SoC02 Ili kupunguza ukosefu wa ajira, bodi ya mikopo itoe mikopo ya kujiajiri kwa wanachuo wahitimu wanaotaka kujiajiri

Stories of Change - 2022 Competition

FrankTitus

New Member
Dec 1, 2019
3
1
Hello wadau wa JF,

Nimekuja kuwashirikisha wazo ambalo likifanyiwa kazi linaweza likaleta mabadiliko makubwa kwa watanzania. Andiko langu limelenga katika sekta ya elimu kwa sababu ya imani yangu juu nchi yetu yenye Mali nyingi na wasomi wengi lakini tunaishi kimaskini.

Licha ya kwamba elimu yetu ni ya nadharia sana lakini bado naviamini vichwa vya wanachuo wetu, kichwani wana mawazo mazuri kuhusu kutengeneza Biashara, viwanda, na fursa mbalimbali za kujikwamua kimaisha lakini wanakosa misaada. Watu wanasema kwamba katika harakati za kutafuta mafanikio; fedha sio jambo la msingi sana, jambo la msingi ni WAZO LAKO na kulifanyia kazi WAZO HILO. Lakini amini amini nawaambieni, kinachokwamisha MAWAZO mengi yasifanye kazi ni FEDHA (MITAJI).

-Sio kwamba wahitimu hawataki kujiajiri, bali hawana mitaji.
-Sio kwamba wasomi wanashindwa kutumia elimu zao kujiajiri, bali hawana mitaji
-Sio kwamba vijana wanapenda umaskini, bali hawapati msaada wa kifedha ili waondoe umaskini kupitia MAWAZO yao.

EBU FIKIRIA;
-Kuna watu wanasomea ufundi Veta, halafu wakifika mtaani wanakosa kazi za kufanya.
-Mtu kasomea masoko na kozi ya Biashara, halafu akifika mtaani analia hakuna AJIRA.
-Wengine wamesomea uvuvi na viwanda, halafu wakifika mtaani wanageuka kuwa tegemezi kwa wazazi
-Wapo ambao wamesomea umeme, kwani ukisomea umeme ni lazma uajiriwe Tanesco?
-Ina maana mtu akisomea misitu ni lazma awe bwana misitu? Mtu akisomea kilimo ni lazma awe bwana shamba?

Wapo wanachuo ambao kijijini kwao wana mashamba ya kutosha, ila sasa wanajiuliza watapata wapi pesa za kuwalipa vibarua ili waweze kulima ekari 5? watapata wapi pesa za mbolea?. Wapo wanachuo wanaowaza kufuga samaki, ila wanajiuliza watapata wapi fedha za kuchimba mabwawa na kuingiza maji bwawani? Wapo wasomi ambao wanawaza kutengeneza magari na pikipiki, lakini wanawaza watapata wapi fedha za kununulia vifaa?

Elimu yetu inawasusa wanachuo wakajitafutie maisha yao wao mwenyewe. Ni kweli kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake, lakini kamba zingine ni fupi sana kiasi kwamba hazifiki sehemu yenye chakula. Ebu tujiulize kwa mwaka nchi inatoa wahitimu wangapi wa uhasibu? Na je inaajiri wahasibu wangapi?..... Nchi inatoa wahitimu million 1 alafu inaajiri wahitimu elfu 1, hao waliobaki 999,000 wataenda wapi? Mnawaacha wapambane na hali zao mwisho wa siku panya road wanaongezeka, machangudoa wanajazana, na wavuta unga wanatapakaa kila kona!!

Ebu fikiria, serikali inatoa mikopo na boom kwa wanachuo ambao wanategemea kulipa mikopo hiyo endapo wataajiriwa. Ubaya ni kwamba nchi yetu haina uwezo wa kuajiri wasomi wengi, hivyo basi wasomi wote wasioajiriwa wanabaki kuwa WADAIWA SUGU WA BODI YA MIKOPO.
Kumbukeni kuwa bodi hii ya mikopo ni taasisi ambayo haitaki kukopesha kwa hasara, hivyo basi kila siku bodi inapiga kelele ikiimiza wadaiwa walipe madeni. Nao wadaiwa wanashindwa kulipa kwa sababu hawana kazi, pia hawana AJIRA zozote. Mwisho wa siku bodi ya mikopo inawashauri wahitimu wa chuo wasio na ajira- WAJIAJIRI WAO WENYEWE ili waweze kulipa mikopo yao.

