Igunga OFFICIAL Results: Dr. Kafumu atangazwa mshindi

Igunga OFFICIAL Results: Dr. Kafumu atangazwa mshindi

We will issue an official statement soon this evening .

Tutaeleza nini kilitokea na nini kimefanyika na nini muelekeo wetu na nini kitafanyika .
Can't wait to learn what has happened because sequence of events does not add up to the results.
 
Mkuu wangu unafikiri mimi napinga hilo...sipingi hata kidogo na nadhani ndio ilikuwa kazi yangu kubwa sana hapa JF kujaribu kuwaunganisha wananchi tuondoe tofauti zetu za dini.

Nachopinga mimi kuhusiana na Chadema ni pale mnapodai Chadema walifanya hivyo, hii si kweli isipokuwa wapo watu walitumiwa na CCM kueleneza Udini na hata hao Mapadre hawakufanya hivyo kwa sababu waliipenda Chadema au Dr.Slaa isipokuwa walitumiwa na CCM kuleta mgawanyiko huo. Hata wakati wa Ukoloni mkoloni hakuingia Makanisani bali MaPadre wetu na ndio waliifanya kazi hiyo kwa niaba kama Bakwata wanavyofanya leo. hawa wote ni mamluki wanaopewa fedha kusambaza udini na Mungu awalaani wote!

Na ndio maana nawataka nyie wananchi mfahamu tofauti zetu haziwezi kuleta mafanikio yoyote isipokuwa UMOJA wenu na kutambua mbinu chafu zinazoenezwa. Lakini kwa bahati mbaya wengi wetu bado hawajafahamu kwamba chombo kinachokukwaza sii imani ya mtu wala JK kuwa rais bali ni system nzima imejengwa ili tuendelee kutawaliwa. JK is as bad as Mwinyi na Mkapa..

Kwa hiyo sii kazi ya Chadema wala CUF kutambua hitilafu hizi, bali ni sisi wenyewe wananchi kupingana na vyombo hivi vya dini vinapoingilia maswala ya kisiasa na sisi wenyewe kutambua na kujiepusha kabisa na maswala yoyote yanayohusiana na tofauti zetu za kiimani na tuelekeze nguvu zetu kutafuta haki na maendeleo yetu. Watawala wakishindwa kutugawa hatutatawalika!

N.B Habari mpya niloipata sasa hivi nasikia Ofisi ya Chadema huko Igunga imevamiwa na Mapolisi wamerusha mabomu ya machozi kuwasambaza wanaChadema waliokusanyika kuwasikiliza viongozi wao. Igunga nzima sasa hivi ni vurugu tupu!...

Kaka nimekuelewa, ingawa ni vigumu sana kukubali kwamba kampeni za kanisani ilikuwa mpango wa CCM kutugawa. Haiyumkini, nakubali kwamba mtazamo wako pia una ushawishi mpana. Mimi binafsi nimekaa sana vijiwe vya waislamu, na waislamu wengi sana ambao nimeongea nao wana imani kwamba Chadema ni chama cha kidini. Chadema wenyewe hawajisaidii katika hili, wanachama wao wanakosa staha ndogo ndogo tu. Huwezi kumkwida mama yule wa Igunga. CCM wanaweza kuwa wanapandikiza udini, lakini Chadema vitendo vyao vinawatuhumu wenyewe. Ukiingia humu jamvini, huwezi kukosa kejeli kuhusu Madrasa au Bakwata, vitendo kama hivi vinawafukuza waislam Chadema.

Nitakwambia hoja nyingine ya Waislam wa mtaani. Wao wanasema hivi huyu Dr.Slaa alikuwa wapi kipindi cha Mkapa? Wakati Mkapa alikuwa anakula hela hadi kajiuzia mwenyewe mali za serikali? Mbona wanapiga kelele wakati wa Kikwete, ilhali Jakaya mwenyewe hajawahi kuhusishwa na kashfa hata moja? Huu lazima utakuwa mkakati wa kanisa. Halafu wanaona chama kama Christian Democratic Party kinawasomesha vijana wa Chadema. Hoja yangu ni kwamba, kama CCM inapandikiza udini, basi Chadema kwa vitendo vyao wenyewe wanadhihirisha ukweli wa CCM.

