononi mwake kwa kushindwa kusoma alama za wakati na kwa kuelewa uchaguzi huu ni “referendum on governance” alipaswa asigombee lakini yeye kwa uroho wa madaraka alitumia madaraka yake vibaya ndani ya chama tawala na kuwazuia wana ccm wengine wasijitokeze na wasimpinge. Alipanua demokrasia ya ubunge na udiwani lakini alisita kuifikisha hiyo demokrasia kwenye nafasi ya uraisi. Kwa kubinya demokrasia ndani ya chama chake ngazi ya Uraisi na kwa kula sahani moja na mafisadi JK amechangia kulikoni

Sasa ni nani kati ya hawa abebeshwe mzigo wa kuiua ccm?
 
JK ana kihoro cha kuona CCM inamfia na kusambaratika mikononi mwake
 
Nimechagua Nyerere.

Mwaka 1999. Saa 5 kasoro hivi asubuhi. ***** Secondari, Mbeya. Mkapa anatangaza kifo cha Baba wa Taifa. Nililia machozi. Kikwete ameanguka zaidi ya mara 10. Huwa ninawashangaa wanaolia.

Anyway. Nyerere kama muasisi ametufikisha hapa tulipo.

Amewajenga Watanzania katika nidhamu ya woga. Watanania wanasifika kwa amani na utulivu. Lakini nadhani walitakiwa kusifika kwa uoga na kutokuthubutu.

Sijui niseme nini, lakini nadhani Nyerere ni chanzo cha matatizo yetu leo hii
 
Kila mtu ana shea yake.

Nyerere alikuwa na nafasi nzuri ya kutuachia katiba na taasis imara za kiutawala lakini hakufanya hivyo. Kwa kosa hilo naye alitaka CCM iendelee kututawala milele.

Mwinyi huyo tunaweza kumpa lawama kidogo kwa sababu sina hakika kama alikuwa anajua alilotakiwa kulifanya. He was an innocent man in a wrong place.

Mkapa aliona jinsi ambavyo wananchi walitamani mageuzi, kwa hiyo alitakiwa kutuwekea misingi imara ya kidemokrasia ili mshindi yeyote ajaye atuongoze vizuri. Badala yake alianza upuuzi wa kulipiza visasi kwa watu ambao hawakuipenda CCM. Huyu ana share kubwa ya lawama kwa mambo ambaye yeye na mshikaji wake Sumaye waliwafanyia Watanzania.

JK.. Huyo hata kumlaumu ni kumwonea. Amefanya yoote kadri ya kikomo cha uwezo wake. That's the best he could achieve.

Kwa maana hiyo wooooote wanabeba lawama siyo kwa kuiua CCM ila kwa kutendea madhambi makubwa sisi Watanzania ambayo yataathiri hata watoto wetu na wajukuu zetu.
 
Hey members,
I believe in what most of jf members believe... I am here as new member joining the active and proactive community jf.
Thanks for accepting me and I promise to give my input for the wellbeing of the Jf community which is the Tanzania mirrow this time around.
 
Juzi nilikuwa na rafiki yangu mmoja ambaye anafanya kazi usalama wa taifa! tulikuwa tunabadilishana mawazo kuhusiana na uchaguzi wa mwaka huu, dakika za mwisho kabla ya kuachana nilifurahi nilipoona jamaa kakiri mbele yangu kwamba " Anatambua ya kuwa watu wengi wamepoteza matumaini na serikali iliyoko madarakani" na huo ndo ukweli!
 
Malaria sugu una lolote la kuchangia katika hili? nakupa nafasi ili walau wanaokulipa kwa kuanzisha thread mbalimbali ndani ya JF waone kwamba unafanya kazi kwa kuchangia na hii! hata kama ni upupu we lete tu .....tumeshakufahamu wewe na mtu mwenye akili za kiwango gani!
 
Sasa kwanini umtukane MS? Hayo uliyoandika yanafahamika kwa kila mtu, siyo usalama tu hata jeshini wanajua hali ya serikali ni mbaya.
 
Jamani watu wamechelewa sana kumchoka jk mimi mwezi wa kwanza tu tayali nilikuwa nipo hoi!
Mbeya ndo usiseme wamechoka kweli wamelazimishwa kupelekewa mbolea ya Minjingu imegoma, always wanatumia CAN but kwa sasa ipo juu sana hiyo mbolea toka 30,000 mpaka 120,000. Siyo mnakaamijini huko hata hamjui tabu anayopata mkulima! Tumechoka na jk.
 
