Ifikie mahali tuelewe na kukubali kuwa Rais wa Tanzania ana uhuru wa kuvunja Katiba ya nchi kwa makusudi, na hakuna utaratibu wa kuzuia hilo kwa sasa

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
8,302
2,000
Maneno mengi sana yanasemwa nchini kuwa mara nyingi Rais Magufuli anavunja katiba ya Jamhuri ya Tanzania kwa makusudi. Nakiri kuwa hata mimi kuna wakati nilishazungumzia hilo.

Baadae nilijiuliza ikiwa mimi ningekuwa ndio Magufuli, nikijua ninaweza kuvunja katiba kimakusudi na hakuna utaratibu wa mimi kuchukuliwa hatua yeyote, na pia sheria za nchi haziko kwa namna ya kufanya iwe rahisi kuchukuliwa hatua nikivunja katiba, je ningevunja katiba kimakusudi? Je, kiongozi wa upinzani angekuwa raisi angefanya hivyo?

Sasa suala la msingi ni kwamba, kwa nini Rais anavunja katiba? Lazima anakuwa na sababu - na najua sababu yake ni kwamba anafanya kitu ambacho anaona kina manufaa kwa Watanzania na Tanzania - yaani the end justifies the means. Nikatambua kwamba hiyo ndio mentality ya Magufuli, kwamba yeye akiona anataka kufanya jambo ambalo lina manufaa kwa nchi, basi yuko tayari kuvunja katiba ili kulifanya kwa manufaa ya nchi. Amefanya hivi katika mambo mengi sana.

Lakini sasa ni sahihi kikatiba? Hapo ndipo nilijiuliza sana. Nikagundua kwamba nchi yetu inatoa fursa, bila kutamka wazi, ya raisi kuvunja katiba kwa sasa. Suala la raisi kuvunja au kutovunja katiba limefanywa kuwa utashi wa raisi katika mazingira ya katiba na sheria zetu. Sasa sio kila raisi tutakaekuwa nae hapa Tanzania atakuwa na mentality au utashi wa aina ya Nyerere. Nyerere aliheshimu sana Katiba, alikuwa akitembea nayo mfukoni na kuisoma kila wakati japo alijua katiba ilimruhusu kuivunja.

Lakini ikumbukwe kuwa, mazingira ya katiba yetu kuvunjwa huenda ni jambo lilifanywa kwa makusudi kabisa kwamba tuwe na katiba inayotoa mazingira ya raisi kuivunja bila kuchukuliwa hatua katika mazingira fulani fulani ambayo anaona inafaa kuvunja katiba. Yaani kwa kifupi, tuna katiba ambayo inaruhusu raisi kuivunja kwa manufaa ya taifa, kwa hiyo raisi kuvunja katiba ni suala la kikatiba! Katiba yetu inampa raisi utashi wa kuivunja au kutoivunja. Ni sawa na mtu kuambiwa usiendeshe gari eneo hili zaidi ya 50km/hr, lakini hata ukiendesha zaidi ya 50km/hr, hutapewa adhabu. Sasa hapo ina maana kutoendesha zaidi ya 50km/hr ni suala la utashi, kama una sababu nzuri ya kuendesha zaidi ya 50km/hr ni wazi utafanya hivyo!

Kwa hiyo ifikie wakati tukubali tu, kwamba mazingira yaliyopo yanatoa fursa kwa mtu yeyote akiwa Rais wa Tanzania, (sio Magufuli pekee) kuvunja Katiba kwa makusudi na kusiwe na namna ya kudhibiti hilo. Ifikie mahali badala ya kupiga kelele juu ya Rais Magufuli kufanya hivyo basi tutafakari jinsi gani tunaweza kufanya hilo lisitokee huko mbele. Na pia kusema tunahitaji katiba mpya haitoshi, maana ni kelele tumeshaisikia sana. Suala sasa linapaswa kuwa ni nini cha kufanya ili tuwe na katiba mpya.
 
