If Only Mama Could See Me Now. I Miss Her So So Much Jamani.

Karucee

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
18,146
34,190
Leo mie Karucee ngoja niwape story ya maisha yangu. Natanguliza kwa kusema please msinipe sorry. Sihitaji kuambiwa pole kwasababu nimeshakubali niliyoyapitia kama sehemu iliyonijenga na leo hii mimi ni Karucee because of my past.

Mie ni mtoto wa kwanza katika familia yetu. Nina mdogo wangu wa kike ambae hatujapishana sana umri. Tulivyokuwa wadogo, tulikuwa na kawaida ya kwenda kumtembelea bibi yetu likizo nzima shule zinapofungwa. Shule zinapokaribia kufunguliwa wazazi wetu walikuwa wanatufata.

Basi likizo moja, shule zilifungwa na tukaenda kijijini kama kawaida. Tulikuwa tunapenda sana kwenda kijijini manake Grandma was so much fun. Tulikuwa tunapenda kukamua ng'ombe na kupeleka Creameries, tunaenda kuwalisha ng'ombe, Fishing, Swimming etc. Basi, Likizo ilipokaribia kuisha wazazi wetu hawakutufata. Shule zikafunguliwa, wapi? Siku zikaenda, wapi? MAma alikuja kututembelea mara moja moja, tukawa tunaandika notes anampelekea Daddy.

Basi, tukapelekwa shule huko huko kijijini. MAisha yalibadilika sana. Tulikuwa tunaamka kukiwa bado na giza, tunatembea mbali kwenda shule. Mchana tunatembea tena kuja kula.. ikafika mahali tukawa tunabeba chakula to save us the lunch time trip. Halafu tulikuwa kama tu celebs flani hali ambayo nilikuwa sipendi. Mfano tulikuwa watoto pekee waliokuwa wanavaa viatu. BAsi baba akaanza kuja kutufata shule siku za Ijumaa, halafu anaturudisha Jumatatu asubuhi mapemaaaa. Jioni tukirudi kwa bibi anatuchapa. Nikawa nagoma kwenda kwa baba ili nisipigwe na bibi. Mdogo wangu alikuwa anaenda kama kawaida, ila akirudi Jumatatu jioni tunachapwa wote. Nikaona bora tu nijiendee kwa baba nisichapwe bure.

Grandma had changed so much. Hakuwahi hata kutufokea even once. Leo hii alikuwa anatuchapa? Tena kwa haasira? Why couldnt anyone just tell us tatizo ni nini? What wrong had we done? Why were we suffering?? Where we our parents? Why werent we at home??

Shule zilipofungwa, baba alituiba. Alitusubiri tunatoka getini akatuiba. Nasema alituiba kwa sababu hakumpa bibi taarifa. MAisha na baba yetu yakaanza. Mie mpaka hapo pamoja na umri wangu wa miaka 10 nilikuwa nimeshapata picha kuwa wazazi wetu wameshaachana. Sikujua mama alikuwa wapi, I always assumed she was taking a breath angerudi. All these years.

I really admire my little sister. She was like a butterfly on a sunny day. Flying from flower to flower with no care in the world. Mimi ndie nilikuwa naumia. Mtoto wa baba alikuwa hata hajui nini kinaendelea. Labda ndio maana mpaka leo she misses Ma but isnt bothered as such by her absence. She doesnt even remember how Ma looked. Poor Girl.

BAsi, life with Daddy began. Life was carefree. Hamna kulazimishwa kula vegetables. It was a carefree life. Cookies, French fries, sausages, burgers... It was just the three of us. Shule nilikuwa naenda kama kawaida. Ila dogo bwana alikuwa anaenda siku anazotaka. Spoilt brat. Asubuhi tunaenda garage na baba.(Baba ni fundi magari) tunarudi jioni tukishakula icecream na ku watch movies. Siku zikaenda, miaka ikapita, mama didnt come back.

