Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

Mkandara

Nimekusikia mkuu lakini sikupingi hebu tuangalie some facts ambazo mimi naona valid:

MIKATABA:- Umezungumzia Arbitration...nadhani JK kesha fanya hiyo na hao Barricks! jambo ambalo wengi hatuweza kulikubali ni kile tulichopewa!.. ongezeko la dau kidogo hali hakuna mahesabu!..
Tumetaka zaidi lakini haikuwezekana kwa sababu tulisha jifunga na hiyo 3%. Swala la hisa ni nje ya mjadala kabisa labda JK akubali kupindua mikataba!


Sasa hili limefanyika kwa Barrick peke yake, na muda unaotumika ni mrefu mno Kwa sababu mikataba mingi imeingizwa kwa rushwa hivyo kipengele cha unfair contract kinaweza kutumika ukilinganisha na nchi zingine kwenye mikataba yao. Vile vile mbona hata kile walichokuwa wamekubali kutoa walikuwa hawatoi mpaka walipokumbushwa?

Ukumbuke biashara ya madini ni ngumu hivyo faida wakati wa majadiliano ilikuwa ya kubuni sana lakini sasa madini yanatoka sana, mambo ya kubuni yawekwe karibu na matarajio yenyewe. Sikatai hizi kampuni vile vile lazima zianze kuajiri watanzania na kuwalipa vizuri kama wanavyolipwa wageni- ndio hilo tunaloligombea kwani wenzetu wanakula keki kubwa mno kuliko wenye mali. Kitu kingine hapa wataalamu wa Kitanzania wananyanyaswa sana na haya makampuni why? Kwa sababu serikali ni bubu sana hawajali maslahi ya wananchi wake.


BENJAMIN MKAPA: we have assured [potential foreign investors] that we will not put any unfair restrictions upon them at all. It's all legislated for, and in some sectors there's even special legislation. For instance, we had a particular legislative and tax regime for the mining sector, and they've been able to come in quite confident that they are secure for the life of their mines, which is anything between 15 and 20 years.


Sasa kuna faida gani kwa watanzania kuendelea na mikataba hii ikiwa faida yote inakwenda nje? Tunarudi pale pale wakati mwalimu alipotaifisha mashamba ya katani na kadhalika, ambapo wakati ule ndio tulikuwa bado kabisa kimaendeleo.

Ipigwe hesabu tuone nini tutapata na nini tutapoteza kama mikataba hii ikivunjwa. Usiri mkubwa unaotawala hii mikataba ndio chanzo cha matatizo yote haya kwanini Kamati ya bunge isihusishwe kufuatilia hili na wananchi tuelezwe kuliko kufichaficha.

Kweli kuna mikataba ambayo kuivunja ni vigumu lakini siyo yote, ile ambayo rushwa imetumika kuiweka – haya makampuni watuambie ukweli nani wamempa pesa na kwa kitu gani? Hawa watu wakibanwa kisheria watawasema walikotoa pesa. Mbona huku majuu watu mambo yakichacha wanatajwa – Tanzania tusijifanye kama tunaishe kwenye sayari nyingine – Mikataba inavunjwa kwa interest ya nchi sio mtu au kikundi kilichokula rushwa.

Hapo juu mwenyewe kasema ‘not put any unfair restrictions upon them (kwa nini walitoa rushwa katika mikataba mibovu?) it must be fair on both parties.

sidhani kama kuna Mtanzania ambaye yupo tayari kumtetea JK pindi ikitokea hali ya Zimbabwe!.. .. That is a Fact na tumeyaona kwa Wazimbabwe wenyewe ambao walipiga makelele kwa mikaa zaidi ya ishirini. Mugabe akawaambia tusubiri hadi mwisho wa ahadi ya Waingereza kisha tutaidai ardhi yetu kwa nguvu kwani kisheria hawawezi kutufunga. Well, Mugabe kayafanya aliyowaahidi leo hii wanamlaumu kwa kila kitu. Sheria ile ile aliyoiogopa kwa miaka ishirini pia imepindishwa aonekane yeye mkosa!



