If Only Mama Could See Me Now. I Miss Her So So Much Jamani.

If Only Mama Could See Me Now. I Miss Her So So Much Jamani.

Kiswanglish could be a creole. Even in Europe, the European Commission has just announced an agreement whereby English will be the official language of the EU rather than German which was the other possibility.

As part of the negotiations, Her Majesty's Government conceded that English spelling had some room for improvement and has accepted a five year phase-in plan that would be known as "Euro-English".

In the first year, "s" will replace the soft "c". Sertainly, this will make the sivil servants jump with joy. The hard "c" will be dropped in favour of the "k". This should klear up konfusion and keyboards kan have 1 less letter.

There will be growing publik enthusiasm in the sekond year, when the troublesome "ph" will be replaced with "f". This will make words like "fotograf" 20% shorter.

In the 3rd year, publik akseptanse of the new spelling kan be ekspekted to reach the stage where more komplikated changes are possible. Governments will enkorage the removal of double letters, which have always ben a deterent to akurate speling. Also, al wil agre that the horible mes of the silent "e"s in the language is disgraseful, and they should go away.

By the fourth year, peopl wil be reseptiv to steps such as replasing "th" with "z" and "w" with "v". During ze fifz year, ze unesesary "o" kan be dropd from vords kontaining "ou" and similar changes vud of kors be aplid to ozer kombinations of leters.

After zis fifz yer, ve vil hav a reli sensibl riten styl. Zer vil be no mor trubl or difikultis and evrivun vil find it ezi to understand ech ozer. Ze drem vil finali kum tru! And zen world!

Aha! Europe English

Duuuuuuhh nimechoka...pipo mnajua mambo
 
asante love kwa pole. hahaha. ningezikubali zingeanza mwanzo mpaka mwisho. lols

Sometimes tunasema pole ili tujipooze na sie wenyewe. Mtu unahisi kuwa walao ukisema pole kwa kumhurumia mwenzio na wewe pia utapata ahueni kwa uchungu uliopata.
 
Pole. Unawezakuta jitu zima limesoma Kiingereza kuanzia darasa la tatu hadi chuo kikuu halafu linasizitiza kwa wengine watumie Kiswahili.

Yaani uzembe wake wa kutojua lugha anatupia kwa wengine. Atajibebea zigo lake mwenyewe.
EMT nadhani umemkandamiza mwenzako kuliko kawaida, binafsi namuunga mkono japo ni tatizo tumekuwa nalo wengi, inapendeza mtu kuandika au kuongea lugha moja. Na tatizo la kuchanganya lugha kunatuathiri tulio wengi, hata mwisho hatujui (baadhi) kuongea au kuandika vizuri..sio kingereza wala kiswahili..ni maoni tu mkuu EMT
 
Last edited by a moderator:
Karucee... Oh dear..anyway hutaki pole mamy...basi tena sijuw nsemeje
 
Last edited by a moderator:
Karucee mpenzi niko sehemu hatarishi and it is late lakini nashangilia kwa hii story yako and i know,you know why why am saying this.Nataka wanangu wawe mashahidi kwamba dad was there for us hata kama mama hakuwepo.AM TRYING TO GIVE MY KIDS THE BEST OF EVERY THING hata kama ni kwa gharama ya furaha yangu.................lol!

Nisingekuwa sehemu hatarishi ningekutafuta tukavute bangi pamoja......lol!
 
Kiswanglish could be a creole. Even in Europe, the European Commission has just announced an agreement whereby English will be the official language of the EU rather than German which was the other possibility.

As part of the negotiations, Her Majesty's Government conceded that English spelling had some room for improvement and has accepted a five year phase-in plan that would be known as "Euro-English".

In the first year, "s" will replace the soft "c". Sertainly, this will make the sivil servants jump with joy. The hard "c" will be dropped in favour of the "k". This should klear up konfusion and keyboards kan have 1 less letter.

There will be growing publik enthusiasm in the sekond year, when the troublesome "ph" will be replaced with "f". This will make words like "fotograf" 20% shorter.

In the 3rd year, publik akseptanse of the new spelling kan be ekspekted to reach the stage where more komplikated changes are possible. Governments will enkorage the removal of double letters, which have always ben a deterent to akurate speling. Also, al wil agre that the horible mes of the silent "e"s in the language is disgraseful, and they should go away.

