Igunga OFFICIAL Results: Dr. Kafumu atangazwa mshindi

Igunga OFFICIAL Results: Dr. Kafumu atangazwa mshindi

gamba lile limejivua lenyewe sio kwa shinikizo la nape ati! la chenge limeishia kiunoni, la lowasa hata kichwani halijaanza kutoka.
 
gamba lile limejivua lenyewe sio kwa shinikizo la nape ati! la chenge limeishia kiunoni, la lowasa hata kichwani halijaanza kutoka.

Lakini kapiga sana kelele mpaka RA kakereka
 
Natamani Nape aendelee na mradi wake wa kuvua magamba vigogo ili kampeni iendelee.

Baada ya ya Igunga tunaelekea wapi kwa kampeni.

Nyie mnataka chama kifilisike , leo hii ya igunga mmetumia 1.345bn na mmeambulia patupu na mnataka kwingine. Ni bora hizi fedha mngefungulia matawi tu na kulipa wafanya kazi wenu vizuri
 
Ilala, Temeke na Kinondoni!!
Hamna miji kama hii Tanzania... na yote inashikiliwa na CCM, sasa hao watu wa vijijini sijui ni wapi tena!

Kaka hebu jaribu kuangalia education level ya majority ya watu wanaoishi Ilala, Temeke na Kinondoni halafu linganisha na jimbo la Kawe hapo unaweza kupata correlation relationship iliyopo kati ya elimu na uamuzi katika kuchagua kiongozi.
 
Nyie mnataka chama kifilisike , leo hii ya igunga mmetumia 1.345bn na mmeambulia patupu na mnataka kwingine. Ni bora hizi fedha mngefungulia matawi tu na kulipa wafanya kazi wenu vizuri

Sishangai CCM kutumia kiasi hicho kwani kunakuhonga watu, kununua kadi na mengine mengi.

Kwani lazima kuhonga ?
 
Jeykey, hana heshima kwa CDM, ana lugha chafu.
 
Acha vitisho wewe, jenga hoja yenye mantiki ueleweke.
 
Mkandara my brother. Kiukweli, vyama vyote viwili vinatumia udini. Nina uhakika wa 100% uchaguzi wa Uraisi wa mwaka jana, zilipigwa kampeni za waziwazi kanisani--kumchagua Slaa. CCM wakajibu na Mashehe. Kwenye udini, vyama vyote viwili viko hatiani.

Wanachokosea wadau wengi wa upinzani ni dhana kwamba 1)kiongozi wa upinzani ndio pekee wenye uchungu wa nchi na kuweza kutuongoza 2) ukiwa mwanachama wa CCM, basi wewe ni fisadi. Hizo dhana mbili ni potofu. Nikifuata analog yako ya mkoloni, TANU/CCM sio ndio hao hao waliomtoa mkoloni? sasa mbona na wao wamegeuka wakoloni.

Ili waTanzania tutoke, inabidi kufuata mikondo ya demokrasia, kwanza kabisa tuache ushabiki wa kisiasa na tuwe independent/objective thinkers. Kwa sababu GodBless Lema na Prof Maji Marefu hawana uwezo (kielimu) kuwa mawaziri wa nchi hii, pamoja na Nchimbi, Mama Sofia Simba, au Ezekiel Wenje. Ushanielewa? Mimi nadhani tatizo kubwa la wabongo wanazama penzini na wanasiasa, badala ya kuchambua sera kiuwazi.

Wanasiasa wote (sio Chadema au CCM) lao moja. Wanatafuta dola, na wakiikamata hawataki kuiachia. Wapiga kura tuna jukumu moja tu--kuchagua less greedy of them all.
Mkuu wangu unafikiri mimi napinga hilo...sipingi hata kidogo na nadhani ndio ilikuwa kazi yangu kubwa sana hapa JF kujaribu kuwaunganisha wananchi tuondoe tofauti zetu za dini.