Hilo la Zimbabwe naona huna fact nalo kwa sababu Ule mkataba wa Lancaster uliisha baada ya miaka 10yrs i.e 1990. Mugabe alikataa kuchukua ardhi wakati ule lakini ilipofika fujo ya Congo kwa Kabila yeye ndiye alishinikiza Congo waingie SADC ambapo Tanzania walikuwa hawataki kutokana na Historia ya nchi hiyo na USA, na vile vile wakati ule TZ walishaamua kutoingilia mambo ya vita kwa maslahi ya watu wengine i.e. Tujenge nchi yetu ukombozi umekwisha ndio maana wakati Mugabe anapeleka majeshi kule TZ iliwarudisha wataalamu wa jeshi 1000 waliokuwa kule maana sasa ilikuwa ni vita, hata Zambia walikataa kupeleka majeshi kule na tangu pale uhusiano wa TZ na Zimbabwe kuzorota. Zimbabwe walitegemea ku-recover pesa yao kwa dhahabu n.k. lakini mambo yalikuwa magumu hivyo uchumi wa Zimbabwe ukaanza kuzorota na popularity ya Mugabe. Mugabe kuona vile ndio akaanza kutaka Kujisafisha kuchukua mashamba kutoka kwa wazungu bila compensation (ukitazama ya Zimbabwe huyo jamaa ni dictator tangu aingie kwani aliuwa watu wengi sana kule matebeleland na wale wote waliokuwa wanampinga. Suala lake ni tofauti sana na Tanzania.

Ongea na Zimbabweans ambao wako neutral watakwambia kinachoendelea kule huyu jamaa anauwa waafrika wenzie it’s a pity.
 
Dua,
Hizi habari mbona unazizungusha sana?..
Unfair contract gani ikiwa contract hizi zimewekwa na rais wa nchi? na mwenyewe anatangaza kuwa tumewapa urahisi ili waweze kuwekeza!... Labda unataka kupotosha maana ya Legislative. Hii ni sheria ambayo tumeiweka sisi sio wao!... hapa nani kamuonea nani?
Na ni nani kakuambia kuwa Barricks walikuwa hawalipi hiyo ruzuku? toa ushahidi hapa maanake ni kosa letu tumezigawa hizo 3% kwa walanguzi ndani nchini. Labda unataka kusema JK aondoe hao walanguzi,yet hiyo 3% itasaidia nini?...Hapa sioni nje bob, ni sawa na kuzaliwa Mkerewe hali wewe hukupenda uwe kabila hilo!...Muhimu ni kukubali Ukererewe wako na kuanza kujichanganya, ndio JK anayoyafanya hapa!