SASA WAZO LANGU NI KWAMBA, KAMA SERIKALI INAWEZA KUTOA MIKOPO YA ADA NA BOOM (MIKOPO AMBAYO HAIZALISHI), KWANINI SERIKALI HIYO HIYO ISHINDWE KUTOA MIKOPO INAYOZALISHA KWA WANACHUO WAHITIMU AMBAO WAKO TAYARI KUJIAJIRI?

Nchi hii ina miradi mingapi ambayo haifanyiwi kazi? Kwanini msiwatumie wahitimu kufanikisha miradi huyo?. Nchi hii ina viwanda vingapi ambavyo vinakufa, kwanini msiwatumie wanachuo kufufua na kuendeleza viwanda hivyo?... Narudia tena, wanachuo wetu wana mawazo mazuri kichwani ila hawajui wayapeleke wapi. Na inawezekana hata wao wenyewe hawapendi sana kuajiriwa, ila sasa watafanyaje kama hawana pesa za kujiajiri?

VIGEZO VYA KUKOPA VIWE KAMA IFUATAVYO; Muhitimu aombe mkopo kwa kutumia MPANGO KAZI WA BIASHARA (BUSINESS PLAN) ambao utaeleza atafanya Biashara gani, soko lake ni lipi, mtaji kiasi gani, mapato yatakuaje na kadhalika.

Au Wahitimu wenye mawazo ya project waandae project zao, waorodheshe mahitaji na gharama, waeleze namna ambavyo project itarudisha fedha. Pia kama kuna vikundi vya ujasiriamali navyo viandae maombi yao kama nilivyoeleza.

Mimi naamini kuwa msomi ndiye mtu anayepaswa kuanzisha kiwanda kisha aajiri vijana wa mtaani. Kama wanachuo watakopa ili wafanye Biashara basi itakuwa rahisi kwao kulipa mikopo hiyo, kutengeneza vipato vyao, kuendeleza elimu zao, kuondoa au kupunguza idadi ya watu wasio na ajira, kulipa kodi na kuchangia pato la taifa, kusaidia maendeleo ya nchi.

ILI JAMBO LIFANIKIWE KWA USAHIHI, BODI INATAKIWA IFANYE YAFUATAYO;
-Kutengeza kamati maalumu ambayo itasimamia mchezo mzima kuanzia kipindi cha kuomba mikopo, kuanzisha biashara, kusimamia na kuendeleza biashara za wahitimu, kusimamia marejesho ya mikopo.
-Bodi inaweza ikashirikiana na taasisi zingine za fedha kama vile benki.

HITIMISHO:
Umaskini wetu unatokana na matumizi mabaya ya elimu yetu, kiukweli kabisa wasomi wengi hawazitendei haki elimu zao. Ebu tujiulize; Kama elimu ni mkombozi wa umaskini, sasa kwanini nchi yetu ina wasomi wengi lakini ni maskini? Au wasomi wetu hawana elimu?...

Bila shaka elimu wanazo ila hazitumiki. Pia katika kuboresha zaidi; Napendekeza elimu yetu ilenge sana katika mafunzo ya vitendo ili kutoa wahitimu waliokamilika. Mafunzo hayo ya vitendo yatasaidia wahitimu wapate mawazo mazuri katika kuanzisha Biashara au miradi. Pia sio lazima mikopo hiyo ya kujiajiri itolewe kwa kila muhitimu, bali kuwe na vigezo na masharti ambayo yataangalia Wazo bora, makazi ya kudumu ya mwombaji, na kadhalika.
 
Lakini kaka, Kama serikali wamekupatia mkopo umesoma umemaliza elimu ya chuo
Ni muhimu sana tena wakupe MTAJI?
Inawezekana kwa sababu serikali ina fedha, ni suala la kuamua tu katika hali ya kuwawezesha wahitimu wasiende kupoteana mtaani.

Ukisoma maelezo yote vzr kuna sehem nimeandika kwamba wanaweza wakashirikiana na taasisi zngne za fedha, kwa mfano benki. Wafinance mawazo ya kibiashara ya wahitimu wanaotaka kujiajiri.