By the fourth year, peopl wil be reseptiv to steps such as replasing "th" with "z" and "w" with "v". During ze fifz year, ze unesesary "o" kan be dropd from vords kontaining "ou" and similar changes vud of kors be aplid to ozer kombinations of leters.

After zis fifz yer, ve vil hav a reli sensibl riten styl. Zer vil be no mor trubl or difikultis and evrivun vil find it ezi to understand ech ozer. Ze drem vil finali kum tru! And zen world!

Aha! Europe English
EMT,IQ yako ni kubwa sana,i salute you
 
Mhhh! Hongera zako wewe na mdogo wako. Thanks a lot for sharing this very powerful article....hadi machozi yamenilengalenga. Pole sana

Leo mie Karucee ngoja niwape story ya maisha yangu. Natanguliza kwa kusema please msinipe sorry. Sihitaji kuambiwa pole kwasababu nimeshakubali niliyoyapitia kama sehemu iliyonijenga na leo hii mimi ni Karucee because of my past.

Mie ni mtoto wa kwanza katika familia yetu. Nina mdogo wangu wa kike ambae hatujapishana sana umri. Tulivyokuwa wadogo, tulikuwa na kawaida ya kwenda kumtembelea bibi yetu likizo nzima shule zinapofungwa. Shule zinapokaribia kufunguliwa wazazi wetu walikuwa wanatufata.

Basi likizo moja, shule zilifungwa na tukaenda kijijini kama kawaida. Tulikuwa tunapenda sana kwenda kijijini manake Grandma was so much fun. Tulikuwa tunapenda kukamua ng'ombe na kupeleka Creameries, tunaenda kuwalisha ng'ombe, Fishing, Swimming etc. Basi, Likizo ilipokaribia kuisha wazazi wetu hawakutufata. Shule zikafunguliwa, wapi? Siku zikaenda, wapi? MAma alikuja kututembelea mara moja moja, tukawa tunaandika notes anampelekea Daddy.

Basi, tukapelekwa shule huko huko kijijini. MAisha yalibadilika sana. Tulikuwa tunaamka kukiwa bado na giza, tunatembea mbali kwenda shule. Mchana tunatembea tena kuja kula.. ikafika mahali tukawa tunabeba chakula to save us the lunch time trip. Halafu tulikuwa kama tu celebs flani hali ambayo nilikuwa sipendi. Mfano tulikuwa watoto pekee waliokuwa wanavaa viatu. BAsi baba akaanza kuja kutufata shule siku za Ijumaa, halafu anaturudisha Jumatatu asubuhi mapemaaaa. Jioni tukirudi kwa bibi anatuchapa. Nikawa nagoma kwenda kwa baba ili nisipigwe na bibi. Mdogo wangu alikuwa anaenda kama kawaida, ila akirudi Jumatatu jioni tunachapwa wote. Nikaona bora tu nijiendee kwa baba nisichapwe bure.

Grandma had changed so much. Hakuwahi hata kutufokea even once. Leo hii alikuwa anatuchapa? Tena kwa haasira? Why couldnt anyone just tell us tatizo ni nini? What wrong had we done? Why were we suffering?? Where we our parents? Why werent we at home??

Shule zilipofungwa, baba alituiba. Alitusubiri tunatoka getini akatuiba. Nasema alituiba kwa sababu hakumpa bibi taarifa. MAisha na baba yetu yakaanza. Mie mpaka hapo pamoja na umri wangu wa miaka 10 nilikuwa nimeshapata picha kuwa wazazi wetu wameshaachana. Sikujua mama alikuwa wapi, I always assumed she was taking a breath angerudi. All these years.

I really admire my little sister. She was like a butterfly on a sunny day. Flying from flower to flower with no care in the world. Mimi ndie nilikuwa naumia. Mtoto wa baba alikuwa hata hajui nini kinaendelea. Labda ndio maana mpaka leo she misses Ma but isnt bothered as such by her absence. She doesnt even remember how Ma looked. Poor Girl.

