Ikiwezekana, Bunge lianze na mswada wa dharura kujadili Katiba Mpya; hii Katiba ya sasa kitendo cha Makamu kutambuliwa kuwa mrithi ni hatari

Mi naangalia tu hizi senema.
Eti muheshimiwa rais Samia Suluhu tafadhalini jamani.
Majaliwa angetosha vizuri tu hapo.
 
Binafsi napendekeza hiyo nafasi ya makamu ifutwe kabisa, in case of any emergency judge mkuu au spika anashika nchi kwa siku chache then tunarudi kwenye uchaguzi.
 
Ni kweli hao hawapo, ila kupendekeza mkuu wa majeshi kuwa miongoni kati ya watu ambao wanaweza kushika nafasi ya Urais endapo yule aliyeko madarakani atakuwa hayupo kwa sababu zozote ikiwemo kifo sio sahihi maana ya yeye anaweza kushikwa na tamaa ya madaraka akaamua kumfitini aliyeko madarakani kwa njia za siri au kufanya uasi. Kwa hiyo Makamu wa Risi na Jaji mkuu ni sahihi kutokana na kuwa tayari wanafanya majukumu ya kitaifa; kasoro moja ni kwa Jaji mkuu kumtumia kuongoza/kutawala nchi kwenye mambo ya kisiasa.
Hahahah haya mambo haya 😂😂😂 niliwahi kusikia Mwamunyange alitolewa kwenye cheo mana alikuwa mfuasi wa babu wa Monduli, ila kuhusu tamaa mm nadhan yeyote anaweza kuwa na tamaa bila kuangalia cheo chake mfano kipindi cha Nyerere kuvamia Uganda ili kumtoa idd amini hvy kisheria n Uganda ilikuwa chini ya Tz lakin hatukuonyesha tamaa hizo 🤔🤔🤔
 
Acha utabiri wa tunguli
Acha roho ya husda.
Katiba siku zote ilikuwepo na mlikuwa mnaiona kwanini hamkuleta hiyo mada?
Samia kaukapata udambwi udambwi mnaanza kuteseka
Uraisi wa kuangukia sio?! Lakini wazo langu ni kumlinda Rais dhidi ya fitna na hila. Makamu angekuwa Rais wa mpito tukingoja uchaguzi mwingine na ikiwezekana na yeye ashiriki.
 
Watu wanaweza wasikuelewe hapa au hata usieleweke Kwao upesi ila umekuja si tu na Hoja nzuri na Muhimu lakini pia kuna Fumbo umelifumba hapa hasa kutokana na Tetesi za chini chini kuwa kuna Kundi fulani lenye Sifa ya Umafia na pia lina Pesa limecheza Mchezo wote Kiufundi kabisa na Mission ya Siku nyingi imekuwa Accomplished.

Nakubaliana nawe 100% juu ya Hoja yako Ndugu ili tuepuke Misiba mingine isiyo ya Kilazima huko mbeleni. Na hata aliyeshika hatamu sasa namshauri awe Makini kuliko wakati wowote kwani hata wanaomzunguka sasa wana Ubobezi mkubwa tu wa Kimafia na Wanajulikana kutokana na Washirika wao.
Hofu inatoka wapi?
je unakumbuka hili neno na nafasi ya uMakamu ilileta maloloso sana wakati wa Vyama vingi, na hasa kutokuelewana na ndipo wakamtoa Rais atokaye Zanzibar asiwe Makamu kwani ingeleta matatizo km hivi leo. Tulivyoungana na Zanzibar Mh Karume alikuwa Makamu na angekuwa hai kabla ya Mh J Nyerere ingebidi aje atawale mpaka huku.

