Huyu ndiye mbunge wa Morogoro mjini!

Huyu ndiye mbunge wa Morogoro mjini!

Wakazi wa moro wamemlipa fadhila kisa huwa anawasaidia misibani! ki ukweli huyu bwana hata yeye mwenyewe kujieleza hajui sijui kama atafanya lolote huko bungeni

Atatusaidia sana, mwe... Mjomba, huoni mwenzio katusadia mabasi ya kwenda kuzika... kila tukifiwa basi... kila tukifiwa basi, sasa we wataka tumtose, kha...

Haya ndiyo ya kupima mbunge?
 
Haya ndiyo ya kupima mbunge?

Hivi mkuu!Mbona unamshikia pumzi hivyo huyo Mmbunge? Mbunge gani unayemfahamu wewe hapa Tanzania ambaye anasifa hizo unazozitaja wewe? Hivi unaifahamu kweli barabara ya Mazimbu ilivyokuwa na jinsi ilivyopigwa kalenda na waliomtangulia? Hebu niambie huyo mbunge wa Tanzania mwenye sifa hizo unazozitaja? Kama lengo lako ni kutangaza nia Morogoro mjini bora useme tu tujue moja kuwa unafanya siasa za maji taka.
 
Huyu jamaa kwa kutumia fedha zake, nakumbuka alimshinda profesa Ishengoma ktk kuwania nafasi hii ya kugombea ubunge kwa tiketi ya ccm. Amejitahidi kwa kuajiri mshauri wake msomi ambaye huwa anamuelekeza mambo ya kufanya kila siku. Mbali na kutoa basi lake moja chakavu litumike kwenye misiba, pia Ofisi yake huwa inatoa mikopo kwa vikundi vya kina mama wajasiliamali (kina baba hataki kuwaona). Pia amefanikisha ujenzi wa daraja la mwere pamoja kusimamia ujenzi wa barabara za rami hapa manispaa ya moro, na mabasi yake kwa sasa yameacha kupata ajali kila mwezi desember. Hayo ndio mafanikio yake. ila kuongea mbele ya kadamnasi huwa hawezi, yani utamuonea huruma jinsi anavyoona aibu. Huyu ndio mbunge wetu wa moro mjini- mji uliojaa wasomi, vyuo luluki.
 
jamaa ananiachaga hoi ana basi maalumu la kwenda kuzikia watu msiba ukitokea tu gari linapelekwa ,sijawahi ona akitoa gari kumpeleka mgonjwa hosipitali ,ila kwenye msiba haraka, mpaka kunakamati maalumu ya mazishi
na hii amefanya kitambo kabla ya kuwazia ubunge nawasifu kwa hilo maana si yeye peke yake na mdogo wake lakini sina hakika kama wagonjwa hua anapata taarifa na kuuchuna lakini lakuzika nampa kudos
 
kuna tatizo kwa wapiga kura wa morogoro maana hata aliyekuwa mbunge awamu iliyopita alikuwa ni mzigo kwa wananchi kama huyu tu!
wananchi wakiogwa sabuni na kanga kwisha!
 
Hivi mkuu!Mbona unamshikia pumzi hivyo huyo Mmbunge? Mbunge gani unayemfahamu wewe hapa Tanzania ambaye anasifa hizo unazozitaja wewe? Hivi unaifahamu kweli barabara ya Mazimbu ilivyokuwa na jinsi ilivyopigwa kalenda na waliomtangulia? Hebu niambie huyo mbunge wa Tanzania mwenye sifa hizo unazozitaja? Kama lengo lako ni kutangaza nia Morogoro mjini bora useme tu tujue moja kuwa unafanya siasa za maji taka.

Kama wabunge wote wakiwa na pesa kama yeye na kuahidi vimiradi kuridhisha wananchi, nani atatunga sheria? Nani ataangalia vision ya nchi? Nani atakosoa mwenendo wa nchi pale ambapo una walakini?