BAsi, life with Daddy began. Life was carefree. Hamna kulazimishwa kula vegetables. It was a carefree life. Cookies, French fries, sausages, burgers... It was just the three of us. Shule nilikuwa naenda kama kawaida. Ila dogo bwana alikuwa anaenda siku anazotaka. Spoilt brat. Asubuhi tunaenda garage na baba.(Baba ni fundi magari) tunarudi jioni tukishakula icecream na ku watch movies. Siku zikaenda, miaka ikapita, mama didnt come back.

We no longer we Daddy's little girls. Tukakua. Hapo ndio nahisi ugumu wa kulea mabinti wakubwa ulipoanza. BAba akaoa. On condition that huyo mdada ajue amekuja kwa ajili yetu and she would leave if she did us wrong. Mie I didnt welcome her. Nilimpotezea mpaka namaliza form four.

Siku moja, nakaribia kufanya mtihani wa kumaliza Shule ya msingi kuna mgeni alikuja home. Nakumbuka nilikuwa nakosha vyombo. Nikafuta mikono na kwenda kumsalimia. Halafu nikaendelea na kazi yangu. BAsi nimemaliza kuosha vyombo nikawa naenda nje kununua sijui nini, ile napita karibu na mgeni nikaangusha coin. BAhati mbaya ikaenda mpaka miguuni kwa mgeni. Nikazunguka nikajificha nyuma yake nikaokota huku na blush kwa aibu. Ile nainama kuokota nikaangalia ukucha wa kidole gumba cha mgeni. Moyo wangu ukastuka. Nikamwangalia usoni. Alikuwa ni Mama Yangu. Na alikuwa analia kishenzi.

Mh. Tukaanza kulia sote watatu. Ma mdogo ametuangalia ameduwaa. Anyway baba alikuja na wakasalimiana vizuri tu. Tukaenda kwa bibi yetu kukaa na mama kwa siku mbili tatu halafu mama aliondoka. Alituambia anaishi mji mwingine na alituambia anatupenda and nothing will ever change that. Alituomba yule ma mdogo tusimuite mama hata siku moja because she was the original and biological mother. Akaniambia always work hard, for some day you will save me. Nililia sana.

Basi maisha yakaendelea. Miaka ikapita. NIkafaulu vizuri tu nikajiunga na shule ya sekondari, nikamaliza. Nikaingia chuo kikuu, nikafaulu, nikaendeleza masomo. Mama never came back. To date. I really miss her. The pain is gone, nimeacha kulia whenever I think of her. Nimeolewa na najua ndoa ina mengi so na hiki kimechangia kunipa nguvu. People suggest kwamba hayupo duniani but my heart tells me yupo na ipo siku atarudi.

If she could see me now. Her little girls are no longer tiny. I am a mother now. Ma ameondoka sina hata nyonyo. Now I have a child of my own. Aliniambia niwe kama mama kwa mdogo wangu, my sister is doing well too. Atarudi lini? I do not know. But kila siku ya Mungu namuombea. Asilale na njaa, Mungu ampe chakula. Asishinde na kiu, Mungu ampe maji. Asitembee uchi, Mungu ampe nguo, Asimsahau Mungu, Mungu awashe taa moyoni mwake, amuongoze kwenye njia iliyonyooka. Ipo siku atarudi. Bibi mzaa mama alifariki Mama hakuja kwenye msiba. NImeolewa hakuwepo. It was just my sis and Daddy. But I refused to cry, labda baba angejisikia vibaya. But I continue to believe Mama yupo hai, somewhere beneath God's skies.

Mungu hakunyimi kila kitu. Alitupa baba yetu. Anaetupenda kuliko kitu chochote duniani. Alipooa alipata watoto wengine wanne, ila nafasi yetu ipo palepale. Ma mdogo alibadilika alipozaa ila tulivumilia ili baba apate amani. My Daddy is the wind beneath my wings. He is my friend. I can call him any time, to tell him anything. He has opened my eyes into this world. Whenever we were overwhelmed by the sight of other girls with their mothers he was always there for us.