Mtego huu umemkuta Mh Mama Samia naona sasa waZanzibar watanyamaza mambo ya muungano kwani wapo wengi sasa hapo juu, Hussein Mwinyi na makamu Mwanasheria Othman, je watauvunja Muungano

MY TAKE ikionekana km kuna njama imefanyika kumtoa Rais ili Makamu achukue mara moja haitakubalika kwani kuna TISS na UWT
 
Uraisi wa kuangukia sio?! Lakini wazo langu ni kumlinda Rais dhidi ya fitna na hila. Makamu angekuwa Rais wa mpito tukingoja uchaguzi mwingine na ikiwezekana na yeye ashiriki.
Katiba imeandikwa kabla hujazaliwa hakuna kitu kimetokea leo dola kashika Mwanamke wa shoka mnaanza ufukunyuku,
Poleni sana ngoma ndio kwaaanza inaanza.
 
Uraisi wa kuangukia sio?! Lakini wazo langu ni kumlinda Rais dhidi ya fitna na hila. Makamu angekuwa Rais wa mpito tukingoja uchaguzi mwingine na ikiwezekana na yeye ashiriki.
Muache amepata ubwete
Yule mwanachama mwenzetu wa Uwabata ale kuku kwa mrija
 
Hicho kipengele cha katiba ni kama kimewatenga wananchi ambao kimsingi ndio wenye jukumu la kuwaweka viongozi.

Halafu mbaya zaidi huyo Rais anayekuja anakuwa na mamlaka ya kuunda upya Baraza lake la mawaziri, na kuwateua wote, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wapya kama akipenda kufanya hivyo.
Kinawatenga vipi wananchi ilhali kura wanapigiwa wote-Rais na Makamu wa Rais. Au ndio ile mnapiga kura kama unaaccept terms and conditions kwenye Internet!
 
Hata mtu aliye nje ya mfumo wa utawala anaweza kumdhuru Rais aliye madarakani ama kwa nia ya moja kwa moja au kupitia wasaidizi wa Rais.

Nia yako ni kwamba pindi nafasi ya Urais inapokuwa wazi kwa sababu zozote ikiwemo kifo unataka uchaguzi mpya uitishwe.

Sio kweli kwamba hilo wazo lako halikuwemo kwenye moja ya uwezekano wa kuwekwa kwenye katiba lakini hatimaye kifungu kilicho salama zaidi ndicho kilichowekwa kuepusha mambo mengi oambayo yangesababisha matumizi ya gharama, vurugu, kukosa utulivu.

Sijui umewaza nini mpaka kufuikia hatua ya kutoa pendekezo hilo finye ambalo halijafikiria hasara na faida kisha ukaziweka kwenye mizania.

Wanasiasa ndio mnamatamanio ya kutaka uchaguzi ufanyike ili mpate manufaa yenu binafsi na sio wananchi. Una wasiwasi gani makamu wa Rais kuchukua nafasi hiyo ya juu kabisa ya utawala wa nchi?

Ninahisi ana maoni kwamba,mara nyingi kwenye uchaguzi mkuu huwa tunampigia kura Rais,mgombea mwenza wake mara nyingi huwa hawaumizi watu vichwa kwa kuwa wanaamini atafanya kazi chini ya Rais aliepigiwa kura...mawazo yake nilivoyasoma ni kuwa huyu makamu anakuwa Rais gafla wakati watu kisaikolojia hawakujishugulisha na kujua sifa zake wakati anagombea na Rais,kwa hiyo mtoa mada anahisi tunapata Rais ambae hatukumchagua

maoni yangu mimi...huo utaratibu wa kikatiba unaousemea wewe,watunga katiba hii ni kama walikuwa wanawaza kuwa hata Rais ikitokea akafariki,hawezi kufariki mwanzoni mwa mhula namna hii, waliamini Rais lazima avute vuteee ikiwezekana walau hata miezi michache kabla ya mhula wake kuisha ndiyo anaweza kufa, kwetu limetokea mwanzoni kabisaaa, ni mhula mzima wa miaka mitano
 
Dogo nilivuka umasikini miaka 22 iliyopita, na unaweza kupata aibu ukikutana na mimi macho kwa macho. Mimi ndio mmoja wa wenye mawazo huru kwa kuwa sitegemei maoni yangu yanipe chakula. Riziki ya kula, kusaza na ya kugawa ipo tuu, na mimi ni mdingi ki umri dogo.