Swala la Zimbabwe mshikaji wala usianze na hizi propaganda za hao wanaodai hiyo Lancaster ilikuwa jukumu la serikali ya Mugabe... ndio maana nimesema hiyo hiyo sheria aliyokuwa akiiogopa Mugabe ilipindishwa na Mugabe kuonekana mkosefu. Mkutaniko wa Lancaster ulikuwa mwaka 1979 na hata constitution yao ilitengenezwa na waingereza. Hiyo unayozungumzia ya 1990 ni ku amend baadhi ya sheria za Lancaster ikiwa ni pamoja na kumfanya Mugabe awe rais badala ya waziri Mkuu.
Serikali ya Uingereza ndiyo ilitakiwa kutoa fedha za compesation kwa serikali ya Mugabe... hawakutoa! na Mugabe mwenyewe kisha wa-challenge Waingereza ana kwa ana kuhusu hilo hakuna aliyesema ni UONGO.
Tena kwa taarifa yako Mugabe alitaka kuifganya nchi hiyo iwe ya Kijamaa toka siku ya kwanza, Nyerere akamshauri asifanye hivyo!..Swala la Ardhi lilianza zamani kabla kabisa ya hata Mugabe hajaingia ktk picha... wewe umewahi kusikia kitu kinaitwa CHIMURENGA? ...Bob Lancaster ni matokeo kama suluhisho la mapambano ya ardhi ambayo wananchi walipamba moto!....
Leo hii hao waingereza ktk magazeti yao wanadai kuwa Mugabe kujiingiza ktk vita ya Congo ndiko kumefanya serikali yake ishindwe kulipa..
Dua nimekwenda Zimbabwe nchi bado kabisa changaa ikiwa ktk nepi. Najua mengi sana wala sina haja ya kuuliza Wazimbabwe ambao wengi wao hawaifahamu kabisa historia ya nchi yao zaidi ya kusoma magazetini kama tulivyoshindwa sisi ktk historia ya Uhuru wetu.
wazungu wachaf sana wanapotaka kuharibu jina la mtu. Kosa kubwa la Mugabe ni kukalia kiti cha Urais kwa muda mrefu!... lakini kama akiondoka basi hata mwelekeo wa nchi yake utabadilika vibaya vibaya. Huyu jamaa kweli dikteta kama Sadaam Hussein. Akitoka ktk madaraka hali hakuna wa kumrithi nakwambia Washona na Wandebele watazipiga wenyewe kwa wenyewe huku mzungu akikusanya zake...Wewe si unakumbuka wakati alipokamata Bishop Muzorewa?... Unakumbuka kuwa weusi walifanyiwa unyama kuliko tunavyoweza kufikiri leo kuwa mwafrika kweli anaweza kuwaacha wenzake wateseke kiasi hiki?..
Kwa hiyo hapa tupate picha mbili kwa kila tunalo jadili...Yes JK anaweza kuwa sii kiongozi mzuri lakini ukweli ni kwamba hatujawahi kuwa na kiongozi toka enzi ya Nyerere!...Na Nyerere made the mistake ambayo labda inampa kusita mtu kama Mugabe!
 
Dua,
Barrick walishapewa 100%ownership ya madini yote Tanzania. Hata leo ikija kampuni mpya lazima ilipe license fee to Barrick and not toTanzania. Ndio maana ilibidi makubaliano yafanywe na Barrick. Na kila ziara anapokuja Kikwete Marekani Sinclair anahakikisha wanakutana.
 
Mkandara,
rudia maelezo yangu....nimeeleza kwamba JK na EL wamefanya ziara nne marekani na canada. JK ametembelea marekani mara mbili, na EL ametembelea marekani safari ya kwanza,safari ya pili amekwenda canada, na mexico.

kwa mtizamo wangu haya ni matumizi makubwa mno kwa nchi masikini kama tanzania. ati raisi anakwenda kujitambulisha!! hivi haitoshi kufanya mazungumzo na balozi wa marekani tanzania? IMF na WB nao si wana wawakilishi tanzania? mpaka leo, mwaka mmoja tangu achaguliwe, JK anafanya ziara za kushukuru wananchi kwa kumchagua!!

mkutano wa un ambao JK alihudhuria, kenya walituma waziri wa mambo ya nje. sisi mikutano miwili un, mmoja tumemtuma raisi, mwingine waziri mkuu. waziri mkuu kwa kawaida ni mtu wa ndani, tofauti kabisa na huyu wa sasa hivi.

kuhusu ile safari ya sumaye, ninavyoelewa mimi ilipangwa na kuratibiwa na wizara ya mambo ya nje. waziri aliyekuwa anahusika ni jk. hata bungeni walipouliza mahesabu yake waziri aliyejibu alikuwa ni dr.shareef.

ilikuwa ni kampeni za wanamtandao kuvujisha habari ile na kumbebesha lawama sumaye. kama ulikuwa humjui jk na kampeni zake chafu basi pale ndiyo ulipaswa kumjua.

kama waandishi waliweka hadharani matumizi ya safari ya sumaye, basi wanapaswa kufanya hivyo kwa hizi safari zisizokwisha za JK na EL.
 