Malezi ya baba yalikuwa ya kisela sana. Pata picha sote tumevaa overalls sare tupo garage tunahangaika. Baba akitukana na sisi tunatukana. Tumeshika spanner zetu. Baba akiita naomba namba 13 tunakimbia fasta kwenye toolbox tunamletea. Tukienda kuvuta magari yalopata ajali na breakdown unatukuta tumekaa juu kwenye bodi tumening'inia tunaenda na baba yetu. Baba ametufundisha mengi sana. We could see through men. Tulijulikana kama watoto wa simba. Ole wako akuone ukimtazama his lovely daughters the wrong way. Unachezea za usoni fasta. Hatukudanganyika mapema. Malezi ya baba yametufanya tuwe very strong women. Hatukupapa opportunity ya kukua around women so kidogo hatujui ku relate na wanawake wenzetu and since udogoni men have been our best friends.

Natamani arudi. Natamani aone tu binti twake. NAtamani aone how hard I worked at school. It has been 20 years. Ndugu zake hawasemi chochote. Tumefikia mwisho wa kumtafuta. Hatujui kilichobaki isipokuwa kusubiri tuone Mungu amepanga nini. If only she could see us now. Would she be proud of us? Would she commend Daddy on the good job he has done?

If you are a single dad, know that you can make it. Mtangulize Mungu. Na kama upo kwenye ndoa na pamoja na matatizo yake kuna option ya kuendelea kuwepo please tulia uwalee wanao. Maisha ya kulelewa na mama wa kambo sio rahisi. NI wachache sana ambao wanaweza ku share interest ulizo nazo kwa wanao.

Ni hayo tu.:yo:

EMT, Wi-Fi SnowBall, Mentor, Kaizer, gobore, snowhite, KIKUNGU, Kaunga, King'asti, Kongosho, The secretary, figganigga, Hoshea, Kamanda Moshi, mzabzab, Mjuni Lwambo and a couple others.
 
Oooh mimi nisipo kupa pole ntakua heartless maybe

But am happy for standing still and be a superwoman despite of everything...Mungu asikie kilio chako cha kutaka kumwona mama tena...we all goin to pray for her superdiaaa
 
karucee mbona hujani cc na nilikuomba?
ila MUNGU ni mwema muombe atakurudishia mama yako.
nitakuombea pia.
pia pongezi nyingi kwa baba yako,but what if yeye ndo chanzo cha mama kupotea..hayo mazuri yake yataweza kulipa uchungu wa kumpoteza mazeri hivo?

Mhhhhh smile i don think kama that words ni constructive maana zinachochea chuki kwa baba yake kipenz. U just cheer out with her that she can still get comfort
 
this is one of the best story in jf.na mimi nimekulia malezi ya single mum,nimejifunza mengi tu,moja wapo kutokuwa tegemezi na ku work hard in life.na kushukuru kwa jambo lolote lile,hata liwe dogo vipi.
kisukari. Gratitude, hata kwa jambo dogo vipi ni muhimu kwakweli. HAta uwe huna shilingi mfukoni mshukuru Mungu kwa kuwa na afya. etc etc. Big up to your Ma.
 
Last edited by a moderator:
Karucee mpenzi niko sehemu hatarishi and it is late lakini nashangilia kwa hii story yako and i know,you know why why am saying this.Nataka wanangu wawe mashahidi kwamba dad was there for us hata kama mama hakuwepo.AM TRYING TO GIVE MY KIDS THE BEST OF EVERY THING hata kama ni kwa gharama ya furaha yangu.................lol!

Nisingekuwa sehemu hatarishi ningekutafuta tukavute bangi pamoja......lol!

HAhahahahaahah. KIKUNGU. Pole kwa kuwepo sehemu hatarishi Mungu akutangulie. As for your kids, do not worry. They will turn out just right. Mtangulize Mungu. They know you are truly doing your very best. Mungu akupe afya nzuri, umri mrefu na uwezo mupate ku grow old together. There shall be a very beautiful ending to the story.
 
Last edited by a moderator:
Mhhhhh smile i don think kama that words ni constructive maana zinachochea chuki kwa baba yake kipenz. U just cheer out with her that she can still get comfort
Thanks Khakhi kwa kuliona hilo. My Daddy is flawless in my eyes. He is not capable of doing any wrong no matter what anyone says. We have cut off people from our lives for simply trying to turn our Daddy against us.
He was there for us when we were on the verge of becoming street urchins. He was there for us when no one else was. Who dares to point an accusing finger at him?
 