We no longer we Daddy's little girls. Tukakua. Hapo ndio nahisi ugumu wa kulea mabinti wakubwa ulipoanza. BAba akaoa. On condition that huyo mdada ajue amekuja kwa ajili yetu and she would leave if she did us wrong. Mie I didnt welcome her. Nilimpotezea mpaka namaliza form four.

Siku moja, nakaribia kufanya mtihani wa kumaliza Shule ya msingi kuna mgeni alikuja home. Nakumbuka nilikuwa nakosha vyombo. Nikafuta mikono na kwenda kumsalimia. Halafu nikaendelea na kazi yangu. BAsi nimemaliza kuosha vyombo nikawa naenda nje kununua sijui nini, ile napita karibu na mgeni nikaangusha coin. BAhati mbaya ikaenda mpaka miguuni kwa mgeni. Nikazunguka nikajificha nyuma yake nikaokota huku na blush kwa aibu. Ile nainama kuokota nikaangalia ukucha wa kidole gumba cha mgeni. Moyo wangu ukastuka. Nikamwangalia usoni. Alikuwa ni Mama Yangu. Na alikuwa analia kishenzi.

Mh. Tukaanza kulia sote watatu. Ma mdogo ametuangalia ameduwaa. Anyway baba alikuja na wakasalimiana vizuri tu. Tukaenda kwa bibi yetu kukaa na mama kwa siku mbili tatu halafu mama aliondoka. Alituambia anaishi mji mwingine na alituambia anatupenda and nothing will ever change that. Alituomba yule ma mdogo tusimuite mama hata siku moja because she was the original and biological mother. Akaniambia always work hard, for some day you will save me. Nililia sana.

Basi maisha yakaendelea. Miaka ikapita. NIkafaulu vizuri tu nikajiunga na shule ya sekondari, nikamaliza. Nikaingia chuo kikuu, nikafaulu, nikaendeleza masomo. Mama never came back. To date. I really miss her. The pain is gone, nimeacha kulia whenever I think of her. Nimeolewa na najua ndoa ina mengi so na hiki kimechangia kunipa nguvu. People suggest kwamba hayupo duniani but my heart tells me yupo na ipo siku atarudi.

If she could see me now. Her little girls are no longer tiny. I am a mother now. Ma ameondoka sina hata nyonyo. Now I have a child of my own. Aliniambia niwe kama mama kwa mdogo wangu, my sister is doing well too. Atarudi lini? I do not know. But kila siku ya Mungu namuombea. Asilale na njaa, Mungu ampe chakula. Asishinde na kiu, Mungu ampe maji. Asitembee uchi, Mungu ampe nguo, Asimsahau Mungu, Mungu awashe taa moyoni mwake, amuongoze kwenye njia iliyonyooka. Ipo siku atarudi. Bibi mzaa mama alifariki Mama hakuja kwenye msiba. NImeolewa hakuwepo. It was just my sis and Daddy. But I refused to cry, labda baba angejisikia vibaya. But I continue to believe Mama yupo hai, somewhere beneath God's skies.

Mungu hakunyimi kila kitu. Alitupa baba yetu. Anaetupenda kuliko kitu chochote duniani. Alipooa alipata watoto wengine wanne, ila nafasi yetu ipo palepale. Ma mdogo alibadilika alipozaa ila tulivumilia ili baba apate amani. My Daddy is the wind beneath my wings. He is my friend. I can call him any time, to tell him anything. He has opened my eyes into this world. Whenever we were overwhelmed by the sight of other girls with their mothers he was always there for us.

