Igunga OFFICIAL Results: Dr. Kafumu atangazwa mshindi

Igunga OFFICIAL Results: Dr. Kafumu atangazwa mshindi

mi nadhani ana sifa sote za kuongoza w2 wa igunga basi tu chama chake kinamponza...
 
Hongera zenu mlioshinda,... japo msome alama za nyakati maana pamoja na kupeleka viongozi wanao/waliokuwa wanaheshimika kijamii kama rais wastaafu na mawaziri bado ushindi ni mwembamba na sehemu kubwa ya jimbo ni vijiji ambapo hata kusoma na kuandika ni taabu, maali ambapo siasa za upinzani ni ngeni na wengi hata taarifa za habari wala harakati za kisiasa hawajui ni nini, wanajua raisi ni nyerere na chama ni CCM. SASA HII NI DALILI TOSHA KUWA MWISHO WA HATI MILKI YA SIASA ZA TANZANIA UMEWADIA. Sasa ni kugawana kura,. madhara ya haya ni kuwa na serikali inayopendwa na asilimia chache ya umma ukizingatia wengi hawapigi hata hizo kura. kwa uuwiano huu ni bora hata sheria ibadilishwe mtu asipopata 50% basi jimbo liongozwe kwa zamu maana kuna sehemu ataenda mbunge aitishe mkutano wa hadhara aambulie wananchi watatu (3) tu! ni maoni yangu jamani.
 
CDM kama wameshindwa kwa asilimia 6,ama sawa na kura elfu tatu na ushee kati ya 56,072.Ukweli ni kwamba hapo kuna za BAKWATA zilizochochewa na udini wa ccm.Mimi nashangaa mnawabembelezea nini wadini na watu wakabila.Hizo chuki ni ngumu sana kuzifuta.Hata ufanyaje huwezi kuzifuta chuki za kidini kama zikishapandikizwa.Hawa watu wanawapima kwa kila hali na nyie mmekaa tu mnakubali.Hawezekani ccm waendelee kudekezwa kwenye haya kwasababu tu ni walafi ambao hawataki kuyaachia maslahi yao binafasi ya kuifisadi hii nchi.Hilo haliwezekani kabisa.Chama kina kashafa ya ufisadi,kinakuja eti na kauli za kujivua magamba.na wakati magamba yenyewe bado yamo.Na gharama za uchaguzi bila hata ya watuhumiwa kufikishwa mahakamani!Linchi la hovyo hili kwasababu tunachaguliwa viongozi na mijitu ya hovyo ambayo hadi unajuta kuzaliwa Tanzania.Ila kwasababu nyumbani ni nyumbani.Basi ni lazima tusafishe nyumba.Nani kasema hii nchi ni ya watu wachache wenye uchu na wenye kufuja rasilimali?Halafu wenye kupanda chuki za kidini?There is no way we can move forward like this.Something has to be done.Something very imminent!Otherwise we are heading to a "Failed State" status.Si kila mtu atakubali kuongozwa na hawa watu.
Mkuu wangu CDM haiwezi kushinda CCM ikiwa mfumo wa uchaguzi unaendelea kuwa kama ulivyo. Kati ya wapiga kura 171, 019 wamejitokeza 56,072 tu inaleta picha gani kwenu hasa ktk uchaguzi pekee ulofanyika Jumapili?..

JMushi1, mkuu naona kama unasahau ya kwamba Hata wakoloni walitumia sana mbinu hii ya Udini na Ukabila kuwekza kuendelea kutawala. Walikuwa mafisadi na mabaya mengine yote ya CCM walikuwa nayo tena mara mbili lakini waliweza kututawala zaidi ya miaka 200?. CCM ni mtawala mwingine kama mkoloni tofauti zao ni rangi tu ya bendera na ngozi zetu lakini haipotezi mbinu ya utawala husika. CCM wanaeneza Udini iwe kupitia Bakwata au chombo chochote kutugawa ili wapate kuendelea kutawala na ni kujumu letu sisi kutambua hivyo sii kazi yao..

Swali kwetu sisi ni kwa nini wananchi wanapokea uchochezi huo na kujenga chuki baina yao wakati tunajua hiii mbinu ilitumiwa na wakoloni! Elewa jambo moja kubwa sana ambalo CCM imeweza kulijenga ni kuwaonyesha waislaam ya kwamba Chadema ni chama cha Kikristu na wameweka hoja ambazo wao hawana majibu lakini zimebakia hai kwa muda mrefu makusudi sana.
1. Mahakama ya Kadhi
2. OIC
Hoja hizi mbili zipo makusudi kabisa kujenga utengano wa nguvu ya wananchi kupitia dini, na hata hao viongozi wa kiislaam ndani ya CCM wakiulizwa wao husema sii wao wanaokataa isipokuwa hukataliwa na wakristu. JK akimsukumia Pinda na kuwaonyesha Waislaam sii yeye anayepinga mahakama ya Kadhi bali kina Pengo (Pinda) na wakristu wengine. Hivi ndivyo waislaam wanavyoamini na hawajawahi kupokea sababu za maana zaidi ya kuwa wakristu hawataki kusikia mahakama ya kadhi na OIC!..Why wakristu hawataki? Majibu hutolewa na Maaskofu, Kardinali na WanaChadema!. Sasa Mnategemea kipi waislaam wanaweza kujiunga na CDM ili hali wanajibu maswali yasiyowahusu kabisa kujibu kisiasa...

Na kwa ujinga huo huo, Bakwata na waislaam wanaamini kabisa kwamba Wakristu ndio wapinzani wa Uislaam kutokana na majibu wanayoyapata. Wakiitazama Chadema ndio hawaoni hata mwanga, wakristu wanapinga vitu hivyo wazi wazi bila sababu za kisiasa isipokuwa kwa kutumia imani zao za dini wakasahau whjo is their enemy.. na huwezi kutumia sababu ya kidini kupinga ibada ya mwenzako hata siku moja - Itakuua kisiasa.

Mkuu wangu katika historia ya nchi zetu kutawaliwa na mkoloni, utakuta kwamba ni pale wananchi walipokubali kutengana wakamsahau adui yao kuwa mkoloni wakaanza kupambana wao kwa wao ndivyo mkoloni alivyoweza kutawala kwa miaka mingi zaidi.. Historia siku zote inatueleza kwamba halikuwa swala la kuunda vyama vya Upinzani vingi aukuwa na mawazo ya wagombea binafsi ndio ulikuwa na suluhisho Uhuru wao isipokuwa ni pale wananchi wengi walijipanga nyuma ya chama kimoja, chama ambacho kilikana kabisa kuzungumzia tofauti zao, wakapuuza na kuondoa tofauti zao, wakaunda UMOJA wenye nguvu kubwa na wakaifanya kazi moja nayo ni kumwondoa Mkoloni.

Kuzaliwa kwa TANU ni fundisho kubwa sana kwa WanaChadema, Nyerere aliweza hata kwenda misikitini na kuhutubia aliweza kucheza bao na waswahili na hata kuhudhuria ibada za Maulidi na Idd nasi tukahudhuria Christmas na Pasaka. Nyumba ya Mkristu walikuwa hawali nyama bila kuchinjwa na Muislaam hali kadhalika kina mama wakivaa wakivaa ushungi (mtandio) bila kubadilisha imani zao za dini kwa sababu tulihitaji UMOJA wetu zaidi ya vyama.

Na matokeo yake, TANU waliibuka Kidedea dhidi ya vyama vyote vilivyoendekeza ubaguzi wa kidini au kikabila. Na leo hii kutotambua kwamba adui wa Chadema sio Muislaam wala sii Bakwata isipokuwa ni CCM, hivyo kwa kila unapozungumzia Bakwata na Waislaam ndivyo hamta tofautiani na wanachama wa vyama vingine vya kina Marealle, Mtemvu na wengineo waliojikita ktk mutetea makundi ya watu.

Wewe jiulize why swala la Mahakama ya Kadhi na OIC linazungumziwa hadi kesho?..
 
ni
crappp ,useless head
ki ukweli ccm wana fanya siasa chafu na hili halina kificho kwani hata RA alikiri hilo. kuhusu udini ccm ni moja ya mbinu yake nyingine. tamko lolote likitolewa na taacc za dini kusifia ccm ni halali, ila likipongeza upinzani tayari utackia wakitoa tamko kwamba viongozi wa dini wanachanganya dini na siasa. kuhusu ukabila marangapi viongozi wamekuwa wakihusisha cdm na uchaga wakati wakati cdm kama vyama vingine kimeanzishwa kwa mujibu wa sheria za nchi. napenda kumaliza kwa kusema uvunjaji wowote wa amani kiini chake ccm, watanganyika wote yatupasa tuamke tuungane kutoa elimu kwa baadhi ya wenzetu juu ya ulinzi wa taifaletu lilotukuka kwa neema pamoja nutu wetu. naamini katika kufanyakazi kwa juhudi na maarifa na sikuombaomba.
 
Huo ushindi ni wa kununua kwa fedha za kuweka kwenye ijabu, ngoja twende kupiga kampeni vijijini.
 
NIMEJARIBU KUJUMLISHA KURA ZA CHADEMA, CUF, AFP, CHAUSTA, SAU, DP, UPDP lakini hazijafikia kura za CCM!
Kweli nimeamini CCM inapendwa!
Hongera sana Dr. Kafumu.
Viva CCM
Umejaribu lakini hukupata jibu sahihi. Vyama ni vingapi hapo? Katika mbio za marathon kuna serious competitors na fun runners. Hivyo vingine vilkuwa fun runners.
 
Hivi magwanda toka lini mkakubali matokeo hata leo ikawa mara ya pili? mlikuwa mnajisifu humu kuwa mmedhibiti kila mahali na mmewagawa vijana wenu kila mahali kudhibiti wizi wa kura na mpaka dakika ya mwisho mmekiri kuwa vijana wenu walifanya kazi njema kabisa.

Nashangaa sana ikiwa mmeshindwa kupima kilichowaharibia kura zenu.

Matokeo ya kuanzisha fujo kama kumdhalilisha Mkuu wa wilaya kwa kumvuwa hijab ni moja ys mambo yaliyowakosesha kura. Hata mwizi ana haki Tanzania ya kufikishwa kwenye viombo vya sheria kiustaarabu, leo nyinyi mnakwenda mvuwa mtu hijab? halafu mnashangaa vipi mmeshindwa? naona m mapanguani msio na mfano. Na kwa msingi huo na mengine mengi ambayo si lazima sisi tuwafunulie hamtoshinda uchaguzi mwingine wowote.

Na leo Igunga ndio mwanzo wa kifo cha magwanda, mmeanza na kususa mtamalizia kwa kukamatana uchawi wenyewe kwa wenyewe. Hamna mliwezalo zaidi ya fujo na kususa.

Sijui mnategemea nini ikiwa chama kinaongozwa na watu walioasi hata kanisa lao na wanaoendesha vilabu vya usiku maarufu kwa uvunjifu wa maadili? Na wanaoingia kwa staili ya sauti ya uchungaji kwenye mikutano ya hadhara, halafu mtegemee ushindi?

Poleni sana magwanda nawasikitikia kuongozwa na watu kama hao, laiti mngelikuwa mnaongozwa na watu kama Zitto, Lema, Safari, mngetisha na mngechukuwa kila kiti mnachokihitaji.

Wanaowarudisha nyuma ni Mbowe, Slaa, Mdee. Kwa ukosefu wao wa maadili katika jamii.
 
Ilala, Temeke na Kinondoni!!
Hamna miji kama hii Tanzania... na yote inashikiliwa na CCM, sasa hao watu wa vijijini sijui ni wapi tena!
Nimepata elimu mpya. Hivi Ilala, Temeke na Kinondoni siku hizi ni miji? Where was I?
 
CCM Kama vichwa vinafanya kazi vizuri lazima wakae chini na kufanya tafakuri ya nguvu kwa kura walizopata CDM! Kwani 2015 nguvu iliyotumika this time haitakuwepo kila mmoja atakuwa busy na Jimbo lake!
 
Niliwahi kuumizwa sana na namna Watanzania wanavyochagua viongozi wao mpaka nikajuta kuwa Mtanzania, lakini baadae nikakubali hali halisi ili kuepuka kupata vidonda vya tumbo buree, na kuyaangalia maisha yangu na jamii yangu binafsi kwanza.

Watanzania ni zaidi ya uwajuavyo..., ukiviweka hivi vitu seriously moyoni utakosa furaha yako buree, kula maisha yako binafsi, Watanzania wakiamua kubadilika tutakutana nao mbele ya safari, by the way ujamaa ulishakufa ati...