Last edited by a moderator:
Daaah hii story naisoma mara mbili mbili kwakweli ni moja ya story zilizo ni vutia sana! Me like your stories Karucee!

Yani kwakweli hapo kwenda garage na baba yenu yani ndio pame ni bamba sana, sijui kama mabinti wa sasa wanaweza kukubali, hakika baba yenu aliwafanya kuwa strong kwa hii life style.
Sipati pichaaa!
spellbound Ruttashobolwa, huh? hahahhahaa. I wish unione leo hii riding a tyre napeleka izibwe pancha kwa fundi halafu nafungua na kufunga mwenyewe. Gari kubwa inanishinda but vi saloon havinishindi kubadili tyre. God bless my Dad and All the JF Daddies.
We are really strong. Tunamshukuru Mungu.
 
Last edited by a moderator:
Karucee, kama alivyosema Snowhite, hii ni zaidi ya thread, ina vitu flani ndani yake ambavyo binafsi nakosa maneno ya kuelezea,
Imenifanya nimejiona mpweke na mkiwa sana japo mimi mama mzazi yupo hai kijijini na nawasiliana nae marakwa mara nikiwa sina nafasi ya kwenda kumuona.
Kinachosababisha nisitoe chozi ni kwa kuwa tu mimi ni mtoto wa kiume na ninaamini kulia ni ishara ya udhaifu.

Everything which happened, happened for a purpose, yaani ni kama movie vile kwamba kila unachokiona kina implication yake,
Mungu anajua ni kwa nini hayo yametokea, na furahini kwa kila jambo, this post has made me motionless and thoughtfuly.
 
Mhhh! Hongera zako wewe na mdogo wako. Thanks a lot for sharing this very powerful article....hadi machozi yamenilengalenga. Pole sana
Thanks BAK, tunamshukuru Mungu kwa yote.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Leo mie Karucee ngoja niwape story ya maisha yangu. Natanguliza kwa kusema please msinipe sorry. Sihitaji kuambiwa pole kwasababu nimeshakubali niliyoyapitia kama sehemu iliyonijenga na leo hii mimi ni Karucee because of my past.


Naelewa kwa nini haujataka pole. What you, your dad and your sis deserve ni pongezi kwa kuwa na ujasiri wa kuhimili hii changamoto na kufikia hapo mlipofikia. Kuna wengi ambao wamekutana na madogo kuliko hili na wameishia pabaya kwa kukosa ujasiri kama wenu, hawa ndio wanatakiwa kupewa pole. Msiache kumshukuru Mungu kwa kuwasimamia siku zote, na mimi naungana na wewe kumuombea mama yako popote alipo, maana deep down naamini, whatever her reasons for leaving you are, anaumia sana kukosa kuwa nanyi watoto wake. Na nakubaliana na wewe you are who you are today because of that past.

Story yako ni kama ya mama yangu mzazi. Yeye mama yake aliondoka when my mom was only 13 na hakuwahi kurudi hadi leo na inasemekana bado yupo hai ktk nchi moja jirani. Marehemu babu yangu aliwalea mama yangu na ndugu zake yeye mwenyewe hadi wote walipokuwa na kuondoka nyumbani ndipo alipooa mke mwingine. Mama yangu ndiye alikuwa last born so ndiye alikuwa wa mwisho kuondoka home na ndiye aliyeexperience zaidi malezi ya baba peke yake, but she emerged to be the strongest of all the siblings. Namuona mama yangu kuwa ni mwanamke wa kipekee na naamini hio imechangiwa kwa kiasi kikubwa na past yake. Imani yangu kuwa mama yangu ni mwanamke wa kipekee inasababishwa na malezi aliyotupa mimi na ndugu zangu.

Unlike Karucee, my mom au @Zongwale, mimi simjui baba yangu kabisa, wala ndugu yeyote wa upande wake. Mama yangu alipomwambia mwanaume anayetakiwa kuwa baba yangu kuwa ana ujauzito wake, mwanaume huyo alikataa kuhusika na huo ujauzito. Mama yangu akaona isiwe shida akampotezea mazima. Na hiyo ni miaka ya nyuma ambapo mtu unatoka kijijini kwenu kuja Dar kusoma chuo, na si ajabu ukawa hauna ndugu hata mmoja Dar (Mama yangu hakuwa na ndugu yeyote Dar na vivyo hivyo huyo "baba" yangu) so baada ya kumpotezea huyo baba ndio ilikuwa ndio ntolee hiyo, hakuna ndugu mwingine aliyemfahamu na hakuona sababu ya kuwafahamu at that point, na namuelewa. The last she heard of him ni kuwa aliondoka na kuelekea ktk nchi moja kusini mwa Africa, whether he is dead or alive I don't want to know.