Tatizo lingine la Chadema ni mkakati wao wa kuchukua nchi. Kuna rika la vijana, watu wazima wa kati, na wazee. Vile vile katika vijana kuna vijana wasomi na vijana wa mtaani. Chadema wanachama wake wengi ni vijana wa mtaani, na vijana wachache waliosoma. Mtu huwezi kuwa na usomi wako wa ukweli halafu ukakubali kushurutishwa na "peoples power" bila kutuwekea sera mnazoamini. Inabidi Chadema itambue kwamba, ingawa vijana wa mtaani ni rahisi kuwakusanya kwa maandamano, lakini huwezi kuwategemea kupiga kura. Na mbaya zaidi wanawachefua wakina mama na watu wazima. Ndio maana sisi tunasema Chadema sio chama makini. Ni bora tusubiri mabadiliko makubwa ndani ya CCM, kuliko kuitegemea Chadema kuchukua nchi.
 
Igunga imepiga fullstop kuhusu stori za magamba, hautakaa umsikie mtu yeyote kutoka magamba anaongelea kuhusu kujivua gamba, akitokea kiongozi yeyote kutoka magamba anatangaza ama kuongelea kuhusu uvuaji wa magamba naomba MODS ANIPE BAN MPAKA ATAKAPOAMUA AU ASIAMUE
 
CHADEMA..............so predictable......kila siku mnakataa matokeo.......kila siku kusema wenzenu wamechakachua.....??...ina maana ushindi ulio wa halali ni ule waloshinda CHADEMA pekee???.........
There too much "irregularities" in favor of the party in power that we have witnessed in this as we have in various elections in this country. This is the base of the cry for the foul play in this election as it has been in many.
 
Okey wana haki ya kususa. na wanastahili pongezi jaribu kufikiri , wanapambana na ccm, cuf , bakwata na serikali, we kataka akiri yako na elimu yako ya madrasa unategea haki hapo????? acha kufikiri kwa kutumia masaburi .
ZITTO muislamu, Mzee Arfi pale mpanda Bakwata,Mbowe ni Serikali pia(Msemaji rasmi wa kambi ya upinzani} Muhonga muislamu sasa unataka kusema CDM haina wanachama au viongozi waislamu? Unataka kusema CDM imejaa WAKRISTO/Hapo ndo mnapokosea kutoa majibu rahisi kwa maswali magumu.
 
Lazima watu tukubali kuwa kelele za Nape ndio zimesababisha rostam kujivua gamba. No nape no rostam kujiuzulu no starehe tuliyoipata igunga. But kwa lowassa no,namkubali sana yule mdingi
 
ZITTO muislamu, Mzee Arfi pale mpanda Bakwata,Mbowe ni Serikali pia(Msemaji rasmi wa kambi ya upinzani} Muhonga muislamu sasa unataka kusema CDM haina wanachama au viongozi waislamu? Unataka kusema CDM imejaa WAKRISTO/Hapo ndo mnapokosea kutoa majibu rahisi kwa maswali magumu.

Hujui hata unachokiandika. Zito na Arfi ni viongozi wa bakwata? Tangu lini kiongozi wa upinzani bungeni akawa ni sehemu ya serikali? Unahitaji kurudi shule wewe hauna kitu kichwani.
 
Mkandara my brother. Kiukweli, vyama vyote viwili vinatumia udini. Nina uhakika wa 100% uchaguzi wa Uraisi wa mwaka jana, zilipigwa kampeni za waziwazi kanisani--kumchagua Slaa. CCM wakajibu na Mashehe. Kwenye udini, vyama vyote viwili viko hatiani.

Wanachokosea wadau wengi wa upinzani ni dhana kwamba 1)kiongozi wa upinzani ndio pekee wenye uchungu wa nchi na kuweza kutuongoza 2) ukiwa mwanachama wa CCM, basi wewe ni fisadi. Hizo dhana mbili ni potofu. Nikifuata analog yako ya mkoloni, TANU/CCM sio ndio hao hao waliomtoa mkoloni? sasa mbona na wao wamegeuka wakoloni.

Ili waTanzania tutoke, inabidi kufuata mikondo ya demokrasia, kwanza kabisa tuache ushabiki wa kisiasa na tuwe independent/objective thinkers. Kwa sababu GodBless Lema na Prof Maji Marefu hawana uwezo (kielimu) kuwa mawaziri wa nchi hii, pamoja na Nchimbi, Mama Sofia Simba, au Ezekiel Wenje. Ushanielewa? Mimi nadhani tatizo kubwa la wabongo wanazama penzini na wanasiasa, badala ya kuchambua sera kiuwazi.