Malezi ya baba yalikuwa ya kisela sana. Pata picha sote tumevaa overalls sare tupo garage tunahangaika. Baba akitukana na sisi tunatukana. Tumeshika spanner zetu. Baba akiita naomba namba 13 tunakimbia fasta kwenye toolbox tunamletea. Tukienda kuvuta magari yalopata ajali na breakdown unatukuta tumekaa juu kwenye bodi tumening'inia tunaenda na baba yetu. Baba ametufundisha mengi sana. We could see through men. Tulijulikana kama watoto wa simba. Ole wako akuone ukimtazama his lovely daughters the wrong way. Unachezea za usoni fasta. Hatukudanganyika mapema. Malezi ya baba yametufanya tuwe very strong women. Hatukupapa opportunity ya kukua around women so kidogo hatujui ku relate na wanawake wenzetu and since udogoni men have been our best friends.

Natamani arudi. Natamani aone tu binti twake. NAtamani aone how hard I worked at school. It has been 20 years. Ndugu zake hawasemi chochote. Tumefikia mwisho wa kumtafuta. Hatujui kilichobaki isipokuwa kusubiri tuone Mungu amepanga nini. If only she could see us now. Would she be proud of us? Would she commend Daddy on the good job he has done?

If you are a single dad, know that you can make it. Mtangulize Mungu. Na kama upo kwenye ndoa na pamoja na matatizo yake kuna option ya kuendelea kuwepo please tulia uwalee wanao. Maisha ya kulelewa na mama wa kambo sio rahisi. NI wachache sana ambao wanaweza ku share interest ulizo nazo kwa wanao.

Ni hayo tu.:yo:

EMT, Wi-Fi SnowBall, Mentor, Kaizer, gobore, snowhite, KIKUNGU, Kaunga, King'asti, Kongosho, The secretary, figganigga, Hoshea, Kamanda Moshi, mzabzab, Mjuni Lwambo and a couple others.
 
Last edited by a moderator:
Dada kisa chako kizuri isipokuwa mi naushauri mmoja. Kama mtanzania anejivunia lugha yake ya taifa. Nikikuwa nashauri ukiandika mbeleni tumia kiswahili tu. Inatosha! Ukichanganya na lugha za wakoloni unachangia kudhaifisha kiswahili lugha iliyo tamu kuliko asali.
Ahsante kwa kusoma.
 
thread zako huwa zinanipa raha lakini hii imeniliza!
imeniliza kwanza kwa maumivu
lakini pili kwa furaha!
YOU ARE MY GIRL!yu know tht!
NAKUPENDA bure!
thread yako ni zaid ya hii tunachokisoma hapa!
thread yako ina mengi sana!
zaid ya wewe kummiss mama!
dah!
sijui hata naongea nini!ngoja tu ninyamaze!
 
Nimependa ulivyotimiza aliyokuambia, that's best gift to her. Even in her absence you are still good. Hongera
 
mh!!!ni wanaume wachache sana ambao wanaweza leo watoto wao after mama s death au depart wababa ni wazito sana katika malezi wazito sana na hawana chembe ya uchungu wa mwana anaweza mpeleka mtoto mahali anajua kabisa anaowakabidhi sio salama yeye anarudi kuoa mke mwingine na kula bujugwa kwa uhuru zaidi,nampongeza sana baba yako Karucee
 
Last edited by a moderator:
If I could turn back time, rewind
If I could make it undone I swear that I would
I would make it up to you
Mom I'm all grown up now
I'ts a brand new day
I'd like to put a smile on your face everyday
Mom I'm all grown up now
And it's not too late
I'd like to put a smile on your face everyday


 
duu kweli maisha ni maisha tu hata ufanye nini what if na wewe ukawa kama mamako na je ulijuaje that woman is your mother.. Karucee
 
Last edited by a moderator:
Nimependa ulivyotimiza aliyokuambia, that's best gift to her. Even in her absence you are still good. Hongera
double R, umenisababisha nimwage chozi. Atarudi na najua atafurahi. I will take good care of her.
 