MARKYAO

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
673
1,000

Lakini ikumbukwe kuwa, mazingira ya katiba yetu kuvunjwa huenda ni jambo lilifanywa kwa makusudi kabisa kwamba tuwe na katiba inayotoa mazingira ya raisi kuivunja bila kuchukuliwa hatua katika mazingira fulani fulani ambayo anaona inafaa kuvunja katiba. Yaani kwa kifupi, tuna katiba ambayo inaruhusu raisi kuivunja kwa manufaa ya taifa, kwa hiyo raisi kuvunja katiba ni suala la kikatiba! Katiba yetu inampa raisi utashi wa kuivunja au kutoivunja.

Chanzo cha kuleta mabadiliko ama kusimamia katiba mi binge then mahakama huru.. Wote hawa wameshagegedwa kwa nguvu na papasi mkuu.. Hakuna taasisi yoyote wala mhimili wowote zaidi ya CCM imara na yenye maono chanya wenye uwezo wa kunusuru hii hali.
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
8,302
2,000
Kuna mfano nimeweka hapo juu sijui kwa nini hauonekani. NImesema, kwa sasa kwa raisi wa Tanzania kuvunja katiba ya nchi, ni sawa na dereva kuambiwa, hata kwa kiapo, usiendeshe gari eneo hili zaidi ya 50km/hr, lakini hata ukiendesha zaidi ya 50km/hr, hutapewa adhabu. Sasa hapo ina maana kutoendesha zaidi ya 50km/hr ni suala la utashi, kama una sababu nzuri ya kuendesha zaidi ya 50km/hr ni wazi utafanya hivyo! Hakuna kitu tunaita "law enforcement" kukuzuia kuendesha zaidi ya 50km/hr, kama vile ninavyosema hakuna mazingira nchini ambayo yako effective katika kumdhibiti raisi kutovunja katiba. Akiamua anataka kuvunja katiba kwa jambo analoona kwa maoni yake linafaa kwa taifa ataivunja.

Ukitaka kuelewa kirahisi ni kwamba, kwa sasa, raisi wa Tanzania anaweza kuamua kumpiga risasi na kumuua raia hadharani, ikiwa ataona inafaa kufanya hivyo kwa manufaa ya taifa, na hawezi kufanywa lolote.
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
8,302
2,000
1572857927853.png

Alichomaanisha ni kwamba, wewe kama CAG, serikali ikiamua kuvunja taratibu za kifedha, na Bunge kutoidhibiti serikali katika kuvunja taratibu za kifedha, hilo sio suala lako, halikuhusu! Huna mamlaka ya kukemea au kutoa maoni hata kama wewe nio "Mkaguzi" wa fedha za serikali.
 
Zawadini

JF-Expert Member
Feb 2, 2012
1,293
2,000
Nikatambua kwamba hiyo ndio mentality ya Magufuli, kwamba yeye akiona anataka kufanya jambo ambalo lina manufaa kwa nchi, basi yuko tayari kuvunja katiba ili kulifanya kwa manufaa ya nchi. Amefanya hivi katika mambo mengi sana.

Lakini sasa ni sahihi kikatiba? Hapo ndipo nilijiuliza sana. Nikagundua kwamba nchi yetu inatoa fursa, bila kutamka wazi, ya raisi kuvunja katiba kwa sasa. Suala la raisi kuvunja au kutovunja katiba limefanywa kuwa utashi wa raisi katika mazingira ya katiba na sheria zetu. Sasa sio kila raisi tutakaekuwa nae hapa Tanzania atakuwa na mentality au utashi wa aina ya Nyerere. Nyerere aliheshimu sana Katiba, alikuwa akitembea nayo mfukoni na kuisoma kila wakati japo alijua katiba ilimruhusu kuivunja.

