Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

Mzee MKJJ
Hii imekaa vyema . Kama kawaida tusambaze copy kwenye Bunge , Waziri Mkuu , HE wote wajue what we want to see. Miaka hii CCM ina kazi kubwa sana .Ijue siku zake za kudanganya zinaisha sasa . Kazi ni mwendo Mdundo . Tupo hapa hapa .
 
NDUGU ZANGU - SOMENI HAPA.

Kufungiwa HakiElimu serikali yajipalia mkaa

WASOMI na wasasiasa wamesema kwamba serikali imevunja haki za kidemokrasia kwa kuyafungia matangazo na machapisho yote ya Shirika lisilo la kiserikali la HakiElimu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam jana, baadhi ya wanasiasa na wasomi hao waliionya serikali kuwa inatumia ubabe na inakwenda kinyume na haki za kikatiba.

Walikuwa wanatoa maoni yao kufuatia Ofisi ya Waziri Mkuu kutishia kulichukulia hatua kali za kisheria HakiElimu, iwapo litaendelea kutoa machapisho na matangazo yahusuyo shughuli za elimu nchini, kwa madai kuwa kila shirika hilo linapochapisha neno, picha au filamu linakiuka sheria.

Mkuu wa Idara ya Elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Peter Chonjo, alisema ameshtushwa kusikia kwenye vyombo vya habari jana asubuhi kuwa HakiElimu imefungiwa tena na serikali.

“Mimi kwa mtazamo wangu matangazo ya HakiElimu yanaielimisha jamii na pia yanachochea utendaji kazi bora wa idara mbalimbali serikalini, hivyo kinachofanywa na taasisi hii ni kuwaasa viongozi wasiwe wababishaji,” alisema Profesa Chonjo.

Alisema anakumbuka wakati wa uongozi wa aliyekuwa Waziri wa Elimu na Utamaduni, Joseph Mungai, tatizo hilo lilikuwepo na ilionekana kuwa serikali kupitia wizara hiyo inalikandamiza shirika hilo ili lisiweze kueleza mabaya yanayotokea katika wizara hiyo.

“Ninachokiona hapa ni kwamba, hawa HakiElimu wanafanya kazi nzuri ya kuweka wazi mambo mabaya na madhaifu yaliyopo katika sekta ya elimu nchini,” alisema Profesa Chonjo.

Alieleza kuwa yeye anaamini kuwa lengo la HakiElimu sio baya, na akashauri kama serikali imeona kuna ubaya ndani yake, basi itakuwa ni busara kuwaita na kuwaonya kuhusu huo ubaya ama tangazo ambalo limeonekana kuwa ni baya na linagusa maslahi ya jamii.

Mhadhiri Msaidizi katika Kitivo cha Sheria wa UDSM, Baraka Kanyabuhinya, alisema neno ‘maslahi ya jamii’ ni neno ambalo mara nyingi limeleta utata katika tafsiri na matumizi yake na wakati mwingine limetumika vibaya.

Alisema yeye haoni ubaya wa matangazo, ama vitu vinavyofanywa na HakiElimu, kwa mfano hata katika uhuru wa habari, mwananchi ana haki ya kupata taarifa, hivyo kwa kuifungia kunakiuka haki ya mtu kusikilizwa ama kutoa maoni.

“Unaposema kuwa jambo fulani linagusa maslahi ya jamii ni vizuri usiishiie hapo, bali ueleze hayo maslahi ya jamii ni yapi hasa. Kwa mfano unapomuondoa mtu kwenye eneo lake kwa sababu unataka kujenga shule, hapo utaeleweka na kisheria huwa unamlipa fidia,” alifafanua Kanyabuhinya.

Mhadhiri mwingine, Dk Johannes Mutanyata wa Kitivo cha Elimu UDSM, alisema inafaa Haki Elimu waachwe huru wafanye kazi yao, na kama serikali imeona kuwa wamekosea, basi watoe maelezo ya kitaalam kuthibitisha hilo.

“Kama HakiElimu imetamka jambo kwa makosa basi ni wajibu wa serikali kulikanusha kitakwimu ili kuuthibitishia umma kuwa hilo ni kosa na sio kusema tu maslahi ya jamii,” alisema Mutahinywa.