Mtalii,
Thanks. Ni uungwana kukubali kutokubaliana na kukubaliana pale lengo letu linapooana. Uzalendo kwangu ni dam dam.
 
Shukrani mzee wangu Dua,

Jamani kwa taarifa tu ni kwamba issue ya Rich-Monduli ndio kwanza huku bongo imeanza, leo magazeti yalikuwa na party ya Rich-Monduli, kwa hiyo tutafute ukweli tuuweke kwenye forum maana wazee wanatafuta independent info kuhusu the issue!
 
JokaKuu,
Nakuunga mkono kwa hilo. JK alishajua kuwa wapinzani wake katika urais mmojawao ni Sumaye. Kwa hiyo alikuwa tayari anakusanya data za kumharibia. Kama alivyofanya kwa Salim.
 
Jokakuu,
Ama kweli mmeamua kumshikia bango JK... Yaani kila Mtanzania alilalamika na safari ya Sumaye leo hii jamani mmeisha sahau?...
Tumezungumza haya kule Bsctime na wote mlikuwa msitari wa mbele aliposhindwa na wengi tulisema atashindwa kwa sababu ya matumizi yake mabaya.. including Mkapa mwenyewe. Leo hii mmesahau kabisa matumizi yao hata mnadiriki kusema kuwa JK alikuwa na njama against Sumaye!...damn..
Jamani mwee basi itakuwa humu tunadanganyana maanake sisi wengine yote tumeyafahamu kupitia mtandao na nyie mlikuwa vinara wa kutupa kila alofanya huyo Sumaye...ambaye mimi sikumjua kabisa.
Kuhusu Mkutano wa UN:- Nooo! Jokakuu, yaani Kenya wakipeleka waziri mkuu na sisi tufanye hivyohivyo au sio! Who are they na wamefanikisha kipi kwa mwendo huo?
Ndugu yangu Kibaki kashika madaraka muda na sii mara yake ya kwanza kuwepo UN kama JK. Kenya wamepeleka waziri mkuu hatufahamu yaliyomkuta Kibaki lakini mkutano ule ulikuwa wa viongozi wote...unless unataka kusema 90% ya nchi zilizopeleka marais wao walikuwa wrong!
Soko kuu:- Kuinadi nchi mshikaji inahitajiwa rais wa nchi hasa zetu za Kiafrika wakati wa mabadiliko ya utawala. JK na EL kutembelea nchi hizi haiwezi kuwa bomu ikiwa sote hatufahamu zaidi kilichopatikana ktk ziara hizi..infact wote hapa tunatamani kufahamu kilichopatikana zaidi na ndio maana tunalalamika kwa kutofahamu...Hii si ajabu kwani ndio Watawala hufanya hivyo kwa kura zetu wenyewe.
Kisha nataka kuwauliza vizuri, toka lini safari za waziri mkuu zikapangwa na Wizara ya mambo ya nje ktk matumizi ya waziri huyo?.. I mean nambieni kama waziri mkuu huwakilisha hesabu zake wizara ya mambo ya nje! Huko kupangiwa sehemu atakazo hutubia na watu wa kukutana naye havihusiani kabisa na matumizi ya Waziri Mkuu...foreign affair sio watchdogs!
Jokakuu, tumefanya kazi serikalini na tumefanya idara za fedha ambako viongozi kibao huenda nje hata mikoani tu na hutumia fedha zaidi ya posho walizopewa! Hii kawaida kabisa na wanaporudi huwa wakali kurudishiwa fedha zilizotumika zaidi hali receipt zimechapishwa kimazishi, sasa itakuwa safari ya US na lini viongozi wetu wakakosa sababu ama watu wa kuwatetea. Wee umeona Zitto anavyopata taabu huko Bungeni! akiuliza swali waziri huyu, jibu hutolewa na waziri mwingine kabisaaa tena la kihuni!..
Mimi nataka mnipe vitu kama hiyo scandal ya Rich -Monduli ambayo naanza kuamini kuwa sii ajabu kabisa kuwa hizi deals zinatembea nje ya mkono wa JK. mathlan hilo la bwawa la Rufiji umeona mwenyewe hawa jamaa wanafuta mikataba kwa sababu zao binafsi...Sioni mkono wa JK wala Bunge hapa zaidi ya hivi vitengo uchwala vya KULA!..Yaleyale yaliyomwangusha Nyerere -WATEKELEZAJI ndio walaji!..
Toka Mkapa ambaye alikuwa akisisitiza kujenga infrastructure ktk interview yake hakufanya kitu na tunazidi kusahau yaliyopita... ama kweli sii ndwele!
 
