Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

Dua,
kwanza napenda kuwapongeza kwa jitihada zenu kunitoa ktk kiza. Kumbukeni tu kuwa hapa najaribu kutazama upande wa pili wa hii shilingi.. Sina maana namtetea mtu yeyote ila tusifanye makosa kama yale tulofanya kwa Sumaye. Labda niseme hasa mimi kwani nilikubali maovu yake kirahisi bila kufanya uchunguzi kuhakikisha zile lawama zilikuwa na ukweli ndani yake.
Swala la RichMonduli bado tunalifanyia uchunguzi wa vijiweni kwani bado kabisa siamini kuwa JK ana mkono ndani yake na sababu ndio kama nilivyosema. Tanzania kuna hivi Vitengo vilivyopewa madaraka ya kupitisha Tender bila rais, waziri mkuu wala wananchi (bunge maalum) kupitisha...
Labda niseme inabidi toka sasa hivi kuwepo na Bunge maalum kwa ajili ya upitishaji wa
hizi Tender. Hapa ndipo wizi mkubwa umekuwa ukitokea na tumefungiwa kanya boya mara mia kidogo! Inabidi vitengo hivi vitatoa majina matatu hadi matano as finalists kwqa hawa wawakilishi wetu na Uwazi wa Tender hizi utajadiliwa kama vile kortini..Maanake Umaskini ndiye adui wetu mkubwa na umefika wakati tuchunge sana kila senti tunayoitumia ama kuigawa! Ni lazima kuondoa RUSHWA... kwani hawa wabunge watatoka vyama tofauti.

Yet, bado sioni kabisa pungufu la JK, kama kiongozi ktk mikataba hii...
Kama unakumbuka vizuri bunge la Marekani walikataa ile Tender ya bandari ambayo UAE waliichukua na Bush alijaribu sana kutetea lakini alipovutwa na wataalam mwenyewe alinywea...What are the facts though!.. Sii Bush aliyepitisha ile Tender isipokuwa watekelezaji wake...Na wala haiwezi kumfanya aonekane weak ama mwenye mapungufu. Hivyo basi nachoweza kumlaumu mimi JK ni pale policy ya nchi inapokuwa amended kuhifadhi waovu ama policy mpya zinazotufunga.
Jokakuu,
Kuhusu hizi safari za North America, mshikaji hilo tuachane nalo maanake hadi sasa hujanieleza mafanikio ya safari zote hizo mbili au Nne za viongozi hawa! Tunazungumzia matumizi makubwa lakini hatufahamu nini matumizi hayo yametuletea... No one knows!...nataka data kama za Mzee ES anapozungumza mabaya ya kiongozi!... huchambua kama karanga na kinachobaki ni wewe kumeza tu. Haya ya JK hadi sasa naona tuna-judge kila kitu kutokana na hisia zetu...
Well, swala la wizara hizi mbili kuwa na matumizi ktk idara moja ya mambo ya nje bado nahitaji uhakika zaidi.. Mnataka kunambia Ofisi ya waziri mkuu pale nyuma ya Ikulu hawana kitengo cha Uhasibu? Je, ni kweli bageti ya serikali ktk wizara hizi mbili zinashikwa na wizara ya mambo ya nje?...
Ikiwa kuna ukweli fulani, je hii wizara inaweza vipi kuratibu matumizi yake ktk Sikukuu za kitaifa, sera za habari na vyombo vyake, maafa na hata kuratibu matumizi ya uhamiaji makao makuu Dodoma!..Unataka kusema hizi idara zote zote zipo chini ya wizara ya mambo ya nje, kitengo cha Uhasibu?...
Besides, kwa nini waziri wa mambo ya nje awe responsible ktk matumizi ya waziri mkuu?.. Kwani responsibility sii ya kila kiongozi kwa ngazi yake? Yaani wewe unataka kunambia JK alipokuwa waziri wa mambo ya nje aliweza kumwambia ama kumpangia Sumaye matumizi ya ofisi yake?.. Hivi kweli mama yetu Asha Rose anampangia EL matumizi yake ya misafara? if Yes! than why we don't question her kama tulivyotolea mifano ya JK!.. Why this time around tunamkosoa EL mwenyewe hali mpangaji safafri ni Bi. Mkubwa!
Haaa! Haa ! Jokakuu hapa unacheza na wakili mkuu wa ofisi ya Uwanja wa Fisi, Tandale..Kumbuka tu mimi ni wakili sina maslahi zaidi ya kuhakikisha haki ya kijiwe inatumika.
Jokakuu, Kupanga safari za waziri mkuu na watu atakaokutana nao ni mambo ambayo yanaweza kabisa yasiingiliane na Security ya kiongozi ama wapi atakula na kulala. Hizi zinaweza kuwa idara mbili tofauti kabisa! ndio maana Bush anapotaka kusafiri, vichwa zaidi ya 12 hukaa kitako kujadili na kupanga safari nzima wakati kila kitengo kina majukumu yake. Na fedha za msafara mzima hazitoki idara wala wizara moja..But kila wizara hukamilisha hesabu zake wakijumuisha matumizi ya safari hizo. Meaning wewe ukisafiri safari moja na mimi hata kama tunafanya kazi moja, idara ama wizara moja lazima kila mmoja wetu awasilishe hesabu zake ktk idara yake ya Uhasibu na sio jumla yetu kuwasilisha matumizi ya msafara mzima. Hakuna wizara inayoweza kunipa fedha mimi hali sipo ktk Payroll yao! It doesnt make sense!
Katika kujibu maswala la waziri mkuu mara nyingi hujibiwa na wizara zake, kumbuka kuwa majukumu ya waziri mkuu ni kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa shughuli za wizara zote. Wao wamezungumzia safari nzima na Abdoul Shareef hakutoa data za msafara mzima bali kutetea safari nzima kisiasa na sio Kiuhasibu....
Mimi nataka mnipe mchunga wa huyu JK!...Hizi safari kusema kweli ktk nchi yetu hatuhitaji mume mkaa ndani kabisa.. Njaa kali sana!
Wenzetu Kenya tayari mzee wa nyumba kesha weka biashara zake sawa! Kenya inajulikana kila kona na wawekeshaji hawaulizi mara mbili tofauti na sisi...Kwa hiyo ukimwona mzee wa nyumba hatoki ndani kisha hakikisha kuna chakula cha kutosha na vijana wake wanafanya kazi kuzalisha. Sisi Bongo bado tunaenda shule, tunalishwa kwa kila kitu, mzee lazima akazisake na zaidi kama karithi mradi wa Umalaya...(progressive). Pimp mzuri ni yule anayejua wapi wenye kulipa wanakojichimbia!...Mama tanzania sasa hivi anaweza kuhimili vishindo.. sii malaya?
 