Wakati wasomi wakitoa maoni hayo, baadhi ya wanasiasa wameiunga mkono taasisi hiyo na kupingana na uamuzi wa serikali wa kuiziba mdomo.

Naibu Katibu Mkuu (Bara) wa Chama cha Wananchi (CUF), Wilfred Lwakatare, alisema serikali imelishughulikia suala la HakiElimu kibabe na hiyo “inadhihirisha wazi kwamba serikali isivyopenda kukosolewa.”

“Serikali wakati wote inapenda kusifiwa sifiwa tu, lakini pale inapotokea taasisi za kijamii zikaishika pabaya kwa kufunua pale penye uvundo, kitakachotokea ni kukemewa vikali pamoja na kupewa vitisho,” alisema Lwakatare.

Alisema kama serikali ingekuwa inatekeleza wajibu wake kikamilifu kama inavyojieleza kwa wananchi kuwa inaendeshwa kwa uwazi, inawajali wananchi, inahimiza utawala bora, basi ingeipongeza harakati za HakiElimu na kuwapa moyo wa kuongeza bidii katika kufunua utendaji mbovu katika elimu.

Aliihadharisha HakiElimu kuwa isijihangaishe kutaka kuingia kwenye mazungumzo na serikali katika kutafuta maridhiano, kwa madai kwamba itafumbwa mdomo ili isiendelee kufunua uozo wa watendaji wake katika utekelezaji wa mipango ya elimu nchini.

“Ninachoishauri HakiElimu ni kwamba izibe masikio na badala yake iendelee kuchapa kazi zake kama kawaida kwa sababu zipo ndani ya Katiba ya nchi,” alisema Lwakatare.

Katibu Mwenezi wa Chama cha NCCR-Mageuzi Taifa, Joseph Selasini, alisema kwamba nchi yoyote yenye demokrasia haiwezi kukataa maoni ya watu hata kama ni machungu kama shubiri.

“Tamko la Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu linatamka uhuru wa kutoa na kupokea habari. Tanzania imeridhia na kutia saini tamko hilo, lakini kinachoonekana wao ndio wanaolivunja,” alisema Selasini.

Aliitetea HakiElimu akisema kwamba machapisho na matangozo yake ambayo walikuwa wanayatoa kupitia redio na televisheni yalikuwa ya ukweli kwa sababu ni mambo ambayo yamekuwa yakijirudiarudia katika mfumo wa utendaji kwenye sekta ya elimu.

Alitoa mfano wa tangazo linalohusu mwalimu aliyekopa fedha ya nauli aende mjini kuchukua mshahara wake na alipofika akakuta bado haujaingia kwenye akaunti yake ya benki na kuanza kujishauri namna atakavyomweleza aliyemkopesha, kwamba halina ubishi kwani ni jambo linalowakuta walimu wengi.

Ukweli huo aliuelezea kuwa ndio uliomfanya Rais Jakaya Kikwete aingilie kati na kuamuru watendaji wahakikishe kuwa walimu wanapata mishahara yao tarehe 23 kila mwezi.

Kinachojitokeza katika sakata hili, Selasini alisema, ni mgogoro kati ya serikali na wananchi, hivyo akaishauri HakiElimu kwenda mahakamani ili kuitaka ifafanue juu ya ukandamizaji huo.

Desemba 5, mwaka jana, Ofisi ya Waziri Mkuu ililiandikia shirika hilo, ikilitishia kuwa italichukulia hatua kali za kisheria iwapo litaendelea kufanya au kuchapisha tafiti kuhusu shule, kuandaa na kuruhusu filamu ama matangazo katika redio na televisheni pamoja na kusambaza machapisho mashuleni kwa sababu yanakiuka sheria na maslahi ya jamii.

Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa serikali kuikemea HakiElimu, kwani Septemba 8, 2005, iliyokuwa Wizara ya Elimu na Utamaduni katika serikali ya awamu ya tatu ambayo sasa inajulikana kama Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ilikuwa imeipiga marufuku kutoa matangazo na machapisho yaliyodaiwa kuidharirisha sekta ya elimu.

HakiElimu ni shirika la hiari lenye usajili halali wa kisheria, linalolenga kufikia usawa, ubora haki na demokrasia katika elimu na jamii, kwa lengo la kuiwezesha jamii kupata habari, kubadili shule na mfumo wa uundaji wa sera, kuibua mijadala, tafiti, uchambuzi wa sera na kushirikiana na wadau kwa manufaa ya pamoja kwa kuzingatia haki za jamii.
 