Nachopinga mimi kuhusiana na Chadema ni pale mnapodai Chadema walifanya hivyo, hii si kweli isipokuwa wapo watu walitumiwa na CCM kueleneza Udini na hata hao Mapadre hawakufanya hivyo kwa sababu waliipenda Chadema au Dr.Slaa isipokuwa walitumiwa na CCM kuleta mgawanyiko huo. Hata wakati wa Ukoloni mkoloni hakuingia Makanisani bali MaPadre wetu na ndio waliifanya kazi hiyo kwa niaba kama Bakwata wanavyofanya leo. hawa wote ni mamluki wanaopewa fedha kusambaza udini na Mungu awalaani wote!

Na ndio maana nawataka nyie wananchi mfahamu tofauti zetu haziwezi kuleta mafanikio yoyote isipokuwa UMOJA wenu na kutambua mbinu chafu zinazoenezwa. Lakini kwa bahati mbaya wengi wetu bado hawajafahamu kwamba chombo kinachokukwaza sii imani ya mtu wala JK kuwa rais bali ni system nzima imejengwa ili tuendelee kutawaliwa. JK is as bad as Mwinyi na Mkapa..

Kwa hiyo sii kazi ya Chadema wala CUF kutambua hitilafu hizi, bali ni sisi wenyewe wananchi kupingana na vyombo hivi vya dini vinapoingilia maswala ya kisiasa na sisi wenyewe kutambua na kujiepusha kabisa na maswala yoyote yanayohusiana na tofauti zetu za kiimani na tuelekeze nguvu zetu kutafuta haki na maendeleo yetu. Watawala wakishindwa kutugawa hatutatawalika!

N.B Habari mpya niloipata sasa hivi nasikia Ofisi ya Chadema huko Igunga imevamiwa na Mapolisi wamerusha mabomu ya machozi kuwasambaza wanaChadema waliokusanyika kuwasikiliza viongozi wao. Igunga nzima sasa hivi ni vurugu tupu!...
 
Mkuu,

Naandika makala nadhani inalenga vp CCM itashindwa na Chadema wapi wanatakiwa kuwekeza waweze kushinda uchaguzi 2015. Nitarudi kuchangia vizuri zaidi nikiimaliza.
 
Nawapongeza chadema kwa ushindi. Cha msingi ni kuongeza mashambulizi ili mwaka 2015 uwe wa mabadiliko ya kweli. Nchi zetu za jirani wameweza kwa nini sisi tushindwe? Cha msingi ni kuwa na strategy zitakazoweza kutuweka madarakani
 
Nimekua nafuatilia japo kwa mbali uchaguzi wa Igunga.

Analysis yangu imebaini kulikua na makundi mawili hasimu.

Kundi la CCM + CUF + BAKWATA Vs CHADEMA + CCM Walengwa wa kuvuliwa gamba.

Katika huu ushirika wa pande zote, kuna waliojua the full deal na kuna waliobebwa msukule kishabiki.

Moja ya ushahidi wa CCM Walengwa wa kuvuliwa gamba kutaka Igunga iende kwa wapinzani, ni pale mmoja wa makada
maarufu aliporipotiwa akimpiga mkwala Katibu Mkuu, kwamba "ngojeni yatayowakuta Igunga, halafu ndio tutaheshimiana".
Na kulikua na taarifa za kundi kubwa la vijana wa CCM kuweka kambi Nzega na pesa ya kutosha (ingawa taarifa hii itawakwaza
baadhi yetu), na kueneza upupu aganist CCM giza likiingia.

Kuhusu ushiriki wa BAKWATA kwa kukihujumu chama kimojawapo, hilo halina mjadala. Ni bahati tu kwamba hiyo BAKWATA
yenyewe ilishapoteza credibility yake kwa majority ya waislam long time ago. Na serikali ya Umoja wa Kitaifa zanzibar kati ya
CCM na CUF nayo ni open secret.