Mkandara
Heshima yako mkuu ila nadhani wewe na wengine wengi hamjui madaraka ya waziri mkuu na mipaka yake labda niseme muundo mzima wa serikali ya Jamhuri ya Muungano. Wizara ya Mambo ya Nje ni wizara ya muungano ambayo haiko chini ya EL. EL ni bosi wa wizara ambazo siyo za muungano. EL kuiwakilisha nchi ni makosa ndiyo maana kwenye safari zake wanatumia lugha nyingine anamuakilisha rais. Waziri wa Mambo ya nje anaweza Zenji kumwaga chache EL havuki bahari kuna waziri Kiongozi ambaye anafanya kazi kama zake.
Pia, naomba utuombe msamaha kwa kusema Kenya iliwakilishwa na waziri mkuu. Kenya haina waziri mkuu. Mto hoja wa kwanza alisema iliwakilishwa na waziri wa mambo ya nje.
Mwisho, nadhani ni makosa sana kusema Marekani wana bunge. Kuna watu ambao hawajawahi kufika Marekani utakuwa unawapotosha sana. USA kuna Congress ambayo imegawanyika sehemu mbili Senate na House. Structure na madaraka ya Congress hayalingani na bunge letu. Na kwa kumalizia gharama za ziara za rais wa marekani zinagharamiwa na White House, hakuna Mawaziri Marekani.
 
Nilisahau kitu kimoja, mtu anaweza kuniuliza ni kwa nini Waziri Mkuu ndiye kiongozi mkuu wa serikali katika bunge la jamhuri wa muungano. Nadhani waulizeni viongozi wenu kwa nini makamu wa rais asiwe kiongozi wa bunge. Kwangu hai-make any sense kuwa na kiongozi wa serikali bungeni wakati kuna mambo mengine hawezi kujibu. We real need reform ya katiba na structure nzima ya serikali ni upuuzi mtupu uliopo sasa.
 
