Leo mie Karucee ngoja niwape story ya maisha yangu. Natanguliza kwa kusema please msinipe sorry. Sihitaji kuambiwa pole kwasababu nimeshakubali niliyoyapitia kama sehemu iliyonijenga na leo hii mimi ni Karucee because of my past.
Naelewa kwa nini haujataka pole. What you, your dad and your sis deserve ni pongezi kwa kuwa na ujasiri wa kuhimili hii changamoto na kufikia hapo mlipofikia. Kuna wengi ambao wamekutana na madogo kuliko hili na wameishia pabaya kwa kukosa ujasiri kama wenu, hawa ndio wanatakiwa kupewa pole. Msiache kumshukuru Mungu kwa kuwasimamia siku zote, na mimi naungana na wewe kumuombea mama yako popote alipo, maana deep down naamini, whatever her reasons for leaving you are, anaumia sana kukosa kuwa nanyi watoto wake. Na nakubaliana na wewe you are who you are today because of that past.
Story yako ni kama ya mama yangu mzazi. Yeye mama yake aliondoka when my mom was only 13 na hakuwahi kurudi hadi leo na inasemekana bado yupo hai ktk nchi moja jirani. Marehemu babu yangu aliwalea mama yangu na ndugu zake yeye mwenyewe hadi wote walipokuwa na kuondoka nyumbani ndipo alipooa mke mwingine. Mama yangu ndiye alikuwa last born so ndiye alikuwa wa mwisho kuondoka home na ndiye aliyeexperience zaidi malezi ya baba peke yake, but she emerged to be the strongest of all the siblings. Namuona mama yangu kuwa ni mwanamke wa kipekee na naamini hio imechangiwa kwa kiasi kikubwa na past yake. Imani yangu kuwa mama yangu ni mwanamke wa kipekee inasababishwa na malezi aliyotupa mimi na ndugu zangu.
Unlike
Karucee, my mom au @Zongwale, mimi simjui baba yangu kabisa, wala ndugu yeyote wa upande wake. Mama yangu alipomwambia mwanaume anayetakiwa kuwa baba yangu kuwa ana ujauzito wake, mwanaume huyo alikataa kuhusika na huo ujauzito. Mama yangu akaona isiwe shida akampotezea mazima. Na hiyo ni miaka ya nyuma ambapo mtu unatoka kijijini kwenu kuja Dar kusoma chuo, na si ajabu ukawa hauna ndugu hata mmoja Dar (Mama yangu hakuwa na ndugu yeyote Dar na vivyo hivyo huyo "baba" yangu) so baada ya kumpotezea huyo baba ndio ilikuwa ndio ntolee hiyo, hakuna ndugu mwingine aliyemfahamu na hakuona sababu ya kuwafahamu at that point, na namuelewa. The last she heard of him ni kuwa aliondoka na kuelekea ktk nchi moja kusini mwa Africa, whether he is dead or alive I don't want to know.
Mama yangu alinilea peke yake na kunipa mapenzi yote na ya ziada maana alijijua yeye ndiye mama na baba. Hii haikuwa rahisi lakini hakutetereka. Na kwa mapenzi aliyonipa, sikuwahi hata siku moja kuuliza baba yangu yupo wapi maana sikuhisi kama napungukiwa chochote ktk maisha yangu. Na mara zote mama yangu alizojaribu kunielezea kuhusu baba yangu, sikuwahi kuonyesha any interest japo nilikuwa mdogo, hadi alijiachia. Mama yangu hakutaka kuolewa kwa sababu hakutaka mimi nijiskie mpweke ninapowaona ndugu zangu wakiwa na baba yao wakati wangu is nowhere to be traced (Hii niliiskia akimwambia aunt yangu fulani hivi, wakati huo nikiwa na miaka kama 10 hivi). In fact hakupanga kuzaa tena ila later aligundua kuwa ni bora azae anipe ndugu kuliko kuniacha peke yangu, ndio maana kuna gap kubwa sana kati yangu na wadogo zangu.
She has other kids with other men but wote ametupa surname yake. Wanaume aliozaa nao hao ndugu zangu walikuwa na familia zao so the fact kuwa mama yangu alionekana kuwa willing kulea watoto mwenyewe waliichukulia poa tu. Wadogo zangu wanawajua ndugu za baba zao but hawana any formal communication nao kama ndugu. Cousins wao ambao wana mawasiliano nao ni mawasiliano ya kirafiki zaidi kuliko ya kindugu na ni kwa sababu labda wamekutana shuleni au vyuoni. Mimi na wadogo zangu ni watoto wa mama na ni watoto wake peke yake, na mama yetu hajawahi kuwakataza wadogo zangu kuwa na mahusiano na ndugu za baba zao, lakini I guess wao wenyewe hawoni umuhimu huo. Hata katika nyakati ngumu zaidi tulizopitia ktk maisha yetu na mama yetu, hakuna hata mmoja wetu aliyewahi kutaka kwenda kwa baba yake wala kunung'unika kuwa maisha yangekuwa tofauti kama baba zetu wangekuwepo, hii ni kwa sababu ya upendo mama yetu aliokuwa anatupa. Mimi alishanipa links za kuweza kumjua mtoto mwingine wa "baba" yangu (ambaye naye alimkataa anyway; nahisi alikuwa na pepo huyo baba, LOL!) ila sijawahi hata kuhisi nataka kumjua huyo kijana maana sioni kama tuna uhusiano wowote. Hatuwachukii baba zetu ila they are insignificant kwetu.
Sote ni watu wazima now na tunamshukuru Mungu maisha yetu si mabaya. Mimi nina familia (spouse na watoto), wadogo zangu bado wapo wapo. Tunampenda mama yetu hadi hatumpendi tena. Si mama yetu tu bali ni rafiki yetu.
I grew up to become a strong, positive and happy person, maana maisha niliyoishi yamenifundisha to always look at the bright side of life na kuyaangalia maisha kama yalivyo rather than vile yanavyotakiwa kuwa. Nimejifunza kuenjoy every moment of my life maana huwezi kujua kesho itakuwaje, coz maisha yangu yalikuwa ni yale ya what if Mungu akimchukua mama kesho. Namshukuru Mungu kwa kila jambo na sitaacha kumtegemea yeye, maana hakumchukua mama yetu hadi leo so tumekuwa tukifurahia maisha hadi leo. Namuomba Mungu kila siku amzidishie maisha marefu, aone mafanikio ya watoto wake maana hiyo ndio faraja yake na mapozo ya shida zote alizopitia kutulea peke yake. Namuomba pia anijalie nami niweze kuwapa upendo watoto wangu kama alionipa mama yangu.