Tahadhari: Huyu ni tapeli wa Kujiaminisha?

Sep 1, 2011
45
60
Naomba nikiri hoja yangu imelenga kuleta hoja vijana wajitume na sio kuwa ombaomba ilihali wana nguvu.
REC20240310-214047-774-A.00_01_08_10.Still008.jpg

Mwaka 2023 mwezi wa 5 nikiwa natembea maeneo ya Ubungo jirani na NBC bank alikuja kijana ambaye anaonekana kwenye video hapa na akaniambia yeye ni mwalimu amemaliza SUA na amepata kazi Songwe hivyo anaomba nimuongezee nauli ili aweze kufika. Alinifuata kwa nidhamu na kwa namna alivyokuwa akiongea (Angalia hata hii video hapa anavyojieleza kwa ustadi) niliamini kweli ni mtu mwenye elimu yake na pengine kweli hana kazi ndio amepata. Nikaona si vibaya nikijigeuza kuwa malaika wa zamu kwake ili afanikishe safari ya kwenda Songwe alipodai amepata kazi. Nikamuuliza nauli akanitajia na na akasema aka niasi kidogo kama elfu 10, nikampa, Sikumbuki ni kiasi gani ila kama sio kwenye 40,000 maana nilihakikisha nampa nauli ya kumfikisha. Akanishukuru sana akanipa na namba yake but sikuiSave kiukweli (Good enough alikuwa na smartphone)

Tarehe 10 Machi, Mwaka 2024 nikiwa kwenye gari nimetoka Mazimbu naenda mjini, nimefika na kusimama sehemu ya mataa, Mtu yuleyule niliyemsaidia nauli ya kwenda Songwe kwenye kazi, nimekutana nae tena na akagonga kioo na kuomba nisimame mbele baada ya mataa. Mawazo yangu nikajua pengine ameniona na amenikumbuka anataka kunishukuru kwa msaada niliowahi kumpa, Baada ya kuvuka mataa na kusimama kumsikiliza pengine anashukuru kwa msaada wa awali, nikashangaa analeta maombi ya aina ileile.

Bahati mbaya baada ya kumwambia siku nyingine aliondoka na wakat namuita ili nimkumbushe akawa ameondoka hakutaka hata kusikiliza. Wakati namtafakari hasa kuwaza umbali wa kutoka relini ambako amedai aliponiona ndio amenikimbilia, nikakumbuka kuwa Dashboard camera yangu ilikuwa on nikataka kuprove kweli aliniona tangu relini? nikaendelea kujiridhisha kuwa ni Muongo.

Baada ya kutembea takriban Mita 400 kutoka relini, (sehemu ambayo yeye alisema ndipo aliniona na kunikimbilia) ndipo alionekana akitembea kuelekea uelekeo ambao nilikuwa nakwenda kupitia camera ya mbele. Nilipofika usawa wake mbele kidogo ndipo alionekana kuangalia gari kupitia camera ya kulia. ndipo akaamua kuja na kuvuka upande wa abiria kama anavyoonekana kupitia camera ya nyuma. na hatimaye maelezo yake ni kama anavyoonekana kupitia camera ya kushoto japo hajaonekana vizuri.

Tujihadhari na huyu mtu ni wazi atakuwa ndio mchezo wake kujipatia pesa kwa udanganyifu na pengine kafanya hivyo mikoa mingi.

Tazama Video nilipokutana nae Morogoro

View: https://youtu.be/sd2-OcpDkv0

UPDATE ZA ZA WADAU WENGINE WALIOKUTANA NA HUYU BWANA:
Kwa jina alijitanabaisha kuwa anaitwa Joseph krisant kwangu .
Kwangu alibadili story kutoka kwako akidai yeye ana familia maeneo ya Boko na hapo awali amesimamishwa kazi ya ualimu kwa mambo yaliyotukia hapo kazini kwake .

Sasa lengo lake kwangu ilikuwa nini kuwa kama kuna kibarua nimsaidie ila pia kama nitaweza nimsaidie walau hela ya kusogeza siku yeye na familia yake .

Imani iliniingia alipogusa neno familia , nikampa 15,000 yangu na akaendelea na safari zake na mimi nikaendelea na maisha yangu .

Siku moja nikiwa mjini kati , rafiki yangu wa Mburahati kanikaribisha walau tupate maji baada ya kipindi kirefu mimi kuukimbia mji , huko nakutana na bwana huyu akiwa mtaani anakula soga na wana wa mtaani hapo .

Sikutaka anikumbuke maana nilijihisi kukumbusha nilivyomsaidia kama nitampa fedhea kwa wale mabrazamen aliokuwa nao .

Hatua mbili mbele niko kwa mwenyeji wangu ila huku na kule nikampa kisa cha rafiki yangu huyu niliyemsaidia , kicheko cha mwenyeji wangu kinanitoa katika wimbi la huruma mpaka hasira pale anapohitimisha kicheko chake kwa kusema huyu alikudanganya ni mtoto wa hapa mtaani ila utapeli utapeli ndiyo kazi yake .🤔

Hivyo ndugu pole kwa yote lakini popote ulipo ukiwa na uwezo wowote waza kumuinua japo kijana mmoja kwa kufanya hivi tutawapunguza omba omba na matapeli njaa .

Jioni njema.

Aisee huyu jamaa nilikutana nae Mbezi Beach pale Massana nimetoka tu kwenye ATM za CRDB pale naingia kwenye gari akaja kunigongea kioo na ongea yake hiyo hiyo ya kuchanganya lugha... Akaniomba pesa sijui familia haijala na maneno mengi sana... Baada ya kumwambia siku nyingine alikasirika na kuondoka chap...

Utashangaa kusikia huyo jamaa nimekumbana naye Dar, Morogoro na Mbeya. Mbeya nami nikiwa napita kama mgeni, nikiwa nimepaki gari pembeni ya barabara, huku mwenyeji wangu kaniachia usukani, (mwenyeji aliingia ofisi za ardhi) mara paapu, akatokea huyo jamaa (anachagua watu). Akajifanya alikuwa anafanya kazi kama intern ofisi za ardhi Mbeya kipindi cha Lukuvi. Akasema hawajalipwa bado pesa za miezi kadhaa, hivyo anaomba msaada aisitiri familia yake. Nikasema bwana mimi miguu hata haijapoa moto na ndio nimefika tu Mbeya kwa mtu, kawaombe wenyeji wenye pesa. Aliniharibia siku. Dar vuupu, karibu na Mlimani City, story zilezile, mara mji kasoro bahari akajihusisha na SUA kusoma Master. Nikamwambia shida ukiwa tapeli unahitaji usiwe unasahau, ukisahau utakuja kukamatwa. Nilidhani Afro zangu au rangi yangu ni rahisi kunikumbuka na kunikwepa. Nikamwambia utakufa maskini.

Huyo mjamaa ukisema huna pesa, au ukashtuka, atakufanya nafsi yako ijutie. Utajiona kama shetani, kumbe yeye ni tapeli kubwa. Wako wengi matapeli wa namna hiyo.

Namjua, aliwahi niomba nauli hivyohivyo akiwa maeneo ya Shekilango mabus yanapopaki. Jamaa anajua kupanga maneno mno. Nilimpa 10,000 hakuridhika nikawasha gari nikaondoka

Huyu jamaa nilikutana naye mwaka jana Lake Oil petrol station pale Tabata njia panda ya kwenda Segerea/Kimanga. Akanipa story hiyohiyo ya kuwa ni mwl alitumbuliwa na sasa kapata kazi na anatakiwa kuripoti kazini siku inayofuata.

Muda huo nilikuwa nimetoka kujaza mafuta kwenye gari. Ilikuwa saa 1 jioni. Akaomba elfu 40 aweze kuungaunga apande gari za IT asubuhi aweze kuripoti kazini. Nilimpa elfu 10 ila ndio huyuhuyu na story yake ni hiyohiyo.

Daaah, hawa ndo wanasababisha watu waishi kama wanyama....

Kwa huruma na ubinadamu, nilimtumia kiasi cha pesa kwenye simu, apate nauli ya kwenda Songwe, kula njiani na kumtumia mama watoto wake kwa ajili ya chakula cha jioni hiyo.

Alinifuata nikiingia kwenye ka-mini supermarket pale Goba, nikipanga ninunue vilevi nikaburudike, nika ahirisha ili kutoa msaada!

Pumbavu sana!

Na mimi namkumbuka vizuri sana. Nilikutana nae mwaka jana Mbezi, Dar maeneo ya jirani na Magufuli bus terminal. Alinisimamisha na kunipa mkono wa salaam ambao mimi sikuupokea nikijifanya kupiga chafya ya ghafla maana uwa sina kawaida ya kushikana mikono na mtu nisiyemfahamu. Akaanza kunieleza kuwa ni mmoja wa watumishi wa serikali waliotumbuliwa kwa vyeti feki na sasa anatafuta nauli elfu 30 akapande magari ya IT ili awahi kazi aliyoitiwa Songwe. Uongeaji wake ndiyo huo huo wa kuchanganya lugha ya kiswahili na kiingereza maana alishajua akikutana na watu wa aina fulani akitumia mbinu hiyo ya kuchanganya lugha atawafanya kumwamini na kumsaidia. Mimi pamoja na kumsikiliza nilimshitukia na hivyo nikamwambia hapa nilipo nami sina kitu. Ajabu baada ya kumwambia vile alisonya na kuondoka kwa hasira. Wakati anaondoka kwa staili ile nilimpazia sauti na kumwambia "Oya wewe vipi? Nimekusikiliza shida yako nami nimekwambia sina hela halafu unanisonya?! Huna lolote wewe ni msanii tu na hapa kwangu umekwama". Yeye akaendelea kwenda na hasira zake. Kiukweli baada ya kuwa ameondoka baadae mimi moyoni nilibaki najilaumu kwa kumwambia maneno yale ya kumsindikizia maana pengine kweli alikuwa na shida na siyo kwamba alikuwa akifanya utapeli. Sasa kwa kumwona kwenye video hii na kwa kusoma shuhuda za wadau nimejipongeza kwa kutokupoteza hela yangu kwa tapeli maana kiukweli hela ya kumpa nilikuwa nayo mfukoni.
 
Watu kama hawa ukitaka kiwakomoa wapeleke stand uwalipie nauli umpe tiketi. Kama muda upo hakikisha anapanda bus na kuondoka. Ukigundua ni Tapeli, Piga picha tuma hata polisi waendelee na majukumu ya kunyoosha taifa.

Tusiache kutenda mema, maana wengine kwa kufanya hivi wamewasaidia na malaika -Biblia
 
Kwa jina alijitanabaisha kuwa anaitwa Joseph krisant kwangu .
Kwangu alibadili story kutoka kwako akidai yeye ana familia maeneo ya Boko na hapo awali amesimamishwa kazi ya ualimu kwa mambo yaliyotukia hapo kazini kwake .

Sasa lengo lake kwangu ilikuwa nini kuwa kama kuna kibarua nimsaidie ila pia kama nitaweza nimsaidie walau hela ya kusogeza siku yeye na familia yake .

Imani iliniingia alipogusa neno familia , nikampa 15,000 yangu na akaendelea na safari zake na mimi nikaendelea na maisha yangu .

Siku moja nikiwa mjini kati , rafiki yangu wa Mburahati kanikaribisha walau tupate maji baada ya kipindi kirefu mimi kuukimbia mji , huko nakutana na bwana huyu akiwa mtaani anakula soga na wana wa mtaani hapo .

Sikutaka anikumbuke maana nilijihisi kukumbusha nilivyomsaidia kama nitampa fedhea kwa wale mabrazamen aliokuwa nao .

Hatua mbili mbele niko kwa mwenyeji wangu ila huku na kule nikampa kisa cha rafiki yangu huyu niliyemsaidia , kicheko cha mwenyeji wangu kinanitoa katika wimbi la huruma mpaka hasira pale anapohitimisha kicheko chake kwa kusema huyu alikudanganya ni mtoto wa hapa mtaani ila utapeli utapeli ndiyo kazi yake .🤔

Hivyo ndugu pole kwa yote lakini popote ulipo ukiwa na uwezo wowote waza kumuinua japo kijana mmoja kwa kufanya hivi tutawapunguza omba omba na matapeli njaa .

Jioni njema.
 
Watu kama hawa ukitaka kiwakomoa wapeleke stand uwalipie nauli umpe tiketi. Kama muda upo hakikisha anapanda bus na kuondoka. Ukigundua ni Tapeli, Piga picha tuma hata polisi waendelee na majukumu ya kunyoosha taifa.

Tusiache kutenda mema, maana wengine kwa kufanya hivi wamewasaidia na malaika -Biblia
Hapo umewakomoa ? Vipi gharama ya muda wako ?
 
Naomba nikiri hoja yangu imelenga kuleta hoja vijana wajitume na sio kuwa ombaomba ilihali wana nguvu.
View attachment 2933415

Mwaka 2023 mwezi wa 5 nikiwa natembea maeneo ya Ubungo jirani na NBC bank alikuja kijana ambaye anaonekana kwenye video hapa na akaniambia yeye ni mwalimu amemaliza SUA na amepata kazi Songwe hivyo anaomba nimuongezee nauli ili aweze kufika. Alinifuata kwa nidhamu na kwa namna alivyokuwa akiongea (Angalia hata hii video hapa anavyojieleza kwa ustadi) niliamini kweli ni mtu mwenye elimu yake na pengine kweli hana kazi ndio amepata. Nikaona si vibaya nikijigeuza kuwa malaika wa zamu kwake ili afanikishe safari ya kwenda Songwe alipodai amepata kazi. Nikamuuliza nauli akanitajia na na akasema aka niasi kidogo kama elfu 10, nikampa, Sikumbuki ni kiasi gani ila kama sio kwenye 40,000 maana nilihakikisha nampa nauli ya kumfikisha. Akanishukuru sana akanipa na namba yake but sikuiSave kiukweli (Good enough alikuwa na smartphone)

Tarehe 10 Machi, Mwaka 2024 nikiwa kwenye gari nimetoka Mazimbu naenda mjini, nimefika na kusimama sehemu ya mataa, Mtu yuleyule niliyemsaidia nauli ya kwenda Songwe kwenye kazi, nimekutana nae tena na akagonga kioo na kuomba nisimame mbele baada ya mataa. Mawazo yangu nikajua pengine ameniona na amenikumbuka anataka kunishukuru kwa msaada niliowahi kumpa, Baada ya kuvuka mataa na kusimama kumsikiliza pengine anashukuru kwa msaada wa awali, nikashangaa analeta maombi ya aina ileile.

Bahati mbaya baada ya kumwambia siku nyingine aliondoka na wakat namuita ili nimkumbushe akawa ameondoka hakutaka hata kusikiliza. Wakati namtafakari hasa kuwaza umbali wa kutoka relini ambako amedai aliponiona ndio amenikimbilia, nikakumbuka kuwa Dashboard camera yangu ilikuwa on nikataka kuprove kweli aliniona tangu relini? nikaendelea kujiridhisha kuwa ni Muongo.

Baada ya kutembea takriban Mita 400 kutoka relini, (sehemu ambayo yeye alisema ndipo aliniona na kunikimbilia) ndipo alionekana akitembea kuelekea uelekeo ambao nilikuwa nakwenda kupitia camera ya mbele. Nilipofika usawa wake mbele kidogo ndipo alionekana kuangalia gari kupitia camera ya kulia. ndipo akaamua kuja na kuvuka upande wa abiria kama anavyoonekana kupitia camera ya nyuma. na hatimaye maelezo yake ni kama anavyoonekana kupitia camera ya kushoto japo hajaonekana vizuri.

Tujihadhari na huyu mtu ni wazi atakuwa ndio mchezo wake kujipatia pesa kwa udanganyifu na pengine kafanya hivyo mikoa mingi.

Tazama Video

View: https://youtu.be/sd2-OcpDkv0

Polisi wangekuwa wanafanya kazi kama hivi hii nchi ingekuwa ulaya isee..
 
Nakumbuka siku moja Buguruni sheli dogo wa shule ya msingi alinifuata akaniambia anakaa G/mboto hana nauli nikampà jero baadae nikiwa bado niko hapo stendi nikamuona anaongea na mtu fulani nikamsogelea kimya kimya kumsikiliza anamwambia nini yule mtu nilikuwa nimeshahisi anampiga sound yule mtu na kweli nilimsogelea nikamsikia anadai Hela ya nauli nilimtimua yule dogo pale stendi.Mitapeli ya dizaini hii ipo mingi
 
Naomba nikiri hoja yangu imelenga kuleta hoja vijana wajitume na sio kuwa ombaomba ilihali wana nguvu.
View attachment 2933415

Mwaka 2023 mwezi wa 5 nikiwa natembea maeneo ya Ubungo jirani na NBC bank alikuja kijana ambaye anaonekana kwenye video hapa na akaniambia yeye ni mwalimu amemaliza SUA na amepata kazi Songwe hivyo anaomba nimuongezee nauli ili aweze kufika. Alinifuata kwa nidhamu na kwa namna alivyokuwa akiongea (Angalia hata hii video hapa anavyojieleza kwa ustadi) niliamini kweli ni mtu mwenye elimu yake na pengine kweli hana kazi ndio amepata. Nikaona si vibaya nikijigeuza kuwa malaika wa zamu kwake ili afanikishe safari ya kwenda Songwe alipodai amepata kazi. Nikamuuliza nauli akanitajia na na akasema aka niasi kidogo kama elfu 10, nikampa, Sikumbuki ni kiasi gani ila kama sio kwenye 40,000 maana nilihakikisha nampa nauli ya kumfikisha. Akanishukuru sana akanipa na namba yake but sikuiSave kiukweli (Good enough alikuwa na smartphone)

Tarehe 10 Machi, Mwaka 2024 nikiwa kwenye gari nimetoka Mazimbu naenda mjini, nimefika na kusimama sehemu ya mataa, Mtu yuleyule niliyemsaidia nauli ya kwenda Songwe kwenye kazi, nimekutana nae tena na akagonga kioo na kuomba nisimame mbele baada ya mataa. Mawazo yangu nikajua pengine ameniona na amenikumbuka anataka kunishukuru kwa msaada niliowahi kumpa, Baada ya kuvuka mataa na kusimama kumsikiliza pengine anashukuru kwa msaada wa awali, nikashangaa analeta maombi ya aina ileile.

Bahati mbaya baada ya kumwambia siku nyingine aliondoka na wakat namuita ili nimkumbushe akawa ameondoka hakutaka hata kusikiliza. Wakati namtafakari hasa kuwaza umbali wa kutoka relini ambako amedai aliponiona ndio amenikimbilia, nikakumbuka kuwa Dashboard camera yangu ilikuwa on nikataka kuprove kweli aliniona tangu relini? nikaendelea kujiridhisha kuwa ni Muongo.

Baada ya kutembea takriban Mita 400 kutoka relini, (sehemu ambayo yeye alisema ndipo aliniona na kunikimbilia) ndipo alionekana akitembea kuelekea uelekeo ambao nilikuwa nakwenda kupitia camera ya mbele. Nilipofika usawa wake mbele kidogo ndipo alionekana kuangalia gari kupitia camera ya kulia. ndipo akaamua kuja na kuvuka upande wa abiria kama anavyoonekana kupitia camera ya nyuma. na hatimaye maelezo yake ni kama anavyoonekana kupitia camera ya kushoto japo hajaonekana vizuri.

Tujihadhari na huyu mtu ni wazi atakuwa ndio mchezo wake kujipatia pesa kwa udanganyifu na pengine kafanya hivyo mikoa mingi.

Tazama Video

View: https://youtu.be/sd2-OcpDkv0

Polee mkuu
Mimi nilishaachaga kuwasikiliza watu aina hiyo..

Mie mwenyewe nikiwa katikati ya mji kisha nikala nauli huwa natembea mpaka Gongo la Mboto siombi nauli
 
Hapo umewakomoa ? Vipi gharama ya muda wako ?
Hapo ni kama nimeamua kulipia hiyo gharama ya muda. Niliwahi kujaribu hivyo kwa jamaa aliyekuwa anashida ya chakula, nilipompleleka cafe ili ale alinigomea kabisa, akasema yeye anasehemu yake huwa anakula kwa bei rahisi Ukoko.

Kama uwezekano upo toa huduma usitoe pesa. Hii ndio kanuni nilijifunza kwa yule msamalia mwema wa kwenye Boblia. Alitoa huduma huku akizingatia na muda na ratiba yake huko alikokuwa anaenda (Yeriko)
 
Jamaa anaonekana smart kichwani, angetuliza kichwa chake naamini angeweza jipatia kipato kihalali.

Tone ilibadilika ghafla kutoka muungwana mpaka kwenda kibabe ghafla baada ya kumwambia siku nyingine; naamini ndipo pia alikukumbuka kuwa alishawahi kuvuna toka kwako.

Kweli mjini mipango😂
 
Aisee huyu jamaa nilikutana nae Mbezi Beach pale Massana nimetoka tu kwenye ATM za CRDB pale naingia kwenye gari akaja kunigongea kioo na ongea yake hiyo hiyo ya kuchanganya lugha... Akaniomba pesa sijui familia haijala na maneno mengi sana... Baada ya kumwambia siku nyingine alikasirika na kuondoka chap...
 
Kwa jina alijitanabaisha kuwa anaitwa Joseph krisant kwangu .
Kwangu alibadili story kutoka kwako akidai yeye ana familia maeneo ya Boko na hapo awali amesimamishwa kazi ya ualimu kwa mambo yaliyotukia hapo kazini kwake .

Sasa lengo lake kwangu ilikuwa nini kuwa kama kuna kibarua nimsaidie ila pia kama nitaweza nimsaidie walau hela ya kusogeza siku yeye na familia yake .

Imani iliniingia alipogusa neno familia , nikampa 15,000 yangu na akaendelea na safari zake na mimi nikaendelea na maisha yangu .

Siku moja nikiwa mjini kati , rafiki yangu wa Mburahati kanikaribisha walau tupate maji baada ya kipindi kirefu mimi kuukimbia mji , huko nakutana na bwana huyu akiwa mtaani anakula soga na wana wa mtaani hapo .

Sikutaka anikumbuke maana nilijihisi kukumbusha nilivyomsaidia kama nitampa fedhea kwa wale mabrazamen aliokuwa nao .

Hatua mbili mbele niko kwa mwenyeji wangu ila huku na kule nikampa kisa cha rafiki yangu huyu niliyemsaidia , kicheko cha mwenyeji wangu kinanitoa katika wimbi la huruma mpaka hasira pale anapohitimisha kicheko chake kwa kusema huyu alikudanganya ni mtoto wa hapa mtaani ila utapeli utapeli ndiyo kazi yake .🤔

Hivyo ndugu pole kwa yote lakini popote ulipo ukiwa na uwezo wowote waza kumuinua japo kijana mmoja kwa kufanya hivi tutawapunguza omba omba na matapeli njaa .

Jioni njema.
Hii story ndio alinipa na mimi maeneo ya mbezi beach
 
Mwili mkubwa, wanang'ang'ania mjini bila mishe, Pale maeneo ya Upanga laribu kona ya Muhimbili, napo kulikuwa na jamaa ana rafudhi ya kipemba, gia yake ana mgongwa Muhimbili! ,siku ya kwanza sikumjua nikampa Ten, nikapita tena mitaa hiyo akanisimamisha akapiga kizinga tena...aisee sikumchelewesha nikamchana mbaya....
 
Back
Top Bottom