Serekali isiojiamini kabisa, Hataki kukosolewa. Imedhibiti vyombo vya habari kwa hongo na vitisho pia wameandaa mswada utakaomaliza kabisa uhuru wa vyombo vya habari.

Hili la Haki Elimu, linakazia mtazamo wa serekali ya awamu ya nne katika utawala bora.

Ni hatari kuwa na serekali ya namna hii, isokubali au kutokuwa na uwezo wa kuukabili ukweli, haitaki changamoto.Hii ni hatua juu ya kabisa ya udikteta, tupo hatua moja kabla ya mafisadi kuanza kuua wale wote wanaowakosoa.
 
Wale waliofikiri kumchangua Kikwete ni ukombozi, wajiulize tena. CCM ni moja na lao ni limoja. Haitasaidia kitu kubadilisha sura. Kinachotakiwa ni kubadilisha mfumo huu dhalimu. Tutaupendaje mzizi na tuuchukie mti hapohapo? I hope ipo siku watanzania tutaelewa hili!
 
Jamani, mtaendelea kuomba ruhusa mpaka lini.? Nimeshatoa ruhusa ya kusambaza kila ninachokiandika kwa manufaa ya umma isipokuwa kazi zangu za kisanii (Hadithi, mashairi n.k) Mnaweza kuandika jina hilo au "Mwandishi Maalumu"

My fellow citizens, let freedom reigns, from the sparkling snow-capped mount Kilimanjaro, to the green valleys of Southern Highlands, from the golden sands of the coast of the Indian ocean to the praised shores of Lake Tanganyika! Let Freedom Rings! May our nation dare to rise to be all it can be, may we as a people and as a nation ascend to the heights that our forebearers never dreamed of, may we build a nation that is freer, modern, and yet very African! Yes, may we one day, pass to the next generation of Tanzanians, a nation that has finally taken its rightful place among the nations of the world! If our esteemed leaders won't lead now to fulfill such an ambition of ours, they'll find themselves following later! For Freedom never ceases to ring!
 
Mwanakijiji,

Hiyo article imetulia , tafadhali kama utaweza jaribu kumtafuta Prof .Mbilinyi ufanye naye majadiliano katika hili suala , ni jambo la kushangaza kwa nini haki elimu awajaiburuza serikali mahakamani
 
Mwanakijiji,

Hiyo article imetulia , tafadhali kama utaweza jaribu kumtafuta Prof .Mbilinyi ufanye naye majadiliano katika hili suala , ni jambo la kushangaza kwa nini haki elimu awajaiburuza serikali mahakamani

Haswaa Rufiji,
M/Kijiji mtafute Prof. Mbilinyi au Kijo Bisimba maana Ulimwengu alishajichokea labda kama unataka habari za bongo fleva, kisha watuambie ni kwanini hawajaenda mahakamani hadi dakika hii na wanakalia kuandika barua tu kila kukicha.
 
contacts za wazee... huku kijijini kazi kweli kupata vitabu vya simu...

M/Kijiji,
Sina hakika kama hiyo simu yao inafanyakazi lakini kama ndivyo inaweza kuwa sehemu nzuri ya kuanzia ili kumpata mhusika mmoja wapo. No zao kwa ofisini ni +255 22 2151852/3. Pengine tutaweza kupata undani wa haya mazingaombwe
 
Tabasamu hiyo ya HE nimeipata na nimezungumza nao leo lakini Rajani mwenyewe hakuwepo...
 
2007-02-01 10:52:42
Na Mwakwaia wa Kuhenga


Mheshimiwa Edward Lowassa, MB.,
Waziri Mkuu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mheshimiwa Waziri Mkuu,

Nadhani tunafahamiana! Kwa kuwa ni hivyo, nina hakika utapenda kusoma waraka huu wa mimi nduguyo, mwananchi mwenzio wa nchi hii.
Nathubutu kukuandikia nikitiwa moyo na ule msemo wa lugha yetu ya Kiswahili: ``Zimwi likujualo halikuli likakuisha!`` Lakini kwa kweli sina sababu ya kuwa na hofu yoyote kuwasiliana nawe kupitia safu hii kwa sababu kwanza wewe siyo zimwi - ni mtu mwenzangu tu - hata kama ni mtawala. Wadhifa ni matokeo tu, siyo msingi wa utu!