Wanasiasa wote (sio Chadema au CCM) lao moja. Wanatafuta dola, na wakiikamata hawataki kuiachia. Wapiga kura tuna jukumu moja tu--kuchagua less greedy of them all.
Mkuu,hapo kwenye rangi ya mgamba,ni vigezo gani umetumia kuona kwamba ccm ni less greedy of them all?
 
Kaka nimekuelewa, ingawa ni vigumu sana kukubali kwamba kampeni za kanisani ilikuwa mpango wa CCM kutugawa. Haiyumkini, nakubali kwamba mtazamo wako pia una ushawishi mpana. Mimi binafsi nimekaa sana vijiwe vya waislamu, na waislamu wengi sana ambao nimeongea nao wana imani kwamba Chadema ni chama cha kidini. Chadema wenyewe hawajisaidii katika hili, wanachama wao wanakosa staha ndogo ndogo tu. Huwezi kumkwida mama yule wa Igunga. CCM wanaweza kuwa wanapandikiza udini, lakini Chadema vitendo vyao vinawatuhumu wenyewe. Ukiingia humu jamvini, huwezi kukosa kejeli kuhusu Madrasa au Bakwata, vitendo kama hivi vinawafukuza waislam Chadema.

Nitakwambia hoja nyingine ya Waislam wa mtaani. Wao wanasema hivi huyu Dr.Slaa alikuwa wapi kipindi cha Mkapa? Wakati Mkapa alikuwa anakula hela hadi kajiuzia mwenyewe mali za serikali? Mbona wanapiga kelele wakati wa Kikwete, ilhali Jakaya mwenyewe hajawahi kuhusishwa na kashfa hata moja? Huu lazima utakuwa mkakati wa kanisa. Halafu wanaona chama kama Christian Democratic Party kinawasomesha vijana wa Chadema. Hoja yangu ni kwamba, kama CCM inapandikiza udini, basi Chadema kwa vitendo vyao wenyewe wanadhihirisha ukweli wa CCM.

Tatizo lingine la Chadema ni mkakati wao wa kuchukua nchi. Kuna rika la vijana, watu wazima wa kati, na wazee. Vile vile katika vijana kuna vijana wasomi na vijana wa mtaani. Chadema wanachama wake wengi ni vijana wa mtaani, na vijana wachache waliosoma. Mtu huwezi kuwa na usomi wako wa ukweli halafu ukakubali kushurutishwa na "peoples power" bila kutuwekea sera mnazoamini. Inabidi Chadema itambue kwamba, ingawa vijana wa mtaani ni rahisi kuwakusanya kwa maandamano, lakini huwezi kuwategemea kupiga kura. Na mbaya zaidi wanawachefua wakina mama na watu wazima. Ndio maana sisi tunasema Chadema sio chama makini. Ni bora tusubiri mabadiliko makubwa ndani ya CCM, kuliko kuitegemea Chadema kuchukua nchi.
Mkuu Selemani, Kwanza nikushukuru sana kwa mchango wako ambao kwa mara ya kwanza nimeona mchango uliokaa wazi sana kuhusu mawazo ya Waisilamu kuhusu Chadema. Nataka kukupongeza tena kwa kuwa umeisaidia jamii ya kitanzania kuwasiliana kwa uwazi zaidi. Kuambiana ukweli ni jambo zuri sana na ukweli huondoa makosa, hurekebisha hali na kutibu ugonjwa wa jamii kutoaminiana.
Jambo ambalo tu nataka uelewe au nikukumbushe labda ukubali pia ni kuwa hata waislamu wanaoipenda nchi yetu sawsawa, wanakubali kuwa CCM inahitaji chama cha upinzani chenye uwezo wa kukitikisa ili kitekeleze wajibu wake wa kutumikia wananchi wake kama inavyostahili na kwa sasa chama pekee kilicho na uwezo huo ni kimoja tuu! NI CHADEMA.
Mimi binafsi nakubaliana na wewe kuwa CDM haijajiweka katika "position" nzuri ya kuchukua nchi na kuiongoza, ila sasa, wanachotakiwa kufanya zaidi ni kuendelea kupata majimbo mengi na namba ya Wabunge wa Chadema iendelee kuongezeka mpaka itakapofikia 50% hata zaidi. Hapo ndipo sasa washike Dola sawasawa. Najiuliza wakishika dola sasa hivi na wabunge finyu namna hiyo itakuwaje?? Bunge litakuwa kuwaje? Wizara zitaongozwa ongozwa je? Mikoa je? wewe angalia CCM yenyewe leo hii imeshindwa kuchagua wakuu wa mikoa, iko mikoa iko wazi hadi sasa nadhani watu wanakaimu kwa muda sasa.
Kwa kifupi kwa sasa jamii inakosea kutochagua wagombea ubunge wa Chadema kwa sababu ya hisia za kidini. Tunairudisha nchi nyuma!!!!
 
