Mwandishi wa thread hii anaonyesha madhaifu makubwa sana. kwanza aidha ni mjinga wa historia au ni mdini au ana chuki zake na Azizi Abood.
ukiwa ni mtaalamu wa historia huhitaji kufahamu kuwa wakoloni wa awali east africa walikuwa wareno ambao walitutawala baina ya karne ya 14 mpaka ya 16 kabla ya wareno hawa kufurushwa na waarabu. lakini je waarabu pekee ndio walihusika na biashara ya utumwa? jibu si kweli, wareno walihusika kwa kiwango kikubwa na utumwa ule wa trans-atlantic trade, vilevile kumbuka waarabu hawa walikuwa wakinunua watumwa kutoka kwa viongozi wa kiafrika ambao leo hii sisi huwa tunawaita mashujaa, je wafahamu kuwa mirambo alihusika sana na biashara ya utumwa?
Alikuwa mwarabu huyu? Biashara ya utumwa inaonekana katika biblia ambayo ninyi mwaona kuwa ni kiongozo chenu, yusufu aliuzwa na nduguze huko mosri vipi hawa nduguze walikuwa waarabu? Ibrahimu hakumiliki watumwa? mbona biblia tena agano jipya waefeso 6:5 inatetea utumwa?je wakristo hawa na huyu paulo ni mwarabu?basi twaweza semawaarabu hawa walikuwa wakinunua watumwa kuwapelekea wakristo walioruhusiwa kumiliki watumwa
lakini kwa kuwa hayo yote ni upuuzi sikupata kufikiria kuwa wananchi wa mpanda kati waliomchagua said amour arfi wa chadema awe mbunge wao kumbe walikuwa wajinga sana. vipi kuhusu yule gulam wa nccr aliyekuwa mbunge kule kigoma alichaguliwa na majuha?vilevile halmashauri kuu yote ya chadema iliyomchgua said amour arfi awe makamu wa chama hicho ni wajinga na majuha makubwa? vipi wananchi kutoka wilaya zinazosadikiwa kuwa ndizo zenye wasomi kuliko wote tanzania(vigezo?) za ilala , kinondoni na kawe zilizopata kuwachagua adamjee, mussa azzan na idd azzan ,je wananchi hawa ni wajinga ? mifano inaendelea na kuendelea
Muhimu tuweke ubaguzi kando, ila tuweke utanzania mbele, nani aliyekwambia kuwa watu weusi ndio wana upendo zaidi kwetu?huyu chenge anayelalamikiwa ni mwarabu?vipi lowasa, mramba , mkapa, anna mkapa, na mafisadi kadha wa kadha wenye rangi nyeusi na majina ya kikristo unayoyajua hawa wote ni waarabu? it is very pathetic kuona mtu anakaa kwenye kompyuta na kuanza kuandika threads zenye mwelekeo wa kibaguzi halafu anajiita yeye ana roho njema moyoni
I'm very dissapointed with the thread writer lakini siwezi kumlaumu ni upeo finyu alionao ndio unaomsababishia kuandika up[uzi huu