CCM wametufikisha pabaya kwa kupotosha kazi za wabunge. Wabunge si wajenga madaraja. Wabunge ni wasimamizi wa kuhakikisha kodi inayolipwa na wananchi inawarudia na kuwatengenezea miundo mbinu ya maendeleo. Wabunge wanapaswa kutolea muda wao wote kufikiri masuala ya uelekeo wa nchi, kiuchumi, kielimu, afya, na sekta nyingine za uzalishaji.

Kama tukirudi kwenye masuala ya msingi ya mbunge na si kudanganyia watu kwa pipi kama watoto wadogo, tunahitaji wabunge wanaoweza kuelewa duniaa inavyoenda na kutafakari changamoto zetu ili kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo yetu.

Pia naomba nikwambie kuwa wabunge ni public figures, na ni lazima wafanyiwe tathmini: Angalia threads kama hizi.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/349724-mnyika-watchout-maji-ubungo-yatakuondoa.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/349724-mnyika-watchout-maji-ubungo-yatakuondoa.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/323991-kipindi-kigumu-jimboni-kawe.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-amshambulia-zitto-dhidi-ya-prof-muhongo.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/270031-is-zitto-kabwe-naive-or-a-dangerous-populist.html

Kama ni mwanasiasa au ni mshabiki wa mwanasiasa, haya ni mambo ya kawaida. Kuyakwepa ni kuamua kuacha siasa.

Leo ni thread ya Abood acha watu watajadili itapita. Na hii si Tanzania tu, pote penye demokrasia inafanyika hivyo.
 
tunataka maendeleo...hizo swagga za maji taka...mbona wasomi wengi tuu afu kuna madudu mengi tuu? njia ya choo isikauke...ala..
 
Lakini mbona tajiri? maprofesa wengi hawamfikii hata robo ya utajiri wake?!

Kipi kinampa mtu heshima, hela au uprof?
 
Hao wasomi wameipeleka wapi Tanzania kwa miaka 50? ndio kwanza tunaona Kikwete anaweka vitu sawa.
 
Kama wabunge wote wakiwa na pesa kama yeye na kuahidi vimiradi kuridhisha wananchi, nani atatunga sheria? Nani ataangalia vision ya nchi? Nani atakosoa mwenendo wa nchi pale ambapo una walakini?

CCM wametufikisha pabaya kwa kupotosha kazi za wabunge. Wabunge si wajenga madaraja. Wabunge ni wasimamizi wa kuhakikisha kodi inayolipwa na wananchi inawarudia na kuwatengenezea miundo mbinu ya maendeleo. Wabunge wanapaswa kutolea muda wao wote kufikiri masuala ya uelekeo wa nchi, kiuchumi, kielimu, afya, na sekta nyingine za uzalishaji.

Kama tukirudi kwenye masuala ya msingi ya mbunge na si kudanganyia watu kwa pipi kama watoto wadogo, tunahitaji wabunge wanaoweza kuelewa duniaa inavyoenda na kutafakari changamoto zetu ili kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo yetu.

Pia naomba nikwambie kuwa wabunge ni public figures, na ni lazima wafanyiwe tathmini: Angalia threads kama hizi.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/349724-mnyika-watchout-maji-ubungo-yatakuondoa.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/349724-mnyika-watchout-maji-ubungo-yatakuondoa.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/323991-kipindi-kigumu-jimboni-kawe.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-amshambulia-zitto-dhidi-ya-prof-muhongo.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/270031-is-zitto-kabwe-naive-or-a-dangerous-populist.html

Kama ni mwanasiasa au ni mshabiki wa mwanasiasa, haya ni mambo ya kawaida. Kuyakwepa ni kuamua kuacha siasa.

Leo ni thread ya Abood acha watu watajadili itapita. Na hii si Tanzania tu, pote penye demokrasia inafanyika hivyo.

Umeona ulivyoingia kingi mwenyewe sasa? Kumbe suala hili ni tatizo la ccm kuwafanya wabunge wote wa Tanzania kuwatumikia matatizo ya wananchi wao directly na siyo tatizo la mbunge wa Morogoro!Na ccm ndiyo imetufikisha hapo kwamba kupiga kelel bungeni kwa kurekebisha sheria mbalimbali na kutunga sheria tu huku jimboni kwako hakuna madaraja na barabara hazipitiki basi wananchi wanakuona huna faida na wanakupiga chini kwenye uchaguzi!
Sasa tu-conclude hivi kuwa kwa tanzania ya sasa ilipofikishwa hapa na CCM bila kuwatumikia wananchi directly kama Abood anavyofanya basi wananchi hawataona umuhimu wako.Basi kumbe Abood apongezwe kwa kujiweka karibu na wananchi sasa.
 