Pia mikopo hiyo iendeshwe kibiashara zaidi. Yaani ni kama mtu anavyoenda kukopa benk ili aanzishe Biashara

Mikopo ya ada na boom inatolewa kwa watu weng lakn hawailipi, hawalipi kwa sababu mikopo hiyo huwa inaishia pale pale chuoni, mikopo hiyo ni kama pesa za matumizi tu (mikopo isiyozalisha pesa)

Mkopo wa kujiajiri utamsaidia muhitimu aanzishe Biashara yake, kisha ataanza kurudisha mkopo taratibu
 
Hello wadau wa JF,

Nimekuja kuwashirikisha wazo ambalo likifanyiwa kazi linaweza likaleta mabadiliko makubwa kwa watanzania. Andiko langu limelenga katika sekta ya elimu kwa sababu ya imani yangu juu nchi yetu yenye Mali nyingi na wasomi wengi lakini tunaishi kimaskini.

Licha ya kwamba elimu yetu ni ya nadharia sana lakini bado naviamini vichwa vya wanachuo wetu, kichwani wana mawazo mazuri kuhusu kutengeneza Biashara, viwanda, na fursa mbalimbali za kujikwamua kimaisha lakini wanakosa misaada. Watu wanasema kwamba katika harakati za kutafuta mafanikio; fedha sio jambo la msingi sana, jambo la msingi ni WAZO LAKO na kulifanyia kazi WAZO HILO. Lakini amini amini nawaambieni, kinachokwamisha MAWAZO mengi yasifanye kazi ni FEDHA (MITAJI).

-Sio kwamba wahitimu hawataki kujiajiri, bali hawana mitaji.
-Sio kwamba wasomi wanashindwa kutumia elimu zao kujiajiri, bali hawana mitaji
-Sio kwamba vijana wanapenda umaskini, bali hawapati msaada wa kifedha ili waondoe umaskini kupitia MAWAZO yao.

EBU FIKIRIA;
-Kuna watu wanasomea ufundi Veta, halafu wakifika mtaani wanakosa kazi za kufanya.
-Mtu kasomea masoko na kozi ya Biashara, halafu akifika mtaani analia hakuna AJIRA.
-Wengine wamesomea uvuvi na viwanda, halafu wakifika mtaani wanageuka kuwa tegemezi kwa wazazi
-Wapo ambao wamesomea umeme, kwani ukisomea umeme ni lazma uajiriwe Tanesco?
-Ina maana mtu akisomea misitu ni lazma awe bwana misitu? Mtu akisomea kilimo ni lazma awe bwana shamba?

Wapo wanachuo ambao kijijini kwao wana mashamba ya kutosha, ila sasa wanajiuliza watapata wapi pesa za kuwalipa vibarua ili waweze kulima ekari 5? watapata wapi pesa za mbolea?. Wapo wanachuo wanaowaza kufuga samaki, ila wanajiuliza watapata wapi fedha za kuchimba mabwawa na kuingiza maji bwawani? Wapo wasomi ambao wanawaza kutengeneza magari na pikipiki, lakini wanawaza watapata wapi fedha za kununulia vifaa?

Elimu yetu inawasusa wanachuo wakajitafutie maisha yao wao mwenyewe. Ni kweli kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake, lakini kamba zingine ni fupi sana kiasi kwamba hazifiki sehemu yenye chakula. Ebu tujiulize kwa mwaka nchi inatoa wahitimu wangapi wa uhasibu? Na je inaajiri wahasibu wangapi?..... Nchi inatoa wahitimu million 1 alafu inaajiri wahitimu elfu 1, hao waliobaki 999,000 wataenda wapi? Mnawaacha wapambane na hali zao mwisho wa siku panya road wanaongezeka, machangudoa wanajazana, na wavuta unga wanatapakaa kila kona!!

Ebu fikiria, serikali inatoa mikopo na boom kwa wanachuo ambao wanategemea kulipa mikopo hiyo endapo wataajiriwa. Ubaya ni kwamba nchi yetu haina uwezo wa kuajiri wasomi wengi, hivyo basi wasomi wote wasioajiriwa wanabaki kuwa WADAIWA SUGU WA BODI YA MIKOPO.
Kumbukeni kuwa bodi hii ya mikopo ni taasisi ambayo haitaki kukopesha kwa hasara, hivyo basi kila siku bodi inapiga kelele ikiimiza wadaiwa walipe madeni. Nao wadaiwa wanashindwa kulipa kwa sababu hawana kazi, pia hawana AJIRA zozote. Mwisho wa siku bodi ya mikopo inawashauri wahitimu wa chuo wasio na ajira- WAJIAJIRI WAO WENYEWE ili waweze kulipa mikopo yao.