Pamoja na hayo, Mheshimiwa Waziri Mkuu, nina hofu kidogo. Nachelea kwamba kadiri mambo yanavyokwenda na hapa tulipofika tusije tukaishia kujenga taifa la mazimwi!

Naona umestuka kidogo PM! Nitakueleza:
Mbele yangu ninayo rasimu ya ule muswada wa Uhuru wa Vyombo vya Habari. Lakini pia ninayo taarifa kutoka ile taasisi isiyo ya kiserikali, HakiElimu. Juzi, Jumanne, taasisi hiyo imeitisha mkutano na waandishi wa habari kufahamisha kuwa Ofisi yako imepiga marufuku matangazo na machapisho yake yote yanayotolewa kwa redio, luninga na vyombo vingine vya habari.

Bahati nzuri au mbaya masuala yote haya mawili ile rasimu ya serikali ya muswada wa Uhuru wa vyombo vya Habari au Uhuru wa kupashana na kutoa habari na kupigwa marufuku matangazo ya HakiElimu yana sura inayofanana na inayogusa Uhuru wa kimsingi wa watu wa nchi hii kwa mujibu wa Katiba yetu.

Waziri Mkuu, kama unavyofahamu, moja ya Uhuru wa kimsingi wa sisi watu wa nchi hii kwa mujibu wa kifungu cha 18 cha Katiba yetu ya Jamhuri inasema hivi:
Kila mtu:
Anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake
Anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila kujali mipaka ya nchi Anao uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake na
Anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii.

Nina hakika unafuatilia kwa njia moja au nyingine kilio cha wanahabari kama mimi kuhusu rasimu ya muswada unaokuja Bungeni Bill for the Freedom of Information Act 2006.

Mimi ni mmoja wa hao wanaopigia kelele muswada huu kama haupendezi na haufanani hata kidogo na serikali hii ya awamu ya nne ambayo inatokana na ushindi na ridhaa maradufu ya wananchi wa Tanzania waliochagua kwa zaidi ya asimilia 80.

Nilitazamia serikali yangu hii ya CCM ambayo kura yangu ni miongoni mwa kura za mamilioni ya Watanzania kuiweka madarakani, ingekuwa inafikiria mambo makubwa zaidi siyo tu kuimarisha bali kuboresha uhuru wa kusema, uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa vyombo huria vya habari na siyo kufikiria kutunga sheria, ambazo ni kinyume cha uhuru wa kimsingi wa mwananchi wa nchi hii katika zama na karne hii.

Kwa mfano muswada unaweka masharti ya mwandishi kuwa na digrii ya taaluma ya Uandishi wa Habari kana kwamba digrii au karatasi yenyewe iliyoandikwa ``degree`` ndiyo inayoandika makala au habari!

Kuweka masharti haya ni mfano wa nchi kama Uingereza kutunga sheria kwamba kiongozi wake wa shughuli za serikali lazima awe na digrii! Wanaojua wanafahamu, kwa mfano kuwa Sir Winston Churchill au John Major hawakuwa na digrii walipokamata nchi kama mawaziri wakuu wa Dola la Uingereza!

Hivi kweli, watu wakisoma makala nzuri ya Mheshimwa Waziri Mohamed Seif Khatib anayotoa katika safu yake ndani ya gazeti MZALENDO au Mudhihir Mudhihir aliyekuwa anaandikia gazeti la Daily News itawajia hata kwa sekunde moja, kuuliza kuwa mabwana hawa wana digrii au lazima wana digrii ili kumudu kuandika makala? Si ni �interest� ya mtu au kipaji chake tu?

Ni mambo ya ajabu sana haya yanayotaka kupenyezwa hapa kwetu!
Itazame tena rasimu hii, PM. Inashangaza kwamba watu wazima wanaweza kujifungia mahala wakaja na dude kama hili na bado wakadiriki kuliita �Freedom of Information Act�!