Sifa ya kuwa mbunge ni kusoma na kuandika
 
Mkuu naona hunielewi. Mie naongelea principles, hata kama hali halisi ya sasa imekataa principles hizo. Lengo pia si kumshambulia Abood, kwani hilo linalenga wabunge wote na ni sehemu ya elimu ya uraia. Inakuja kuwa majitaka pale ninapomshambulia mtu binafsi na si utendaji wake. Mfano kumkosoa kiongozi kuwa hafai kisiasa kwa kuwa hajafunga ndoa n.k hayo ndio majitaka.

Kwenye forum hii si vibaya kukumbushana kuwa mambo mengine tunayofanya kwa mazoea, hayapaswi kuwa hivyo hata kama tumezoea hivyo.

Kwenye mjadala mwingine nilishawahi kupost post hii:

Imekuwa jambo la kawaida kwa wananchi kuwaomba viongozi wao, hasa wabunge wawasaidie kugharamia miradi ya maendeleo. Mazoea haya yametufanya tusahau majukumu halisi ya wawakilishi wetu na pengine jukumu letu la kuwawajibisha pale wanapokwenda kinyume na wajibu wao.

Wabunge wamesahau majukumu yao ya msingi (legislative), badala yake wanajitwika majukumu ya serikali (excecutive). Hali hii pia inasababisha wananchi tusahau vigezo muhimu vya kuchagua viongozi na kutumbukia kwenye mkumbo wa kuchagua viongozi matajiri-ambao nao wanaitumia fursa hiyo vilivyo kuimarisha utajiri wao pamoja na kuulinda.

Ieleweke kuwa sio wajibu wa wabunge kulipia/kugharamia miradi ya maendeleo majimboni mwao. Wabunge wengi wamekuwa wakitoa ufadhili mbalimbali katika majimbo yao, na kusahau majukumu yao ya msingi ya kuwawakilisha wananchi na kuwasilisha mawazo yao Bungeni ili yapatiwe ufumbuzi na kuisimamia, kuishauri na kuikosoa serikali katika kutoa huduma za jamii na kufanya miradi ya maendeleo.

Aidha, mfuko wa jimbo ambao, wabunge wa upinzania na chama tawala, CCM walisahau tofauti zao na kuupitisha kwa kishindo umekuwa nao ukitumika kama mali ya mbunge na katika kutafuta wema kwa wapigakura, wamekuwa wakiahidi mambo kadhaa huku wakiacha kuwaweka wazi wapigakura. Mwishowe wananchi wanaamini hizo ni huruma za mbunge wao.

Hali hii hakika umetupeleka pabaya kwani umesababisha na unaendelea kusababisha yafuatayo:

Mosi, hali ya wabunge kulipia miradi ya maendeleo kunavuruga utaratibu wa mchakato mzima wa mipango ya maendeleo. Tunazo sera nzuri za kusaidia jamii kuibua miradi ya maendeleo na fursa za hiyo miradi kuweza kugharamiwa. Hivyo wabunge wanapochukua jukumu la kugharamia miradi hiyo, kunafanya wananchi wanakosa imani/hawaoni umuhimu wa kufuata mchakato uliwekwa kwa ajili ya kuwaletea maendeleo na badala yake wanatupia jukumu hilo kwa wabunge.

Pili, hali hii inapunguza uwajibikaji wa pande zote mbili hasa uwajibikaji wa wananchi. Mradi unaogharamiwa na wabunge, unakuwa mradi wa mbunge. Hivyo wananchi wanakosa umiliki wa miradi hii kitu ambacho kinafanya miradi hii isiwe endelevu, na zaidi isiwanufaishe wananchi kwa upana wake.