I short it was a tense battle,... But i dont expect the same kind of competitiveness come 2015, since many of the other "players"
will be busy with their own campaign. Besides wakati naona CCM wakiendelea kumsimamisha Dr. Kafumu, i dont see Mwalimu Kashindye
akipita kura za maoni ndani ya CHADEMA, baada ya mwamko wa wana Igunga kwa chaguzi huu... maana nimeona kama kuna umachachari flani unaowanasibisha wanaCHADEMA kama hana hivi!

Jambo muhimu kwa CHADEMA ni kuweka utaratibu mzuri wa kutokua na huruma kwa mwanachama yeyote atakayetoa rushwa kwenye
kura za maoni, ili kibaki na sura yake ya wananchi halisi wa Tanzania. Maana trust me, come 2015 ile vita ya kura za maoni tuliyoizoea CCM
itahamia na kwa CHADEMA, kwa watu kujua chakula sasa kimeiva, wakati wa kula nawao umefika.
 
Ingawa tunapaswa kuwa na mipango ya muda mrefu, lakini Mla ni mla leo, hayo ya 2015 ni maajliwa ya Mwenyezi Mungu. Mwaka 2015 Afrika Mashariki itakuwa nchi moja na Rais atakuwa Y. M7.

ujinga wako peleka kwenu!
 
Dr Kafumu kawafumua Magwanda,kamfumua Mshamba Kashindye! CCM oyeeeeeeeeeeeeeeeee!
 
hongereni sana chadema...!much love

saa ya ukombozi ni kama imewadia
 
Lowasa yuko chuchi,chenge anafatilia pesa za dowans ili kufidia pengo la igunga
 
Aibu. Kati ya watu 171,000 waliotakiwa kupiga kura, wamepiga kura less than 50%! Jiulizeni kwa nini, lakini tathmini yangu ni hii:

  1. Askari polisi waliopelekwa Igunga, wakiwa na magari ya deraya, pamoja na FFU, ni vitisho tosha vya kuwafanya watu wasiende kupiga kura
  2. Tume ya Uchafuzi imetumia mbinu chafu, za kuwabadilishia vituo watu walioonekana (kwa tathmini ya wajumbe wa nyumba kumi wa CCM) wapinzani kwa CCM, waende kupiga kura vituo vya mbali, huku wakijua kwamba ingekuwa vigumu kwao kwenda kufanya hivyo kutokana na uhaba wa vyombo vya usafiri. Watu wengine wamedaiwa kuhamia kata nyingine, fikiria, mtu aende kwa mguu, mwendo wa saa tano, kupiga kura kwenye eneo ambalo yeye si mkazi, kama hii si hujuma na kumnyima mtu haki yake ya kupiga kura, sijui ni nini? Huu si uvunjaji wa katiba huu?
  3. CCM (kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari) wamenunua shahada nyingi za wapiga kura, kwa bei ya chee, hivyo kupunguza idadi ya wapiga kura.
  4. Mbinu nyingine chafu mnazijua.
Bado mnasema kuidai Katiba Mpya (ya Watanzania wote) ni UHAINI? Mwenye kusema hivyo asimame, anyoshe mikono yake yote miwili, tumwone!
 
cCM msipobadilika mkawa chama cha kileo mmekwenda na maji,shindeni kwa kutumia rekodi ya mambo mnayoyafanya na sio kushinda kwa kutumia pesa lukuki, timizeni ahadi basi,sio kunyima miradi pesa na kukusanya kwa ajili ya uchaguzi ujao
 
gamba lile limejivua lenyewe sio kwa shinikizo la nape ati! la chenge limeishia kiunoni, la lowasa hata kichwani halijaanza kutoka.

Zumbe ni kwamba kama wanjiamini wayavue kwa nguvu hayo magamba yalionasa ili tuwapelelke puta tena !
 
Back
Top Bottom