Mzee ES; heshima yako mkuu! Uzalendo wako wastahili pongezi.
Ndugu yetu Dua amejitolea kukukusanyia data; nami nilikuwa tayari kutumia masaa ya mwaka huu yaliyobakia kufanya hiyo kazi kwa manufaa ya wote.
Rest assured kuwa pamoja na wengi wetu kuwa na kazi nyingi hizi za uzalendo tutazipa kipaumbele. Tupe kazi mzee!
 
Mzee ES,Maneno yako makubwa yana mguso mzito,cha maana na msingi ni kumwambia Mzee mzima Butiku arudi Musoma kwani enzi zake zimekwisha! Ndugu Zanaki naomba ufafanuzi nani huyo amepewa tender na watu wa MNF ni Gunini,Mayenga au Liku?kwani hao ndio watoto wa Mama Kamba,ambao Baba yao alipelekwa Brussels ili Mzee Butiku apate muda na huyo mama!Oooh wazee wetu wana mambo machafu ambayo hayawezi kusemeka.Kwa mtazamo wangu "kiongozi mzuri ni yule anayejali familia yake"lakini kwetu ni versi versa kwani kiongozi mzuri ni yule mjuzi kwa wanawake!.

Mwawado,ntakudanganya kama nikitaja jina,lakini ntalipata na will keep u posted
 
Huu ni mwanzo tu . Kama wamachinga wameanza kushituka je wajanja zaidi ?
 
Halima Mlacha
HabariLeo; Thursday,December 28, 2006 @00:06

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, John Malecela, amewataka Watanzania kuwa na subira katika suala zima la uchumi kwani ni mapema mno kumlaumu Rais Jakaya Kikwete.

Aidha ameiisifia Serikali ya Awamu ya Nne kwa jitihada zake katika kipindi cha mwaka mzima wa 2006; na kuongeza kuwa imejitahidi kwa kufanya vyema kwenye uchumi hali inayoashiria kuwa mwaka 2007, utakua kwa asilimia kubwa zaidi.

Malecela ametoa kauli ya kuisifia Serikali ikiwa ni wiki moja tu, Rais Kikwete kuadhimisha mwaka mmoja kukaa madarakani ambapo Watanzania wengi walitoa maoni mbalimbali.

Wakati wa maadhimisho hayo, Malecela alikuwa nje ya nchi. Akizungumza na HabariLeo, jana nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, alisema suala la uchumi linahitaji subira na uvumilivu kwa vile kukua kwa uchumi na maendeleo ya nchi yoyote kunahitaji muda wa kutosha.

“Kiuchumi kwa kweli Serikali ya Awamu ya Nne imefanya kazi nzuri, imeendeleza yale mema ya awamu ya tatu na kuanzisha mengine mapya ambayo tayari manufaa yake yameanza kuonekana, na sidhani kama sasa hivi ni muda muafaka wa kuanza kutoa lawama, kwani ni mapema mno,” alisema Malecela.

Aliwataka Watanzania kuacha tabia ya kulaumu kila kitu na kuvaa miwani mekundu, jambo linalowasababisha kuona kila kitu chekundu na kisha kujitukana wenyewe. Alisema Watanzania wanatakiwa kuwa wavumilivu kwa vile kuwapo kwa Serikali hakumaanishi kuwa inao uwezo wa kutamka jambo kisha litokee, bali kila kitu hufanyika kwa utaratibu na mafanikio yake huonekana taratibu na si kwa ghafla.