Ndugu Waziri Mkuu utaniwia radhi kukuita Ndugu, nina hakika wewe si mmoja wa watu wanaonuna ukiitwa Ndugu Lowassa au Ndugu Waziri Mkuu badala ya Mheshimiwa! Pamoja na matatizo yetu yote, kama vile baadhi yetu wanataaluma au baadhi ya vyombo vyetu vya habari kutumika wakati wa kampeni za Uchaguzi na hata baada ya hapo, tulikuwa tumepiga hatua si haba katika uhuru wa kusema na uhuru wa kutoa mawazo.

Hii leo, kipo chombo cha udhibiti wa vyombo vya habari, na mwenendo wa wanahabari wenyewe kilichoundwa na wanahabari wenyewe na wadau wengine yaani Media Council of Tanzania. Ni chombo kinachoheshimiwa na ni chombo huru.

Sasa muswada huu unaokuja utakiua chombo hiki. Kitaanzishwa chombo cha serikali chenye jina la ghiliba, `Media Standards Board`.

Kwa mara ya kwanza taaluma ya uandishi wa habari itakuwa na leseni katika nchi hii, sikumbuki kama ipo nchi yoyote inayotoa leseni kuandika habari.

Sana sana vipo vitambulisho tu kumrahisishia mwandishi kufanya shughuli zake lakini si vinginevyo.

PM: Yote haya ya nini? Hivi kweli serikali yenye ridhaa kubwa namna hii (popular mandate) lipi itaisibu kama uwanja wa uhuru ukipanuka zaidi?

Sasa tuzungumzie jamaa hawa wa HakiElimu. Binafsi nafurahia sana matangazo yao kwenye luninga na redio. Kwa mtazamo wangu na nadhani wa watu wengi, vibwagizo na matangazo yao yanatoa hali halisi au mtazamo mbadala wa mchakato wa maendeleo ya nchi yetu.

Lakini siyo kweli kwamba wapo baadhi ya walimu wanaozikung�unta kangara na konyagi zao barabarani kabla ya kuingia kufundisha darasani na huko kusababisha kizaazaa kwa watoto wanafunzi? Siyo kweli kwamba maisha ya wananchi walio wengi hapa nchini ni duni nyumba za majani, mavazi duni kama vile uvaaji wa kandambili za rangi mbili tofauti au mguu mmoja, au watu wanaoishi karibu na dampo la takataka kama vile pale Vingunguti?

Kuna ubaya gani kutoa ``contrast`` ya taarifa kuwa uchumi wa nchi hii unakua kwa asimilia saba, wakati hali halisi inaonyesha vinginevyo?

Rais wetu, Jakaya, amesema anakasirishwa sana na kupakwa mafuta au kusifiwa kinyume na hali halisi.

Nadhani huu ndiyo ungekuwa mwendo wa serikali yetu na kwa kweli serikali yoyote duniani hujifunza na kufaidika zaidi kusikia wananchi wanasemaje huko mitaani. Je, kupiga marufuku mawazo mbadala kunasaidia? Je, Tutafika?

Edward: Utaniwia radhi kukuita kwa jina lako la kwanza, nadhani ka-rika kangu kananipa ubavu huo! Utakubaliana nami kwamba si rahisi kuyaona mambo kama navyoyaona mimi nikiwa nje ya serikali. Pengine ni vizuri unichukulie very seriously - kwa umakini - na wewe mwenyewe ukiwa mtu makini.

Namalizia kwa kukuuliza: sijui Edward kama huwa unawaangalia hawa vijana wetu wasomi wa vyuo vikuu hasa wanapofanya mikutano yao au maandamano.

Ujumbe mimi naopata ni kwamba kizazi kinachokuja baada yetu sisi kuondoka kitakuwa hakina mchezo na kwa maana zote!
Ni vizuri twende mwendo unaofanana na vijana hawa ambao ndiyo tunaowaachia nchi hii wakati sisi tutakuwa hatupo tena.
Nakushuru. Wasalaam!

Makwaia wa KUHENGA ni Mwandishi Mwandamizi.

