Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

Shukrani JeiKei aka JK mwenyewe?!

Binafsi naona hotuba hizi zinaridhisha kwa ujumla, hasa hiyo kuhusu Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Hiyo ya meza duara na wafanyabiashara nayo si mbaya. Kwa kila moja nimeona kosa moja moja la kiuchapaji au kiuandishi; yaani "recourses" badala ya "resources" (Chattam) na "wetted" badala ya "whetted" (Merryl). Recourses na resources ni vitu viwili tofauti. Sasa hii ya wetted badala ya whetted inaweza kuleta tafsiri mbaya (nadhani nimeeleweka), hivyo waandishi wake wawe makini sana na kupitia na kuhakiki na kurudia!

Akiendelea hivyo atatutia ujasiri!
 
Hata hivyo tukumbukeni kuwa Wahenga walisema:-

Kizuri HUJIUZA na kibaya HUJITEMBEZA...
(kuna tofauti kati ya kujitangaza na Kujitembeza).
 
Big service Jeikei.

I am intrigued by his candid conclusion: "we lose the right to govern and even tax people if we do not deliver services to them. The question is, is his government livin up to this commitment?

Wish we had the audio version of the speech as well.
 
Jk punguza speed basi babake...utatumbukiza gari baharini kwa kasi zako..mzee wa kasi..hehehehe
 
Tanzania: Country to Relax Work Permit Rules

The Nation (Nairobi)
January 23, 2007
Posted to the web January 22, 2007

Tony Kago
Nairobi

Tanzania is ready to open its border to Kenyan workers, a top official of the East African Community said yesterday.

Ms Mary Makoffu, an economist in the EAC's social sector, said the two countries' immigration departments had harmonised the procedures on the issuance of work permits.

She told media executives and journalists attending a one-day briefing seminar on the EAC Political Federation at a Nairobi hotel that Tanzania had relaxed its strict immigration rules and taxes that have in the past discouraged the entry of Kenyan workers into that country.

Kenya has been pushing for the abolition of the work permit as the East African countries set in motion a process to integrate.

At a similar media seminar early this month, Information and Communications minister Mutahi Kagwe asked EAC member states to do away with work permits.

Abolition, he said, would go a long way towards promoting regional integration and also attract investors to East Africa. It would also limit migration of traders searching for better tariffs and tax regimes.

Was inevitable

Participants at the seminar said although the proposed federation was inevitable, there was still a lot of mistrust and suspicion among the member states' people.

Tanzania's membership of the Southern Africa Development Cooperation trade bloc was also raised, with participants asking the country to abandon it so that all EAC countries can chart their next move as a bloc.

Kenya, Uganda and the recently admitted EAC members Rwanda and Burundi are members of Comesa.


Sasa Je, ni kiasi gani wabongo wamepata kazi? Hii ni aibu kwa serikali ya Tanzania. Vile vile wanaanza kutuchagulia marafiki what is happening?
 
Mimi yangu macho . Wakenya wanatutukana sisi tuna wataka . Kazi kubwa sana .
 
Yaani sasa ni open season kwa hawa "wawekezaji" wa hoteli na migodi kuajiri Wakenya eti kwa sababu wanajua Kiingereza zaidi. Ni open season kwa Watanzania kukosa ajira wakati wageni wanaingia na kuchukua hata kazi za kufagia hotelini. Bado tu kichwa cha wendawazimu.
 
Ajira millioni moja kila mwaka hizo. Swali ambalo halikuulizwa ni kwa ajili ya kina nani. Sasa jibu limepatikana; Wakenya!!
 
Kuanza tu na issue hizi hapo shikirisho likianza kutembea si itakuwa balaa ?
 
Ajira milioni moja ?????? Alipoulizwa alisema eti Waalimu, Polisi, Wanajeshi, Jeshi la Magereza, akaficha kusema ni Wakenya, mweeeee kweli sisi ni Wadanganyika
 
Jamani this is too big a bite to chew!
Yaani JK na wezi wenzake wanatupeleka marathon..from Richmonduli > Radar >Rushwa ya Manji kwa wabunge > Albawadi [may be we should give it a name..KILOANYI union =Kikwete + Lowassa + Albawadi + Nyiti..how about that?] then to this ajira thing. Lets brace ourselves..tutaona mengi miaka hii

Kwa waliowahi kufanya kazi na hao jamaa wa KQ {Kenya} atajua vile itakuwa shida kwa wabongo. Ni ukweli ulio wazi kuwa wa-KQ wasomi wenye shahada zaidi ya moja ni wengi kiasi kwamba hawapati ajira kwao.
Ni ukweli wa wazi pia kwamba kimombo ni lugha yao. Ni kweli pia kuwa wako veeery aggressive, whereas wa-TZ tumezoea kusema 'naomba' wao husema 'nipatie' au 'patia mimi' Tuwe na hakika kuwa wakija hapa watasahau kama mji una wenyewe.
Kule kwao wameshindwa kuwaajiri ndio maana serikali yao inaharakisha hicho kipengele; hatushangai kwanini masuala mengine hawaharakishi kama hili?
wanajua kabisa kuwa wao ndo watafaidi..thubutu m-bongo ukahamie kwao ovyoovyo kama wanavyofanya hapa uone vile watakutoa mita.
JK amekosa kabisa uzalendo, yaani, anashindwa kuweka maslahi ya waTZ mbele. Hiyo ajira aliyoiahidi ataipata wapi? Mi nakumbuka jinsi alivyoponda mahoteli kuajiri wakenya hata kwenye post za chini..sijui ndo ilikuwa moto wa Ikulu ! Leo ametusaliti!
Hapa JK mwanangu unawasha moto ndani ya shamba la mabua...watu tushakuchoka na njaa njaa zako na EL bado unaongeza kero? Oohoooo...wait till the shy dog hits the wall, you will never know what hit you!
 
Du! hii kali

Jumuiya ya afrika mashariki itapelekea mtafaruku hapa nchini, kwa sasa wakati milango imefungwa kupata kazi ni mbinde, sasa milango ya ajira ikifunguliwa africa mashariki si itakuwa balaaa!

viongozi wakiamua wameamua, mi nasema wacha waje, watakuja wakenya, waganda na warwanda, ila nawahakikishia wataondoka bila kuaga kwani wadanganyika hawatakubali .........
 
Hivi kweli kuna siku Viongozi wetu wataweka Tanzania kwanza na maswala ya Siasa baadaye ?
 
Mimi hizo ajira za tai shingoni hazinipi presha. Naomba kujua suala la ARTHI LINASIMAMA WAPI KWENYE HII EAC...Hapo ndipo pa kuchinjana kwa mapanga butu..!!!
 
Sasa ndo nazinduka**
Kumbe uli usemi wa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya ni kwa upande wa kutelekeza wazaleeendo/wapiga kura
 
Back
Top Bottom