Mods kama vp hii iunganishwe na hii https://www.jamiiforums.com/uzushi/46060-zitto-atembea-na-barua-ya-kujiuzulu-chadema.html hizi thread za Zitto na CHADEMA mpaka zinakera sasa
Mh. Zitto tuweke sawa Wafuasi wako.
Ha, mwananchi hawajipendi? Litabadilika kuwa rai mda si mrefu
Jamani nimeona article inayosema Zitto yuko mbioni kujiuzulu Chadema katika Mwananchi! Cha kushangazwa article hiyo wameitoa ghafla! Sasa najiuliza kulikoni?
Tuangalieni sana kwa makini juu ya tarifa hizi. Kwenye gazeti la mwanachi la leo kuna tarifa hizo za zito kujiuzuru. Lakini ukienda kwenye mtandao wao www.mwananchi.co.tz hakuna kitu kama hicho. Hii inaonyesha kuwa ni habari ya kupika. Halafu ukiisoma vizuri utaona kwamba Zitto aliwasiliana na mwananchi kwa barua pepe, lakini mwishoni wanasema zitto aliwapigia simu? Kipi kati ya hivyo ni sahihi? Na kwanini hiyo habari iliondolewa online kama inaukweli wowote?
Nadhani Mafisadi wameshajua kuwa Gazeti la Mtanzania halina soko tena na wala halina mashiko kwa WaTz. Bila shaka nyote mnakumbuka kabla ya uchaguzi wa CHADEMA, GAzeti la Mtanzania lilimuandama sana Dk Slaa kwa habari za ajabu na hata kumnukuu kuwa "Dk Slaa kutogombea Ukatibu Mkuu!" na hata kuweka kwenye MAoni yao ya Mhariri "Dk Slaa kwa Kutogombea Ukatibu Mkuu CHADEMA ni jambo la kuigwa!" HAbari za Slaa 'kutogombea' Ukatibu Mkuu ziliripotiwa mara kadhaa. Jambo la Ajabu ni kuwa KAtibu Mkuu wa CHADEMA ni nafasi ya kuteuliwa!
Kwa MAfisadi kugundua kuwa habari za kudhoofisha Upinzani kupitia Mgazeti yao wanayomilimki ya Mtanzania sasa wamehamishia nguvu hizo Mwananchi. Naweza kuona kuwa kwa habari hizo za MWananchi, gazeti hilo litapoteza credibility yake kwa Watanzania kama MAgazeti ya New Habari Corporation (Mtanzania, Rai, Dimba, The African)
Labda Mwananchi nao wameshauza baadhi ya Hisa kwa Mafisadi au Mafisadi wamemkabidhi Ali Mufuruki rungu la kupamabana na Wapinzani. Pia inawezekana lengo la Mafisadi ni kujaribu kutusahaulisha WaTz habari za Mafisadi na Ufisadi hapa TZ.
Watu ninyi mliowekeza kwa watu wengine mtakuwa mnakerwa sana kwa kila habari.
Jisimamieni, na mjiamini na sio kuwekeza kwa watu.
Mkama, ninajisimamia na najiamini. Ukisoma ile thread ya CHADEMA mambo mdundo nimechangia pale na kusema kuwa kuna tatizo katika Uongozi wa CHADEMA Taifa kwa kutoa marejeo tangu enzi ya Chacha Wangwe hadi kwa Kafulila. LAkini katika habari hii ya MWananchi naona kabisa ina walakini kubwa na ina mission yake kwa Wapinzani wa CCM. Hivi wewe Mkama unaamini kabisa kuwa hiyo habari ni kweli? Huyo MWandishi ameiona hiyo barua au ameona bahasha tu akaambiwa kuwa ndani kuna barua ya Zitto kujiuzulu CHADEMA?
Hata kama Zitto ataondoka CHADEMA bado hainifanyi niisaidiki hiyo habari ya MWananchi maana habari imekaa kiumbeya na hata wao Mwananchi hawajiamini kwa habari hiyo.