Na mimi sio lazima niende Kolomije nisiko kujua, Usangi au Lyamungo Sinde kunanitosha. Muulize mwenyekiti wako kuhusu mimi atakuhabarisha.
Acha mikwara mbuzi wewe. Amwulize vipi mwenyekiti wake wakati unatumia fake ID?
 
Dogo nilivuka umasikini miaka 22 iliyopita, na unaweza kupata aibu ukikutana na mimi macho kwa macho. Mimi ndio mmoja wa wenye mawazo huru kwa kuwa sitegemei maoni yangu yanipe chakula. Riziki ya kula, kusaza na ya kugawa ipo tuu, na mimi ni mdingi ki umri dogo.

Na mimi sio lazima niende Kolomije nisiko kujua, Usangi au Lyamungo Sinde kunanitosha. Muulize mwenyekiti wako kuhusu mimi atakuhabarisha.
Hata ukishindia kashata na maji ya kandoro unaweza kulidhika vilevile.

Njaaa inakutafuna
 
Watu wanaweza wasikuelewe hapa au hata usieleweke Kwao upesi ila umekuja si tu na Hoja nzuri na Muhimu lakini pia kuna Fumbo umelifumba hapa hasa kutokana na Tetesi za chini chini kuwa kuna Kundi fulani lenye Sifa ya Umafia na pia lina Pesa limecheza Mchezo wote Kiufundi kabisa na Mission ya Siku nyingi imekuwa Accomplished.

Nakubaliana nawe 100% juu ya Hoja yako Ndugu ili tuepuke Misiba mingine isiyo ya Kilazima huko mbeleni. Na hata aliyeshika hatamu sasa namshauri awe Makini kuliko wakati wowote kwani hata wanaomzunguka sasa wana Ubobezi mkubwa tu wa Kimafia na Wanajulikana kutokana na Washirika wao.
Hofu inatoka wapi?
je unakumbuka hili neno na nafasi ya uMakamu ilileta maloloso sana wakati wa Vyama vingi, na hasa kutokuelewana na ndipo wakamtoa Rais atokaye Zanzibar asiwe Makamu kwani ingeleta matatizo km hivi leo.

Tulivyoungana na Zanzibar Mh Karume alikuwa Makamu na angekuwa hai kabla ya Mh J Nyerere ingebidi aje atawale mpaka huku.

Mtego huu umemkuta Mh Mama Samia naona sasa waZanzibar watanyamaza mambo ya muungano kwani wapo wengi sasa hapo juu, Hussein Mwinyi na makamu Mwanasheria Othman, je watauvunja Muungano.

MY TAKE ikionekana km kuna njama imefanyika kumtoa Rais ili Makamu achukue mara moja haitakubalika kwani kuna TISS na UWT
 
Ni ngumu sana kuelewa maana ya sheria hii. Kama cheo cha juu kama Makamu wa Rais kinaweza kuwa cha uteuzi tu, inakuwaje chaguzi zirudiwe kwa nafasi za chini kama udiwani na ubunge??

Kama chama kinaweza kupewa jukumu la kuteua makamu wa Rais wa nchi - basi chama hicho pia kinaweza kuteua mbunge na diwani!

Tuache kuchezea fedha zinazopatikana kwa jasho kwa kufanya chaguzi za marudio kwa madiwani na wabunge, sawa na tulivokwenda kufanya uchaguzi mpya wa Rais!! Kama hili linakataliwa hasa na CCM, basi lengo lilikuwa ni kuweka mazingira ya kuwa na udhibiti wa Bunge na wabunge na halmashauri. Nia hii ni ovu na kifo cha JPM kimefungua fikra!!
 
Back
Top Bottom