Tujaribu tena kupiga glutter ili kuvua gamba jamaa mwingine tuone kama tutatoka kwa hawa jamaa.Nadhani itakuwa kipimo kizuri kuona mustakabali mwingine
 
Kaka nimekuelewa, ingawa ni vigumu sana kukubali kwamba kampeni za kanisani ilikuwa mpango wa CCM kutugawa. Haiyumkini, nakubali kwamba mtazamo wako pia una ushawishi mpana. Mimi binafsi nimekaa sana vijiwe vya waislamu, na waislamu wengi sana ambao nimeongea nao wana imani kwamba Chadema ni chama cha kidini. Chadema wenyewe hawajisaidii katika hili, wanachama wao wanakosa staha ndogo ndogo tu. Huwezi kumkwida mama yule wa Igunga. CCM wanaweza kuwa wanapandikiza udini, lakini Chadema vitendo vyao vinawatuhumu wenyewe. Ukiingia humu jamvini, huwezi kukosa kejeli kuhusu Madrasa au Bakwata, vitendo kama hivi vinawafukuza waislam Chadema.

Nitakwambia hoja nyingine ya Waislam wa mtaani. Wao wanasema hivi huyu Dr.Slaa alikuwa wapi kipindi cha Mkapa? Wakati Mkapa alikuwa anakula hela hadi kajiuzia mwenyewe mali za serikali? Mbona wanapiga kelele wakati wa Kikwete, ilhali Jakaya mwenyewe hajawahi kuhusishwa na kashfa hata moja? Huu lazima utakuwa mkakati wa kanisa. Halafu wanaona chama kama Christian Democratic Party kinawasomesha vijana wa Chadema. Hoja yangu ni kwamba, kama CCM inapandikiza udini, basi Chadema kwa vitendo vyao wenyewe wanadhihirisha ukweli wa CCM.

Tatizo lingine la Chadema ni mkakati wao wa kuchukua nchi. Kuna rika la vijana, watu wazima wa kati, na wazee. Vile vile katika vijana kuna vijana wasomi na vijana wa mtaani. Chadema wanachama wake wengi ni vijana wa mtaani, na vijana wachache waliosoma. Mtu huwezi kuwa na usomi wako wa ukweli halafu ukakubali kushurutishwa na "peoples power" bila kutuwekea sera mnazoamini. Inabidi Chadema itambue kwamba, ingawa vijana wa mtaani ni rahisi kuwakusanya kwa maandamano, lakini huwezi kuwategemea kupiga kura. Na mbaya zaidi wanawachefua wakina mama na watu wazima. Ndio maana sisi tunasema Chadema sio chama makini. Ni bora tusubiri mabadiliko makubwa ndani ya CCM, kuliko kuitegemea Chadema kuchukua nchi.
Mkuu nakubaliana nawe sana ktk halki halisi ya siasa nchini kwamba Chadema walishindwa kujitetea ktk tuhuma za Udini lakini zipo sababu nyingi za kimsingi. Binafsi nimekuwa sana ktk vijiwe vya Waislaam na imefikia hata siku moja mtu mmoja kunitaka nisihudhulie mazishi yake kama mimi ni mfuasi wa Chadema. Hawa ni ktk kundi la watu ambao unawaacha kama walivyo na rahisi kuwajibu kwa sababu Chadema kinaitwa chama cha kikristu kwa sababu mgombea ni Dr.Slaa mkristu na Padri aliyeasi na kilikuwa chama cha Wachagga kwa sababu mgombea alikuwa Mbowe..Hivyo wapo pia Wakristu wanaompinga JK kwa sababu ni Muislaam hivyo watu kaa hawa wapo na sii rahisi kuwapa maelezo wakayapokea dhidi ya imani zao.