JK ivi uko kuchokwa na wananchi anakufeel kweli?
Tatizo amekaaa na wapambe wanamlisha thumu
 
dakika za mwisho kabla ya kuachana nilifurahi nilipoona jamaa kakiri mbele yangu kwamba " Anatambua ya kuwa watu wengi wamepoteza matumaini na serikali iliyoko madarakani" na huo ndo ukweli!

Proverbs 16:9 for the gifts and calling of God are irrevocable
 
Jamani watu wamechelewa sana kumchoka jk mimi mwezi wa kwanza tu tayali nilikuwa nipo hoi!
Mbeya ndo usiseme wamechoka kweli wamelazimishwa kupelekewa mbolea ya Minjingu imegoma, always wanatumia CAN but kwa sasa ipo juu sana hiyo mbolea toka 30,000 mpaka 120,000. Siyo mnakaamijini huko hata hamjui tabu anayopata mkulima! Tumechoka na jk.

Hili ongezeko jamani wana uchumi mtatusaidia: 30,000 hadi 120,000 ? kweli tunawaletea wakulima Maisha bora?
 
Wakuu hamjasikia zile ahadi za jk? eti atajenga machinga comples 5! Hivi na ccm wamemchoka yuko peke yake anafikiriaa vitu vya ajabu! Machinga complex ndo vipaumbele vya watanzania! Haya ni maajabu ya karne. Pumba zimeanza kumwagika!
 
Malaria sugu una lolote la kuchangia katika hili? nakupa nafasi ili walau wanaokulipa kwa kuanzisha thread mbalimbali ndani ya JF waone kwamba unafanya kazi kwa kuchangia na hii! hata kama ni upupu we lete tu .....tumeshakufahamu wewe na mtu mwenye akili za kiwango gani!

"Kila kitu kimefanywa na wewe. Wee ndiye ulokutana na huyo rafiki yako. Wee ndiye unaotueleza kile alichosema rafiki. Baada ya kutueleza hivyo, ni juu yetu sie kuamini au kutoamini hayo ulotueleza. Huna haja ya kumlazisha mtu aamini kile ulichokisema wee pamoja na huyo rafiki yako. Na pia huna haja ya kumtukana mtu. Umetumia kipimo cha aina gani hata ukagundua kiwango cha akili alonacho malaria sugu????"
 
Wakuu hamjasikia zile ahadi za jk? eti atajenga machinga comples 5! Hivi na ccm wamemchoka yuko peke yake anafikiriaa vitu vya ajabu! Machinga complex ndo vipaumbele vya watanzania! Haya ni maajabu ya karne. Pumba zimeanza kumwagika!

kuna washauli wake wanamhalibia jamani mi naona kama siyo akili yake vile! na usisahau Reli toka tegeta mpaka posta, barabara za juu ameludia tena. WATAKAO MCHAGUA VILAZA SANA HAO BORA YA YEYE!
 
kuna washauli wake wanamhalibia jamani mi naona kama siyo akili yake vile! na usisahau Reli toka tegeta mpaka posta, barabara za juu ameludia tena. WATAKAO MCHAGUA VILAZA SANA HAO BORA YA YEYE!

Well noted Mkuu
 
wakuu hamjasikia zile ahadi za jk? Eti atajenga machinga comples 5! Hivi na ccm wamemchoka yuko peke yake anafikiriaa vitu vya ajabu! Machinga complex ndo vipaumbele vya watanzania! Haya ni maajabu ya karne. Pumba zimeanza kumwagika!

Aweke na lift maana kupanda hiyo machinga hadi ghorofa ya mwisho kununua bidhaa ni issue! Nilitembelea juzi nilichoka vibaya mno....
 
Wakuu juzi nilisikia kati ya ahadi zake kule Mlandizi ni kuwa amefanya mazungumzo na waisraeli kuja kulima nyanya kwenye bonde la mto RUVU.
1. Je hii inawezekana au ni ghiliba tu za mkulu ili apate kura?
2. Je anafahamu kuwa huo mto ni chanzo cha maji yanayotumika Bagamoyo, Dar na Kibaha na kwamba uwekezaji wowote mkubwa katika secta ya kilimo ungeathiri maisha ya watu wengi wanotegemea mto huo?
3. Je anafahamu madhar ya kimazingira yanayoambatana na matumizi ya viatilifu katika kilimo (kemikali)?
4. Je at what point of the river hicho kilimo kitafanyika?
5. Je kwa nini NAFCO walishindwa kuendesha mashamba yale ya zamani?
6. Je Kikwete anatumia ujinga wa ndugu zake kuwadanganya ili apate kura wakati akijua fika kuwa anawadanganya?
7. Je kwa style hii ya ngonjera za ahadi za kikwete tutafika?

Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom