Ifikie mahali tuelewe na kukubali kuwa Rais wa Tanzania ana uhuru wa kuvunja Katiba ya nchi kwa makusudi, na hakuna utaratibu wa kuzuia hilo kwa sasa

Ni kweli kabisa hivyo aendelee kuvunja tu kwani kipindi atakapopatikana raisi nwingine naye ataivunja kwa maslahi ya taifa kumuwajibisha yeye anayeona ana haki akili maarifa kuliko mtanzanaia mwingine anachokipanda mtu ndicho atakachovuna
 
Yule kiongozi wa dini Aliyekwenda Ikulu kumshauri Raisi kikwete Kuhusu mchakato wa katiba na hatimae kikwete akauchukua ushauri wake na kuyapiga na chini maoni ya wananchi (rasimu ya warioba) ndo aliyetuzamisha.
Kikwete Alimuogopa sana kiongozi yule wa dini .akavunja dhamira ya Taifa zima.
Hatuna la kufanya. Yameshatupata, tusubiri Novemba 2025!
 
Maneno mengi sana yanasemwa nchini kuwa mara nyingi Rais Magufuli anavunja katiba ya Jamhuri ya Tanzania kwa makusudi. Nakiri kuwa hata mimi kuna wakati nilishazungumzia hilo.

Baadae nilijiuliza ikiwa mimi ningekuwa ndio Magufuli, nikijua ninaweza kuvunja katiba kimakusudi na hakuna utaratibu wa mimi kuchukuliwa hatua yeyote, na pia sheria za nchi haziko kwa namna ya kufanya iwe rahisi kuchukuliwa hatua nikivunja katiba, je ningevunja katiba kimakusudi? Je, kiongozi wa upinzani angekuwa raisi angefanya hivyo?

Sasa suala la msingi ni kwamba, kwa nini Rais anavunja katiba? Lazima anakuwa na sababu - na najua sababu yake ni kwamba anafanya kitu ambacho anaona kina manufaa kwa Watanzania na Tanzania - yaani the end justifies the means. Nikatambua kwamba hiyo ndio mentality ya Magufuli, kwamba yeye akiona anataka kufanya jambo ambalo lina manufaa kwa nchi, basi yuko tayari kuvunja katiba ili kulifanya kwa manufaa ya nchi. Amefanya hivi katika mambo mengi sana.

Lakini sasa ni sahihi kikatiba? Hapo ndipo nilijiuliza sana. Nikagundua kwamba nchi yetu inatoa fursa, bila kutamka wazi, ya raisi kuvunja katiba kwa sasa. Suala la raisi kuvunja au kutovunja katiba limefanywa kuwa utashi wa raisi katika mazingira ya katiba na sheria zetu. Sasa sio kila raisi tutakaekuwa nae hapa Tanzania atakuwa na mentality au utashi wa aina ya Nyerere. Nyerere aliheshimu sana Katiba, alikuwa akitembea nayo mfukoni na kuisoma kila wakati japo alijua katiba ilimruhusu kuivunja.

Lakini ikumbukwe kuwa, mazingira ya katiba yetu kuvunjwa huenda ni jambo lilifanywa kwa makusudi kabisa kwamba tuwe na katiba inayotoa mazingira ya raisi kuivunja bila kuchukuliwa hatua katika mazingira fulani fulani ambayo anaona inafaa kuvunja katiba. Yaani kwa kifupi, tuna katiba ambayo inaruhusu raisi kuivunja kwa manufaa ya taifa, kwa hiyo raisi kuvunja katiba ni suala la kikatiba! Katiba yetu inampa raisi utashi wa kuivunja au kutoivunja. Ni sawa na mtu kuambiwa usiendeshe gari eneo hili zaidi ya 50km/hr, lakini hata ukiendesha zaidi ya 50km/hr, hutapewa adhabu. Sasa hapo ina maana kutoendesha zaidi ya 50km/hr ni suala la utashi, kama una sababu nzuri ya kuendesha zaidi ya 50km/hr ni wazi utafanya hivyo!

Kwa hiyo ifikie wakati tukubali tu, kwamba mazingira yaliyopo yanatoa fursa kwa mtu yeyote akiwa Rais wa Tanzania, (sio Magufuli pekee) kuvunja Katiba kwa makusudi na kusiwe na namna ya kudhibiti hilo. Ifikie mahali badala ya kupiga kelele juu ya Rais Magufuli kufanya hivyo basi tutafakari jinsi gani tunaweza kufanya hilo lisitokee huko mbele. Na pia kusema tunahitaji katiba mpya haitoshi, maana ni kelele tumeshaisikia sana. Suala sasa linapaswa kuwa ni nini cha kufanya ili tuwe na katiba mpya.
Wa kulaumiwa ni JK kwa kutumia mabilioni yetu katika mchakato wa kuandika Katiba mpya kisha akaitelekeza, huyu katuachia msala mkubwa mno.
 
Politics,politics,politics,politics.Nadhani mmetumwa na mabeberu ku-distabilize our country.Hapa kazi tu,siasa kulee.Napenda China na Japan wao kazi kwanza,siasa hazina nafasi.Ninyi mnatumikishwa na mabeberu sana,lakini arubaini yenu ipo.
 