“Watu wanafikiri Serikali ndio kila kitu, yaani ikisema ajira zije basi zinatokea au umeme uje basi unatokea, kila kitu mafanikio yake huja kutokana na taratibu husika kwani hakuna kitu kinachokuja kwa ghafla, ipeni muda kwanza Serikali kabla ya kuanza kulaumu,” alisema.

Alisema kutokana na kufuata taratibu zinazohitajika, Serikali ya Awamu ya Nne kwa sasa imepata mafanikio katika nyanja mbalimbali yakiwamo matumizi ya rasilimali za nchi hasa katika upande wa migodi ambayo kwa miaka mingi ilikuwa haitumiki. Alisema pamoja na matatizo ya ukosefu wa mvua za kutosha na umeme, bado Tanzania imepata bahati ya kugundua gesi ya Songas na Mnazi Bay ambapo kama itatumia mvua za vuli na makaa ya mawe kuna uwezekano mkubwa mwakani kukawa hakuna tatizo la chakula wala umeme.

Aliiomba Serikali kushughulikia suala la kutoa umeme kwa njia ya makaa ya mawe ili kupunguza bei ya nishati ambayo kwa sasa imepanda na kuathiri shughuli mbalimbali za uchumi ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa viwanda.

Malecela alisema matatizo ya vita vya Mashariki ya Kati yameathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania, hasa katika suala la mafuta, jambo ambalo inabidi watanzania washirikiane na Serikali kutafuta njia ya kupunguza matumizi ya mafuta hayo na kuipunguzia nchi yao na wao gharama.

Akizungumzia suala la kukithiri kwa rushwa na dawa za kulevya alisema tatizo hilo lipo duniani kote na ushirikiano pamoja na ukweli unahitajika ili kuweza kuwafichua wahusika.

“Kila siku tunasikia eti vigogo wana kula rushwa, ni wa kina nani hao vigogo? Mimi mwenyewe ni kigogo wa CCM, basi watu si wawataje ili wachukuliwe hatua? Tatizo la rushwa ndio hilo, tuko tayari kusema rushwa ipo lakini kusema wakina nani tunakuwa na vigugumizi,” alisema.
 
Butiku kama walivyo wengi hapa wana vizia ama kuna kitu kaona sasa anakinyatia .Si bure huyu
 
"Kila siku tunasikia eti vigogo wana kula rushwa, ni wa kina nani hao vigogo? Mimi mwenyewe ni kigogo wa CCM, basi watu si wawataje ili wachukuliwe hatua? Tatizo la rushwa ndio hilo, tuko tayari kusema rushwa ipo lakini kusema wakina nani tunakuwa na vigugumizi," alisema.


Mwalimu alimtaja Edward Lowasa mbona nyie CCM mnamkumbatia? Kama hata mwalimu alimsema halafu hamtaki kumchukulia hatua Je, mnataka mwenyezi mungu aseme ndio msikie?

Kigugumizi mnacho nyie wenyewe CCM.
 
Sorry folks, I had to merge these 'sifas' to JK and EL from Malecela & Butiku as they seem to be of the same content. Hope am well understood hence no prob.

Nawatakia maandalizi mema ya kumaliza mwaka 2007. Kila la kheri na nawaombea nyote mvuke salama tuufikie mwaka 2007 kwa pamoja. Wengine hawaonekani online siku hizi, huenda wako safarini n.k, tuwaombee warejee salama na kujiunga nasi katika mwaka ujao.