ACHANA NA UBUNGE WA IGUNGA, Jana kulikuwa na chaguzi 22 za Udiwani sehemu mbalimbali za Tanzania, na Chama Cha Mapinduzi kimefanikiwa kushinda kwenye kata 17 kati ya kata hizo 22, bado tuna safari ndefu sana...
Nashukuru kwa ushauri.Ila ushauri wa maana lakini si mzuri sana.Kwa mfano hapo penye "Maisha yako binafsi" Mkuu hilo la maisha binafsi ndilo wanalolifanya viongozi wetu baada ya kutambua kuwa divide and rule works as much as it did under colonialism.Coupled with the same fact like "The level of understanding" for most Tanzanians ni still to the lowest points.Na kuzijali interest zao binafsi imekuwa rahisi.Hawahitaji kujiumiza kufikiri kuwasaidia wananchi masikini na wajinga.Kwa hiyo hawa wana kila characteristics za kikoloni except rangi.Tena kwa taarifa yako afadhali hata ya wakoloni walijenga jenga nchi na hadi yale waliyoyajenga tunayategemea hadi sasa.Na hao ccm sometimes waki claim credit.Ukiondoa hapo pa maisha binafsi.Basi ushauri wako mzuri tu.Ofcourse kwa baadhi ya watu.Binadamu ni tofauti na ushauri tofauti unawa fit kwa namna za tofauti.Neways bado nashukuru kwasababu umeutoa kwa nia njema.
 
Hivi magwanda toka lini mkakubali matokeo hata leo ikawa mara ya pili? mlikuwa mnajisifu humu kuwa mmedhibiti kila mahali na mmewagawa vijana wenu kila mahali kudhibiti wizi wa kura na mpaka dakika ya mwisho mmekiri kuwa vijana wenu walifanya kazi njema kabisa.

Nashangaa sana ikiwa mmeshindwa kupima kilichowaharibia kura zenu.

Matokeo ya kuanzisha fujo kama kumdhalilisha Mkuu wa wilaya kwa kumvuwa hijab ni moja ys mambo yaliyowakosesha kura. Hata mwizi ana haki Tanzania ya kufikishwa kwenye viombo vya sheria kiustaarabu, leo nyinyi mnakwenda mvuwa mtu hijab? halafu mnashangaa vipi mmeshindwa? naona m mapanguani msio na mfano. Na kwa msingi huo na mengine mengi ambayo si lazima sisi tuwafunulie hamtoshinda uchaguzi mwingine wowote.

Na leo Igunga ndio mwanzo wa kifo cha magwanda, mmeanza na kususa mtamalizia kwa kukamatana uchawi wenyewe kwa wenyewe. Hamna mliwezalo zaidi ya fujo na kususa.

Sijui mnategemea nini ikiwa chama kinaongozwa na watu walioasi hata kanisa lao na wanaoendesha vilabu vya usiku maarufu kwa uvunjifu wa maadili? Na wanaoingia kwa staili ya sauti ya uchungaji kwenye mikutano ya hadhara, halafu mtegemee ushindi?

Poleni sana magwanda nawasikitikia kuongozwa na watu kama hao, laiti mngelikuwa mnaongozwa na watu kama Zitto, Lema, Safari, mngetisha na mngechukuwa kila kiti mnachokihitaji.

Wanaowarudisha nyuma ni Mbowe, Slaa, Mdee. Kwa ukosefu wao wa maadili katika jamii.
Sijui kama unalitumia hili jina kwa sababu unalipenda au ndio jina lako haswa maanake Faizal Foxy nimjuaye mimi alikuwa mteja mzuri sana wa Club na kujirusha. Katika dunia hii hakuna binadamu aliye kamilika na sii ajabu biashar zako na kazi zako zina urahamu wake vile vile kwa hiyo sii vizuri kuwatazama na kuwapima watu kwa kazi zao zinazowaletea riziki ili mradi kuhalalisha Uislaam wako...

Na fahamu ya kwamba Zitto, Lema na Safari ni kati ya viongozi wa ngazi ya juu sana ktk chama hiki na sio wasemaji wakuu kama kina Mukama, Mnauye, JK na Chiligati ambao wanapambana na Mbowe, Slaa na Mndee...Hivyo itakuwa makosa makubwa kuipima CCM kutokana na uongozi wa kisiasa wa watu hawa..
 
Sio umaasikini wao, ni umasikini walioletewa na CCM unazidi kuwatafuna. Its a sad experience.

nimesema umaskini wao kwakuwa hawajui nini chanzo cha umaskini.
 
ukishasoma signature ya Nyani Ngabu ndio jbu tosha kwa watz..
 