Mkuu nimekusikia

Kitu ambacho tunamlaumu JK hadi sasa ni ahadi ambazo aliwahakikishia wananchi kwamba atafanya ambazo zimeingia mkenge kuanzia hii ya Rich-monduli alikwenda pale Ubungo kwa mbwembwe na kuahidi umeme October matokeo yake umeyaona.

Alipewa majina ya wauza unga wewe niambie ni kigogo gani umesikia ameshitakiwa?

Mikataba mibovu ni mingapi ameamua kuifuta kwa manufaa ya taifa.

Kwa nini anamtetea Waziri mkuu kuwanyamazisha wabunge kuhusu swali la umeme? Huyu jamaa tuliisha ambiwa na mwalimu ni mwizi hatukusikia sasa matokeo ndio hayo.

Kwa nini hii mikataba inakuwa siri kubwa hata kwa wabunge?

Kwa nini wanatoa dharau kwa Bunge ambalo ni chombo muhimu kwa check and balance hii inaonyesha kuna mambo mengi tu ambayo wanaficha WHY?

Sasa kwa vigezo hivyo hapo juu utaona huyu jamaa anatupeleka pabaya, hatutaki kurudia huko ambako tulitoka.

Swala lingine muhimu ni hili la kufast track EAC iwe Union hawa majirani zetu sasa hivi wamekaa mkao wa kula – mkutano wa Oil Exploration utafanyika mwakani Arusha JK ataufungua sasa angalia ni sisi pekee ambao tuna gas ambayo sasa hivi ni commercialised wenzetu bado hawana kitu lakini wamo wamo tu na wanatumia sababu yetu kuvutia wawekezaji. Leo hii waambia Kenya wabadili jina la Kenya Airways kuwa East African Airways kama watakubali? Kwanza sio yao tena utaambiwa wana KLM and the like, ni sisi tu ambao tukiambiwa kitu hiki ni kizuri tunakurupuka. Mpaka hiyo gas kupatikana tumetumia pesa kiasi gani hadi tuanza kuingia mikataba mibovu na majirani? wakati tunahangaika walikuwa wanatanua sasa wakati wa kula keki wanaibuka.

Hizi agenda nyingine sio zetu ni za watu na rais lazima awe makini kwani anavunja hata heshima ya cheo chenyewe kwani akisema hamna kitu kinatokea.

Yapo mambo mengi ambayo inabidi tupike kelele vizazi vijavyo vitatulaumu mkuu.
 
Sam

Katiba ya JMT inasema kama rais akitoka TZ bara lazima VP atoke TZ visiwani lakini kiongozi wa shughuli za serikali TZ bara atakuwa waziri mkuu sio VP aliyetoka TZ visiwani. TZ visiwani wakitoa rais wa TZ basi VP atakuwa kutoka TZ bara ambaye pia atakuwa waziri mkuu.
 
Sam

Nakupa tano.
Utakumbuka kule BCS mimi na wewe tulizungumza hili sana kuhusu Katiba yetu.

Kitu ambacho naweza kukubali ni kwamba CCM wanajua tu siku wakikubali katiba kuandikwa au kusukwa upya utakuwa ndio mwisho wa utawala wao na itasahaulika kabisa. Kenya wana tatizo kama hili lakini wao wana afadhali kidogo, kwani wao wana Society na siyo chama.

Unajua kabla ya mabadiliko ya Katiba ya 15 ya 1984 mambo yalikuwa na afadhali kidogo. Rais wa Zanzibar ndiye aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais ndiyo maana Manunguniko makubwa ya Muungano hayakuwepo sana. Lakini baada ya kubadili mfumo yaani wa kumfanya Waziri kuwa na Madaraka Makubwa kuliko hata Makamu wa Rais. Hivi umeshamsikia Shein tangia awamu ya nne iingie madarakani?

Tanzania ya Leo ni sawa na nchi isiyokuwa na Katiba, na kama Nyerere (rip) alivyowahi kusema kwenye kakitabu kake ka Tanzania, tanzania "Siku tukimpata Rais mwenye kichwa cha Mwendawazimu anaweza kufikisha nchi pabaya.