Mama yangu alinilea peke yake na kunipa mapenzi yote na ya ziada maana alijijua yeye ndiye mama na baba. Hii haikuwa rahisi lakini hakutetereka. Na kwa mapenzi aliyonipa, sikuwahi hata siku moja kuuliza baba yangu yupo wapi maana sikuhisi kama napungukiwa chochote ktk maisha yangu. Na mara zote mama yangu alizojaribu kunielezea kuhusu baba yangu, sikuwahi kuonyesha any interest japo nilikuwa mdogo, hadi alijiachia. Mama yangu hakutaka kuolewa kwa sababu hakutaka mimi nijiskie mpweke ninapowaona ndugu zangu wakiwa na baba yao wakati wangu is nowhere to be traced (Hii niliiskia akimwambia aunt yangu fulani hivi, wakati huo nikiwa na miaka kama 10 hivi). In fact hakupanga kuzaa tena ila later aligundua kuwa ni bora azae anipe ndugu kuliko kuniacha peke yangu, ndio maana kuna gap kubwa sana kati yangu na wadogo zangu.

She has other kids with other men but wote ametupa surname yake. Wanaume aliozaa nao hao ndugu zangu walikuwa na familia zao so the fact kuwa mama yangu alionekana kuwa willing kulea watoto mwenyewe waliichukulia poa tu. Wadogo zangu wanawajua ndugu za baba zao but hawana any formal communication nao kama ndugu. Cousins wao ambao wana mawasiliano nao ni mawasiliano ya kirafiki zaidi kuliko ya kindugu na ni kwa sababu labda wamekutana shuleni au vyuoni. Mimi na wadogo zangu ni watoto wa mama na ni watoto wake peke yake, na mama yetu hajawahi kuwakataza wadogo zangu kuwa na mahusiano na ndugu za baba zao, lakini I guess wao wenyewe hawoni umuhimu huo. Hata katika nyakati ngumu zaidi tulizopitia ktk maisha yetu na mama yetu, hakuna hata mmoja wetu aliyewahi kutaka kwenda kwa baba yake wala kunung'unika kuwa maisha yangekuwa tofauti kama baba zetu wangekuwepo, hii ni kwa sababu ya upendo mama yetu aliokuwa anatupa. Mimi alishanipa links za kuweza kumjua mtoto mwingine wa "baba" yangu (ambaye naye alimkataa anyway; nahisi alikuwa na pepo huyo baba, LOL!) ila sijawahi hata kuhisi nataka kumjua huyo kijana maana sioni kama tuna uhusiano wowote. Hatuwachukii baba zetu ila they are insignificant kwetu.


Sote ni watu wazima now na tunamshukuru Mungu maisha yetu si mabaya. Mimi nina familia (spouse na watoto), wadogo zangu bado wapo wapo. Tunampenda mama yetu hadi hatumpendi tena. Si mama yetu tu bali ni rafiki yetu.
I grew up to become a strong, positive and happy person, maana maisha niliyoishi yamenifundisha to always look at the bright side of life na kuyaangalia maisha kama yalivyo rather than vile yanavyotakiwa kuwa. Nimejifunza kuenjoy every moment of my life maana huwezi kujua kesho itakuwaje, coz maisha yangu yalikuwa ni yale ya what if Mungu akimchukua mama kesho. Namshukuru Mungu kwa kila jambo na sitaacha kumtegemea yeye, maana hakumchukua mama yetu hadi leo so tumekuwa tukifurahia maisha hadi leo. Namuomba Mungu kila siku amzidishie maisha marefu, aone mafanikio ya watoto wake maana hiyo ndio faraja yake na mapozo ya shida zote alizopitia kutulea peke yake. Namuomba pia anijalie nami niweze kuwapa upendo watoto wangu kama alionipa mama yangu.
 
Back
Top Bottom