Mijadala myema,

Invisible (Nipo hapooo--- kwenye sofa nimelala) 🙂
 
Mkandara

Dua,
Hizi habari mbona unazizungusha sana?..
Unfair contract gani ikiwa contract hizi zimewekwa na rais wa nchi? na mwenyewe anatangaza kuwa tumewapa urahisi ili waweze kuwekeza!... Labda unataka kupotosha maana ya Legislative. Hii ni sheria ambayo tumeiweka sisi sio wao!... hapa nani kamuonea nani?
Na ni nani kakuambia kuwa Barricks walikuwa hawalipi hiyo ruzuku? toa ushahidi hapa maanake ni kosa letu tumezigawa hizo 3% kwa walanguzi ndani nchini. Labda unataka kusema JK aondoe hao walanguzi,yet hiyo 3% itasaidia nini?...Hapa sioni nje bob, ni sawa na kuzaliwa Mkerewe hali wewe hukupenda uwe kabila hilo!...Muhimu ni kukubali Ukererewe wako na kuanza kujichanganya, ndio JK anayoyafanya hapa!

Swala la Zimbabwe mshikaji wala usianze na hizi propaganda...............


Hapana kuzungusha mkuu kama contract imewekwa kwa rushwa ya kumlipa Richmonduli akiwa kiongozi then it is unfair for the country kwa sababu aliyetoa rushwa alijua hayo na mahakamani watashindwa swali ni ku-prove hiyo hongo? Heads must role ……. Kama ni yeye rais basi ajiuzulu

Hakuna kujifunga na hiyo 3% ndugu yangu. Nakubaliana na wewe na nasema ndio kazi ya rais aamue kusuka au kunyoa. Leo hii rais ana power ya kuwaambia wafungashe virago. Lazima azingatie hasara na faida kwa sababu Tanzania sio yao. Hatuwezi kuwa vibaraka wa kuwaneemesha wageni kuliko sisi wenyewe – charity begins at home.

Kama ni kweli walinunua kwa mikataba ya makaratasi ni kiasi gani walitoa? Je hii tenda ilitangazwa kwamba madini yote ya bongo yanauzwa hivyo highest bidder ndio walikuwa wao? Mbona wengine hatukuisikia hiyo?

Nigeria hivi sasa kila kukicha wataalamu wa mafuta wanatekwa nyara, je tunahitaji Tanzania iwe hivyo? Au iende kwenye kuwateka watu walioajiriwa na makampuni ya kuchimba migodi? NO WAY! BRO, hiyo special legislation inabidi hawa jamaa waelezwe na wakubali kama hawataki basi siyo lazima zipigwe hesabu wachukue chao mapema waondoke. Hiyo 3% ni dhambi na dharau kubwa hata hao Barrick wenyewe wanafahamu.

Hizo ruzuku nilisoma hapa au kwenye magazeti walianza kulipa wakati JK alipokuwa rais ingawaje zilikuwa kwenye makubaliano ya awali.

Kuhusu Zimbabwe nimesema hapo juu nitafafanua, hii siyo propaganda ni facts Mugabe amewapa biashara zote kubwa na zenye faida ndugu zake na marafiki pamoja na mashamba ya dhuluma bila compensation of development. Sabina Mugabe ni dada yake vilevile ni mbunge anatumia cheo cha kaka yake kujitajirisha, mtoto wake Leo Mugabe hatumii jina la baba yake alipewa uongozi wa ZIFA chama cha soka hadi FIFA wakaingilia kati, huyu ni nephew wa Mugabe (President). Phillip Chiyangwa alifungwa ni mbunge lakini ilikuwa kiini macho anatoka alikozaliwa Mugabe – KUTAMA. Kila biashara anafanya kwa ajili ya Mugabe. Mashamba ambayo wazungu wamenyang’anywa hawapewi wananchi bali marafiki wa Mugabe pekee. Wote wana vyeo kwenye serikali yake na hata hawayatumii kulima wameweka kama investment ndio maana wana shida ya chakula.

Zimbabwe walikuwa wanapewa pesa na UK kwa ajili ya hiyo compensation uliyosema lakini ilisimamishwa wakati Mugabe aliposhindwa ku-account matumizi yake na a lot of Zimbabwean walikuwa wanaomba refugee status UK hivyo serikali iliambiwa ni bora izitumie pesa hizo kwa wazimbabwe hapa UK kuliko kumpelekea tapeli kwenye account yake. Fedha nyingi zimejenga Graceland ambaye ni mke aliyemuoa baada ya kufiwa na yule mama wa Ghana. Huyu Grace alikuwa secretary wake.

