Huyu kaka jamani~~~ Nimjibuje mie!

Huyu kaka jamani~~~ Nimjibuje mie!

Wewe huwajui watu wafupi kwa kupenda sifa. Nikimkubali si atataka kila mahali tuandamane kama kumbikumbi!

kwa vile umesema ana heshima ukimwambia una mtu hatarudia tena,ufupi si tija atapata ambaye hataona huo ufupi.
 
Nenda pika mie, nikirudi nitajibu hoja zenu. Naomba mniwie radhi kwa kutoweka kwa muda, leo ni zamu yangu kupika
 
Kwa sifa ulizompa, anaonekana ana hekima na uungwana. Atakushukuru manake hatahangaisha moyo wake kupenda waschana wasiokuwa wa level yako. Afu si wajua siku hizi wanasema m'baya wako muombee njaa, atataka kuwa karibu na wewe akuone utakapoangukia lau akupe tabasamu ukishatendwa na a tall handsome man.
Nashukuru Mungu kakazake AshaDii wote warefu manake Zinduna angetuchekaje?
 
katika jambo ambalo linahitaji uamuzi wako binafsi...maana ni kiu ya nafsi ni MAPENZI!!! ....
 
Utasutwa wewe!!! Sasa kipi kikuchekeshacho wakati klorokwini wangu ni mrefu kama Hashim Thabiti?

mi nnavyopenda vijanaume vifupi! Ngoja nimwambie zinduna anipigie pande. Kloro mfupi kama panadol.
 
Zamu unapangiana na nani? Afu wanaume wafupi wanatoaga ushirikiano kweli, mngekuwa mnapika wote maskini,kha!
Nenda pika mie, nikirudi nitajibu hoja zenu. Naomba mniwie radhi kwa kutoweka kwa muda, leo ni zamu yangu kupika
 
Utasutwa wewe!!! Sasa kipi kikuchekeshacho wakati klorokwini wangu ni mrefu kama Hashim Thabiti?

Yawaje badala ya kutoa ushauri wa namna ya kumjibu mtu mfupi, waishia tu kujipigia promo!

Hujambo dada, nakusalimu huko ulipo.
 
Zamu unapangiana na nani? Afu wanaume wafupi wanatoaga ushirikiano kweli, mngekuwa mnapika wote maskini,kha!


Tupo wadada wanne na waume watatu katika familia ya mama na baba Zinduna. Mie na dada zangu watatu twapeana zamu kupika
 
Yawaje badala ya kutoa ushauri wa namna ya kumjibu mtu mfupi, waishia tu kujipigia promo!

Hujambo dada, nakusalimu huko ulipo.
Jaman Zinduna mie si nimeshakushauri? Mie mzima kabisa.
 
Mpe lile jibu linalotuvunja moyo wanaume wengi - Muambie na "mimi nakupenda lakini kama rafiki".

Au ikiwa unataka kumweka akiba kwa siku za mbele (just in case), mwambie umetoka kwenye uhusiano karibuni n ahuko tayari kuanzisha mwengine kwa sasa, lakini kama iko siku utakuwa uko tayari, mwambie yeye atakuwa wa mwanzo kumwarifu.

Katika hali zote mbili hatokuwa akikufata fata "kimapenzi."
 
Leo naomba kueleza lililo moyoni mwangu, wallahi sitanii, maana najua hapa watu watakuja na vijineno vya kukatisha tamaa~~~~Mabibi na Mabwana naomba saaana jambo hili msilifanyie dhihaka.

Ni hivi, kuna kijana mmoja kahamia huku visiwani Zenji mwaka jana mwishoni. Huyu kijana anaishi mtaa wa pili kutoka hapa nyumbani. Mara nyingi akienda kupunga upepo ufukweni huwa anapita hapa kwetu na hapiti bila kutusalimu, kwani kijana mwenyewe ana heshima kweli na aonekana kuwa amefunzwa huko kwao. Hivi karibuni nilipokuwa huko Dar, kula mwaka mpya alikumpa rafiki yangu kadi aniletee ya kunitakia heri ya mwaka mpya na niporudi na kupewa kadi hiyo nilimpa ahsante wakati anapita hapa kwetu. alifurahi sana.

Sasa juzi nimekutana naye Hoteli moja ya ufukweni nikiwa na dada yangu na tulipata wasaa wa kuzungumza kidogo na hapo ndipo aliposema yaliyo moyoni mwake kuwa ananipenda na angependa tuwe wapenzi. Nimemwahidi nitamjibu. Kusema ukweli ni kijana mzuri kwa sura na nimtanashati hasa na mwenye heshma kwa wakubwa na wadogo. Lakini kuna tatizo. Tatizo lenyewe ni kwamba, huyu bwana ni mfupi mno, yaani tukisimama ananifika kiunoni (Mie ni mwembamba na mrefu kiasi)~~~~~ Mwenzenu mie na wanaume wafupi~~~ akha! Hilo kwa kweli limeniwia gumu kukubali ombi lake, maana hata kutembea naye barabarani mwenzenu sitaweza.....

Sasa naomba msaada mwenzenu, nitumie msamiati gani kumkatalia, maana sipendi nimuumize moyo wake.

Umri wote huo! Wataka kusema hujawahi kataa mtu weye! Woote wawaonea huruma? Acha masihara bwana
 
swahiba nakusalimia. Ukimuona mkwe wangu mwambie ile mikufu ya tanzanite aliyoniagiza ishafika.
Swahiba mie bukheri... Mamkwe wako mpigie mwenyewe bana manake mimi na yeye toka mwaka uanze twapishana sana, hebu fikiria tumeolewa nyumba moja ila hatukutani hata kwenye korido...
 
Haya mambo tumefanyiwa sana kwenye girls hostels.....Nasikia kuna wakati hata kura zilikuwa zinapigwa...

Ngoja tuchukulie kwamba hili bweni moja wapo na tunampa ushauri Da Zindu,

Mie nakushauri umkubali mwaya.....Nahisi atakuwa baba mzuri wa watoto wako.....Hiyo ndiyo kura yangu...Yeees (tena kwa sauti kubwa)!!

Wee waonaje Zindu??

Babu DC!!
 
Usimuharibie mwanangu soko bibie! Manake urefu anamkaribia Hasheem Thabit, ukome kabisaa! Mi nimekuagiza kope na lace wig unaniletea tanzanite wakati diamonds nimetupa stoo!
mi nnavyopenda vijanaume vifupi! Ngoja nimwambie zinduna anipigie pande. Kloro mfupi kama panadol.
 
Raha ya uke wenza ukipika biryani waweka kapuni unamopelekea mwenzio. Sasa wewe mke mwenza mwaka huu wote hata kunikaribisha! Basi naanza mie, kesho karibu ntakupikia dagaa wa zenj, ugali wa nazi na tembele la ndimu.
Swahiba mie bukheri... Mamkwe wako mpigie mwenyewe bana manake mimi na yeye toka mwaka uanze twapishana sana, hebu fikiria tumeolewa nyumba moja ila hatukutani hata kwenye korido...
 
Back
Top Bottom