Lakini ikumbukwe kuwa, mazingira ya katiba yetu kuvunjwa huenda ni jambo lilifanywa kwa makusudi kabisa kwamba tuwe na katiba inayotoa mazingira ya raisi kuivunja bila kuchukuliwa hatua katika mazingira fulani fulani ambayo anaona inafaa kuvunja katiba. Yaani kwa kifupi, tuna katiba ambayo inaruhusu raisi kuivunja kwa manufaa ya taifa, kwa hiyo raisi kuvunja katiba ni suala la kikatiba! Katiba yetu inampa raisi utashi wa kuivunja au kutoivunja.
Kwa maneno haya maana yake Katiba haina maana? waliotunga Katiba waliitunga wakiwa hawana akili? Yaani tutunge Katiba ambayo inampa mtu mwanya wa kuivunja halafu iwe basi? Tukubali tu kwamba sasa ile kanuni ya checks and balances haipo; yaani tuna bunge na mahakama dhaifu au tuna jamii iliyojengwa kwa misingi ya uoga wa hali ya juu.
 
King Maker

Member
Mar 8, 2018
62
150
Jitahidi usome tena Kifungu cha Katiba kwa makini bila mihemuko utaelewa. JPM aliahidi kuilinda na kuitetea.
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
47,019
2,000
UKISHAKUWA RAIS WA JMT WEWE UKO JUU YA SHERIAAAAAAAA!
MBONA HAMUELEWIIIIII

OVA
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
51,640
2,000
Maneno mengi sana yanasemwa nchini kuwa mara nyingi Rais Magufuli anavunja katiba ya Jamhuri ya Tanzania kwa makusudi. Nakiri kuwa hata mimi kuna wakati nilishazungumzia hilo.

Baadae nilijiuliza ikiwa mimi ningekuwa ndio Magufuli, nikijua ninaweza kuvunja katiba kimakusudi na hakuna utaratibu wa mimi kuchukuliwa hatua yeyote, na pia sheria za nchi haziko kwa namna ya kufanya iwe rahisi kuchukuliwa hatua nikivunja katiba, je ningevunja katiba kimakusudi? Je, kiongozi wa upinzani angekuwa raisi angefanya hivyo?

Sasa suala la msingi ni kwamba, kwa nini Rais anavunja katiba? Lazima anakuwa na sababu - na najua sababu yake ni kwamba anafanya kitu ambacho anaona kina manufaa kwa Watanzania na Tanzania - yaani the end justifies the means. Nikatambua kwamba hiyo ndio mentality ya Magufuli, kwamba yeye akiona anataka kufanya jambo ambalo lina manufaa kwa nchi, basi yuko tayari kuvunja katiba ili kulifanya kwa manufaa ya nchi. Amefanya hivi katika mambo mengi sana.

Lakini sasa ni sahihi kikatiba? Hapo ndipo nilijiuliza sana. Nikagundua kwamba nchi yetu inatoa fursa, bila kutamka wazi, ya raisi kuvunja katiba kwa sasa. Suala la raisi kuvunja au kutovunja katiba limefanywa kuwa utashi wa raisi katika mazingira ya katiba na sheria zetu. Sasa sio kila raisi tutakaekuwa nae hapa Tanzania atakuwa na mentality au utashi wa aina ya Nyerere. Nyerere aliheshimu sana Katiba, alikuwa akitembea nayo mfukoni na kuisoma kila wakati japo alijua katiba ilimruhusu kuivunja.

Lakini ikumbukwe kuwa, mazingira ya katiba yetu kuvunjwa huenda ni jambo lilifanywa kwa makusudi kabisa kwamba tuwe na katiba inayotoa mazingira ya raisi kuivunja bila kuchukuliwa hatua katika mazingira fulani fulani ambayo anaona inafaa kuvunja katiba. Yaani kwa kifupi, tuna katiba ambayo inaruhusu raisi kuivunja kwa manufaa ya taifa, kwa hiyo raisi kuvunja katiba ni suala la kikatiba! Katiba yetu inampa raisi utashi wa kuivunja au kutoivunja. Ni sawa na mtu kuambiwa usiendeshe gari eneo hili zaidi ya 50km/hr, lakini hata ukiendesha zaidi ya 50km/hr, hutapewa adhabu. Sasa hapo ina maana kutoendesha zaidi ya 50km/hr ni suala la utashi, kama una sababu nzuri ya kuendesha zaidi ya 50km/hr ni wazi utafanya hivyo!