E-mail: makwaia@bol.co.tz
 
Kila kitu kina Mwisho wake,Huu sasa ndio Mwisho wa Mh.Edward Ngoyayi Lowasa,kwa ujumla Mh. huyu amekwisha kabisa kisiasa,njia pekee itakayomsafisha JK ni kumuondoa huyu Mbabe kwenye wadhifa huo!.Tunapenda kuona tunapata kiongozi anayependa kutatua matatizo kwa njia ya mijadala na sio kiongozi Mbabe kama kiongozi wa Jeshi!.JK kama unatusikiliza muondoe huyu Muungwana kabla unaowaongoza (wananchi) kukushikia mabango!
 
true mjj,rakesh rajani, muhoji prof marjorie m.,kijo au mama lema..nadhani ulimwengu ana ideas nzuri lakini siunajua akishatofautianaga nao huwa wao wanakumbushiaga uraia..utafikiri ni yeye mwenyewe wale tuliosema wa BOT na FOREGN et al hawawaoni
 
Kuna mtu ana access ya hiyo Bill ya Freedom of Information Act..tafadhali aiweke hapa wanabodi wapate kujua kulikoni.

Ila kigezo cha kusema Mwandishi kuwa na "Digrii ya Taaluma ya Uandishi wa Habari" kinanitoa machozi mzee mzima.

Ningependa kujua vigezo vingine ni vipi...tafadhali.
 
Mwandishi Wetu
HabariLeo; Saturday,February 03, 2007 @00:05

SERIKALI imesisitiza kuwa haiwezi kupeleka bungenimikataba inayoingia na wawekezaji mbalimbali kwaniwabunge siyo watendaji.

Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, Dk. Juma Ngasongwa alisema jana kuwa suala la mikataba kati ya wawekezaji na Serikali linahusu zaidi utendaji na Serikali ndiyo mtendaji badala ya wananchi.

“Hatuwezi kuleta mikataba hiyo bungeni. Ninachowashauri wabunge wawe wanawahoji mawaziriwanaohusika na sekta husika na siyo kudai mikataba iletwe hapa bungeni,” alisema Dk Ngasongwa alipojibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Mdee (Chadema).

Halima alitaka kufahamu sababu inayoifanyaSerikali kushindwa kuleta mikataba hiyo bungeni, na akaongeza kuwa uficho usiri uliopo ndiyo unaosababisha wawekezaji hao kushindwa kuwaajiri Watanzania wengi badala yake kuwafanya vibarua na kuwalipa kidogo kutokana na mikataba iliyopo.

Awali katika swali la msingi, Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu (CCM) alitaka kufahamu hatua zinazochukuliwa na Serikali kutokana na uonevu unaofanywa na wawekezaji wa migodi kwa Watanzania kutokana na na kutokuwapo kwa sheria inayowabana wawekezaji hao katika kuwalinda Watanzania waboreshewe maslahi yao.

Naibu Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, Gaudence Kayombo, alisema suala hilo linahitaji kufanyiwa utafiti wa kina kupitia vyombo na mamlaka zinazohusika kuthibitisha kuwapo kwa hali hiyo na baadaye Serikali ishauriwe kuchukua hatua muafaka.

Alisema kuboresha mishahara na maslahi ya wafanyakazi katika sekta yoyote inategemea sana mapato yanayotokana na uzalishaji. Alisema uzalishaji unapokuwa mdogo kipato cha mfanyakazi nacho kinakuwa kidogo. Naibu Waziri alisema ajira nyingi za Watanzania zinapatikana kwa njia ya ushindani unaozingatia ujuzi, elimu na bidii ya uzalishaji.
 
kama wabunge sio watendaji na ndo tulowapa kura zetu, je hoa watendaji ni kina nani ambao hawataki kutujulisha kinachoendelea kuhusu rasilimali zetu?
 
Kwa hiyo nchi zinazopitisha baadhi ya mikataka bungeni huwa wanakosea. Mbona hata hiyo rada tuliyouziwa imepitishwa bungeni Uingereza kutolewa kwa kibali itakuwaje sisi. Ndio hawa wasomi wa Bongo maanake elimu zao zimekomea mwisho wa kurasa za kitabu...They can't think beyond that.
Dk. Juma Ngasongwa, hana exposure ya mambo yanavyokwenda duniani na kwao maana ya Uongozi ni Kutawala.
Huduma za bandari kutopewa UAE tulizisikia ktk vikao vya congress Marekani na mkataba kufutwa hawa wote hawafahamu utaratibu wa mikataba?
Hii ndiyo ukisikia serikali kuendesha nchi bila ridhaa ya wananchi.. Huu ni udikteta!... hamuwezi kutuvalisha nguo tusizopenda kuvaa.
 
Back
Top Bottom