Swala ni nini kifanyike kuwalazimisha CCM kuandika Katiba Mpya: Hili ni swali ngumu kwani wabunge wa CCM hawawezi kupingana na Serikali kwa hiyo hawawezi kuleta mswada wa kufanya White Paper ya Katiba.

Safari ni ndefu sana
 
Sam,
Uncle, karibu tena hapa kijiweni, Tena umeona kuwa Taasisi pia karudi?... eeeh bwna wee Taasissi baada ya miaka 4 karudi kijiweni!..

Aaaah! mkuu hilo la kusema waziri mkuu wa Kenya limenitoka! uzee tena..Hilo la Bunge la Marekani nadhani ndio lugha peke ambayo niliweza kuifikiria kwa wakati huo... sijui nimeweka wapi? lakini ndio hivyo kuna mara kibao hujaribu kutafuta tafsiri za maneno na matokeo yake ndio hayooo!.. Naharibu kabisa mchuzi!..

Dua,
Haya maneno sasa!..
Umeweza kuyaorodhesha haya lakini nakumbuka huko nyuma lilikuwa OMBI la JK kuyatimiza haya kuondoa hizi nuksi za Kiuchumi wa kubebana!...
Kwa hiyo, kama hizi taarifa zitamfikia na bado hakufanya kitu hapo naweza kusema mapungufu yake ni hayaaa!. hapo alipo sii ajabu kabisa hajui kwamba EL aliwanyamazisha wabunge ktk swala la Richmond! nakumbuka kuna mtu mmoja wa karibu sana na JK alinambia kuwa JK aliposikia hizi habari za Richmond na kuwa hawa jamaa ni bomu tu alisema:- 'Mbona mwaka huu nitaua mtu!...Ikiwa hizi habari ni za kweli jamani tutafikishana mbali sana!' maneno haya kayasema JK....
Waliokuwa karibu walimpoza na kusema ni uzushi wa wakereketwa!..Pili generator hazikununuliwa na serikali bali serikali itanunua umeme toka RDC kwa metre pindi utakapo anza kazi!..
Kwa hiyo bado mzee naomba bado makosa kama mchambuzi wetu mkuu Mzee ES anavyoweza kumwacha mtu uchi ndio nataka!...
 
Mkandara,
nilichoeleza mimi ni kwamba fungu la fedha za SAFARI ZA NJE za viongozi wakuu[raisi,makamu,pm] liko chini ya wizara ya mambo ya nje. waziri wa mambo ya nje huomba fungu hilo bungeni.

nimejaribu kuitafuta hotuba ya bajeti ya waziri wa mambo ya nje lakini sijaipata. nina imani kabisa hotuba hiyo ingepatikana basi tungeelewana katika suala hili.

vilevile, hata sumaye alipoulizwa kwanini ametumia millioni 500 kwa safari ile, jibu lake lilikuwa "waulizeni wizara ya mambo ya nje, wao ndiyo walioandaa safari hiyo."

ndani ya bunge, swali kuhusu matumizi hayo lilielekezwa wizara ya mambo ya nje na siyo ofisi ya waziri mkuu. ukweli huo unazidi kutetea hoja yangu kwamba ziara za viongozi nje zinagharimiwa na wizara ya mambo ya nje.

hoja yangu ni kwamba kama 2004 tulimlaumu sumaye kwa kufuja fedha za umma kwa safari za nje, basi 2006 tunapaswa kuwalaumu Kikwete na Lowassa kwa safari zenye gharama kubwa kwa taifa masikini kama tanzania.

kuhusu kujitambulisha nje ya nchi, sioni ulazima wa Kikwete kujitambulisha wakati serikali yake ni ya CCM, na amekuwa kwenye uongozi kwa miaka mingi kama waziri wa mambo ya nje.

Ile hotuba yake bungeni, na pale uwanja wa taifa, inatosha kumtambulisha huko nje. katika nyakato zote mbili kulikuwa na wawakilishi/mabalozi wa nchi zote ambazo amekwenda kujitambulisha.

Zaidi, hivi leo hii Marekani wakichagua Raisi mpya, je Kikwete atakwenda kujitambulisha? Maana ninavyoelewa mimi huyo Raisi mpya atakuwa hamfahamu Kikwete. Je, Benki ya Dunia, au IMF, wakichagua Raisi mpya Kikwete atakimbia huko nako akajitambulishe?

