Ikiwezekana, Bunge lianze na mswada wa dharura kujadili Katiba Mpya; hii Katiba ya sasa kitendo cha Makamu kutambuliwa kuwa mrithi ni hatari

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,397
Suala la katiba lipewe kipaumbele sana.

Katiba ni uhai.

Yapo mengi ya hatari sana kwenye katiba hii.

Lakini hili la Mrithi wa rais anayefariki dunia, kuwa ni makamu wa rais (automated) ni hatari sana kwa marais endapo tukipata Makamu asiyemwaminifu.

Pia linachangia sana kumuweka mbali makamu wa rais kuwa karibu na rais kwa hofu ya kutoaminia! (Naturally internal conflict)

Kwa gharama yoyote naomba tuanze na katiba inafaida kwetu sote matajiri na masikini, viongozi na watawaliwa.
 
Suala la katiba lipewe kipaumbele sana!
Katiba ni uhai!
Yapo mengi ya hatari sana kwenye katiba hii!
Lakini hili la Mrithi wa rais anayefariki dunia, kuwa ni makamu wa rais (automated) ni hatari sana kwa marais endapo tukipata Makamu asiyemwaminifu!
Hii ni lesson kubwa sana kwa wahusika. Next time pick ya VP iwe inafanyika kwa umakini mkubwa mno bila mihemuko maana huyu ni Rais in waiting.

Imagine sasa hivi. Tuna mama mpaka 2025, potentially mpaka 2030.
 
Kuubadilisha katiba ya nchi ni wazi zuri Ila itachukua muda mwingi Sana kukusanya maoni na kuitunga.

Tuanze na katiba ya chama, katiba iondoe ukomo wa mwenyekiti, Kuna wenyeviti ving'ang'anizi sana. Kaanza uenyekiti toka raisi mkapa, akaja kikwete, akaja magu, na Sasa Samia. Aah sio demokrasia hiyo
 
Suala la katiba lipewe kipaumbele sana!
Katiba ni uhai!
Yapo mengi ya hatari sana kwenye katiba hii!
Lakini hili la Mrithi wa rais anayefariki dunia, kuwa ni makamu wa rais (automated) ni hatari sana kwa marais endapo tukipata Makamu asiyemwaminifu!
Pia linachangia sana kumuweka mbali makamu wa rais kuwa karibu na rais kwa hofu ya kutoaminia! (Naturally internal conflict)

Kwa gharama yoyote naomba tuanze na katiba inafaida kwetu sote matajiri na masikini, viongozi na watawaliwa!
 
Kuubadilisha katiba ya nchi ni wazi zuri Ila itachukua muda mwingi Sana kukusanya maoni na kuitunga.
Tuanze na katiba ya chama, katiba iondoe ukomo wa mwenyekiti, Kuna wenyeviti ving'ang'anizi sana.
Kaanza uenyekiti toka raisi mkapa, akaja kikwete, akaja magu, na Sasa Samia. Aah sio demokrasia hiyo
Maoni yapo tayali, na samia alikuwa mjumbe wa bunge la katiba! Hakuna kinachoshindikana
 
Kunaweza wekwa hata utaratibu mwingine wa bunge kuprndekeza jina la mrithi anaweza malizia miaka iliyosalia!
Lakini hiyo ya automatic kuwa makamu awe rais ni hatari mno
Ww unawasiwasi na kuuwawa na raisi kwa njama za makamu wake si ndio?
 
Namna nyingine ya kupata mrithi bora ikijitokeza dharura kama ya sasa ni kuhakikisha mgombea urais na mgombea mwenza wote wanaweza kuimudu vema nafasi ya urais.
 
IMG-20210318-WA0000.jpg
 
Kwamba una wasiwasi na SAMIA si ndio! Kwamba humuamini SAMIA si ndio!
Kwahiyo ulikua na VP ambae huamini katika uwezo wake wa kuongoza si ndio!




URAIS ni taasisi ... Nahisi kuna watu wana chuki tu na huyu Mama
 
Suala la mabadiliko ya katiba limesemwa Sana na nadhani wajuvi wa sheria na katiba wanaweza kueleza sana maana huu ndo uga wao.

Binafsi katika marekebisho ya katiba ninayoyaona, baada ya kufariki Rais aliyeko madarakani, makamu wa Rais, awe kaimu Rais ndani ya muda utakaopendekezwa Ili baada ya hapo uchaguzi mpya wa Rais ufanyike.

Nchi nyingine kwa mfano Kaimu Rais ambaye obvious anakuwa ni makamu wa Rais anaweza kukaimu kwa muda wa miezi mitatu na wengine sita Ili kupisha uchaguzi mpya wa Rais.

Kuna mantic hapo. Maana ukweli wenyewe ukisemwa, watu huwa hawamchagui makamu wa Rais katika uchaguzi.
Uhalisia unaonyesha kwamba makamu wa Rais huwa tu amabebwa na mgombea urais. Hata sababu za kimantic zinaonyesha, ndo maana huitwa mgombea mwenza. Huyu huwa ni chaguo la pili kwa umaarufu kwa hiyo kumfanya awe Rais moja kwa moja huondoa imani kwa wananchi, niseme wengi kwa sababu huwa anaonekana ni second selection.

Lakini Jambo jingine ni uwezo. Tunaweza tisilione hili,lakini ukweli ni kwamba second selection mahali popote ina percentage za upungufu ktk Jambo lolote. Hivyo kumuacha awe Rais moja kwa moja kuna hatari ya kuwa na mtu asiye na uwezo wa kuongoza maana nafasi aliyokuwa nayo kama mgombea mwenza kwa wengi huwa ni ya dhuru nini maana wao nguvu kubwa huwekeza kwa mgombea Urais.

Hivyo napendekeza mabadiliko ya katiba Ili baada ya Rais kufa au kushindwa kufanya kazi zake kea sababu nyingine yoyote, makamu asiwe Rais moja kwa moja bali kuwa na uchaguzi mwingine wa kumchagua Rais.

Lakini hatari kubwa ni huyu mrithi kukosa kile kinachoitwa power of legitimacy. Najua makamu huchagiliwa kwa tiketi moja na Rais, lakini kama nilivyosema hapo juu, watu humchagua Rais hasa na makamu huwa ni suala la " pitisha tu".
Let us think on this.
 
Katiba mpya ilitakiwa iwe imepatikana, ila rais huyu marehemu yeye na kundi lake akiwemo huyu mama makamo wa rais ndio waliihujumu.

Rais Magufuli yeye alivuka mipaka mpaka kusema katiba mpya sio ajenda yake akiamini yeye ndio nchi, na katiba ni suala la utashi wake! Acha aongoze huyu mama mwenye uwezo mdogo, ili kila mtu ajue katiba ni zaidi ya madaraka ya urais yanayotumika vibaya.
 
Mafeminist watakuparua, watakunyandua, watakushupalia kua umeona mwanamke mwenzao hawezi ?!

Hoja yako inaeleweka wazi sio jinsia ila mafeminist hawatatambua hilo
 
Back
Top Bottom