Wakati mbunge kwa upande wake anashindwa kutumia nafasi yake ya uwakilishi kwa kujenga hoja kwa lengo la kupata fedha kwa ajili ya kugharamia miradi ya wananchi. Hatima yake ni kwamba serikali haioni umuhimu wa kutenga fedha kwa ajili ya miradi ya wananchi kwani mbunge anazo hela na hataki ibainike kwamba serikali/wananchi wanaweza kuendeleza miradi yao wenyewe.

Pia, mwenendo huu wa wabunge husababisha migongano kwenye Serikali za Mitaa; hii hutokea pale panapokuwepo fedha ambazo tayari zimeshatengwa kwa ajili ya miradi husika, ambapo fedha hizo zinaweza kuishia mikononi mwa wajanja. Wajibu wa mbunge katika hili ni kuwahamasisha wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi hii na kusimamia matumizi ya fedha ya miradi hii.

Tatu, wabunge kugharamia miradi ya maendeleo inachochea hali ya utegemezi ndani ya jamii zetu. Serikali kupitia sera ya ugatuzi wa madaraka inalenga kuijengea jamii utamaduni wa kujitegemea kwa kuitaka jamii ishiriki moja kwa moja katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuchangia gharama. Sasa mbunge anapofadhili hii miradi, inafanya wananchi wajijengee utamaduni wa kusubiri kufanyiwa kila kitu. Na ndiyo hali ilivyo sasa kwani mara nyingi wenye fedha ni rahisi kupata madaraka.

Nne, wananchi wanajikuta wanapima viongozi wao kwa ufadhili waliotoa badala ya kutathmini utekelezaji wa majukumu yao kama wabunge. Hii inasababisha watu wasiokuwa na uwezo wa kifedha kukosa nafasi za uongozi hata kama wanao uwezo wa kuongoza vizuri. Hali imesababisha wananchi wengi kukosa uwakilishi na kuongezeka kwa matatizo makubwa ya uongozi mbovu, ufisadi, rusha na hali ngumu ya maisha huku wachache wakiendelea kunufaika na rasilimali za nchi hii.

Tano, wabunge wanaelemea katika kutafuta fedha za kugharamia miradi ya maendeleo badala ya kufanya majukumu yao ya msingi. Hii imesababisha wabunge kutoonekana majimboni kwa sababu inawabidi watafute mbinu mbalimbali za kupata fedha badala ya kutumia muda wao kutimiza majukumu yao ya msingi.

Badala ya kuwapigania wananchi ili kuwakwamua kutoka hali waliyonayo, wabunge wamejikuta wakipigania maslahi yao binafsi mfano wa sasa wa wanavyopambana kufa na kupona kuhalalisha kupanda kwa posho kwa madai ya kuwa wanatoa hela nyingi kwa wapiga kura kufadhili shughuli mbalimbali za maendeleo. Amenena mtu mmoja kuwa wanatumia fedha za walipa kodi kuwahonga wapiga kura.

Concern yangu ni hii:
1. Kama wabunge wakiacha kazi ya msingi ya kibunge, na kuvamia kazi za watu wengine, kazi za mbunge atafanya nani? Kazi hizi ni kutunga sheria na kusimamia serikali katika kutekeleza majukumu yake. Nchi yetu itakosa sheria makini, na uwajibishwaji wa watu wenye dhamana ya uongozi wa umma utazorota.
2. Kama kuwa na uwezo wa fedha ndio kigezo kikubwa cha kupata wawakilishi, tukubali kuhongwa, tukubali kukaribisha mafisadi wakubwa (Tumeshuhudia Rostam Aziz alivyokuwa ametufikisha pabaya). Tukubali kuzorotesha bunge letu.
3. Tukubali kila siku kuongeza mishahara na marupurupu ya wabunge ili waendelee kutupumbaza kwa kuturudishia asilimia ndogo ya kodi yetu wanayolipwa (asilimia kubwa wanabakia nayo wao). Na wanadai waongezewa kwa kisingizio hiki.
4. Tukubali miradi yenye fedha za serikali kuliwa na wajanja kwa kuwa hatimaye ni mbunge ndiye afisa miradi wa Jimbo.
5. Tukubali uholela utakaotufanya kila siku kufikiria project moja moja badala ya vision ya maendeleo endelevu.