Hii habari ya kujitambulisha ni kufuja tu fedha za nchi bila sababu ya msingi. Kilichopaswa kufanyika ni Kikwete kuonana na mabalozi wa nje, na kuwaeleza msimamo wake, na nini utakuwa mwelekeo wa utawala wake.
 
Mkandara

Haya maneno sasa!..
Umeweza kuyaorodhesha haya lakini nakumbuka huko nyuma lilikuwa OMBI la JK kuyatimiza haya kuondoa hizi nuksi za Kiuchumi wa kubebana!...
Kwa hiyo, kama hizi taarifa zitamfikia na bado hakufanya kitu hapo naweza kusema mapungufu yake ni hayaaa!. hapo alipo sii ajabu kabisa hajui kwamba EL aliwanyamazisha wabunge ktk swala la Richmond! nakumbuka kuna mtu mmoja wa karibu sana na JK alinambia kuwa JK aliposikia hizi habari za Richmond na kuwa hawa jamaa ni bomu tu alisema:- 'Mbona mwaka huu nitaua mtu!...Ikiwa hizi habari ni za kweli jamani tutafikishana mbali sana!' maneno haya kayasema JKWaliokuwa karibu walimpoza na kusema ni uzushi wa wakereketwa!..



Hao waliosema ni uzushi wana proof kwamba ni uzushi au lilikuwa jambo la kubebana? Na kama sio hivyo JK amemuua nani hadi hivi sasa? je JK bado anawaamini hao watu wake wa karibu?


Pili generator hazikununuliwa na serikali bali serikali itanunua umeme toka RDC kwa metre pindi utakapo anza kazi!..



Mgawoooo Umekwisha unaweza kutuambia ni pesa kiasi gani serikali imetumia kwa huu mkataba? Je nani awalipe maana Tanesco wamesema mwaka huu tena mgawo ni mwisho – Kwa hiyo serikali iweke au ifunge huu mkataba maana hawajazalisha kitu chochote. Unaweza kufafanua hili na contact zako za karibu na JK? Ili tuache kudiscuss hii issue maana hatujapoteza fedha zozote?


Kwa hiyo bado mzee naomba bado makosa kama mchambuzi wetu mkuu Mzee ES anavyoweza kumwacha mtu uchi ndio nataka!...


La umeme sasa limekwisha unaweza kunipa mantiki ya kampuni nyingine kuinunua Richmonduli bila kuwa na kazi ya uzalishaji maana mabwawa yamejaa maji hivyo Richmonduli hatuwahitaji tena? Kama ulivyosema hapo juu.

Tafadhali fafanua vile vile kwamba rais hana habari kwamba Mwalimu alisema Edward Lowasa ni kibaka na hafai uongozi.

Vile vile Edward Lowasa kuwakemea wabunge wa CCM kutoa mawazo yao kuhusu swali la umeme Bungeni. Je kama huyu PM hamwelezi JK kitu kinachoendelea kwanini JK hamfukuzi mara moja?

Uongozi ni kuongoza na kutoa maamuzi ya msingi katika wakati unaotakiwa sio kusuasua.
 
Dua,
kama mgao umekwisha, wananchi tunahaki ya kuomba maelezo ya gharama za safari za JK, na EL, kutafuta wawekezaji wa majenereta, na mvua za kutengeneza, Marekani na Asia.

Mgao umekwisha ina maana hawa viongozi wametumia fedha zetu for NOTHING!! Kama siyo usanii huo ni nini?
 