SASA WAZO LANGU NI KWAMBA, KAMA SERIKALI INAWEZA KUTOA MIKOPO YA ADA NA BOOM (MIKOPO AMBAYO HAIZALISHI), KWANINI SERIKALI HIYO HIYO ISHINDWE KUTOA MIKOPO INAYOZALISHA KWA WANACHUO WAHITIMU AMBAO WAKO TAYARI KUJIAJIRI?

Nchi hii ina miradi mingapi ambayo haifanyiwi kazi? Kwanini msiwatumie wahitimu kufanikisha miradi huyo?. Nchi hii ina viwanda vingapi ambavyo vinakufa, kwanini msiwatumie wanachuo kufufua na kuendeleza viwanda hivyo?... Narudia tena, wanachuo wetu wana mawazo mazuri kichwani ila hawajui wayapeleke wapi. Na inawezekana hata wao wenyewe hawapendi sana kuajiriwa, ila sasa watafanyaje kama hawana pesa za kujiajiri?

VIGEZO VYA KUKOPA VIWE KAMA IFUATAVYO; Muhitimu aombe mkopo kwa kutumia MPANGO KAZI WA BIASHARA (BUSINESS PLAN) ambao utaeleza atafanya Biashara gani, soko lake ni lipi, mtaji kiasi gani, mapato yatakuaje na kadhalika.

Au Wahitimu wenye mawazo ya project waandae project zao, waorodheshe mahitaji na gharama, waeleze namna ambavyo project itarudisha fedha. Pia kama kuna vikundi vya ujasiriamali navyo viandae maombi yao kama nilivyoeleza.

Mimi naamini kuwa msomi ndiye mtu anayepaswa kuanzisha kiwanda kisha aajiri vijana wa mtaani. Kama wanachuo watakopa ili wafanye Biashara basi itakuwa rahisi kwao kulipa mikopo hiyo, kutengeneza vipato vyao, kuendeleza elimu zao, kuondoa au kupunguza idadi ya watu wasio na ajira, kulipa kodi na kuchangia pato la taifa, kusaidia maendeleo ya nchi.

ILI JAMBO LIFANIKIWE KWA USAHIHI, BODI INATAKIWA IFANYE YAFUATAYO;
-Kutengeza kamati maalumu ambayo itasimamia mchezo mzima kuanzia kipindi cha kuomba mikopo, kuanzisha biashara, kusimamia na kuendeleza biashara za wahitimu, kusimamia marejesho ya mikopo.
-Bodi inaweza ikashirikiana na taasisi zingine za fedha kama vile benki.

HITIMISHO:
Umaskini wetu unatokana na matumizi mabaya ya elimu yetu, kiukweli kabisa wasomi wengi hawazitendei haki elimu zao. Ebu tujiulize; Kama elimu ni mkombozi wa umaskini, sasa kwanini nchi yetu ina wasomi wengi lakini ni maskini? Au wasomi wetu hawana elimu?...

Bila shaka elimu wanazo ila hazitumiki. Pia katika kuboresha zaidi; Napendekeza elimu yetu ilenge sana katika mafunzo ya vitendo ili kutoa wahitimu waliokamilika. Mafunzo hayo ya vitendo yatasaidia wahitimu wapate mawazo mazuri katika kuanzisha Biashara au miradi. Pia sio lazima mikopo hiyo ya kujiajiri itolewe kwa kila muhitimu, bali kuwe na vigezo na masharti ambayo yataangalia Wazo bora, makazi ya kudumu ya mwombaji, na kadhalika.
Shukrani
Ila kipindi unasoma serikali ilikusaidia mkopo tena wengine asilimia 100 unatak useme zile fedha unafanyia nini ?? Umeshindwa kuwekeza hata buku buku ukaja kutumia kama mtaji wako ??? Sio kila kitu kutegemea serikali kuna shughuli nyingine hazihitaji hata milioni ili ufanikiwe basi tu ni uwezo finyu wa vijana kufikiria.... tusilaumu serikali wakupe mkopo af tena waje kukupa mtaji 😂 how come..
 
Back
Top Bottom