Swala la mama yule halina mshiko na wala sii la kuwalaumu Chadema kwa sababu wapo wahusika na walitakiwa kuchukuliwa chini ya sheria kama sheria imeshindwa basi tuilaumu serikali yetu. Mbona mke wa Dr.Slaa ambaye angeweza kuwa first lady alivuliwa hadi nguo na hamkupiga makelele haya! au kwa sababu yeye ni mkristu halafu basi yulke mama DC, yeye ni mkristu kama tulivyojuzwa na vazi la mtandio haliwezi kuwa ndio Uislaam bali ni staha ya mwanamke yeyote hata kama kavaa khanga. Kuvuliwa kwake hakuwezi kuwa swala likachukuliwa na Bakwata kiasi kile.

Kuhusu Dr.Slaa, mkuu wangu unashindwa kuelewa kwamba unapopigania Urais unakuwa na ilani yako kaa mgombea hivyo huwezi kuchambua ilani ya mgombea na kuuliza alikuwa wapi wakati wa Mkapa.. Kama Dr.Slaa angegombea wakati wa Mkapa tungesema yote haya licha ya hivyo Chadema walikuwa nyuma ya mgombea wa CUF Lipumba ambaye labda niseme alishindwa kuwashawishi wananchi. Na kisha Mkapa kayafanya yote mabaya akiwa ktk awamu yake ya mwisho hivyo hapakuwepo na nafasi ya kumpiga vita Mkapa isipokuwa uchaguzi uliofuata na alisimama Kikwete. Hivyo ukitazama argument zao hazina maana isipokuwa kwa Udini walioujenga kwa Dr.Slaa..Kisha basi Dr.Slaa anapiga vita UFISADI ambao sii lazima awe Kikwete isipokuwa yeye ndiye rais mwenye mamlaka makubwa ya kupambana na Ufisadi. Na list yuake waliowengi ni wakristu iweje liwe swala la Uislaam?

Kuhusu swala la vijana wasomi na wasiokuwa wasomi... Katika siasa mkuu wangu maumivu na adha hazina elimu hata yule ambaye hakwenda shule au alosoma sana huwa na mahitaji sawa ktk misingi ya kibiadamu yaani UHURU wa KUISHI na kuthamnini UTU wake. Na hakuna dawa isipokuwa MAISHA BORA kwa wananchi wake, hivyo msomi anayepingana na CCM ama yule hakwenda shule wote wamekuwa ktk maumivu haya. Sera za Chadema ziko wazi kabisa na sii kweli sera ndio tiba ya maisha magumu ya wananchi isipokuwa kumwendeleza mwananchi hivyo kinachotangulia kwanza ni kujikwamua, kuwaondoa CCM kwa sababu huwezi kutibu kidonda bila kuondoa kwanza mwiba.

Tatizo la wasomi wengi nchini wanataka kujua sera za Chadema kama zinaweza kufanya kazi kwa kutumia elimu zao wakati we all don't have the right tools anyway! Siasa za sera sii dawa ya maisha bora hata iwe Marekani, Ujarumani au Uingereza, kama ingekuwa hivyo chama kimoja kingeongoza miaka yote..Lakini tunaweza kuuondoa mwiba tukapunguza maumivu na dawa ikatumika hata ikiwa miti shamba. Ndivyo wanavyofanya wenzetu uchaguzi huu Republican wakivurunda wanaingia Demokratic na kadhalika ili mradi wananchi wenyewe ndio wenye mamlaka ya kuchagua upande wenye nafuu kwao..kwa hiyo huwezi kutumia elimu ktk siasa wakati hakuna dawa moja iliyobora zaidi..

Tatizo la kusubiri mabadilko ndani ya CCM ni sawa na kusubiri urithi baba akisha kufa..Kwa kila baya linalofanywa na vijana wa CDM lazima utambue kwamba hawa vijana wanasukumwa na matatizo yao ya kimaisha. Na wengia ya hawa vijana ni washabiki tu hawana hata kadi ya chama..Studies nyingi zimefanyika kutazama sababu zinazowasukuma vijana weusi huko Marekani na Canada kuwa majambazi na hakika imeonekana kwamba adha za maisha wanayokua nayo, matatizo ya elimu bora na kutengwa ktk jamii ndiko kunasababisha zaidi hawa vijana kuchukua maamuzi magumu na ya mwisho ili wapate nafuu ya maisha. Kwa hiyo usiwaone hawa vijana kama sii sehemu yako bali tambua ni matendo yako mabaya ndio yamewafanya kutokuwa na elimu..Hawakupenda kutokwenda shule, bali system iliwatenga na ndio unatakiwa wewe msomi kuitazama picha kubwa zaidi.

