Igunga OFFICIAL Results: Dr. Kafumu atangazwa mshindi

Igunga OFFICIAL Results: Dr. Kafumu atangazwa mshindi

mtatiro kaumia kweli......
Huyu Bwn Mtatiro akitaka kuibuka kwenye siasa za nchi hii basi ajiunge tena CDM, YEYE MWENYEWE AMEJIONEA MOTO WA CDM Igunga!!!!!!!! Mtatiro jiunge tena baba na CDM utaibuka kidedea kwenye siasa za nchi hii, CUF ni CCM-B. Mpeni pole Mtatiro!!!!!!!!!
 
Mbowe analia sasa

images

alie kwa lipi. Anatafakari, awaonea uchungu wananch wa Igunga kwa kuweka maisha yao rehani.
 
Wiki nzima shughuli zangu hazitaenda vizur nipo affected na haya matokeo.
Wakazi wa Igunga wamedanganywa na wakadanganyika.

Tupo wengi mkuu ipo siku kila kitu kitakuwa sawa sawa.Hivi huwezi kuona kuwa Chadema ilishambuliwa na Serikali nzima dhidi ya chama kimoja cha Chadema tu.
 
hawa wajinga wa vyama vingine wangeunga cdm vikura vyao vingesaidia. ccm hawawez kufurahia chama kisichokuwa na mizizi ugunga kimewapeleka hvy
 
Nilitegemea wafuasi wa magamba wawe wengi kushangilia ushindi lakini cha kushangaza eti hata hamsini hawafiki! Kweli kabisa GAMBA linalazimisha kuwa madarakani.
 
Cdm ni dume walahi. Kama pamoja na wizi kafumu kafumua 3200 tu basi cdm hii inatosha
 
Magayane ametangaza kuwa imebidi wachakachue ili chama cha magamba kishinde, amesema mwenyewe baada ya kubanwa sana. kwa hiyo ni ushindi wa wizi
 
Check na hii Mbowe akiwa amegikunja Chobisi akitabasamu kilichotokea

images

anatafakari kwa uchungu hatima ya wana Igunga. Anawaonea huruma kwa dhuluma wanayofanyiwa na magamba.
 
Hongera CCM, kwa wale ambao kura hazikutosha msipoteze muda. Jipange kwa chaguzi zijazo.
 
CHADEMA..............so predictable......kila siku mnakataa matokeo.......kila siku kusema wenzenu wamechakachua.....??...ina maana ushindi ulio wa halali ni ule waloshinda CHADEMA pekee???.........
 
Ccm hawajachakachua hizi kura kweli??? Maana Watu wengi wana support CDM!
 
Yule jamaa wa CUF amezungumza jambo moja la nsingi sana. PESA, siasa za kitanzania na kiafrika kwa ujumla ni pesa tu, wananchi wengi hasa hawa wa vijijini wana uelewa mdogo juu ya katiba na maendeleo kupiga kampeni kazi bure, unaweza kupata kura zao kwa kuwarubuni na vijizawadi vidogo-vidogo, hata buku kumi kumi wanakugaia kura.

Huo ndio ukweli na ndio strategy pekee inayofanya kazi kwa sasa. Hadi pale wananchi walio wengi watakapoelimishwa na wakafahamu sababu za umasikini wao nachelea kusema mambo yatakuwa yanajirudia hivi kila chaguzi.

Itachukua muda zaidi ya tunavyofikiria unless Chadema wakubali falsafa ya if you can't beat them join them nao waanze kampeni ya mapesa ama waanze kufanya kazi ya ziada kupeleka elimu ya maendeleo kwa wananchi wa mikoani na vijijini, venginevo hiyo 2015 mambo yatakuwa ni yale-yale

. Money Talk- Hata Rostam akisema arudi kugombea atashinda tena kwa vile ana hela na yuko tayari kuitumia, huo ndio ukweli.
 
Nawapongeza CCM kwa kutangazwa washindi. Ni kweli uchaguzi umeisha na matokeo yametangazwa.

1. Cha kushangaza waliokuwa wanaonekana katika TBC 1 wakihojiwa au walioonekana hawakuonyesha uso wa furaha.
2.Mugulu Nchemba amewalalamikia CDM kuwa wamefanya mambo mengi mabaya
a) Wamemwagia mtu tindikali
b) Wamechoma nyumba ya kiongozi wa CCM
c) Wamemvua DC (Kimario) vazi lake la kiimani na kulitupa chini
Pamoja na malalamiko mengine anaomba vyombo vya dola viishughulikie CDM.

CHADEMA mnasemaje juu ya malalamiko haya? Je Ninyi mnalalamikia nini waliotangazwa washindi?

CUF wamekubali matokeo na kusisitiza kuwa ni halali. Mtatiro ameongeza kuwa sasa kinachokubalika ni kuhonga wapiga kura na amesema chama chake ndicho kilichokuwa na mgombea bora kuliko wote. Lakini anaona wananchi wameamua walivyotaka.

Mimi sina chama chochote lakini ni mfuatiliaji mzuri sana wa siasa za nchi yetu. Nataka kujibu uliyoorodhesha kama ifuatavyo:
Imefika mahali CCM huwa wanakuja na mbinu mbalimbali na zingine za kitoto na zingine za hatari ili tu wafanikiwe wanachokitaka. Kukwagiwa tindikali hakuna uthibitisho wowote ambao unadhihirisha kwamba waliomwaga hilo tindi ni wafuasi wa Chadema. Labda tuulizane Mwandishi wa habari mahiri Said Kubenea alipomwagiwa tindikali tungeweza kusema ni CCM wamefanya kitendo hicho kwa sababu anaandika sana kuikosoa Serikali?

Kwa taarifa zilizotolewa hakuna nyumba yoyote ya kiongozi iliyochomwa moto kilichoungua ni jiko na yawezekana kabisa moto huo ulitokea kwa bahati mbaya au ni mkakati mwingine wa CCM na huenda kutokana na CCM walivyo wa ajabu wanaweza walichoma hilo jiko makusudi ili wapate kuwasingizia na kuwavurugia Chadema machoni kwa wananchi! Kwa CCM ya leo anything is possible!!!

Kuhusu vazi tumeishaaelezwa na tumeona picha zinazothibitisha kwamba mama hiyo hakuvaa hijabu yoyote bali mtandio na wala si muumini wa kweli wa dini ya Kiislamu kwa sababu kaolewa na Mkristo jambo ambalo halikubaliki katika dini ya kiislamu. Hiyo nayo ni mbinu nyingine ya CCM ili kuwawekea Chadema doa!

Ni jambo la kusikitisha sana kwamba sasa CCM wanaweza kufanya lolote lile kujipatia ushindi. It is a shame really.
 
Tupo wengi mkuu ipo siku kila kitu kitakuwa sawa sawa.Hivi huwezi kuona kuwa Chadema ilishambuliwa na Serikali nzima dhidi ya chama kimoja cha Chadema tu.

nakiri kuwa japo tumeshindwa ila kwa upande mwingine tumeshinda. Ni mengi tumefanyiwa. Dua nying mbaya tumeombewa, lengo ni kumdidimiza mwana Igunga.
 
Back
Top Bottom