Kwa hiyo ifikie wakati tukubali tu, kwamba mazingira yaliyopo yanatoa fursa kwa mtu yeyote akiwa Rais wa Tanzania, (sio Magufuli pekee) kuvunja Katiba kwa makusudi na kusiwe na namna ya kudhibiti hilo. Ifikie mahali badala ya kupiga kelele juu ya Rais Magufuli kufanya hivyo basi tutafakari jinsi gani tunaweza kufanya hilo lisitokee huko mbele. Na pia kusema tunahitaji katiba mpya haitoshi, maana ni kelele tumeshaisikia sana. Suala sasa linapaswa kuwa ni nini cha kufanya ili tuwe na katiba mpya.
Kuna tatizo kubwa sana na dhana ya kwamba anavunja katiba kwa minajili ya "the end justifies the mean".

Unajuaje hilo?

Unajuaje kwamba havunji katiba ili aibe?

Akisema uuawe na firing squad kwa sababu "the end justifies the means" utakubali?
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
29,012
2,000
Kuna mfano nimeweka hapo juu sijui kwa nini hauonekani. NImesema, kwa sasa kwa raisi wa Tanzania kuvunja katiba ya nchi, ni sawa na dereva kuambiwa, hata kwa kiapo, usiendeshe gari eneo hili zaidi ya 50km/hr, lakini hata ukiendesha zaidi ya 50km/hr, hutapewa adhabu. Sasa hapo ina maana kutoendesha zaidi ya 50km/hr ni suala la utashi, kama una sababu nzuri ya kuendesha zaidi ya 50km/hr ni wazi utafanya hivyo! Hakuna kitu tunaita law enforcement" kama vile ninavyosema hakuna mazingira nchini ambayo yako effective katika kumdhibiti raisi kutovunja katiba akiamua anataka kuvunja katiba kwa jambo analoona kwa maoni yake linafaa kwa taifa.

Ukitaka kuelewa kirahisi ni kwamba, kwa sasa, raisi wa Tanzania anaweza kuamua kumpiga risasi na kumuua raia hadharani, ikiwa ataona inafaa kufanya hivyo kwa manufaa ya taifa, na hawezi kufanywa lolote.
Niliwahi kusema enzi za kuwa na katiba inayompa rais mamlaka yasiyohojiwa na kisha kutokushitakiwa kwa kosa lolote, hizo zama zimeshapita, kwani hiyo ndio sababu haswa ya msingi ya taasisi zetu nyingi kuwa dhaifu. Na hapa ndio unapokutana nchi inaendeshwa kwa utashi wa rais na sio kwa mujibu wa sheria na katiba. Unapopata rais mlevi wa madaraka udhaifu huo unajidhihirisha moja kwa moja.
 
LIMBOMAMBOMA

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
6,013
2,000
Mbaya zaidi watu wote wako kimya, kwa sasa hakuna mtetezi Wa katiba.Rais anavunja katiba apendavyo...
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
3,385
2,000
Ni muhimu sana tupate katiba mpya ili kuiweka vizuri mihimili ya check and balance, ili taratibu za kumwajibisha rais anapovunja katiba au sheria ziwekwe wazi. Kama ni kupitia bunge, mahakama au moja kwa moja kwa kupitia petitions za wananchi. Tukiacha loopholes tunaweza kushuhudia siku moja yanajitokeza yale ya zimbabwe, na hali ikawa mbaya sana.
 
battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
1,421
2,000
Yule kiongozi wa dini Aliyekwenda Ikulu kumshauri Raisi kikwete Kuhusu mchakato wa katiba na hatimae kikwete akauchukua ushauri wake na kuyapiga na chini maoni ya wananchi (rasimu ya warioba) ndo aliyetuzamisha.
Kikwete Alimuogopa sana kiongozi yule wa dini .akavunja dhamira ya Taifa zima.
 
Top Bottom