Natamani Nape aendelee na mradi wake wa kuvua magamba vigogo ili kampeni iendelee.

Baada ya ya Igunga tunaelekea wapi kwa kampeni.
 
Hivi majirani zetu kwa mfano Zambia wakisikia nchi ipo katikati ya giza la kutokuwa na umeme na la umasikini na bado kwenye uchaguzi CCM wanashinda huwa wanatuonaje, me nadhani hawapati picha hawa ni watu wa namna gani.

Ila bila ya kufight for a brand new constitution tukabaki na hii ambayo Rais (mwenyekiti wa CCM) anamteua kila mtu pamoja na referee wa uchaguzi we are in for a massive trouble.

Wanaharakati na wapenda usawa tupige kelele bila kuchoka haya mabadiliko yanakuja kwa kasi ya ajabu.

Mwisho hongera sana CDM kwa kustage a good fight na kuendelea kuporomosha umaarufu wa CCM kwa kasi ya ajabu. Na on Saturday ntakuja ofisi zenu kukata kadi ya CDM ili niwe mpambanaji kwa hali na mali zangu. Big up CDM.
 
Mkuu wangu CDM haiwezi kushinda CCM ikiwa mfumo wa uchaguzi unaendelea kuwa kama ulivyo. Kati ya wapiga kura 171, 019 wamejitokeza 56,072 tu inaleta picha gani kwenu hasa ktk uchaguzi pekee ulofanyika Jumapili?..

JMushi1, mkuu naona kama unasahau ya kwamba Hata wakoloni walitumia sana mbinu hii ya Udini na Ukabila kuwekza kuendelea kutawala. Walikuwa mafisadi na mabaya mengine yote ya CCM walikuwa nayo tena mara mbili lakini waliweza kututawala zaidi ya miaka 200?. CCM ni mtawala mwingine kama mkoloni tofauti zao ni rangi tu ya bendera na ngozi zetu lakini haipotezi mbinu ya utawala husika. CCM wanaeneza Udini iwe kupitia Bakwata au chombo chochote kutugawa ili wapate kuendelea kutawala na ni kujumu letu sisi kutambua hivyo sii kazi yao..

Swali kwetu sisi ni kwa nini wananchi wanapokea uchochezi huo na kujenga chuki baina yao wakati tunajua hiii mbinu ilitumiwa na wakoloni! Elewa jambo moja kubwa sana ambalo CCM imeweza kulijenga ni kuwaonyesha waislaam ya kwamba Chadema ni chama cha Kikristu na wameweka hoja ambazo wao hawana majibu lakini zimebakia hai kwa muda mrefu makusudi sana.
1. Mahakama ya Kadhi
2. OIC
Hoja hizi mbili zipo makusudi kabisa kujenga utengano wa nguvu ya wananchi kupitia dini, na hata hao viongozi wa kiislaam ndani ya CCM wakiulizwa wao husema sii wao wanaokataa isipokuwa hukataliwa na wakristu. JK akimsukumia Pinda na kuwaonyesha Waislaam sii yeye anayepinga mahakama ya Kadhi bali kina Pengo (Pinda) na wakristu wengine. Hivi ndivyo waislaam wanavyoamini na hawajawahi kupokea sababu za maana zaidi ya kuwa wakristu hawataki kusikia mahakama ya kadhi na OIC!..Why wakristu hawataki? Majibu hutolewa na Maaskofu, Kardinali na WanaChadema!. Sasa Mnategemea kipi waislaam wanaweza kujiunga na CDM ili hali wanajibu maswali yasiyowahusu kabisa kujibu kisiasa...

Na kwa ujinga huo huo, Bakwata na waislaam wanaamini kabisa kwamba Wakristu ndio wapinzani wa Uislaam kutokana na majibu wanayoyapata. Wakiitazama Chadema ndio hawaoni hata mwanga, wakristu wanapinga vitu hivyo wazi wazi bila sababu za kisiasa isipokuwa kwa kutumia imani zao za dini wakasahau whjo is their enemy.. na huwezi kutumia sababu ya kidini kupinga ibada ya mwenzako hata siku moja - Itakuua kisiasa.