Jokakuu,
Kwanza nitafutie hiyo ya wizara za mambo ya nje kugharamia misafara ya rais na waziri mkuu, maanake hii itawaondoa kabisa ktk madai yenu.
Nasema hivi kwa sababu ikiwa wizara ya mambo ya nje ndiyo hupanga misafara(jambo nalolifahamu) na pia kuigharamia hii misafara (nisilofahamu), then mgonvi wetu hapa ni Bi. Mkubwa.
Pili, swala la kujitambulisha sidhani kama nimesema kwa marais wa nchi nyingine ila kwa Wawekeshaji kulingana na sera zetu.
Hapa kijiweni umeona mwenyewe kukosekana kwa Freeman tumekuwa tukizungushwa huku na kule na kazi nzito imempata J.J kutafuta data kamili. Kujitambulusha kwa Freeman hapa kijiweni kulikuwa na uzito tofauti na J.J Mnyika ama Zitto. Pili, naamini Freeman angeaminika zaidi kwani ndiye kitovu cha Chadema...Umesoma mwenyewe kuhusu Mtei na Nyerere wakati Mtei kakubali ya IMF lakini Nyerere kaja kuwatimua.
Ikiwa Marekani watamchagua rais mwingine huyo rais atajitambulisha nje ktk hasa nchi ambazo watakuwa na interests zaidi. Pia wapo watakaokuja kujitambulisha na JK anaweza kuja kulingana na uzito wa mahusiano kati yake na rais huyo. Vilevile rais huyo anaweza kuja Bongo na sidhani wamarekani watauliza kwa nini kaenda Tanzania wakati Bush hakuwahi kwenda.
Mimi nachoomba mnipe sababu ambazo mnadai kuwa safari hizi ni fruitless pamoja na kwamba tumetumia fedha nyingi kutokana na safari kuwa nyingi na zisizokuwa na msingi.
Hilo la JK na EL kuwa answerable na matumizi makubwa, hapo mshikaji unapiga danadana maanake ni wewe unayenipa facts kuwa ni wizara ya mambo ya nje inayohusika kifedha!...it make sense zaidi nikizingatia kuwa balozi zetu ndio hukodisha hotel in advance n.k.
Unaposema JK na EL wako responsible, hii ina maana ofisi zao ndizo hupanga na kulipia matumizi ya hizi safari...Sasa tukubaliane moja ni nani anayehusika na kupanga misafara ya hawa jamaa...kifedha!
Mimi kusema kweli I have no idea kabisa tukishafika huko juu kiuhasibu..ila natumia elimu ya kitabu baada ya kushidnwa kuelewa ikiwa watu 10 toka Ikulu wamesafiri - how do you account matumizi haya kwenye wizara ya mambo ya nje (watu wasiokuwepo ktk payroll yao)!...Na umenipa jibu kuwa lipo fungu (item) ktk bajeti ya wizara ya mambo ya nje inayo deal na safari hizi.
Up to now they are cleared..... Bi. Mkubwa ndiye mgonvi wenu!
 
Mkandara,
Umesahau kuwa balozi ziko chini ya foreign affairs. Bajeti yao hutoka huko huko.
 
Jasusi,
Ina maana hata lile fungu tulilonunulia jengo la ubalozi Roma lilisainiwa wizarani! bila shaka aliyesaini anajulikana...
 
JK ama vasco da Gama anajua sana nani na zile pesa zimeenda wapi sasa hushangai kimaya kikuu ? Lakini msisahau anajimbulisha kama Mkapa mambo yake ni yao .
 
Jasusi,
nadhani hukunisoma vizuri hapo nyuma.
Nimesema maelezo ya Jokakuu yana make sense kwa kuzingatia kuwa balozi wetu huwa ndio wanakodisha hotels na mipango ya usafiri kabla rais ama Waziri mkuu hajafika. kwa hiyo nakubaliana na Jokakuu kwa misingi hiyo. yaani wizara ya mambo ya nje ndiyo hulipia gharama za usafiri.
Utaratibu wa huko juu kabisa - IKulu na Ofisi ya waziri mkuu, kusema kweli sielewi unakwenda vipi ktk mahesabu.
Navyofahamu mimi na elimu yangu hii ya madrasa, huwezi kulipa Posho wala expenses za mtu yeyote yule nje ya watu waliokuwa ktk payroll (wafanyakazi wako) unless watu hao ni service providers (vendors) kibiashara. Na ktk dunia hii ya PC hizo software haziwezi kukubali kabisa matumizi ya mtu nje kama mfanyakazi ikiwa mtu huyo hayupo ktk payroll, inawezekana kuwa Rais na PM wapo ktk payroll ya wizara hiyo pia.
Sasa tukiacha hilo ambalo nimekubali kuchukua mtazamo wa Jokakuu, nadhani hapa sisi tunatakiwa kumpa kitimoto Bi. mkubwa Asha Rose na ndiye anatakiwa kuja na majibu kwani wizara yake ndiyo inayopanga hii misafara na matumizi yake.. Je, haoni kuwa serikali hizi (nyingi) ni matumizi mabaya?...
Jasusi, kumbukeni mara nyingi misafara ya Marais na PM huwa wanapangiwa zaidi ya wao kupanga...Na mara nyingi utakuta hata appointment nao inakuwa ngumu lazima upitie kwa mtu ambaye anazo ratiba zote... Tena basi rais anaweza kuuliza ratiba yake ya kesho, hii ikiwa na maana yeye hajui kichwani.
hapa najaribu tusije kuwalaumu bure na hizo safari kumbe ni muhimu sana kama Bi. Mkubwa alivyoziona...Huyu Bibie ndiye wa kumuuliza zaidi tupate facts kisha hapo tutajua tuanze na nani!
 
