Mimi ningekuwa mshauri wa Zitto ningemshauri kuhama si sulihisho la matatizo yake na hatapacha chama ambacho ataishi milele bila misukosuko.
Zitto wakati akishutumiwa kununuliwa na mafisadi wakati wa ajenda ya kununua mitambo ya Dowans nilikuwa mmoja ya watu niliyemkingia kifua saaana tukiwa kwenye mijadala mbalimbali kufikia hata wakati wa kuhitilafiana na mume wangu. Na kuanzia pale zto amekuwa haelewi eleweki ila kwa mambo yanavyoendelea sasa naanza kupata wasi wasi.
Kuhama anaweza ila ajue asitegemee kwamba umaarufu utaendelea kama ulivyo. Asipewe kichwa na wapambe wake wachache na wana CCM walio na lengo la kuibomoa chadema akajiona bila yeye CHADEMA itakufa.
Sasa hivi anawalaumu watu ndani ya chadema kwamba wanamtuhumu fisadi, ila ajue hata wananchi wengi wana wasiwasi na hilo kwa namna fulani na ilianza mara aliposimama kidete mitambi ya Dowans inunuliwe. Pale alianza kuharibu. Na ni wapiganaji ndani ya CCM ndio waliosimama kidete kulisimamisha hilo. Je wakati ule ni CHADEMA ilimtuma? Mpaka leo Zitto hajawahi kutoa maelezo ya kuturidhisha kuhusu msimamo wake wa kununua Dowans. Zitto kuwa makini na kila maamuzi unayochukua.
Kwa mtazamo wangu mimi, Ukihama CHADEMA utanidhihirishia kwamba kuna mikono ya mafisadi. Jua kwamba hatukupendi sababu wewe ni zitto tunapenda kazi unayoifanya ndania ya chadema. Ukihama unahama mwenyewe na si rahisi kupata kundi la kuhama nalo kama Mrema.
Utaenda wapi? CCM si shwari wanafukuzana, NCCR ndio wale wale karibu kinakufa, TLP haitaweza kukaa na Mrema, CUF, lWEKATARE KAKIMBIA.