Wasomi wanasema uki corner mnyama (Paka) ktk ukuta akashindwa kurudi nyuma zaidi, huwa hana hila isipokuwa kukushambulia wewe ili apate uhuru wake. Hii haina maana Paka ni mnyama anayependa kushambulia watu, vivyo hivyo wewe unatakiwa kupata solution ya hawa vijana na sii kuwahukumu kwa sababu una elimu na maisha bora zaidi yao. Chadema watafika tu maadam wakiendelea kujenga nyoyo za watu wapate kukiamini zaidi, kuwa na matumaini na kuamini kwamba ni chama mbadala.
 
Nyie mnataka chama kifilisike , leo hii ya igunga mmetumia 1.345bn na mmeambulia patupu na mnataka kwingine. Ni bora hizi fedha mngefungulia matawi tu na kulipa wafanya kazi wenu vizuri

we chizi mbona umekomali ishu ya matawi? Umetumwa kulivalia njuga hizo pumba.boya wewe.
 
huu mfumo mbovu wa kupiga kura tanzania nafikiri wahitaji kubadilishwa, mtu atashindaje hajapata hata 50% ya kura zilizopigwa!! Tuangalie baadhi ya nchi zinazokuwa kidemocrasia na ambazo zimeshakomaa kidemocrasia hawatumii mfumo huu butu!!
Na kwa mfumo huu tulio nao, tanzania tutaendelea kuwa na "pseudo democracy" for years to come na "chama cha wakulima na wafanyakazi" kitaendelea kupata kura nyingi "popular votes" kutoka maeneo ya vijijini.
Nafikiri hata kwenye uchaguzi wa wabunge utafutwe mfumo labda "popular votes" ipatikane kutokana na kata!
Idea nayotaka kusema ni kwamba chaguzi zetu ziwe zinafanyika katika ule mfumo kama wa ile show ya big brother! Kila nchi (jimbo au kata) ina kura moja, hivyo hata ikatokea eti kuna jimbo moja lina watu wengi zaidi ya wengine haitoathiri wapiga kura wa maeneo mengine! Kwa mfano mfumo wetu unawapa sana watu wa vijijini nguvu kulinganisha na wa mijini! Na huko ndiko chama fulani kinakobeba kura!hivyo hata kama vijijini wako wengi, wawe kwa jumla wana kura moja kutokana na jimbo na jimbo!
Hii itatupa usawa kidogo watu wa mjini kura zetu kuwa na maamuzi pia kwenye chaguzi!
 
Kaka haya yote ni magamba lakini yanatofautiana

Lile gamba moja lililoondoka halina shida sana maana lilikuwa na ushawishi mkubwa kwenye chama kiuchumi zaidi lakini sio influence kubwa ya kisiasa

Sasa haya magamba mengine mawili hasa lile la kule umasaini influence yake kisiasa ni kubwa kiasi kwamba najua kulichuna na kulitoa mwilini ni sawa na kuchuna ngozi ya kitimoto........hawana ubavu nae huyu maana kisiasa yuko level nyingine zaidi ya magamba wenzake wengine
 
Nape kwa kelele kama chura kwenye maji, haaa, safari hii sijui atamfukua nani.
 
Lengo la falsafa lilikuwa ni kuwatoa waisilamu Makamba na Rostam. Magamba yameisha, chama kinaendelea na mambo mengine, waisilamu wanaendelea kudanganywa !
 
Hawezi kuthubutu hata kuwasogelea wale Jamaa wawili waliobaki,pili mziki wa Chadema wanauogopa sn

Chadema ni nouma CCM wamekusanyana ukoo wote ili kuikabili Chadema,Unafikiri wana ham tena ya kuvuana magamba?
 
Chadema we have seen you .We salute you .Tunawakubali mno.Mliitwa chama cha ukoo , msimu, wachaga , kanda nk lakini ukweli wamejua Chadema ni chama cha kitaifa .Wameiga hata style ya kampeni kupaa angani .Ila wameshindwa kuiga mpango mzima kwamba sera then kura ila wao wanaendelea kuhonga na kununua shahada .Hongera Chadema .
 
Back
Top Bottom