Yule kiongozi wa dini Aliyekwenda Ikulu kumshauri Raisi kikwete Kuhusu mchakato wa katiba na hatimae kikwete akauchukua ushauri wake na kuyapiga na chini maoni ya wananchi (rasimu ya warioba) ndo aliyetuzamisha.
Kikwete Alimuogopa sana kiongozi yule wa dini .akavunja dhamira ya Taifa zima.
mkuu ni nanihuyo nimsomee arbadir
 
Chanzo cha kuleta mabadiliko ama kusimamia katiba mi binge then mahakama huru.. Wote hawa wameshagegedwa kwa nguvu na papasi mkuu.. Hakuna taasisi yoyote wala mhimili wowote zaidi ya CCM imara na yenye maono chanya wenye uwezo wa kunusuru hii hali.
Huyo Spika ni CCM. Jaji Mkuu ni CCM na huyo papasi mkuu ni CCM. Safari hii mbona mtakoma? Kila majina mtaita ila mjue mmeshikwa pabaya. CCM hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Jitahidi usome tena Kifungu cha Katiba kwa makini bila mihemuko utaelewa. JPM aliahidi kuilinda na kuitetea.
Soma tena utaelewa. Labda ainish vifungu vya Katiba vinavyomtia hatiani raisi akivunja katiba, kisha njoo uniambie utaratibu wa kisheria wa kufuata, halafu uniambie ikiwa utaratibu huio utaweza kutekelezwa katika mazingira yetu.

Katiba hutakiwi kujitahidi kuilinda, unatakiwa kuilinda na usipoilinda iwe na kipengele cha kukuwajibisha. Lakini tunachosema hapa ni kwamba Katiba ya Tanzania haiko hivyo. Inakuruhusu kuivunja ukiwa raisi bila kuwajibishwa.
 
Niliwahi kusema enzi za kuwa na katiba inayompa rais mamlaka yasiyohojiwa na kisha kutokushitakiwa kwa kosa lolote, hizo zama zimeshapita, kwani hiyo ndio sababu haswa ya msingi ya taasisi zetu nyingi kuwa dhaifu. Na hapa ndio unapokutana nchi inaendeshwa kwa utashi wa rais na sio kwa mujibu wa sheria na katiba. Unapopata rais mlevi wa madaraka udhaifu huo unajidhihirisha moja kwa moja.
Hewaaaa! Na hilo ndilo Nyerere alitaumbia hatukumuelewa. Tulidhani kwamba katiba haikuwa na tatizo tukitarajia kila raisi tutakaekuwa nae atakuwa kama Nyerere, Mwinyi na Kikwete!
 
Huyu nyerere ndio mnafki namba moja na leo mambo mengi tunagharimika kama taifa sababu ya upuuzi wake. Jitu lilikuwa rais,linaona mapungufu ya kikatiba then linaenda mbele za wananchi kuwatahadharisha wakati lilikuwa na nafasi ya kurekebisha.
Hewaaaa! Na hilo ndilo Nyerere alitaumbia hatukumuelewa. Tulidhani kwamba katiba haikuwa na tatizo tukitarajia kila raisi tutakaekuwa nae atakuwa kama Nyerere, Mwinyi na Kikwete!
 
Huyu nyerere ndio mnafki namba moja na leo mambo mengi tunagharimika kama taifa sababu ya upuuzi wake. Jitu lilikuwa rais,linaona mapungufu ya kikatiba then linaenda mbele za wananchi kuwatahadharisha wakati lilikuwa na nafasi ya kurekebisha.
Hahaha! Nyerere alikuwa akiona mema ndani ya kila mtu. Hivi unajua Nyerere inawezekana kabisa kuna watu Nyerere aliwasaidia kuwa maraisi na akasikitikia na kujutia huo uamuzi. Kwa hiyo tusimlaumu sana, aliamnini sana watu kuwa wana moyo kama wake.
 
Kwa uvunjaji huu Wa katiba kwa awamu hii, tungekuwa Na taasisi serious impeachment ingemuhusu rais wetu.Watu kwenye nchi zilizoendelea kidemokrasia ukivunja katiba hawana time Na wewe off you go!
 
Katiba Mpya ya wananchi ni hitaji letu since before 1992/95,tulikosea na tukarudia makosa tena 2014.Siyo jukumu la mtu,chama au taasisi mmoja,Watanzania wote kwa kada zetu tuwajibike.Hakuna Haki bila kuidai na kuipigania pale inapokosekana.
Kuna watu wanataka kutulazimisha tuamini kuwa wao ni bora kuliko wengine,nchi hii ni yetu sote.
 
Hapo naona kuna utata kidogo.Yaani yeye aamue mchakato wa katiba mpya ufanyike halafu tena yeye huyo huyo apige chini.Utata mtupu!
Wa kulaumiwa ni JK kwa kutumia mabilioni yetu katika mchakato wa kuandika Katiba mpya kisha akaitelekeza, huyu katuachia msala mkubwa mno.
 
Back
Top Bottom