Mchango wangu kwenye thread hii unaishia hapa, wenye kunielewa wamenielewa.
 
Uzuri wake ni mtu wa vitendo tu. Akiahidi kitu anatekeleza. Hao wenye CV nzuri wamefanya nini?
Watu wa mkoa wa Morogoro wanaendekeza sana njaa na ndio maana hupenda kuwachagua hao wahindi /waarabu wenye hela anzia kwa marehemu Gulamali,Aboud,huyo aliyekuwa/sijui kama bado yupo wa Turiani,wa Gairo na yule mama wa kihindi enzi hizo,hata Jamal nae alitokea Moro
 
Akiahidi nini?

Kwani jukumu la wabunge ni nini?

Kama wabunge wote wakiwa na pesa kama yeye na kuahidi vimiradi kuridhisha wananchi, nani atatunga sheria? Nani ataangalia vision ya nchi? Nani atakosoa mwenendo wa nchi pale ambapo una walakini?

CCM wametufikisha pabaya kwa kupotosha kazi za wabunge. Wabunge si wajenga madaraja. Wabunge ni wasimamizi wa kuhakikisha kodi inayolipwa na wananchi inawarudia na kuwatengenezea miundo mbinu ya maendeleo. Wabunge wanapaswa kutolea muda wao wote kufikiri masuala ya uelekeo wa nchi, kiuchumi, kielimu, afya, na sekta nyingine za uzalishaji.

Kama tukirudi kwenye masuala ya msingi ya mbunge na si kudanganyia watu kwa pipi kama watoto wadogo, tunahitaji wabunge wanaoweza kuelewa duniaa inavyoenda na kutafakari changamoto zetu ili kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo yetu.

Wabunge vihiyo na mafisadi ni janga kubwa la Taifa. Tuwakatae kwa kutowapigia kura.

Wewe hapa unaongea siasa tu na mambo ya kinadharia halafu unazunguka unarudi kule kule. Bunge hili la sasa hivi ndio lililo na madokta na maprofessa wengi kuliko mabunge yaliyopita. Hiyo vision unayoiongelea mbona hatuioni, hizo sheria za kutungwa mwaka huo huo na kurudishwa mwaka huo huo kwa ajili ya marekebisho ndo zimetawala (kumbuka sheria ya matumizi ya fedha katika uchaguzi, sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii). Tulitegemea bunge lenye watu wasomi hili lisotokee lakini ndo imekuwa afadhali ya kipindi cha nyuma. Nikirudi kwenye hoja ya Mbuge huyu, mdau aliyesema afadhali yeye anatenda hakumaanisha anatoa fedha zake kutenda, kumbuka pia kazi ya mbuge ni kuhamisisha maendeleo kwa kuhakikisha halmshauri na watendaji wanatumia rasilimali za wananchi kama inavyotakiwa. Morogoro, tulikuwa na Dr. Mzeru kipindi cha 2005 -2010, hakufanya chochote, hakuongea lolote ndani na nje ya bunge pamoja na sijui udokta wake. Iweje wewe, unaambiwa angalau huyu ameonyesha jitihada kuna miradi ya maji tumeona ameibana halmashauri imeanza, angalau kuna vijimaendeleo kidogo katika miundombinu ya barabara nk. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Mkuu naona hunielewi. Mie naongelea principles, hata kama hali halisi ya sasa imekataa principles hizo. Lengo pia si kumshambulia Abood, kwani hilo linalenga wabunge wote na ni sehemu ya elimu ya uraia. Inakuja kuwa majitaka pale ninapomshambulia mtu binafsi na si utendaji wake. Mfano kumkosoa kiongozi kuwa hafai kisiasa kwa kuwa hajafunga ndoa n.k hayo ndio majitaka.

Kwenye forum hii si vibaya kukumbushana kuwa mambo mengine tunayofanya kwa mazoea, hayapaswi kuwa hivyo hata kama tumezoea hivyo.