Mzimbabwe yeyote anayeanza biashara ikiisha kolea ni lazima auze kwa ndugu wa Mugabe sivyo utafuatwa na vyombo vya usalama . Strive Masiyiwa alianzisha biashara ya kwanza ya cellular phones aliambiwa auze kwa kina Mugabe akakataa leo hii anaishi Botswana alikokimbilia na harudi Zimbabwe hadi jamaa afe na kampuni yake iko Zimbabwe, Botswana na Nigeria.

Morgan Changirai kabla hajaanzisha opposition alifuatwa ofisini ili ajirushe kutoka ghorofa ya saba (au zaidi) ili ajiue akakataa lakini walifanikiwa kumpiga ile mbaya hivyo utaona style ya huyu jamaa. Economy ya Zimbabwe ilikuwa driven by white farmers (Tumbaku) na makampuni ya UK na South Africa (madini). kampuni nyingine ya Australia imekimbia kwa ajili ya matatizo ya sasa.

Wenyewe kwa wenyewe hawapendani i.e. Ndebele and Shona makabila mawili makubwa. Hivyo utaona ni matatizo ambayo ni tofauti kabisa na yale ya kwetu bongo. Hata ule mkutano wa kuwaingiza congo kwenye SADC na kupeleka majeshi kule ulifanyika Zimbabwe na Tanzania wakati ule iliwakilishwa na balozi Muganda wakati ule kule Zimbabwe kwani Mkapa alikuwa kwenye ziara za Scandinavian countries.

Ukipenda tembelea hapa http://www.zimbabwesituation.com/ au http://www.newzimbabwe.com/

Hili la Zimbabwe naona tuliache na inabidi JK akate mzizi wa fitina na hizi contracts period!
 
mkandara wrote:
Jokakuu,
Ama kweli mmeamua kumshikia bango JK... Yaani kila Mtanzania alilalamika na safari ya Sumaye leo hii jamani mmeisha sahau?...
Tumezungumza haya kule Bsctime na wote mlikuwa msitari wa mbele aliposhindwa na wengi tulisema atashindwa kwa sababu ya matumizi yake mabaya.. including Mkapa mwenyewe. Leo hii mmesahau kabisa matumizi yao hata mnadiriki kusema kuwa JK alikuwa na njama against Sumaye!...damn..

Mkandara,
ninachoweza kukueleza ni kwamba safari za viongozi wakuu NCHI ZA NJE huandaliwa na kuratibiwa na wizara ya mambo ya nje. waziri wa mambo ya nje huomba fedha kugharimia safari hizo kutoka bungeni kupitia bajeti ya wizara ya mambo ya nje.

ikiwa kutatokea ubadhirifu katika matumizi ya fedha hizo, anayepaswa kuwajibika ni waziri mhusikia-- waziri wa mambo ya nje.

mimi nakubaliana na wewe kwamba kulikuwa na ufujaji wa fedha wakati sumaye aliposafiri marekani. ninachosema mimi ilikuwa ni makosa kumlaumu yeye peke yake, bila kumhusisha waziri mhusika, waziri wa mambo ya nje.

hata wabunge walipohoji kuhusu gharama za safari ile, hawakumhoji waziri mkuu, waliihoji wizara ya mambo ya nje. alikuwa ni dr.aldulshareef aliyesimama kujibu hoja ya wabunge. kama fedha hizo zingekuwa zimetoka bajeti ya waziri mkuu basi, naibu waziri wa mambo ya nje asingelazimika kuijibu hoja ile.

sasa,maadam waandishi tuliamua kumhoji sumaye kutokana na safari zile, basi sasa hivi tunapaswa pia kumhoji jk na el kuhusu gharama za hizi safari zao. huu uchungu wa matumizi ya fedha za serikali usichague mfujaji, wala kuangalia sura yake.
 
Back
Top Bottom