Mkuu wangu katika historia ya nchi zetu kutawaliwa na mkoloni, utakuta kwamba ni pale wananchi walipokubali kutengana wakamsahau adui yao kuwa mkoloni wakaanza kupambana wao kwa wao ndivyo mkoloni alivyoweza kutawala kwa miaka mingi zaidi.. Historia siku zote inatueleza kwamba halikuwa swala la kuunda vyama vya Upinzani vingi aukuwa na mawazo ya wagombea binafsi ndio ulikuwa na suluhisho Uhuru wao isipokuwa ni pale wananchi wengi walijipanga nyuma ya chama kimoja, chama ambacho kilikana kabisa kuzungumzia tofauti zao, wakapuuza na kuondoa tofauti zao, wakaunda UMOJA wenye nguvu kubwa na wakaifanya kazi moja nayo ni kumwondoa Mkoloni.

Kuzaliwa kwa TANU ni fundisho kubwa sana kwa WanaChadema, Nyerere aliweza hata kwenda misikitini na kuhutubia aliweza kucheza bao na waswahili na hata kuhudhuria ibada za Maulidi na Idd nasi tukahudhuria Christmas na Pasaka. Nyumba ya Mkristu walikuwa hawali nyama bila kuchinjwa na Muislaam hali kadhalika kina mama wakivaa wakivaa ushungi (mtandio) bila kubadilisha imani zao za dini kwa sababu tulihitaji UMOJA wetu zaidi ya vyama.

Na matokeo yake, TANU waliibuka Kidedea dhidi ya vyama vyote vilivyoendekeza ubaguzi wa kidini au kikabila. Na leo hii kutotambua kwamba adui wa Chadema sio Muislaam wala sii Bakwata isipokuwa ni CCM, hivyo kwa kila unapozungumzia Bakwata na Waislaam ndivyo hamta tofautiani na wanachama wa vyama vingine vya kina Marealle, Mtemvu na wengineo waliojikita ktk mutetea makundi ya watu.

Wewe jiulize why swala la Mahakama ya Kadhi na OIC linazungumziwa hadi kesho?..

Mkandara my brother. Kiukweli, vyama vyote viwili vinatumia udini. Nina uhakika wa 100% uchaguzi wa Uraisi wa mwaka jana, zilipigwa kampeni za waziwazi kanisani--kumchagua Slaa. CCM wakajibu na Mashehe. Kwenye udini, vyama vyote viwili viko hatiani.

Wanachokosea wadau wengi wa upinzani ni dhana kwamba 1)kiongozi wa upinzani ndio pekee wenye uchungu wa nchi na kuweza kutuongoza 2) ukiwa mwanachama wa CCM, basi wewe ni fisadi. Hizo dhana mbili ni potofu. Nikifuata analog yako ya mkoloni, TANU/CCM sio ndio hao hao waliomtoa mkoloni? sasa mbona na wao wamegeuka wakoloni.

Ili waTanzania tutoke, inabidi kufuata mikondo ya demokrasia, kwanza kabisa tuache ushabiki wa kisiasa na tuwe independent/objective thinkers. Kwa sababu GodBless Lema na Prof Maji Marefu hawana uwezo (kielimu) kuwa mawaziri wa nchi hii, pamoja na Nchimbi, Mama Sofia Simba, au Ezekiel Wenje. Ushanielewa? Mimi nadhani tatizo kubwa la wabongo wanazama penzini na wanasiasa, badala ya kuchambua sera kiuwazi.

Wanasiasa wote (sio Chadema au CCM) lao moja. Wanatafuta dola, na wakiikamata hawataki kuiachia. Wapiga kura tuna jukumu moja tu--kuchagua less greedy of them all.
 
nape chokonoa chokonoa tena.igunga ilikua mechi ya kirafiki.vueni gamba lingine tucheze mechi ya kweli.mia
 
mkuu nimeamua kuleta hii post baada ya ile ya kwako kufungwa na mods
ulisema chadema wamejichimbia kaburi kwa kupeleka wabunge wote igunga
hivi mkuu unaishi nchi hii hii au?unajua nilikuwa naheshimu sana post zako huko
kumbe na wewe ni hovyo,hujui kufanya analysis,umekosa mwelekeo
waombe radhi wakuu hapa jamvini kabla hatujatangaza vita na wewe!
 
Hawezi kuthubutu hata kuwasogelea wale Jamaa wawili waliobaki,pili mziki wa Chadema wanauogopa sn
 
Back
Top Bottom