Mzee ES umeshusha kitu...

Nilichofurahia mimi binafsi ni kuwa, Dar watu imekuwa kama wamepitiwa na upepo fulani hivi. Ilikuwa ni kuanzisha ubishi mkubwa kabisa pale mtu akisema, jamani, huyu ni candidate wa CCM and don't expect too much changes - ilikuwa unaonekana unaitakia nchi mabaya. Pamoja na kuwa niukweli wa wazi kuwa kazi kubwa na tele imejaa mbele na kuna nafasi nyingi tuu ambazo hazikuoana na hulka mtandao wa JK uliopigilia debe, bado KILA mtu aliona si vyema kumpinga manaje huyu jamaa ni different style - tumpe muda.

Angalia magazeti yanvyochombeza with pages and pages za hongera? Hawa watu ni kujipendekeza na kujiweka sawa eti akiwaona awakumbuke. Ni sawa alivyowashushua pamoja na kuwa ni wazi ila kuna hatari Tanzania kuendekeza siasa za personality cults. We need stronger institutions sio majina na sura.
Saw, lazima apewe muda, ila dalili ya mvua ni mawingu. Kwa majority of vote alizokuja nazo madarakani, JK administration is supposed to capitalise on this and actually waburuze nchi towards maendeleo sio lele mama za kizamani. Ukiuliza hili unaambiwa, baado ngoja utaona! Ngoja hadi lini? Nikupe mfano mdogo mtu, kama Mahita alichemsha (kama kweli na kama data wanazo) basi hakutakiwa hata kidogo apate muda wa kustaafu kistaarabu. Unless kisheria ilishindikana. Ila kama ni simply political, basi safari yetu ni ndefu sana. Alitakiwa aweke zero tolerance kwenye uongozi wake kwa uzembe wowote as he had a full mandate ya 80% sio? Unajua kwanini inashindikana? Ni kwa vile ni maswala yale yale ya CCM.
 
Taasisi
Mahita ana kiburi sana na hata kesi yake itafutwa Mahakani dhiki ya CUF kwa kuwa alikuwa natekeleza maagizo ya CCM. Kila alicho fanya Mahita ilikuw kwa maelekezo. Ujambazi uliota mizizi Nchini si kwamba Polisi hawakuwa wanajua hapana . Ila umempa jina JK sasa .Alijua nini chanzo cha ujambazi na kasema acheni maana anawaju ni wanachama na donors wa CCM. Ila karibia na mwisho Ujambazi utazuka tena na watasema tupeni muda tuendelee kupambana . Mahita hawezi kufanywa lolote sawa na Mahalu . JK anajua yote na alicho fanya ni unafiki tu hana lolote .
 
Linyungu,
Tafadhali fafanua hapa kwani kila pingamizi lina hadithi (sura) nyingineyo!....
Unaweza kutuambia dhumuni la JK kumwondoa Mahita - unafiki ni matokeo ya motive fulani..Ipi hiyo?
 
Topic hii nitakuwa nikijitahidi kuweka Speech zote za JK.

Hapa nimeanza na Speech alizozitoa huko London hivyi karibuni.

STATEMENT BY H.E. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, INVESTMENT ROUNDTABLE LONDON, UNITED KINGDOM, JANUARY 15, 2006 Merril.pdf

STATEMENT BY H.E. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, AT CHATHAM HOUSE ON DEVELOPMENT IN AFRICA: TRANSFORMING THE PUBLIC SERVICE Chatham House.pdf
 

Attachments

Back
Top Bottom