Kwenye mjadala mwingine nilishawahi kupost post hii:

Concern yangu ni hii:
1. Kama wabunge wakiacha kazi ya msingi ya kibunge, na kuvamia kazi za watu wengine, kazi za mbunge atafanya nani? Kazi hizi ni kutunga sheria na kusimamia serikali katika kutekeleza majukumu yake. Nchi yetu itakosa sheria makini, na uwajibishwaji wa watu wenye dhamana ya uongozi wa umma utazorota.
2. Kama kuwa na uwezo wa fedha ndio kigezo kikubwa cha kupata wawakilishi, tukubali kuhongwa, tukubali kukaribisha mafisadi wakubwa (Tumeshuhudia Rostam Aziz alivyokuwa ametufikisha pabaya). Tukubali kuzorotesha bunge letu.
3. Tukubali kila siku kuongeza mishahara na marupurupu ya wabunge ili waendelee kutupumbaza kwa kuturudishia asilimia ndogo ya kodi yetu wanayolipwa (asilimia kubwa wanabakia nayo wao). Na wanadai waongezewa kwa kisingizio hiki.
4. Tukubali miradi yenye fedha za serikali kuliwa na wajanja kwa kuwa hatimaye ni mbunge ndiye afisa miradi wa Jimbo.
5. Tukubali uholela utakaotufanya kila siku kufikiria project moja moja badala ya vision ya maendeleo endelevu.

Mchango wangu kwenye thread hii unaishia hapa, wenye kunielewa wamenielewa.

Mkuu sasa hivi umebadilika kimtazamo sasa,na hapo nipo sawa na wewe!Angalia post za kwanza zilivyokuwa za majitaka jinsi zilivyokuwa zinafanya personal attack kwa Abood na wewe hukuzi-criticize ndiyo maana nikadhani upo pamoja na hao wanaomtuhumu Abood kwa elimu yake na si kwa utendaji kazi wake!

My take: Kwadiasa za Tanzania zilipofikia hilo unalolitaka ni gumu sana kueleweka kwa wananchi! Mkoani kwetu Tabora tulikuwa na Mbunge machachari sana jimbo la Nzega Bwana Lucas Selelii,alikuwa mchangia hoja mzuri sana bungeni na alikuwa ni very active kwa kazi hizo ulizozitaja lakini wananzega walitaka kuona mabadiliko ya kimaisha yao ya moja kwa moja toka kwa mbunge wao na unajua kilichomkuta uchaguzi wa ndani wa ccm mwaka 2010. Kwahiyo Mkuu Mwanaukweli nakubaliana na mawazo yako kwa 100% lakini hayo yatabaki kinadharia tu na kamwe hayatekelezeki kwa tanzania ya sasa.
 
Achana na CV angalia utendaji wake kwenye jimbo lake, kuna Majimbo walichagua Maprof na MaDk lakini hawafanyi kitu majimboni mwao. Ubunge siyo kazi ya kusomea na wala mbunge siyo CEO au MD, Mbunge ni mtumishi wa watu na siyo lazima uwe na degree ndiyo utumikie wananchi wako, huyo jamaa ana resource za kuwasaidia wananchi wake kukabiliana na hali ngumu ya maisha.

Umeambiwa kuwasaidia wananchi wako lazima uwe mbunge?,
Ubunge lazima iwe zaidi ya kuaidi madaraja na madawati, hizo ni adaa kwa wananchi, ubunge lazima uweze kuisimamia na kukosoa serikali, kutunga sheria pia, ndio maana miswada ya kukandamiza wafanyakazi/wananchi inapita tu bungeni bila tabu kwasababu wabunge wengi ni vihiyo wala hawajishughulishi kuisoma.
Tunatakiwa tutambue mbunge siyo mjenga madaraja, wala shule hiyo ni kazi ya serikali, yeye hasimamie hizo shughuli kufanywa na serikali
 
Uzuri wake ni mtu wa vitendo tu. Akiahidi kitu anatekeleza. Hao wenye CV nzuri wamefanya nini?

Hili ndilo raia tunalitaka. Mtu atekeleze anayoahidi. Wasomi km kina DR JK wanaifanya nn nchi?
Watu wa moro wananufaika na ubunge wak kuliko mbunge mwingine yeyote waliewah kua nae.
 
Back
Top Bottom