Last edited by a moderator:
Dada kisa chako kizuri isipokuwa mi naushauri mmoja. Kama mtanzania anejivunia lugha yake ya taifa. Nikikuwa nashauri ukiandika mbeleni tumia kiswahili tu. Inatosha! Ukichanganya na lugha za wakoloni unachangia kudhaifisha kiswahili lugha iliyo tamu kuliko asali.
Ahsante kwa kusoma.
kahtaan. asante kwa ushauri wako. Sikudangayi kuwa nitabadilika manake sitoweza. Ila naomba na wewe ujiite KATANI tujue moja. Pia ungechagua picha ya kibongobongo inayoenzi taifa lako ingependeza. Hata katoni pia sio jina baya. ama katuni.
 
Last edited by a moderator:
karucee mbona hujani cc na nilikuomba?
ila MUNGU ni mwema muombe atakurudishia mama yako.
nitakuombea pia.
pia pongezi nyingi kwa baba yako,but what if yeye ndo chanzo cha mama kupotea..hayo mazuri yake yataweza kulipa uchungu wa kumpoteza mazeri hivo?
 
Hongera kwa kupata malezi ya baba na hadi leo baba ni rafiki yako
Hope one day mama will be back, let us hope......
 
thread zako huwa zinanipa raha lakini hii imeniliza!
imeniliza kwanza kwa maumivu
lakini pili kwa furaha!
YOU ARE MY GIRL!yu know tht!
NAKUPENDA bure!
thread yako ni zaid ya hii tunachokisoma hapa!
thread yako ina mengi sana!
zaid ya wewe kummiss mama!
dah!
sijui hata naongea nini!ngoja tu ninyamaze!

teheteheteheeeeee mbona umecomment aisee..
 
umekataa pole!!!!!!!!!!!!!!!pongezi kwa baba yenu maana wanaume wengine akioa hataki kusikia la mswali sala wala nini huyo mke ndo anakuwa mboni yake,hongereni kwa kuwa watoto wasikivu.
Asnam, yeah. Pole nimekataa mwaya. Asante mpenzi wangu, nashukuru ujana tulivuka salama.
 
Last edited by a moderator:
thread zako huwa zinanipa raha lakini hii imeniliza!
imeniliza kwanza kwa maumivu
lakini pili kwa furaha!
YOU ARE MY GIRL!yu know tht!
NAKUPENDA bure!
thread yako ni zaid ya hii tunachokisoma hapa!
thread yako ina mengi sana!
zaid ya wewe kummiss mama!
dah!
sijui hata naongea nini!ngoja tu ninyamaze!
snowhite, sikutarajia kuwa ningemwaga chozi leo. Ila nitamwaga sana but its all good. I miss her jamani. I cant bear it kumuona mtu anadeka kwa mamake. Oohhh. Dont be sad jamani..... its the path that God destined for my sister and me. Love you too sweets.
 
Last edited by a moderator:
teheteheteheeeeee mbona umecomment aisee..

ah nimejikuta kila ninachoandika nazidi kumwaga michozi!
na bibie kasema hataki pole wala mtu amsorry sitaki kukanusha ombi lake!
ndo nikaona nijikalie tu kimya nisome ya wengine!
 
mh!!!ni wanaume wachache sana ambao wanaweza leo watoto wao after mama s death au depart wababa ni wazito sana katika malezi wazito sana na hawana chembe ya uchungu wa mwana anaweza mpeleka mtoto mahali anajua kabisa anaowakabidhi sio salama yeye anarudi kuoa mke mwingine na kula bujugwa kwa uhuru zaidi,nampongeza sana baba yako Karucee
Asante Nivea. He truly is the best.
 
Last edited by a moderator:
kahtaan. asante kwa ushauri wako. Sikudangayi kuwa nitabadilika manake sitoweza. Ila naomba na wewe ujiite KATANI tujue moja. Pia ungechagua picha ya kibongobongo inayoenzi taifa lako ingependeza. Hata katoni pia sio jina baya. ama katuni.

heee kisa kiswanglish umetisha mkuu...
 
Hongera kwa kupata malezi ya baba na hadi leo baba ni rafiki yako
Hope one day mama will be back, let us hope......
sure ram. Let us wait.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom