John Mnyika
JF-Expert Member
- Jun 16, 2006
- 713
- 1,246
Kumetolewa tuhuma kadhaa kuhusu ubadhirifu wa fedha za wakatoliki zikimlenga Dr Slaa; kwa bahati mbaya hoja hizi zimeanza kujitokeza sasa wakati ambapo Dr Slaa yuko katika heka heka za kuibua ubadhififu BOT, Richmond, Meremeta nk. Kwa vyovyote vile kuchanganya mjadala wa Balali na BOT na Dr Slaa kutapoteza mwelekeo wa mjadala mmoja wapo. Hivyo nimefungua thread hii ili yule anayetaka kumjadili Dr Slaa amjadili hapa. Kule kwa BOT mjadala wa BOT na Balali uendelee kujadiliwa bila kuingiliwa.
Kwa wale walioanzisha hoja kuwa Slaa alifanya ubadhirifu wa mali za kanisa katoliki; huu ndio wasaa wenu sasa wa kutoa facts.
Mimi nimeshaweka maoni yangu bayana kuwa namfahamu Slaa kwake Karatu na Sinza DSM pia ni jirani yangu. Ni mtu wa kawaida sana.
Na pia najua ni kwa nini alitoka upadri kanisa katoliki(ingawa sakramenti ya upadri haifutiki).
Wenye taarifa tofauti waziweke hapa basi zijadiliwe. Kule tuendelee kujadili BALALI, BOT na UFISADI katika taifa letu.
JJ